MAHABA NIUE (27) JINA: MAHABA NIUE Mwandishi: Emmanuel F. Kway SEHEMU YA ISHIRINI NA SABA ILIPOISHIA... Baada ya dakika arobaini tayari alifika dukani kwake, ila katika hali ya kushangaza alivyotaka kuingia ndani ana ona polisi wanne wamemfuata na kumshika mkono KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE BURUDIKA NA VIDEO HII SASA ENDELEA... "wewe ndo Ramsey ?" "ndi ndio ndio ndo mimi" Ramsey alibabaika sana na kuishiwa nguvu kuliko maelezo. "una hitajika kituoni sasa hivi" aliongea polisi mmoja kati ya wengi Ramsey alishusha pumzi nzito sana iliyo changanyika na uwoga, kweli alihisi haja kubwa imem-bana maana alijua kivyovyote vile yalikua ni mahojiano kuhusu kifo cha Doreen . Watu wa pale walianza kumshangaa na prosper aliyekua ndani dukani alitoka nje na kushindwa kuelewa nini kime tokea, jasho jembamba lilianza kumtoka Ramsey na kuanza kupata picha jinsi gani atakavyo kwenda kuozea rumande au pengine jela kabisa, ila alibaki akitoa macho na kushangaa baada ya kumuona ESta ana shuka kwenye piki piki hu…