ROHO MKONONI (12) JINA: ROHO MKONONI Mwandishi: Zuberi Maruma SEHEMU YA KUMI NA MBILI ILIPOISHIA... Anategeshewa madawa ya kulevya anakamatwa anahukumiwa na kuswekwa lupango,mbaya zaidi anaingizwa ndanh ya selo ijulikanayo kama lango la jehannamu,hakuna historia ya kuingia huko na kutoka ukiwa hai naye anajikuta katika mateso makali je atasalimika kweli?! Tusonge kuzidi kuburudika zaidi! KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media BASI INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA 👈 SASA ENDELEA... Kiza kilitanda ndani ya macho yake,kumbukumbu kwa mbali zikaanza kumjia!. Akajaribu kufumbua macho yake, yalikuwa mazito kana kwamba yakigoma kufumbuka ila hatimaye yakafumbuka. Akajaribu kuvuta kumbukumbu ni wapi hapo alipo,kumbukumbu azikumsapoti,zikagoma kabisa,ila alijua muda ule ni usiku kutokana na kiza kizito,kichwa kilikuwa kizito kwa maumivu makali. Akatuliza akili!,hapo hapo sasa ndipo kumbukumbu zilipoanza kumrejea maumivu makali ya kausweka moyo wake,akatak…