ROHO MKONONI (8) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Alhamisi, 7 Julai 2022

ROHO MKONONI (8)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Zuberi Maruma

SEHEMU YA NANE
ILIPOISHIA...
...watu wale wakafunguliwa vitamba usoni mwao,hawakuamini!,ni kweli mbele wali iyona nyumba yao,

"Mama tumewa achia huru atujawatesa wala kuwa ekea alama yoyote,usiripoti polisi kwa chochote juu ya utekaji huu na wala msiende polisi kuripoti chochote kama mnapenda kuendelea kuishi! Sawa?!"

KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media BASI INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI
πŸ‘‰GUSA HAPAπŸ‘ˆ

SASA ENDELEA...
Dereva akamta adharisha mama,alotingisha kichwa kukubali!

"Mkienda kinyume na ichi tulichowaomba tutawachukua na Safari hii amtaishi Kama mlivyoishi hapo awali nadhani mmenielewa"

"Sawa baba tumekuelewa atutaripoti chochote"

Mama yule akajibu kwa unyenyekevu

Dereva akampa ishara kijana mmoja akafungua mlango mama na wanaye wakashuka na gari ile ikaondoka,wali isindikiza kwa macho mpaka ilipoishia ndipo walipopiga hatua kuifata nyumba yao!.

Pamoja na yote wakati ile gari inaondoka mama yule alifanikiwa kuzikaririsha namba za gari lile.

Furaha sasa ilitanda ndani ya mioyo yao,wakalifikia geti na kubonyeza kengele wakasubiri wafunguliwe,geti lilionekana kufungwa kwa ndani!.

Ni katika mazingira ya kutatanisha familia moja ilitekwa,mama na wanaye wawili,wa kike na mdogo wake wa kiume,walikaa kwa muda wa siku tatu wakaachiwa tena wakapelekwa mpaka kwao,wakafunguliwa vitambaa usoni kabla ya kushuka dereva alimuonya mama yule kutoripoti chochote polisi,mama yule alikubali,ila alikaririsha namba za gari lile,je ni watu gani wale,kwa nini walitekwa na walitekwa na watu gani?! Tusonge

Walisubiri kwa muda punde hatua za mtu akikimbia kwa ndani zikasikika,

Na ghafla ikasikika kuguswa kwa geti kama kufunguliwa kwa komeo lililopo ndani,geti likafunguliwa.

"Heeee mamaa!"

Akatoka binti mrembo akamkumbatia yule mama kwa furaha!.

"Salima mwanangu nilishakwambia kabla ujafungua geti uwe una uliza kwanza ni nani?!,we unakimbilia kufungua geti je angekuwa mtu mbaya?"

Mama alianza kuteremsha lawama baada ya kumwachia m

yule binti alotoka ndani ya ile nyumba sasa wakawa wakiingia ndani

"Sawa mama nimesikia,mlienda wapi nawapigia ampatikani mjini ikawa mjini kweli!"

Wakati wakiingia ndani yule binti akaendeleza stori

"Yani we acha,kwanza baba yako yupo?!"

Mama akajibu sambamba na kumpachika swali binti yule.

"Hayupo! toka ile siku mlo ondoka ajarudi nikajua mko wote! "

"Eti?!, Unasema?!"

Mama yule akahoji kwa mshangao pasina kuamini kile alichokisikia.

"Baba ajarudi toka juzi mama,na watu wengi wamekuja kumuulizia wengine wakiwa wafanyakazi wenzake"

"Jamani mume wangu atakuwa salama kweli?!"

Mama aliuliza huku machozi yakimmwagika,walifika sebuleni mama akatangulia kuweka simu yake chaji,ilishazima toka ile ile siku ya kwanza walipotekwa.

"Ukwenda polisi kutoa taharifa juu ya upoteaji wetu?!"

Mama akazidi kumdadisi yule binti...

"Sikwenda mama,mi nilijua mtarudi!"

"Hapana Salima,hali kama hii siku nyingine ikitokea katoe taarifa kituo cha polisi kikawaida atuwezi kusafiri bila kukuaga,ungekaa utusubiri mpaka lini tungekufa je?!"

"Kwani ni nini kilichotokea mama?!"

Ikabidi sasa yule mama aanze kumsimulia mfanyakazi wake kilichowapata!...

"Siku ile nilipokea sms kutoka kwa mume wangu,sms hiyo ilisema kuna gari itakuja kutuchukua hivyo nijiandae basi nikamwambia Martha na Bray wajiandae kweli gari iliwasili tukatoka na kuingia,ile tumeshakaa vioo vikapandishwa palepale tukawekewa silaha tukafungwa macho atukujua tulipopelekwa,tulikuja kuambiwa tushuke tukapelekwa tulipofunguliwa vitamba tulikuwa ndani ya chumba,ndipo tulipokaa uko,chakula tuliletewa huko huko,kila kitu tulifanyia humo humo"

"Mh! Poleni kumbe mlitekwa mama?!"

"Ndio na nahisi pengine watu wale walihitaji ela kwa mume wangu ,ila kitendo cha kunambia naye toka juzi ajaja kinanitia shaka sana"

"Baba atakuwa kwenye matatizo mama lazima ukaripoti polisi!"

Brayson mtoto wa wakiume wa yule mama akashauri,kabla dada yake ajadakia

"Hapana mama!,unakumbuka yule dereva alivyosema?!,ukienda polisi watatuua"

Sasa kila mtu akawa akisema lake kwa kuwa simu ilishapata chaji kidogo mama akaifata na kutafuta namba za mumewe akazipiga!,lakini azikupatikana.

Kwao huu ukawa mtihani mwingine, maskini mama akujua kama kwa sasa yeye ni mjane mumewe alishakufa tena kwa kupitia mikono ya aliyekuwa inspekta wa jeshi la polisi John Butu

Ni baada ya kumuhisi mtu yule kwamba ndo 'MR X' ilikuwa hivi!....

SURA YA NNE
UPANDE WA PILI WA SHILINGI: IKULU
Kilifanyika kikao cha siri katika chumba kimoja cha mikutano ndani ya Ikulu ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ndani walikwepo watu wa tatu,walionekana kuzama katika maongezi yao yalokuwa nyeti

"Mheshimiwa mtukufu Raisi nimemgundua msaliti atoaye siri zetu ni mr Silvester huyu ndiye alimpigia simu afisa wa polisi kwa kutumia namba za siri 15551 na kumjulisha juu ya ule mzigo wetu na pia akamjulisha juu ya mbinu za uokoaji tulizopanga kuzitumia..."

"Saadash Zidu kazi nzuri na nijijua ndani ya masaa 6 utakijua kirusi kilichopo katikati yetu,msaliti wetu utamjua,chakufanya ahukumiwe kifo mara moja!"

Mheshimiwa Raisi akajibu kwa furaha kwani alishajiuliza sana ni nani aliyekuwa na udhubutu wa kuunguza ishu yake polisi mpaka kukamatwa kwa vijana wake na alijua lazima atakuwa mtu wake wa karibu na sasa alishamjua.

"Na si mimi nitakaye muhukumu lah!"

Akashtushwa na kauli ya kijana wake yule alomuamini zaidi ya kitu chochote!

"Bali?!"

Waziri mkuu naye akahoji,Zidu akacheka kabla ajajibu swali lile

"Huyo huyu ampaye habari zetu ndiyo atakayemwangamiza tena kikatili sana"

"Kivipi sasa?!"

Kwa shahuku Raisi Bisau akahoji Zidu akaachia tabasamu tena ,

"Nahitaji niwaoneshe kwa vitendo!"

Alijibu huku akiwa katika tabasamu jepesi,akashika simu yake na kupiga namba kadhaa,akaweka sikioni akasubiri kwa sekunde kadhaa simu ikapokelewa...

"Mzee tunakikao cha siri na muheshimiwa Rais,pamoja na waziri mkuu ivyo tunakuomba nawe ufike hapa katika chimbo langu huku matumbi"

Kumbe kijana yule alikuwa akiongea na Raisi Patrtick Bisau pamoja na waziri mkuu Benson Sai,Zidu alikuwa ni mkuu wa usalama wa taifa ndo mmiliki wa ile namba 0759427653 aliyo iunganisha toka kwenye simu ya Kijana alotambulika kwa jina la Zuberi,na mzigo ule ulikuwa ni wa Raisi pamoja na waziri mkuu wake,ila uliratibiwa na Zidu mwenyewe,Silvestar yeye alikuwa mfanyakazi ofisi ya Raisi akupendezwa na kazi ile kwa siri sana akatafuta namba za siri na kumjulisha inspekta Butu kabla ya kugunduliwa!

Baada ya kumaliza kuongea na mtu yule sasa Zidu akawaomba wakuu wale wa nchi waelekee kwake wakamsubiri huyo kijana

Pasina msafara watatu wale wakaingia ndani ya gari Zidu akiwa dereva Safari ya kuelekea Tabata Matumbi ikafatia.

Dakika kumi tu waliwasili wakawa aKimsubiri Silvester tena kwa hamu kubwa sana.

Pasina kujua alichoitiwa Mr Silvester aliwasili katika jumba ilo la siri la Zidu,akatoa heshima kwa viongozi wale wa nchi akaambiwa aketi!,bila wasiwasi akaketi,Zidu akamuomba simu yake Sili pasina kujua akampa,

"Namba za mke wako umezisevuje huku?!"

Zidu akahoji kishari sasa sura ilibadilika,Sili akajua hapa si salama tena!

"Kuna nini wakuu?!"

Silvestar akahoji kwa wasiwasi!

"Utajua,wewe si msaliti sasa dawa yako ndogo,sema namba ya mkeo umesevuje humu?!"

"Wi..fe" Mzee wa watu akajibu kwa woga huku akishindwa kujizuia kutetemeka!.

"ha ha ha eti wife,sawa hii hapa!..nimeiona"

Zidu akatuma meseji aloijua yeye,kisha akaifuta na kumrejeshea mwenyewe simu yake,muda ule ule akatoa simu yake na kuwapigia watu wake...

"alooh,Isack naomba muelekee nyumbani kwa Silvestar mke wake na watoto watatoka muwapandishe kwenye gari muwafunge macho wasijue mnapowaleta muwalete huku matumbi katika nyumba yangu ya siri sawa?"

Upande wa pili ukaitikia sawa,kweli baada ya kama nusu saa gari ile iliwasili,wakiwa katika chumba kingine kupitia dirishani Silvestar aliona familia yake ikishushwa na kuingizwa katika chumba kingine!

"Ili kuikomboa familia yako lazima wewe ujifanye mimi!,mimi nitawasiliana na huyo mpumbavu wako na kuhitaji kuonana naye then wewe utaenda kama mimi,utapokea malipo yako ya usaliti kwetu ndipo tutaiachia familia yako ukienda kinyume na hichi wewe na familia yako yote tutaiteketeza katika visima vya mamba,hata mifupa yenu aitoonekana"

Hapo ndipo Mh Rais na waziri mkuu wake waliuelewa ukatili wa Zidu k,hapo ndipo walipo muelewa vizur zaidi,palepale Zidu akatoa simu na kumpigia Butu akahitaji aonane naye kivulini bar usiku wa siku hiyo,

Akawaita vijana wake kadhaa na kuwapa kazi wampeleke hapo bar usiku,na ndivyo ilivyokuwa Sili aliamua kufa kuitetea familia yake,usiku aliingizwa garini mpaka Kivulini walipofika dereva akampigia simu Zidu kumtaharifu kuwa amefika,Zidu akaomba wawili wamsindikize mpaka atakapoketi ndipo waondoke,ikawa ivyo,Silvestar akakamatwa Butu akimjua ndiye mr x wake! na kwenda kumwangamiza kikatili pasina kujua.

Sasa ndo wakaiachia familia yake.

Walipofika nyumbani wakakuta hali ya sintofahamu kutoka kwa binti wa kazi Salima.

Zidu anafanikiwa kumgundua mheshimiwa Silvestar kuwa ndiye aliyempa taharifa afisa wa jeshi la polisi John Butu na kumwezesha kukamatwa kwa unga wa madawa ya kulevya,haraka kikao kinafanyika ikulu na mwisho muheshimiwa Raisi Bisau anatoa amri Silivestar kuuwawa,Zidu anahaidi kumtumia huyo huyo Butu kufanya kazi hiyo na ili linatendeka baada ya kuiteka familia yake na kumwambia ili aiachie huru lazima akajikamatishe kwa Butu kama yeye Silivestar anakubali ili kuikomboa familia yake,je nini kitaendelea?! Tusonge katika hatua inayofuata:


Usiku ule hakukuwa na aliye kuwa na hamu ya kwenda kulala,mpaka inatimia saa nane wote walikuwa macho,sebuleni pale wakijadili kipi cha kufanya,japo waliwasha tv ila hakukuwa na aliyefatilia kilichokuwa kikiendelea katika runinga ile,woga uliwatawala!

Bi Glory kwa vyovyote vile alijua lazima mumewe atakuwa kwenye hatari,kama si kupoteza maisha.

Bray alimsisitizia mama yake pakipambazuka aende kituoni,akaripoti,tena kituo kikuu cha polisi,japo Martha alimpinga mdogo wake akisisitiza onyo walopewa na yule dereva,ila bi Glory akakata shauri itakavyokuwa na iwe,atawezaje kukaa kimya bila kwenda kuripoti kupotea kwa mume wake?,na alijua fika akienda polisi pia ni lazima aeleze ukweli,kwamba nao pia walitekwa...

Akazima tv na kuwataka watoto wake wakalale,naye akaelekea chumbani kwake kulala

Kwa kuwa walichelewa kulala pia walichelewa kuamka,Bi Glory kabla ajafanya chochote akachukua simu yake na kumpigia shemeji yake,yani mdogo wake na mume wake,ndo ndugu pekee alokuwa amebakia kwa upande wa mume wake,akamuomba afike nyumbani,kwa kuwa hakuishi mbali kweli alifika akamuelezea,shemeji yake alotambulika kwa jina la Michael alimpa pole sana shem wake!,akamtoa khofu na kumwambia lazima waende kituo cha polisi...

USIIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUTUMIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK, LIKE UKURASA HUU USIPITWE NA SIMULIZI NA MENGINE HUKO FACEBOOK

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE TAZAMA VIDEO HII KAMA MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA

KWA TELEGRAMπŸ‘‡BONYEZA HAPA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni