MAHABA NIUE (50)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
SEHEMU YA HAMSINI
ILIPOISHIA...
Kutokan na kuwa na hali mbaya sana hapo siku za nyuma, ivyo kupona kwa Ramsey ilikua asilimia hamsini peke yake, na wala si vinginevyo, alilia machozi, madaktari wale waliwaomba watoke nje ili wao waweze kufanya kazi yao ya kujaribu kuokoa maisha yake,vile vile hata kwa madaktari hawa kua na uhakika kama mgonjwa wao huyo ataweza kuishinda hali hiyo ya umauti,
KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE BURUDIKA NA VIDEO HII
SASA ENDELEA...
Walichukua vifaa maalumu na mtungi wa gesi ya oxygen na kumuwekea puani huku wengine wakimvua shati na kumuwekea mashine nyingine ya mapigo ya moyo,
Mashine ile ilizidi kupiga kelele kuashiria kuwa mapigo ya moyo yana zidi kushuka chini,
“dokta, ana kufa huyu”
“leta hiyo mashine hapo”
“ipi hii”?
“fanya upesi. ndio hiyo hiyo”
Dokta huyo alikua akipambana kuokoa maisha ya Ramsey alichukua mashine hiyo zilizo fanana na pasi nakuzishika mashine izo ambazo husaidia kushtua mapigo ya moyo, alipasha mashine izo, na kuziweka juu ya kifua cha Ramsey
“puuu”
Ramsey alitupwa juu ila bado hali ilikua ile ile, hawa kukoma, walifanya tena, mashine ile iliyokua ikisoma mapigo ya moyo, ilianza kulia taratibu mwishowe kutulia kabisa, kuashiria kua mapigo ya moyo yame tulia hayaendi.
‘”ame kufa tayari”
Aliongea nesi huyo baada ya kuona mashine ile ime tulia, lakini daktari Yule aliipashaa tena mashine ile iliyo kua ina fanana na pasi na kuiweka juu ya kifua cha Ramsey, ila bado Ramsey alikua ametulia, tayari mapigo yake ya moyo yalikua yame simama alimuangalia nesi kwa macho ya uzuni sana, na kutikisa kichwa kuashiria kuwa tayari mgojwa wao kapoteza maisha, mapigo yake ya moyo yameasimama, maana kwamba tayari ame fariki dunia,
“jaribu tena”
Alishauri nesi kwa unyonge huku akiweka vifaa vingine pembeni na dokta Yule kutii amri ile bila ubishi japo hakua na uhakika kama kile anacho taka kuki fanya kita fanikiwa , ivyo ivyo alipasha tena mashine zile na kuzigusisha na kuzikandamiza ju ya kifua cha Ramsey.
“puuuuu , tiiii tiiiii tiiiii’”
Kwa hali ya kustaajabu sana na kushindwa kuelewa , ili kua ni kama miujiza baada ya kusikia mashine ile imeanza kutoa sauti kwa mbali kuashiria kuwa mapigo ya moyo yameshtuka hakika lilikua ni jambo la miujiza sana,
“ana maisha marefu sana huyu kijana”
“kweli dokta”!
***
Kilio kilizidi nje ya hospitali hapo kutoka kwa Sabrina hakika alijua kuwa kifo ndiko kitu pekee kitakacho mkabili baba wa mtoto wake Ramsey, licha ya kupewa moyo na Kway lakini ilikua kazi bure ilikua ni sawa na kutwanga maji ndani ya kinu, haikua kazi rahisi kumnyamazisha Sabrina wakati huo, alimuwaza sana mwanae Catherine ambae hapo baadae ata pata malezi bila baba,
“shemeji usilie, unakua una mkufuru Mungu , Ramsey atapona usijali kabisa, hawa ni madaktari bingwa”
“noo siwezi, najisikia vibaya, eeeh Mungu weeee,nini nime kukosea”
“nyamaza shemeji”
Wakati huo Loydah alikua amekaa chini sababu ya kulia na machozi yake kukauka, hakikal ilikua ni jambo la kuuzunisha sana, chumba alichokua Ramsey kilifunguliwa na daktari aliiyeeingia kumpa matbiabu hapo awali kutoka, wote walimvamia kama wana taka kumpiga.
“vipi hali yake, tuambie ukweli usitufiche Dokta”
Aliuliza Loydah
“ana hali mbaya sana, kijana naomba tuongee kidogo”
Dokta Yule alimshika mkono kway na kuingia nae ofisini kwake sababu hakutaka kuongea na wanawake wale alijua kivyovyote vile wasingeweza kuvumilia, kway alijua kuna jambo zito sana anataka kuelezwa,
Baada ya kufika ofisini mwa daktari huyo alivuta kiti kilicho kua pembeni yake na kuketi huku akifuatiwa daktari huyo nayeye kukaaa katika kiti chake, alivua miwani ya macho aliyokua amevaa na kuiweka mezani pale,
“una uhusiano gani na huyu mgonjwa”?
“ni kama mdogo wangu”
“sasa nime kuita hapa,wewe ni mwanaume, ndo maana siku taka kuwa ita hao wana wake, nikaamua kukuita wewe moja kwa moja,”
“ndio dokta”
“ngoja nikwambie ukweli huyu mgonjwa hapa hatuwezi kumtibu, huyu bwana labda msubiri miujiza ya Mungu,huo ndo ukweli, ana kansa ya ubongo, labda kidogo mumpeleke india kule kuna madaktari bingwa, wata msaidia tu kusogeza siku zake mbele, lakini hatoweza kupona nina uhakika asilimia mia, sina haja ya kukuficha kitu chochote kile, na nilijaribu sana kuokoa maisha yake.”
“umesema hawezi kupona kabisa”?
“sitaki kuku danganya, ndo maana nika kwambia labda itokee miujiza ya Mungu, lakini mimi na profesheno yangu nime nawa mikono”
Kway alishusha pumzi ndefu sana huku akiwa ana tetemeka hakutaka kuamini kuwa siku chache baadae Ramsey angeenda kufukiwa yalikua ni maneno mazito sana hakuelewa Loydah akiyasikia maneno yale angeli fanya nini, hakuelewa aanzie wapi kumueleza Loydah na SABRINA.
“lakini nakuomba, usi kurupuke kuwaambia hao wana wake, tumia busara sana”
“dokta asante sana”
Kway alitoka na kuweka tabasamu bandia ili kuwafariji Sabrina pamoja na Loydah waliokuwa wakilia hospitalini pale.
****
Baada ya wiki moja Ramsey aliruhusiwa hospitalini na kurudi nyumbani ambapo alikuaakiishi kwa dada yake loydah ki kukweli bado hali yake iliikua mbaya sana, wakati mwingine alikua akitapika damu, , daktari maalumu alikodishwa ili awe akimwangalia kila siku,
Walikaaa kikao kidogo ili waweze kuchanga pesa za kumpeleka Ramsey nchini india kwa ajili ya matibaubu, japokua kuwa Kway alikua na siri nzito lakini hakuwa tayari kuwaambia kuwa Ramsey hatoweza kupona alicho fanya nayeye alijumuika nao na kujitolea kiasi cha dolla mia nne kama mchango, Loydah na Sabrina wote walitoa milioni tano tano,na kiasi kingine cha pesa, kupewa na ndugu jamaa pamoja na marafiki..
Tayari utaratibu wa safari ulipangwa huku Ramey akitafutiwa hati ya kusafiria, kila kitu kilivyo kamilika siku hiyo, gari maalumu kwa ajili ya kubebea wagonjwa lili kua tayari lipo nje ya nyumba ya Loydah likiwa lina piga king’ola huku taa zake za juu ziki waka, Ramsey akiwa juu ya machela walimuingiza ndani ya gari hiyo na safari ya kwenda mwalimu nyerere uwanja wa ndege kuanza.
“sabri,,na”
“abee Mume wangu”
“nikifa leo naomba mwanangu umtunze vizuri, uwe jasiri. Najua uta kua na kazi ngumu sana, uli nipigania sana, nikiwa nina umwa,mimi sio wa kuishi tena, asije kudanganywa na wanaume, nakupenda sana Sabrina najua nime kukosea sana kwa kutembea na wana…..”
“usiseme ivyo baba Catherine, utapona huko una poenda kuna madaktari bingwa, wata kusaidia na utarudi katika hali yako ya kawaida”
“hujui maumivu nayo pata hapa Sabrina sitoweza kuishi, naomba kabla sijafa niongee na mwanangu”
“yupo kwenye gari la nyuma”
“sawa, tuki fika uwanja wa ndege, nataka niongee nae”
Yalikua ni maongezi ya kuuzunisha ndani ya ambulance hiyo, nyuma walikaa madaktari wengine huku pembeni akiwemo Sabrina, likizidi kuchanja mbunga kuelekea uwanja wa ndege , kwa bahati nzuri wali bahatika kupata nafasi katika shirika hilo la ndege la indian airways , ambayo ili kua inaondoka saa kumi jioni,
Magari yalizidi kupisha njia ili gari hilo linalopiga kelele liweze kuwahi kama sheria za barabarani zinavyo takiwa kufuatwa, na aliye takiwa kwenda na RaMSEY INDIA alikua ni Sabrina ambae alichaguliwa aweze kwenda nae nchini huko kwa matibabu,
Gari hilo likiwa linapiga king’ora baadae kidogo lilikua tayari kwenye maegesho ya uwanja wa ndege wa mwalimu nyerere huku wauguzi maalumu walio andaliwa kwa kazi hiyo ya kushusha machela walitokea huku wakiwa wamevalia sare zao nyepe, hakika walikua wakijua ujio wa mgonjwa huyo, Kabla machela ile kuanza kupelekwa ndani ya mlango maalumu kwa ajili ya kusafiri Ramsey aliomba kuongea na mtoto wake Catherine maneno ya mwisho sababu hakuwa na uhakika kama huko anapo enda angerudi, kutokana na maumivu makali sana aliyokua akiya sikia mwilini mwake.
“mwan..angu Catherine, nakupenda sana”
“baba kwani una umwa nini”?
“malaria mwanangu ila nita pona, ukiwa mkubwa mwanangu, mama yako ata kupa ujumbe wangu,”
“kwani wewe hautokuwepo?’, uta kua wapi, ?alafu anco kway kaninunulia saa ya BEN 10 nzuri hiyo nime iacha nyumbaniiii”
“hahaha mwanangu, kwanini hukuja nayo niione”?
“Mama kani kataza nisije nayo. Ila nawewe usi sahau kuni letea zawadi yangu, nataka zile nguo za BAT MAN zile”
“saaaaaawaa nitaaaakulee….”
Ramsey alianza kuongea kwa shida sana na kushindwa kutoa maneno vizuri mdomoni na kuanza kuhema kwa shida sana huku akionekana kuta futa pumzi na wakati mwingine kufungua mdomo ili avute pumzi,
“baba cathrine”
“naaaaaaaam”
Sarina alionesha hali ya kuchanganyikiwa sana, Ramsey alimshika mkono wa sabrina na kuubusu, kila mtu alidondosha chozi, walikua katika roho ya uzuni, hawa kujua kama ile ndo ishara ya Ramsey kuwaaga baada ya hapo ukimnya ulitawala,
jambo lili lowafnya wazidi kupata hofu, daktari mmoja wao alitoa kifaa cha kupima mapigo ya moyo, laikini alijikuta ana pima mara mbili mbili huku akiwatazama wenzake, bila kuuliza chochote kile macho ya daktari yalionesha wazi kabisa kuna hali nyingine mbaya kabisa na habari tofauti ya kutisha.
Daktari Yule alitingisha kichwa na kutoa ishara ya mkono kuashiria kuwa Ramsey amefariki dunia pale pale Sabrina aliishiwa nguvu na kudondoka chini., kutokana na habari zile kumshtua moyo wake.
Baada ya siku mbili taratibu za Ramsey kuzikwa ziliandaliwa na kuamua kuwa waka mzike makaburi ya kinondoni hakika kilikua ni kilio cha kutisha sana kwa Sabrina pengine alitamani kujiua ila hakuelewa akifa Catherine ange baki na nani na angeisi na nani,
tayari alikua amesha zimia mara tisa, alililia machozi yaka kauka yote, akiwa na cathrine wote walikua wakilia , japo alikua mdogo sana alielewa nini maana ya kifo alielewa vizuri kuwa baba yake hatomuona tena japo aliambiwa kuwa ipo siku ata kuja kumuona tena,
Safari ya kuelekea makaburi ya kinondoni ilianza huku msafara wa magari ukiwepo kwenda kuupumzisha mwili wa Ramsey katika nyumba yake milele, wana kwaya walio kodishwa kuomboleza walifanya kazi yao huku wakiwa na uzuni mwingi.
“tuli kuja kwa udongo na tuta rudi kwa udongo, ”
Aliongea mchungaji Patric huku akitupa mchanga juu ya kaburi la Ramsey, hakuna mtu aliyeweza kuamini kuwa leo hiii Ramsey amelala chini hatoamka tena
“uwiiiii Ramsey mdogo wangu, nime baki mwenyewe tulikua wawili tuuu , eeeh MUngu weee, Ramsey mdogo wanguuuu, kwanini mbona mapema ivyooo”
Kilikua ni kilio kutoka kwa Loydah huku wakipokezana na Sabrina kulia, katika hali yakushangaza Sabrina alichomoka na kuingia ndani ya kaburi na kulala juu ya jeneza la Ramsey, huku akilia na kutaka wamfukie nayeye,
vijana watatu walishuka na kumtoa ndani ya kaburi, kila mtu alimuonea huruma sana, macho yake yalikua yasha vimba na kuwa mekundu, taratibu za mazishi zili kamiliaka ila Sabrina hakutaka kuondoka, na kumuacha Ramsey akiwa amelala peke yake kaburini,
jambo ambalo hawa kutaka litokee, walimbembeleza mwishowe kukubali, ila baada ya kutembea hatua chache alichomoka na kuwa sukumiza watu waliomshika na kurudi tena kulala juu ya kaburi la Ramsey huku akilia sana…..
MWISHO
KWA KUTUMIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK, LIKE UKURASA HUU USIPITWE NA SIMULIZI NA MENGINE HUKO FACEBOOK
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni