ROHO MKONONI (13)

Zephiline F Ezekiel
ROHO MKONONI (13)
JINA: ROHO MKONONI Mwandishi: Zuberi Maruma SEHEMU YA KUMI NA TATU ILIPOISHIA... Dunga akaongea kishari mkono wake wenye silaha ukiwa una angalia chini,kijana yule alojulikana kwa jina la Luteni Johnson Mamba ndo alikuwa msaidizi wake,alimfikia akamshika mkono na kumkokota mpaka nje. KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media BASI INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA 👈 SASA ENDELEA... "Mkuu punguza hasira kumbuka huyo ni mwanausalama tena inspekta wa polisi je unadhani ukimtandika risasi jeshi lita acha kufatilia na mashahidi niwafungwa utakaa pabaya mkuu" Wakati wakielekea ofisini Johnson akatumia wasaha huo kumshauri mkuu wake,hata Dunga alipofikiria ni kweli,jeshi la polisi lazima lingechunguza kijana wake kafa katika mazingira gani!,na ingejulikana kuwa yeye ndo kamtandika risasi tena hadharani angejiweka pabaya!. "Lakini ilikuwa ni oda ya usalama wa taifa !," Dunga akaongea kwa sauti ndogo,sauti ilojaa wasiwasi …