ROHO MKONONI (14)

Zephiline F Ezekiel
ROHO MKONONI (14)
JINA: ROHO MKONONI Mwandishi: Zuberi Maruma SEHEMU YA KUMI NA NNE ILIPOISHIA... ...hapo ndipo ilipofuraha ya daktari yeyote ulimwenguni,akampa ishara msaidizi wake,operesheni ikaanza,kwanza kwa kumtolea risasi zote kumi,mwisho maswala ya kitabibu yakafatia,masaa manne wakaitimisha operesheni ile,sasa Butu alilala kitandani akitumia mashine za oxygen hali yake bado ilikuwa mbaya. KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media BASI INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA 👈 SASA ENDELEA... Masaa yakakatika hatimaye Zidu akawasili toka kazini alipoelekea ile mida ya mchana,baada ya kuwasili kwa daktari. "Vipi kazi imekamilika?!" Zidu akamuhoji daktari yule huku akiketi sofani. "Ndiyo mkuu ile miili mitano mfu nimeipandikiza viroba vya unga ulivyo nipatia ila ule mwili mmoja nimeukuta una uhai nimeufanyia operesheni japo hali yake bado mbaya kupona ni kudra za Mungu..." Zidu akakunja sura,hasira zikampanda. "Kwani uliambiwa …