ROHO MKONONI (9) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Ijumaa, 8 Julai 2022

ROHO MKONONI (9)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
πŸ“– KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
πŸ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
πŸ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Zuberi Maruma

SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA...
Kwa kuwa walichelewa kulala pia walichelewa kuamka,Bi Glory kabla ajafanya chochote akachukua simu yake na kumpigia shemeji yake,yani mdogo wake na mume wake,ndo ndugu pekee alokuwa amebakia kwa upande wa mume wake,akamuomba afike nyumbani,kwa kuwa hakuishi mbali kweli alifika akamuelezea,shemeji yake alotambulika kwa jina la Michael alimpa pole sana shem wake!,akamtoa khofu na kumwambia lazima waende kituo cha polisi...

KABLA HATUJAENDELEA NIOMBE KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media BASI INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI
πŸ‘‰GUSA HAPAπŸ‘ˆ

SASA ENDELEA...
Asubuh ile ile safari ya kuelekea kituoni ikafatia.
***

KITUO KIKUU CHA POLISI
Kamishna Nurdini alikuwa kakaa ndani ya ofisi yake kakasirika,kila dakika aliguna,mdomo aliukunja,si muda mrefu alikuwa ametoka kumgombeza kijana wake Inspekta Jonathan,ni muda mrefu sasa toka amemkabidhi kesi ya afande Butu aloipoteza familia yake,ila mpaka muda ule alotoka kuongea naye kijana yule hakuweza kugundua kitu chochote juu ya kesi hiyo.

Kwa upande wa Jonathan alitoka akiwa na hasira ofisini kwa mkuu wake.

Alikumbuka wao wa nne yani yeye Butu,paul na Andrea walishamuua alosemekana ndo mmiliki wa ule mzigo,walimteka kivulini Bar usiku ule wa kampeleka katikati ya msitu na kumuua kikatili sana!

Cha ajabu baadaye Butu akaja kumwambia mtu yule siye,bali ni yule alokuwa akiwasiliana naye kwa namba 15551 na kumpa maelezo,mpaka muda ule akujua mtu yule ni kwa nini aliamua kuuvaa uhusika wa adui yao na kukubali kufa siri yake ikibaki moyoni,aliwaita wenzake Paul na Andrea ofisini kwake na kuwa ambia jinsi mkuu alivyotoka kumgombeza!

"Unadhani tutafanyaje afande na yule mtu atumjui bora tungeijua hata familia yake..."

Ni wakati wakiendelea kujadili upande wa mapokezi akiwa binti Fatma waliwasili,bi Glory na shemeji yake,walikaribishwa wakaketi Fatma aka anza kuandika maelezo yao!

"Ok! Naweza kuwasikiliza!"

"Eleza kila kitu shem usifiche kitu hapa ni usalama wa raia ivyo toa wasiwasi"

"Ni kwamba siku tatu zilizopita nilitumiwa meseji na mume wangu alinambia nijiandae mimi na wanangu kuna gari inakuja kutuchukua,nikijua ni sapraiz nika wa andaa wanangu punde nikasikia honi nje nikamuaga mfanyakazi nasi tukatoka nje tulikuta gari tukafunguliwa mlango tukaingia,ile tumeingia vioo vyote vikapandishwa juu wale watu wakatubadilikia na kutufunga usoni,sijui walitupeleka wapi,ila tulikuja funguliwa macho tukajikuta ndani ya chumba kimoja,tuliletewa chakula mule,tulikaa siku tatu mpaka jana tulipoambiwa tupo huru tukafungwa macho na kurejeshwa nyumbani ambapo watu wale walitupa onyo kuripoti polisi ila tulipofika ndani na muulza Salima habar za mume wangu akanijibu toka tuondoke naye ajarudi,tukimpigia apatikani sijui mume wangu atakuwa kapatwa na nini!..."

"Salima ndo huyo mfanyakazi wako?!"

Fatma akahoji,

"Ndiyo!"

"Watu hao walowateka walishawapiga,au kukupigeni picha au hata kuwapa simu muongee na mume wako?!"

"Hapana awajawahi!"

"Mumeo anaitwa nani?!"

"Silvestar Emanuely!"

"Anafanya kazi gani?!"

"Yupo ofisi ya Raisi ikulu pale"

"Je ulishawahi kumsikia mumeo akigombana na mtu? au unamjua adui yeyote wa mumeo unaye dhani anahusika katika utekaji wenu,au kupotea kwake?!"

"Hapana afande,"

"Ok,nahitaji picha yake,"

Bi Glory akaingiza mkono kwenye pochi yake akatoa picha ya mume wake na kumkabidhi afande yule,

Fatma alizicheki kwa muda kisha akasimama...

"Naomba mnisubiri..."

Akalinyanyua lile kalabrasha aliloliandika,akapanda nalo juu mpaka katika ofisi ya kamishna,katibu muhtas akamruhusu Fatma akagonga na kuzama ndani!

Alimkuta kamishna bado kanuna,akampa lile faili,kamishna akaanza kulisoma...

"Mh!," Nurdin akaachia mguno akishangazwa na maelezo yale,hakika maelezo yale hayakuwa ya kawaida hata chembe!...

Bi Glory ana amua kwenda polisi kushtaki kupotea kwa mume wake,pia anaelezea juu ya kutekwa kwao,yeye na watoto wake wawili Bray na Martha,walimkuta mapokezi afande wa kike alotambulika kama afande Fatma,afande yule alokuwa na cheo cha u koplo,aliandika maelezo yao kisha akaelekea na faili ofisini kwa mkuu wake Kamishna Nurdin,

Kamishna alipitia yale maelezo mwisho akaguna,je unadhani nini kiliendelea?! Twende katika hatua inayofuta...

"Hii kesi na mashaka nayo embu kwanza niitie Insp Jonathan hapa..."

"Sawa afande!"

Fatma akatoka na kuelekea ilipo ofisi ya Jonathan...

Kwa upande wa Jona baada ya kumaliza maongezi na wale marafiki zake,ambapo walikubaliana jioni wakutane kivulini bar sambamba na inspekta Butu waongelee swala ilo Jona akawaruhusu Paul na Andrea wakaendelee na kazi!

Wakati wakiwa kwenye korido ndefu wakielekea mapokezi,njiani walikutana na Fatma ambaye yeye alikuwa akielekea ofisini kwa Jona.

"Afande Jona yupo ofisini kwake?!"

Wakati wakipishana Fatma akawapachika swali ambapo wote kwa pamoja walimwitika,Fatma akazidi kukaza mwendo kuifata ofisi ya Jona!

Afande Paul na mwenzake waliwasili mapokezi walisalimiana vizuri na yule mama na wanaye,wakaachana nao,kila mtu akachukua siti yake!,walijua tayari mama yule atakuwa tayari kashasikilizwa,

Jonathan na Fatma waliwasili ndani ya ofisi ya kamishna,wakapewa ishara waketi.

"Nimeitika wito afande,"

Kamishna sasa akanyanyua kichwa chake ambacho kilikuwa bize kuendelea kusoma yale maelezo katika lile kalabrasha lililoandikwa na Fatma!,

"Nimekuita kwa maana,nataka nikukabidhi zingatio lingine japo la awali ujalikamilisha,utajua jinsi ya kufatilia na vijana wako,pitia hili faili ripoti zote za uchunguzi utaniletea mimi,kwa sasa una mafaili mawili katika mkono wako kazi ipo juu yako"

Kamishna aliongea huku akimkabidhi Jona kalabrasha lile,Jona akalipokea na kuanza kulisoma!

Baada ya kulisoma na kulielewa si ndo akachukua picha aitazame sura ya huyo mtu alopotea.

Ile anaitazama akuamini alichokiona!,

Macho ya mshangao yakamtoka,sura ile aikuwa ngeni machoni mwake,aliikumbuka fika,akajikuta mikono ikimlegea na kushindwa kuishika vizuri ile picha,

Akaiachia!..

Mshangao aloupata ulimshangaza Nurdin na hata Fatma,kwa uzoefu wao wa kipolisi walijua tu kushtuka kwa inspekta yule kuna sababu!

"Vipi inspekta mbona umeshtuka au unamjua mtu huyo?!"

"ha..ha..hapana mkuu!"

Jona akajikuta akipatwa na kigugumizi kikali,kamishna akawaruhusu, wakanyanyuka na kila mmoja akatoa heshima kwa mkuu wao,wakageuka na kuufata mlango kalabrasha lile sasa likiwa mkononi kwa Jonathan,walifika mapokezi,Jona akampa pole yule mama.

"Usijali mama hakuna lolote litakalo wapata na nikuhakikishie tutawakamata wauaji kuwa na amani mama yangu"

Jona aliongea kwa majonzi,kama vile ajui kitu,palepale akamwomba Fatma pamoja na binti mwingine kruta waelekee nyumbani kwa yule mama wakawe walinzi kwa muda,walichukua namba za ile gari,baada ya kuondoka ndipo Jona alipowapa ile picha wenzake ambao nao walishtuka vilevile,wote wakasoma kalabrasha lile na kulielewa vizuri!..

Kumbe huyu jamaa alikuwa ni mfanyakazi wa ofisi ya Raisi!,ila hawakuwa na shaka kuwa pia alikuwa ni muuzaji wa madawa ya kulevya!

Ilikuwa lazima wamjulishe inspekta Butu juu ya jambo lile haraka iwezekanavyo,hawakutaka kusubiri tena usiku kukutana Kivulini Bar.

Inspekta Jona akashika simu yake na kutafuta namba za Butu akazipiga,simu ikaita punde ikapokelewa.....
***
Butu furaha ilienda mbali na yeye,majonzi yalimtawala,alizidi kugida bia kwa uchungu,katu akujua kila anachofanya mwanaume wa kazi Zidu kite alikuwa akifatilia katika simu yake alounganisha na camera ndani ya nyumba ile!

Nje ya nyumba yake,mita kadhaa usawa wa barabara,ni muda mrefu alionekana binti mmoja kichaa pembeni ya mtaro akiwa na pochi lake chafu

Macho ya kichaa yule yalikuwa eneo la geti ilipo nyumba ya Butu!

Pia mtaa wa pili kutoka mtaa ule katika moja ya restraunt ilipaki pikipiki

ambayo ilikuwa ikimilikiwa na kijana mmoja alokuwa ndani ya gwanda za jeshi macho yake yalikuwa bize na tv ilokwepo pale.

Ni toka asbuh mjeda yule alikwepo pale.

Na siyo siku hiyo tu,

Hapana!!!....

Alishamaliza wiki alikuwa akija asubuh na kukaa pale mchana alikula pale usiku alikula pale saa tatu ndipo alipo ondoka

Butu pale sebuleni aliendelea kugida bia ghafla akapata wazo,muda ule ule mwanaume akajinyanyua na kufungua mlango,akatoka mpaka nje na kuchukua pikipiki yake,akaiwasha alipofikia getini akashuka akafungua geti na kutoka,ile katoka tu,yule kichaa akaingia ndani ya mtaro akawasiliana na yule mwanajeshi ambaye mara kibao kwa siri sana alikuwa akimfatilia Butu.

Baada ya mjeda yule kutaharifiwa alitoa simu yake na kumpigia Zidu.

"Mtu wetu katoka bad garl kanambia sijui anaelekea wapi ila ndo namfatilia"

"Nami nakuja akikaa position nzur mwangamize tu amri ishatoka"

Zidu kule nyumbani alinyanyuka naye akapakia tukutuku lake akatoka,silaha kibindoni!,alizidi kuwasiliana na yule mjeda kupitia vinasa sauti kutoka kwenye simu 'earfone' zilizopo masikioni mwake!

Butu alizidi kukanyaga mafuta pasina kuwa na shaka na mwanajeshi alokuwa akimfata nyuma akiwa juu ya pikipiki,

Mwanajeshi yule hakuwa mwingine zaidi ya Isack

"Ukifika usawa wake hakikisha kwa siri sana unammiminia risasi na kutoweka fastar hakikisha uachi ushahidi utakaowezesha kukamatwa kwako!"

Zidu akampa taharifa Isack ambapo alizidisha kasi ya pikipiki yake mpaka akamfikia butu akamuovar take sasa wakawa katika usawa,Isack sasa akaachia mkono mmoja na kuupeleka kibindoni akaanza kuhesabu moja.. mbili..tat..

Akiwa na nia akikamilishe 'u' achomoe pistol na kumaliza kazi palepale!....

*HATARI: KIZAAZAA....
Aliyekuwa Inspekta wa Jeshi la polisi John Butu anafatiliwa kwa kila hatua pasina yeye mwenyewe kujua kama anafatiliwa,nyumba yake yote inategeshwa kamera za ulinzi,mambo ayaishi hapo hapana!,nje ya nyumba yake kandokando ya barabara anaonekana binti kichaa,

Na pia mtaa wa pili katika Restraunt moja anaweka makazi mjeda mmoja akiwa na kazi moja tu!....

Kumfatilia Butu kwa kila hatua....

Wakati huo Butu ana gida bia za kutosha ghafla anapata wazo,pale pale anainuka na kutoka,

Binti kichaa anamtaharifu kijana Isack akae sawa Butu anakuja usawa wake palepale Isack anamtaharifu Zidu anaye mwambia amtwange risasi naye atoweke ahakikishe aachi ushahidi,naye Zidu anakwea pikipiki kwenda eneo aliloambiwa!

Ile anataka kuichomoa bastola ghafla akasita baada ya kuona kamera katika jengo moja kubwa kando ya barabara..

"Usalama aupo vizuri watu ni wengi na magari pia ni mengi si vizuri kulianzisha nitalipaka matope jeshi letu!"

"Ina maana upo ndani ya Gwanda?!"

Zidu akamohoji

"Ndio kamanda"

Isack akajibu kwa majonzi

"ooh! Shit,usifanye chochote but endelea kuifatilia ujue inaelekea wapi"

"Sawa mkuu"

Kwa kuwa Isack alishaipita pikipiki ya Butu ikamlazimu apunguze mwendo,Butu akampita

Isack akaanza kumfata nyuma nyuma kwa siri sana ili hata asitiliwe mashaka!
***
Baada ya Butu kutoka tu kichaa yule wa kike alimsindikiza kwa macho baada ya kupotelea mtaa wa pili,akawasiliana na Isack,kisha akanyanyuka,akabeba pochi lake moja chafu na kuelekea kunapo geti,tena alificha uso wake kwa mikono kusudi kamera za pale getini zisinase sura yake.

USIIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
KWA KUTUMIA AKAUNTI YAKO YA FACEBOOK, LIKE UKURASA HUU USIPITWE NA SIMULIZI NA MENGINE HUKO FACEBOOK

KWA KUWA NAKUPA SIMULIZI BURE TAZAMA VIDEO HII KAMA MALIPO YAKO KWA KAZI NINAYOIFANYA

KWA TELEGRAMπŸ‘‡BONYEZA HAPA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni