Notifications
  • MY DIARY (3)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA TATUTULIPOISHIA...Nazani sasa unanielewa ninaposema nilikuwa sina ndugu kwani baba yangu hakuwa na ndugu yeyeote zaidi ya marafiki ambao na wao kwa sasa ndio hao wameshagawana mali zote. Nimebaki mimi na dunia yangu hivyo basi nilimwomba rafiki yangu wa kufa na kuzikana kwa jina Joyce anisaidie kunisitiri nyumbani kwao.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Likizo ilipoisha tulirusi shuleni na…
  • MY DIARY (2)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA PILITULIPOISHIA...Kwa ufupi japo sitaki kueleza historia yake ila kwa sasa ni shoga na teja. Baba yetu alitupenda sana na alihakikisha tunapata elimu nzuri na bora. Mimi na kaka yangu wote tulisoma International school ya hapo Moshi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Baadaye kaka yangu alianza kuvuta bangi kitu ambacho kilimtia hofu baba yangu na kuamua kumpeleka kusoma nje ya nchi.Alikosea sana…
  • MY DIARY (1)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA KWANZANilikuwa juu ya jukwaaa nikifanya vitu vyangu ili hali nikijua kabisa watu wote waliokuwa wakinitizama walikuwa wanaumia roho kutokana na mvuto wa umbo langu niliokuwa nao. Nilisikia mijibaba miwili ikiulizana hivi lile wowoo ni la kwake au ni la mchina? Mmoja wao akaropoka “wee kitu original hicho,kwani umemsaahau huyu binti tulishakutana nae kule Arusha mpaka tukambatiza jina la soda kubwa tena ya fanta yaani BAMBUCHA.?” Yeah nimekumbuka alidakia…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (18)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA NANETULIPOISHIA...“Mamaaaaaaaa!” Anna akapiga kelele na kutereza vibaya, miguu yake ikaliacha daraja, Seidon akawahi kukaza mikono na kumzuia, lakini miguu yake tayari ilikuwa imeacha daraja na sasa ikining’inia chini ya daraja. Anna akalia kwa uchungu sana, akijua kuwa mwisho wake sasa umefika.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“Jipe moyo Anna, tumefika mwisho sasa,” Seidon…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (17)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA SABATULIPOISHIA...Amatagaimba kabla ya kuondoka akachukua maji kutoka kwa Seidon na kumpa Anna, akayanywa kwa fujo na kuyamaliza. Nguvu zikamrejea. Anna akapanda juu ya farasi na Amatagaimba akatua nyuma yake, safari ikaanza.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Seidon akapiga mbio kwa ustadi akipita vijilima vilivyo ndani yake, “Amatagaimba, Sherhazad na Wafuasi wake…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (16)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA SITATULIPOISHIA...Seidon alikuwa katika hali mbaya sana, kama ni kupambana basi alikuwa kapambana na jitu la kutisha linalowaka moto kila upande. Ilikuwa ni wakati wa kumaliza kazi aliyotumwa, akasikia radi zikipiga huku na huko, yule malaika wa moto akashtuka na akajua kwa vyovyote mvua itapiga hapo muda si mrefu, na kweli alipogeuka ulikotokea mlio ule.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (15)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA TANOTULIPOISHIA...Amatagaimba akarudisha upanga wake na kumpa mkono, akamwinua.“Wewe ni nani?” Amatagaimba akauliza.“Anna, naitwa Anna, Anna Davis,” akajitambulisha kwa sauti ya kukwamakwama.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...“We umeingiaje huku?” Amatagaimba akauliza tena mara hii kwa mshangao zaidi.“Nilikuwa na wenzangu, tulikuja ah, sijui hata kufanya nini, mimi nika,…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (14)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA NNETULIPOISHIA...Seidon alisimama kwa taabu, akaliendea fuvu lile lililokuwa chini katika mchanga, lakini kabla hajaliokota alibaki kinya wazi, pale lilipoangukia mchanga wote uliondoka na kufanya duara, kisha lile fuvu likaonekana likiwa juu ya kitu kama jiwe jeupe safi ambalo halikuwa na hata chembe ya vumbi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Seidon aliinama na kuokota…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (13)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA TATUTULIPOISHIA...“Nimeiona shida yako, nimesikia kilio chako lakini jambo moja ninaloweza kukwambia ni kwamba, nguvu zetu na nguvu za huku ni kinzani sana, nikikuahidi kukuvusha katika daraja la pepo nitakuwa mkaidi mbele ya watu wangu, kwa kukusaidia ewe shujaa wetu, nitakuonesha njia ya kuzunguka ambayo itakufikisha katika lango la Hamunaptra,IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • HAMUNAPTRA - MJI ULIOPOTEA (12)
    Jina: HAMUNAPTRAMtunzi: Richard MwambeSEHEMU YA KUMI NA MBILITULIPOISHIA...“Seidon na Amatagaimba, nilikuwa nikiwasubiri kwa hamu kubwa mfike hapa, niliwaona tangu mbali na nia yenu njema, nifuateni,” Yule mzee akawaambia, Amatagaimba na Seidon wakatazamana kisha wakapeana ishara ya kumfuata wakaenda pamoja naye.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Mbele kidogo wakaingia kwenye piramidi moja dogo lakini lililoonekana kumegekamegeka…

MAHABA NIUE (13)

Mwandishi: Emmanuel F. Kway

SEHEMU YA KUMI NA TATU
ILIPOISHIA...
Msimamo wa JOSEPHINE juu ya kuhama kwa Ramsey bado ana ukazia na kweli kutaka aame maeneo yale ambapo alimwambia tayari kesha mtafutia nyumba MIKOCHENI.
"unajua Ramsey nakupenda sana ndo maaana nafanya ivi"

KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE BURUDIKA NA VIDEO HII

SASA ENDELEA...
Aliongea Josephine wakiwa ndani ya gari aina ya rexus ambapo Ramsey ndie aliye kua akiendesha gari hiyo ambapo nyuma yake kulikua na canter ambalo lina wafuaata nyuma kwa ajili ya kuhamisha mizigo ya RAmsey
"hata mimi mbona nakupenda josephine wangu"
"sijui kwanini nakupenda hivi nipo radhi hata nimuuwe mume wangu wa ndoa ili mradi nisi kukose Ramsey"
"mimi wako peke yako JOSEPHINE usijali"

tayari Ramsey aliegesha gari maeneo ya ubungo maziwa na wote kushuka na kutedmbea kwa dakika kadhaa ambapo walifika tayari anapoishi Ramsey
"baby yaani wewe ndo unaishi ndani ya hiki kibanda?!"
aliuliza Josephine na kumfanya Ramsey ashtuke baada ya kusikia geto lake limna itwa kibanda.
"kibanda?!"
"ndio kibanda tena sijui kwanini nime kuja na gari ya mizigo haina haja ya kuchukua mzigo wowotw ule,"
"na pamba zangu je?"
"nimesema haina haja ya kuchukua kitu chochote utaenda ivyo ivo. kila kitu uta kikuta huko huko"

maneno yale yana mfikia mama khadija akiwa chumbani na kumfanya atoke nje
"Rmsey njoo mara moja"

mama khadija aliita baada ya josephine kutoka nje
"unasemaje?"
"huyo nani yako?"
"huyu hakuhusu hapa nina hama"
"jamani Ramsey wangu uataondokaje nitabaki na nani?"
"una matatizo ya akili wewe siku izi naona, utabaki na mumeo"
"hapana Ramseyn wangu niambie wapi unahamia namimi niwe nakuja Ramsey niambie tafadhali nani ata kidhi kiu yangu. hakuna mwanau me anayenipatia kama wewe"

Ramsey alimwangalia mama khadija machoni na roho ya uruma kumwingia huku roho nyingine ikipingana na jambo ambalo analotaka kulifanya,

alichofanya Ramsey alimpa namba zake za simu mpya,
na baadae kuongea na mwenye nyumba baada ya kumaliza kila kitu alirudi ndani ya gari na kumkuta Josephine akiwa yupo ndani ya gari tayari.

aliwasha gari na safari ya kuelekea mikocheni kuanza. ambapo baada ya nusu saa tayari walifika kwa warioba kukata kulia. njia hiyo ana ikumbuka vizuri ya kwenda nyumbani kwa Doreen kweli, ana iona nyumba ya Doreen na kuiangalia.

"Ramsey una iona hii nyumba?'"
aliongea Josephine huku akimuoneshea nyumba ya Doreen
"ndio nimeiona"
"kwa rafiki yangu hapa anaishi hapa"
"hapa kwenye hii nyumba?"
Ramsey aliuliza mara mbili mbili kana kwamba haja sikia
'" ndio ana itwa Doreen"
Ramsey alimgeukia josephine na kumwangalia kisha akaendelea kuangalia mbele huku akiwa makini juu ya usukani.
"na tukirudi nataka tupite wote hapa tuka msalimie"
"baby nita kua nime choka"
"noo nakuomba twende"

Ramsey hakua na ujanja ili bidi akubali . baada ya dakika kumi tayari Ramsey aliingiza gari hiyo ndani ya geti kubwa na wote kushuka ndani ya gari.
"kariibu makazi mapya Ramsey:"

uzuri wa nyumba hiyo Ramsey hakuamini na mkumfanya awe na furaha sana alitumia nafasi hiyo kuikagua akizunguka nyumba nzima. ambapo kila alilo liona lili mfanya awe na furaha sana.

aliingia ndani ya nyumba na kuona tv kubwa sana na kuzidi kufurahi. alimvuta JOsephine na kumpiga busu la mdomo huku akiwa mwenye furaha sana.

ila baadae ana katishwa furaha yake baada ya kuambiwa kuwa wange takiwa waende kwa Doreen.
RAMSEY anaingia ndani ya gari akiwa na mawazo mengi ambapo aliwaza ita kuaje Josephine akijua kuwa ana mahusiano na rafiki yake Doreen'

walifika nje ya geti la Doreen na kuanza kupiga honi. hakuamini macho yake baada ya kumuona Doreena ana fungua geti na kutoka nje. na baadae kufungua geti ili gari hilo liweze kuingia ndani kutokana na alijua mmiliki wa gari hilo alikua rafiiki yake

"baby ingiza gari ndani"

RAmsey alishtuliwa baada ya kuganda akishangaa na kubaki kujishauri aingize gari ndani au ...


Ramsey alikanyaga mafuta na kuingiza gari ile ndani ya geti hillo ambapo Doreen alikua bado hajamuona kutokana na gari hiyo kuwa tinted yaani vioo vyeusi tena vikali,

baada ya kupaki gari wa kwanza kushuka alikuwa ni Josephine ambapo alimuendea Doreen na kuanza kusalimiana kana kwamba hawajaonana kipindi cha muda mrefu sana.
" nani ana endesha gari nilijua wewe ndo unaendesha gari?"

maneno hayo aliongea Doreen huku akiungalia mlango wa DEreva ambapo ndani yake alikua Ramsey akisikia kila kitu
"hapana ,kuna kijana wangu ana niendesha Ramsey hebu shuka basi nawewe ndani ya gar"

aliongea JOsephine huku akiuendea mlango wa Ramsey na kuufungua ambapo macho kwa macho waligongana na Doreen na wote kubaki kushangaana
"mamii ume mtoa wapi huyu Ramsey?"
"khaa kwani una mfahamu"?
"namfahamu ndio, huyu Ramsey, we ume mtoa wapi?"
"aliniuzia madini ya dhababu ni kijana mzuri sana"

wakati huo Ramsey alikaa kimnya akiwa ana sikiliza maongezi yale bila kusema chochote kile,
"mambo vipi Doreen:"
"poa tu wewe mwana ume wewe una mambo mengi,, enhee hiyo biashara ya dhahabu umeanza lini?"
"mbona kitambo tu"
"Ramsey naomba unisubiri ndani ya gari nina maongezi kidogo na doreen"

aliongea josephine maneno yale na kumfanya Ramsey aingie ndani ya gari haraka sana tena alishukuru sana kupewa nafasi ile la sivyo vinginevyo angeunguza picha na mambo yange haribika pale pale.

baada ya dakika kadhaa Josephine ana ingia ndani ya gari na Ramsey kuwasha gari na kutoka nje ya geti llile huku akishukuru mambo kwenda sawa,

breki ya kwanza ili kuwa nyumbani kwa JOsephine ambapo kwa mbali ana ona gari aina ya Range sport nyeupe na kuanza kushtuka akiingiwa na wasi wasi mwingi sana, na kumfanya Ramsey amuangalie,
"vipi JOsephine mbona ivyo, kuna nini?"
"una ona iyo RANGE nyeupe hapo"?
"ndio nime iona pale nje ya geti lako?"
"mume wangu amerudi"
"una semaje sasa kwaio ita kuaje?"
"hakuna shida wewe twende tu"

Ramsey bila wasi wasi ana fika na kusimamisha gari nyuma range sport nyeupe na wote kushuka baada ya kushuka tu ana ona geti kubwa lina funguliwa na mzee mrefu mweupe ambae mwenye ndevu ndevu zenye sharubu kutoka nje ya geti hilo, huyu ali tambua moja kwa moja alikua ni mume wake na josephine sababu,

josephine alimfuata na kumkombatia kwa furaha huku akimpiga mabusu ya mdomoni.

"mume wangu mbona ghafla ivyo?"
"hapa ni kwangu siku yoyote na muda wowote ule nina uwezo wa kuingia"
"aya baba karibu mume wangu mbona upo juu juu ivyo?"
"nataka kusafiri tena, hapa napo kwambia nita ondoka na ndege ya saa kumi na moja, natakiwa niwahi eapot Mke wangu,,"
"jamani hata kuongea mume wangu?"

upande fulani Josephine aliijifanya kukasirika ila moyoni alikua na furaha sana kwani alitaka kuji vinjari na Ramsey,

"alafu mume wangu sija kutambulisha huyu ana itwa Ramsey huwa ana nisaidia sadia sana, Ramsey huyu mume wangu ana itwa Mr,David Mwasha ndio baba watoto wangu, nampenda sana"

Ramsey alijifanya kujichekesha huku akimpa mkono David Mwasha baada ya utambulisho ule ila David Mwasha, hakutoa mkono wake na kubaki kumwangalia Ramsey kwa macho makali,

"sitaki nikuone na mke wangu kijana iwe mwanzo na mwisho"

aliongea David Mwasha kwa hasira kali sana huku akimwangalia kwa macho ya simba Ramsey

"lakini mume wangu mbona una wivu?"
"QUIT , nitaku labua sasa hivi. hivi mimi nita kua bwege kiasi gani , eti rafiki yako mpaka kwenye magari yangu, kijana naomba upotee sasa hivi kabla sija chukua uamuzi mwingine mba-ya"

Ramsey hakua na la kusema alijizoa zoa na kuondoka akiwa mwenye hofu sana kutokana na mzee huyo hakuwa na masihala na mke wake.

ili mbidi ata fute taxi ambayo ili mpeleka kwenye makazi yake mapya mikocheni.

"WEWE UNA TAFUTA KIFO RAMSEY KAMA UNA TEMBEA NA JOSEPHINE AU UNA MTAKA BORA UACHANE NAE, MAANA UNA JITAFUTIA MATATIZO, UTA UWAWA BURE PLEASE PLEASE, MIMI BADO NAKUPENDA SANA MWAA MWAA!!!!"

ulikua ni ujumbe mfupi kwa njia ya sms kutoka kwa Doreen na kweli meseji ile na jinsi mambo aliyo yakuta kwa Josephine vilikua vina endana kabisa,
alishusha pumzi ndefu na kuingia ndani ya geti lake na baadae kuingia sebleni na kuji tupa kwenye kochi huku akitafakari mambo mengi sana,

pale pale simu yake ilianza kuit na kumshtua kutoka katika dimbwi la mawazo mazito, aliamngalia ile skrin ya simu na kukuta ni Josephine ndo alikua akipiga simu ile ila alikata simu ile na kuipuuzia ila iliendelea kupigwa lakini Ramsey hakuipokea baadae ana sikia ujumbe mfupi wa sms na kuifungua

"BABY PUNGUZA HASIRA USINI FANYIE IVYO RAMSEY WANGU, INEED YOU STIL PSE AM SO SORRY KWA YALIYO TOKEA LEO NAJUA MIMI NDO SOURCE LAKINI NAOMBA UNISAMEHE KWA YOTE,NIPO NJIANI NAKUJA MPENZI WANGU TUYAMALIZE LEO LEO NA NINA ZAWADI YAKO"

Ramsey alijikuta na lainika kusikia na kumpigia simu Josephine akimwambia kuwa tayari ame msamehe,

baada ya hapo Ramsey ana ingia bafuni na kufungua bomba la mvua na kuanza kuoga huku akita fakari mambo mengi sana juu ya maisha yake,
ki ukweli maisha ya Ramsey yalibadilika na kuanza kuishi maish ya kitasha baada ya kumaliza kuoga ana jitupa kitandani ila baadae ana sikia mlio wa honi, na kuinuka na kuku mbuka kuwa Josephine alisema kuwa ata kuja.

alitoka nje na kufungua geti ambapo alionge RANGE SPORT nyeupe ina ingia ndani ya geti na kuanza kutetemeka sababu gari hiyo ili kua ni ya mume wake Josephine aitwae David mwasha,

aliangalia usawa wa geti tayari kwa kukimbia endapo lolote lita kalo tokea kwa wakati huo,

alizidi kukaza macho upande wa mlango wa dereva ili aweze kujua ni nani atae shuka ndani ya gari hilo wasi wasi una zidi kumuingia baada ya kama dakika mbili nzima hakushuka mtu yoyote yule alinza kurudi nyuma akielekea nje ya geti ila alivyo jiangalia alijikuta yupo na boxa peke yake,
'potelea mbali hapa nakimbia hivi hivi'

kimoyo moyo Ramsey aliongea.

"ramsey baby mbona ume kaa kimashaka"
alishuka Josephine ndani ya gari huku akimuendea Ramsey, lakini haku taka kuamini kama Josephine alikuja peke yake alijua wenda ni mchezo wa kutegwa alinyata mpaka ndani ya gari na kuli fungua ambapo hakumuona mtu yoyote alishusha pumzi ndefu na kumuangalia josephine.

"baby nipo mwenyewe"
"hata kama. lazima niji hami"
"uji hami na nini sasa?"
" si na yule mumeo la kauzu hilo, yule jamaa ni mjeda nini?"
"aah wapi hana lolote basi tu ana mikwara ana wivu sana, ila kwangu haongei chochote kile"
"maana pale kidogo nimwage kojo siku fichi, iyo mijicho aliyo nitolea kama kitu gani sijui, nikasema hapa napigwa ngumi, pale nime shukuru ujue maana nili jua kama sito pigwa kelbu basi ngumi"
"asingeweza we akupige mimi nipo, hata siku Ramsey"

Josephine aliingia ndani na moja kwa moja kuingia jikoni kuanza kupika chakula cha usiku ambapo Ramsey alikua sedblen anaangalia tv,

USIIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUTUMIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK, LIKE UKURASA HUU USIPITWE NA SIMULIZI NA MENGINE HUKO FACEBOOK

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE TAZAMA VIDEO HII KAMA MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA

KWA TELEGRAM👇BONYEZA HAPA
40 Mahaba Niue Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni