ROHO MKONONI (6) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Alhamisi, 7 Julai 2022

ROHO MKONONI (6)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Zuberi Maruma

SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA...
Dakika kadhaa zilizofatia watu wa nne walikwepo ndani ya chumba kidogo cha ofisi yake

"Ma afande nyinyi mkiwa kama watu wangu wa karibu,wasiri wangu nadhani mengi tumefanya tukiwa pamoja,kwa taharifa tu yule mtu tulomuua msitu Tasa hakuwa na hatia!"

KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media BASI INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI
πŸ‘‰GUSA HAPAπŸ‘ˆ

SASA ENDELEA...
"What?!" Askari wale wote wa kashtuka,hakuna kitu askari anacho ogopa au kukijutia kama kuhukumu kiumbe kisicho na hatia achia mbali kuua,

Ikabidi Butu awaeleze ukweli wote juu ya simu ile alopigiwa na kuchekwa kupewa maneno ya kejeli! Na mwisho mtu yule kuhitaji kuonana nae!,watu wale wakashtuka!...

"Muonane kirahisi tu?!" Inspekta Jona akauliza,huku wasiwasi ukionekana wazi usoni mwake!

"Lazima kuna kitu atakuwa amepanga dhidi yako!"

Afande Andrea akaongea kwa wasiwasi!

"Na ndo maana nikawaita mnisaidie...

Butu aliongea kwa sauti ya unyonge,akaweka tuo,lengo awape muda hata wa sekunde kadhaa watu wale wayatafakari maneno yake,kisha akaweka kazi yake mezani

...uzuri zaidi jioni sote tutakuwa nyumbani basi kabla ya saa tatu i mean kwanzia saa mbili na nusu muwepo kivulini pale na nguo zenu za kiraia mimi nitafika hiyo saa tatu nitachelewa kidogo kusudi mtu huyo awai kufika kabla yangu then tutamtia nguvuni sawa?!"

Maaskari wale wakakubaliana!

Saa mbili mbili na nusu maaskari wale wa tatu akiwepo inspekta Jonathan rafiki yake mkubwa na inspekta Butu,afande Paul,pamoja na Andrea waliwasili katika bar ile...

Ilikuwa ni bar tulivu,gari kadhaa ziliegeshwa katika eneo maalumu yalikuwa ni mandhari yalopendeza na kuvutia usoni mwa yeyote awewapo eneo lile...

Jona na Andrea wakatafuta siti na kuketi!

"Mambo mrembo,naweza kukupa kampani?!"

"mh karibu!"

Paul kusudi asishtukiwe akaomba aketi na binti alokuwa peke yake,kila mmoja akaagiza kinywaji stori zikaendelea!

Punde nje iliwasili gari ya kifahari aina ya Bmw lx 224 akashuka kijana mmoja alovaa suti ilo mkaa vyema akafungua mlango kisha akashuka mtu umri wa makamo,mtu huyu nyuma aliongozana

na walinzi wake wawili,wote walivaa suti nyeusi,taratibu akaanza kuufata mlango wa bar ile kabla ajaufikia meseji ikaingia katika simu ya mmoja wa walinzi wake!

"Mkuu huku ndani kuna nyigu watatu!"

Mtu yule alotumiwa meseji akamweleza bosi wake aliyeachia kicheko!

"Najua!,ila sina budi kuingia"

Mtu yule akaingia,akatafuta sehemu nzuri akaketi!

Sasa akawa akiangaza macho eneo lile la bar macho yake yalipogongana na ya yule bint aloketi na Paul wote wakatabasamu!.

Inspekta Butu aliwasili nje ya bar ile,akapaki gari yake pembeni ya Bmw ambayo akuitilia shaka kabisa,akutaka kushuka,pasina kupewa maelekezo!,akasubiri...

"Kuna mtu kaingia,ana walinzi wawili,ni mtu wa makamo"

Kabla ajaijibu ghafla simu yake ikaita

"MR X" ndiyo jina alilolisoma akapokea...

"Nishawasili karibu ndani nimekaa uku katika viti vya mwisho mwisho kabisa"

Butu akashuka katika gari yake aka angalia angalia nje ya bar ile ila hakuna alichotilia shaka akazama ndani!

Baada ya mtu yule kuketi aliongea kitu na wale walinzi wake wakatoka,bado maaskari walifatilia kila kitu.

Butu akaingia na kuelekea mpaka eneo aliloelekezwa,wakati Butu akifika pale wale walinzi walishafika nje wakaingia ndani ya Bmw na kuondoka!,

Butu alimfikia mtu wake,huku akitabasamu akamuuliza....

...Sijui ni wewe tulikuwa tukiwasiliana?!"

"Ndiyo ni mimi!,karibu uketi tuzungumze nasikia wanitafuta sana"

Kauli ile ilimdhibitishia kwamba mtu yule ndiye pale pale tabasamu lake lile la bandia likatoweka fumba na kufumbua akachomoa bastola na kumuelekezea yule mzee!,akamweka chini ya ulinzi,na hata maaskar wale wa tatu wakachomoa bastola zao na kumuelekezea mzee yule,

Mzee alibaki kutoa tabasamu!

Watu walibaki kushangaa tukio lile,

"Taratibu usijiguse naomba tutoke hapa si sehemu nzuri ya kupigia story twende eneo zuri,ulijua sitakukamata siyo?!"

Butu aliongea kwa kiburi mzee wala akuzungumza kitu wakamtoa mpaka ndani ya gari alokuja nayo Butu

Wakamwingiza

Mbele katika usukani aliketi Butu,pembeni yake akaketi Inspekta Jonathani,siti ya nyuma aliketi pembeni Paul mkononi akiwa na bastola ndogo katikati aliketi mzee yule wa makamo na pembeni yake akaketi afande Andrea naye silaha yake akiwa kamnyo oshea mzee yule!

'Hatimaye nimempata,ntamuua kifo kibaya sana ntamchuna ngozi akiwa hai mpumbavu sana huyu'

Butu akawaza,akawasha gari lengo ni kuelekea msitu tasa,palepale alipoipotezea familia yake,palepale alipo muulia Zuberi,usiku huu akapanga kwenda kumfyekelea mzee huyu!,amalize kazi yake,awe huru!

Inspekta wa jeshi la polisi John Butu bado yupo katika harakati zake za kulipiza kisasi,

Anafanikiwa kumtia nguvuni mtu aliyekuwa akihisi kuwa ndiye muuaji wa familia yake,ni baada ya mtu huyo kuhitaji kuonana naye,akisaidiana na maaskari wenzake wanamuingiza ndani ya gari na safari ya kuelekea msitu tasa inafatia,lengo ni kwenda kumuulia huko,je watafanikiwa na nini kitaendelea?!

Ulikuwa ni mwendo wa dakika 45 kutoka pale kivulini bar mpaka katikati ya pori tasa,

Hatimaye wakamshusha mzee yule chini,wakaanza kumpiga kwa kumchangia pasina huruma,mwili wote uliharibiwa uso ulichakazwa,mpaka wanamuua walishamtesa sana,saa tisa za usiku ndipo walipo maliza shughuli zote wakaingia ndani ya gari yao tayari kurejea nyumbani,mwili ule wakiwaachia wanyama wa mwituni!

Butu baada ya kufika nyumbani kwake kitu cha kwanza aliweka simu ya yule marehemu chaji,lengo aikague,kisha akaweka na yake alafu akaelekea bafuni kuoga,alipotoka akaelekea kwenye simu yake,kwa kuwa alisikia mlio wa meseji akiwa bafuni,akaifungua hiyo sms na kuanza kuisoma,kila neno alilosoma lilimfanya atoe jicho la mshangao!

Malipo ya msaliti kwetu ni kifo,baada ya kugundua huyu ndo msaliti wetu akunyetishaye siri zetu tumeamua kumuhukumu kwa kukutumia wewe mwenyewe,well done mkuu kaz njema...

Kucheki namba ni zile zile 0759427653

Ina maana yule walo mwangamiza ndani ya dk 45 nyuma siyo 'Mr x?!' ni nani sasa?!,

Palepale akazikumbuka namba '15551' mmiliki wa namba hizi ndiye alikuwa mnyetishaji wake pekee,ndiye aliyempa siri ya madawa yale ya kulevya,na hata walipowakamata pia akampa siri kuwa wanafukuziwa nyuma na mbele kuna tipa la mchanga,baada ya hapo akupata kuiona tena sms yake,ina maana ndo huyu amekuja kumuua tena kikatili namna ile?!,hapana mtu yule akustahili kufa,kwa nini lakini akubali kubeba jukumu lile la kujifanya 'Mr x'?,haraka Butu akaifata simu ya marehemu na kuiwasha,kwani iliisha chaji kabisa,ilipowaka tu ikasoma 'secrety line' ikiwa ndo jina la mtandao, alipokagua upande wa namba zilizokwepo katika simu ile alikuta namba yake tu!,kwa mantiki hiyo line ile ilikuwa ni kwa ajili yake tu au,hapana akakataa bila shaka namba nyingine zilifutwa,haraka akajipigia kuhakikisha namba zile ni kweli zilikuwa ni zilezile '15551' sasa Butu alielekea kuchanganyikiwa kuna siri kubwa sana ilijificha hapo kati na ilikuwa lazima aitambue,kwanza ilikuwa lazima amjue mtu yule familia yake,kazi alokuwa akifanya na hata marafiki zake,palepale akapata wazo,saa kumi ile ile akaingia ndani ya gari lake tayari kurudi kule msituni lengo akauchukue ule mwili autangaze ndugu zake wapatikane,upelelezi wake ndo auanzie hapo!...

Kwa kuwa njiani hapakuwa na magari alfajiri ile alifika katika msitu ule ila alishtuka kutoukuta ule mwili!,akutaka kujidanganya kwamba utakuwa ushaliwa na wanyama mpaka kumalizika lazima kungekuwa na mabaki ya nyama,mifupa ila hapakuwa na kitu kama icho,hata alipotazama vizuri chini akuona mburuzo ambao ungemfanya aamini kuwa mtu yule kabebwa na wanyama,hali ile ikazidi kumchanganya,akarejea ndani ya gari lake na kuliondoa taratibu,alielekea moja kwa moja kazini kwani kulishapambazuka kabisa.

Usiku ule akulala kabisa.

Alipofika kitu cha kwanza aliwaita rafiki zake wale wa tatu na kuwaelezea kila kitu alichogundua,wote walichoka...

"Afande ningeona uachane na wazo la kulipiza kisasi,muachie Mungu pekee aifanye kazi yake tutaendelea kuua viumbe visivyo na hatia mpaka lini?!"

Inspeka Jona akamshauri rafiki yake,

Butu hakuwa tayari kwa hilo,alishakula kiapo mbele ya makaburi ya familia yake kumuua yule alosababisha kuipoteza familia yake kivipi amuache mtu huyo aendelee kudunda?!

"Jona mbona unakuwa wa kwanza kukata tamaa na kunshauri nimwachie Mungu awahukumu,jua fika hapa pia mimi nakusaidia..."

"Ishia hapo hapo Inspekta,tena unyamaze kabisa usiseme kitu,we unanisaidia au unafanya kazi kwangu iendelee kuwa ngumu kila unapo ua upati hata muda wa kufikiria yule wa kwanza mwandishi namba zake ziliakiwa uka ua,huyu naye umeua,je tungemfikisha kwenye vyombo vya sheria?,si ndo ungekuwa mwanzo mzuri wa kumjua adui wa familia yako..."

Jona akaja juu tena akiongea kwa hasira,

"Andrea mbona unaonekana una mawazo sana?!"

Butu Wala hata akuangaika kumjibu Jona akampachika swali askari mmoja aliyeonekana kweli na mawazo!,

"Mi nachojaribu kuwaza hapa na kujiuliza,kama mtu yule alikuwa upande wako kwa nini alikubali kujitoa sadaka? tulimtesa sana,tukampigasi angetuonesha ishara yeyote kwa nini akubali kufa kama 'Mr x'?"

"ilo nalo neno!"

afande Paul naye akadakia

"Na ndo maana nikawashirikisha nyinyi makusudi kwa kugundua mwenyewe sitoweza kuucheza huu mchezo bila msaada wenu...."

Ghafla mlango ukagongwa na askar mmoja akaingia wote wakakaa kimya kumsikiliza...

"Afande Butu unaitwa juu kwa mkuu!"

Wote wa nne wakashtuka,askari yule mleta taharifa akaondoka zake!

"Tukaendelee na kazi,mi ngoja nikamsikilize mkuu"

Wote wakatoka,Butu akaelekea upande zilipo ofisi ya kamishna akaingia,alimkuta mkuu wake akiwa bize na ma faili,alipo muona akaacha lile zoezi alilokuwa akifanya,akafungua droo lake na kutoa bahasha akamkabidhi!

"Hii ya nini tena mkuu?!"

"Barua ipo mkononi mwako soma kilichomo ndani utajua"

Kamishna Nurdin aliongea kimkato macho yake akayarudisha chini,kwenye makalabrasha yaliyopo mezani!

'Nafanya hivi kukusaidia yapaswa ukakae nje kidogo ya jiji hili ukae sawa,'

Nurdin aliwaza wakati huo macho yake yalikuwa katika mafaili,hakuweza kuona mabadiliko alokuwa nayo usoni,Butu alikunja mdomo mishipa ya kichwa ikatuna,

"Mkuu kuliko kuama huu mkoa afadhali niache kazi,sipo tayari kwa huu uamisho.."

"lakini kumbuka uamisho huu umetoka kwa IGP"

"Aijalishi ila sito ondoka ndani ya jiji hili mtanisamehe mkuu"

Palepale Butu akatoka na kuelekea ofisini kwake alipoandika barua ya kuomba kuacha kazi!....

Baada ya kuikamilisha akarejea nayo ofisini kwa mkuu wake na kumkabidhi...

Inspekta wa jeshi la polisi John Butu anapokea barua ya kuamishwa kazi,jambo hilo anapingana nalo na kuamua kuandika barua ya kuacha kazi kabisa je unadhani nini kitaendelea?!

USIIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUTUMIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK, LIKE UKURASA HUU USIPITWE NA SIMULIZI NA MENGINE HUKO FACEBOOK

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE TAZAMA VIDEO HII KAMA MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA

KWA TELEGRAMπŸ‘‡BONYEZA HAPA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni