ROHO MKONONI (13) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumamosi, 9 Julai 2022

ROHO MKONONI (13)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Zuberi Maruma

SEHEMU YA KUMI NA TATU
ILIPOISHIA...
Dunga akaongea kishari mkono wake wenye silaha ukiwa una angalia chini,kijana yule alojulikana kwa jina la Luteni Johnson Mamba ndo alikuwa msaidizi wake,alimfikia akamshika mkono na kumkokota mpaka nje.

KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media BASI INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI
πŸ‘‰GUSA HAPAπŸ‘ˆ

SASA ENDELEA...
"Mkuu punguza hasira kumbuka huyo ni mwanausalama tena inspekta wa polisi je unadhani ukimtandika risasi jeshi lita acha kufatilia na mashahidi niwafungwa utakaa pabaya mkuu"

Wakati wakielekea ofisini Johnson akatumia wasaha huo kumshauri mkuu wake,hata Dunga alipofikiria ni kweli,jeshi la polisi lazima lingechunguza kijana wake kafa katika mazingira gani!,na ingejulikana kuwa yeye ndo kamtandika risasi tena hadharani angejiweka pabaya!.

"Lakini ilikuwa ni oda ya usalama wa taifa!,"

Dunga akaongea kwa sauti ndogo,sauti ilojaa wasiwasi tele!,

"Hata kama mkuu ni oda ya usalama wa taifa ndo si umuue hadharani,lazima upange mpango kabambe ikiwemo kuamishwa gereza then njiani gari ivamiwe auwawe,au njia nyingine yeyote ambacho kifo chake akitokuwa cha utata!"

Wazo lile dunga moja kwa moja akakubaliana nalo,alipofika ofisini kwake akaongea na Zidu juu ya mpango aloupanga kwamba ata andika barua kwa general kuomba kuamisha wafungwa kadhaa sababu ikiwa wingi wa watu,siku ambayo hata amisha wafungwa atamjulisha aandae vijana wake wavamie msafara na wajifanye kumtorosha Butu hapo askari wake wamuue kwa kumtandika risasi,hii isingeleta shida wala upelelezi ndani ya jeshi la polisi.

Pasina kupoteza muda Kapteni Dunga akaandika barua kwa General,ambapo baada ya kuituma siku ilofatia,kesho yake akapokea majibu kwamba Gereza la keko lishajulishwa hivyo aandaye hao wafungwa katika karandinga wasafirishe...
***
Kwa upande wa Butu maswali mengi bado yaliushambulia ubongo wake hasa tukio la mkuu wa magereza kumnyooshea silaha.

'ina maana kama si kutokea Jonson,Dunga angemtandika risasi na kumuulia mbali?!,kisa tu kampiga nyapara?!'

Jambo hilo alilifikiria sana alikumwingia akilini!,alijua lazima kuna kitu kinachoendelea dhidi yake!,akakumbuka yani yeye kuja tu,pasina kosa lolote akaswekwa lango la jehannamu tena ndani ya masaa 24 sawa na siku mbili za kifungwa,lango la jehannamu mahali wawekwao magaidi,majambazi sugu makatili,na viumbe visivyo stahili kuishi!,iweje awekwe yeye?!,yeye aloitumikia serikali tena idara ya polisi ulinzi na usalama wa raia na mali zake leo wamlipe vile?!,yeye ilipaswa awekwe triple A,iweje awekwe triple c?!,kwa uzoefu wake wa kipolisi akamtilia shaka mkuu wa magereza,akajua lazima anatumika,na maisha yake si salama,akajua ilipaswa afanye kitu haraka,kukaa pale ni sawa na kukisubiria kifo,na kingemkuta!.

Sasa angetokaje hali ya kuwa hata kazi nje akuruhusiwa kwenda kufanya pengine angefikiria kutorokea huko.

Japo kwa sasa Gereza lilimuheshimu hakukuwa na alothubutu kumtishia si nyapara,wala magwa,katu akujua hatari aloandaliwa...

Siku ilofatia asbuh alishangaa akiitwa akaelekea mpaka kwa mkuu wa magereza ndani alikuta pia wafungwa wa kutosha,huko ndipo walipoambiwa wa na amishwa gereza,hivyo wakatolewa chini ya ulinzi mkali,wakapakiwa katika karandinga lililozungushiwa nondo ndogondogo kwenye bodi,safari ikafatia wakisindikizwa na gari mbili za polisi

Tayari Zidu alisha waandaa vijana wake wa kutosha eneo la tukio tayari kwa uvamizi pale gari la magereza litakapowafikia.

Butu akujua hili wala lile,safari ikaendelea!....

Gari ilobeba wafungwa ilizidi kukata mbuga huku mbele yake pakiwa na kitara cha polisi na nyuma ikiwepo cruzar ya polisi ikiwa na maaskari takribani wa tano wenye mitutu waloivaa vifuani mwao,kitara cha polisi kilikuwa na askari wa tatu tu pale mbele,safari iliendelea na sasa walikuwa wakiikaribia keko,ila wakiwa katika eneo moja nyuma kidogo ya daraja Swami kitara cha polisi kilisimama,mbele yake paliwekwa mawe makubwa,dizaini kama kuzuia njia,

Askar wale wawili wakashuka kwa lengo la kwenda kutoa yale mawe yaliyopangwa chiani!.

Kosa!.

Ng'afla milio ya risasi ikasikika punde watu wasopungua kumi waloficha nyuso zao wakatokea toka chini ya daraja na kuanza kuwashambulia wale maaskari,wale walokuwa nyuma kuona hivyo nao wakashuka na kuwatupia risasi wavamizi,ila askari walizidiwa na mwisho kusamli amri,wavamizi wale wakaomba wapewe Butu gari ikafunguliwa Butu akatolewa,kisha maaskari wakaruhusiwa kuendelea na safari.

Kitendo kile kiliwashangaza sana wale wafungwa,askari kusamli amri,kukubali kuachia mfungwa pasina kupata jeraha hata moja,kila mmoja alisema lake,ila safari iliendelea.

Hawakuwa na uhuru ni wapi wangepeleka wasiwasi wao?!.

Kwa upande wa Butu machale mapema yalishamcheza hasa baada ya kuona urushianaji wa risasi kati ya pande mbili zile,ulikuwa ni wa uangalifu kuto mlenga mwenzake,kichwani mwake akajenga picha kuna kitu kinachoendelea pale,alikamilisha wazo lake baada ya kuona maaskari eti wanasamli amri na mwisho kukubali kumtoa nao kuendelea na safari yao.

Kipo wapi kiapo walichokula?, kupambana kufa kupona kulinda raia na mali yake,kivipi wakubali kumtoa kwa watu wasojulikana?!,alijiuliza pia je wale ni watu wa aina gani waloamua kumsaidia?!,alijua kwa kipindi kile hapakuwa na msaada wowote kwake asitegemee.

Watu wale walimswaga mpaka mahali walipoifadhi magari yao,walikuwa na magari matano,wakamwingiza katika gari moja wapo wengine wakaingia katika magari yao,yeye bado alibaki na butwaa akitafakari wale ni watu gani na li lipi lengo la wao kumchukua?!...

"Unapaswa ufungwe macho upaswi kujua ni wapi unapelekwa,kingine kaa utulie atutakufunga miguu wala mikono ila tuki gundua unataka ulete janja ujanja fulani hatutosita kukumaliza hata kabla ya muda tulokupangia kukuua nadhani tume elewana?!".

Mtu mmoja alimuongelesha Butu hata hivo kijana yule akujibu kitu,mtu yule akampa ishara mwenzake amfunge macho Butu kusudi asijue anapopelekwa,naye akatii hilo safari ikaendelea.

Redio ikawashwa njia nzima watu wale wakawa wakizungumzia maswala ya wasanii,Butu hakazidi kushangaa kwani alijua labda hata angepata chochote katika maongezi yao,alikaa kwenye gari mpaka akachoka,akujua ni wapi anapelekwa njiani ni kama alitembea masaa matatu hatimaye gari ilisimama.

Akajua sasa kashafika,akashushwa akakokotwa pasina kujua ni wapi anapelekwa ila aliweza kung'amua kuwa yupo msituni kwani alizisikia sauti za wanyama,na hata ndege pia aliundua kuna muda alikanyaga majani kuna muda alipishana na miti mwisho akasikia mmoja akisema...

"Dula hapa panatosha!"

Palepale akabwagwa chini akafunguliwa kitambaa sasa alipata kuona vizuri mazingira ya pale alipokuwepo.

Ni katikati ya msitu,tena katikati ya vichaka mbele yake akizungukwa na wale watu kumi tena wakiwa na silaha.

"Una dakika tano za kuvuta pumzi ilobakia,ndani ya dakika hizo waweza zitumia,'a' kwa kusali Allah aipokee roho yako na kuitunza mahali pema peponi amin,'b'kujitetea ama kwa kupambana na sisi au tukuruhusu ukimbie na che tunakupa nafasi uliza chochote,swali moja tu!,tutakujibu.

Butu alijua sasa anaenda kufa lakini huzuni yake kubwa anakufa bila kumlipizia aloiteketeza familia yake,anakufa na kinyongo,akajikuta machozi yakimchuruzika,ila

akakumbuka ana dakika tano tu alizopaswa achague,alitamani amjue mbaya wake,ila akuona uhafadhali huo hali ya kuwa anaenda kufa akaona ni bora tu asali sala zake za mwisho roho yake ipokelewe,baada ya dakika zile kuisha ndipo silaha zilipo mwelekea ni kwamba angetandikwa zote kumi kwa mara moja uwezekano wa kuendelea kuishi kwake usingekwepo.

"Kabla atujakuua nimeona ni vyema pia kukupa nafasi ya upendeleo uzitambue sura zetu sisi wauwaji wako!"

Palepale watu wale waka anza kuvua sox zile walizovaa vichwani.

Butu kuwaona tu watano kati ya kumi wale aliwatambua.

vipara.

Ndiyo ni wale waloshuka kwenye ndege siku ile wakiwa na madawa ya kulevya akawakamata na kuwatia ndani,simanzi ikamtawala upya,mabwana wale vipara,walimtazama kwa matabasamu mabaya,yalojaa dharau,kisha wakapeana ishara palepale milio ya risasi ikasikika.

Risasi kumi zikikishambulia kifua cha Butu akaporomoka chini,na kutulia tuli,mmoja wa watu wale akaenda na kusikiliza mapigo ya moyo yalitulia,akageuka na kumwonesha mwenzake ishara ya dole,mmoja mwenye kamera akaupiga mwili ule picha kadhaa.

"Mkuu tushaikamilisha kazi vipi huu mwili tuache huku?!".

"No! hiyo ni mali ubebeni muulete hapa kwangu haraka kesho usafirishie mzigo"

Palepale mwili wa Butu ukabebwa na kuwekwa nyuma ya buti kwenye tax moja wapo kati ya zile gari,safari ya kurudi mjini ikafatia...

John Butu anatandikwa risasi kumi na kupoteza fahamu,watu wale wakijua wamesha muua wanambeba na kumuingiza ndani ya Buti ya gari yao,je unadhani nini kiliendelea?!...

Baada ya kuuingiza ule mwili ndani ya Buti safari ikafatia.

Mwisho wa safari ulikuwa ni katika jumba la kifahari la Zidu,jumba ambalo ulitumia kufanya mambo yake ya siri,mwili ule ukatolewa na kuingizwa katika chumba maalumu,vijana wale wa usalama wa taifa hatimaye wakaondoka.

MASAA MATATU BAADAYE
Walinzi walifungua lango gari kadhaa zikaingia,zilielekea mpaka maeneo ya maegesho zikapakiwa vizuri kisha walokuwa ndani ya magari yale wakashuka,wa kwanza akiwa Zidu mwenyewe akaenda kufungua mlango,vijana wale waloshuka walielekea nyuma ya buti zao walipofungua na kutoa miili ya watu wakaingiza ndani,kule alipowekwa Butu,baada ya kukamilisha kazi yao wakarudi katika gari zao wakaingia na kutoka.

Zidu alielekea mpaka sebuleni kwake akaketi kochini,sasa alihitaji kumjulisha mh Rais walipofikia,akashika simu yake na kutafuta namba alizohitaji alipozipata akazitwanga,zilihita hatimaye zikapokelewa...

"Mh Raisi nimefanikiwa kuileta ile miili mpaka hapa pardon je kipi kifatie?!"

"Vizuri sana,ngoja niongee na dk Stanley aje aipasue hiyo miili na kuiyewekea mizigo mara moja kesho asubuh isafirishwe,then itapaswa iondoke na wamama wa tano ambapo watarudi nayo ikiwa na mizigo mingine sawa?!"

"Sawa mkuu!"

Kweli baada ya nusu saa gari ya dokta ikawasili,akiwa na msaidizi wake,dokta alikuwa kakunja sura akuipenda ile kazi sasa angefanyaje na ni amri ya kiongozi wa nchi,haraka wakaingia katika chumba kile cha siri,waka anza kuifanyia operesheni miili ile mitano na kuiweka kiasi kikubwa cha madawa katika matumbo yao,dokta alishtuka baada ya kuukuta ule mwili wa mwisho ukiwa na uhai,japo mapigo yake yalipiga kwa mbali!.

Akajikuta moyo ukimsuta,wajibu wa kazi yake ukamvaa,dhima ya kazi yake ni kupigania maisha ya kiumbe kilicho mahututi kuhakikisha kinakuwa hai,hapo ndipo ilipofuraha ya daktari yeyote ulimwenguni,akampa ishara msaidizi wake,operesheni ikaanza,kwanza kwa kumtolea risasi zote kumi,mwisho maswala ya kitabibu yakafatia,masaa manne wakaitimisha operesheni ile,sasa Butu alilala kitandani akitumia mashine za oxygen hali yake bado ilikuwa mbaya.

USIIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUTUMIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK, LIKE UKURASA HUU USIPITWE NA SIMULIZI NA MENGINE HUKO FACEBOOK

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE TAZAMA VIDEO HII KAMA MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA

KWA TELEGRAMπŸ‘‡BONYEZA HAPA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni