FUPI TAMU (14) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Alhamisi, 16 Februari 2023

FUPI TAMU (14)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
📖 KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
😂 VIDEO za KUCHEKESHA
📑 MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

Jina: FUPI TAMU
Mwandishi: Edgar Mbogo

SEHEMU YA KUMI NA NNE
ILIPOISHIA...
“karibu mzee Ponera, naona hupo na katekister (mwalimu wadini, wa kikatoliki)” alikaribisha baba Eva, “asante sana, kumbe bado unanikumbuka” alisema huyo mzee ponera, huku wana karibia kwenye makochi, japo atukujuwa wanafwata nini lakini nilimwona kaka akiaza kuhema juu juu kwa hofu, japo mwonekanano wa bamdogo, ulikuwa ni wa tofauti na alivyo kuwa mala yamwisho kuja hapa nyumbani kwa kina Eva, “nitakusaauje mshenga tena, alafu ile ndiyo ilikuwa mala yangu ya kwanza kusimama badala ya wazazi”

WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI

SASA ENDELEA...
Alisema baba Eva huku wote wakicheka, na kaka nikamwona akijilazimisha kucheka kidogo, kamwenzie lakini baba mdogo yeye akuweza kabisa kucheka, aliishia kutabasamu.

Naam wakati wakina baba Eva na kaka Denis, wakiwa wanaendelea kusalimia na wageni, mama Eva akatokea upande wajikoni, “hooo jamani kumbe kuna wageni?” alisema mama Eva, na kusimama kisha na kuwasalimia, ila nilimwona akishtuka na kushangaa baada ya kumwona bamdogo, unajuwa leo bamdogo alionekana kuwa rafu sana, ukiachilia suruali yake iliyo pishana na maji kwa muda mrefu, pata picha pale suruali nyeusi inapoonyesha kuwa ni chafu, pia shati alilovaa alikuwa na hadhi ya mtu alie toka nyumbani kwake, ungesema alikuwa anatoka safari ya mbali, ambayo imemchukuwa sikukadhaa, bila kumpa nafasi ya kujifanyia usafi binafsi, “karibu sana shemeji” alisema mama Eva, huku anamtazama bamdogo, kwa macho flani ya mshangao, “asante sana shemeji” alisema ma bamdogo Jems, huku akishindwa kumtazama mama Eva usoni.

Naam baada ya kumaliza kusalimia na wageni wale, mama Eva alielekea chumbani kwa mamdogo, ambako alipotelea huko kwa dakika kadhaa, huku sebuleni niliwaona wazee awa wakiwa wanaongea ili nalile, kama sehemu ya salamu na kukumbushana siku zilizopita, mpaka mshenga alipoamua kulianzisha swala lililo waleta pale, “samahani mzee mwenzangu, nimeona nianze kusema kilicho tuleta mahali hapa” alisema yule mzee Ponera, akimtazama baba Eva, na wakati huo mama Eva pia alikuwa anatoka chumbani, na kukaa pale sebuleni,

“ok! aina shida, unaweza kuongea” alisema baba Eva na hapo kaka akataka kuinuka, ili awapishe waongee yakwao, “hapana Denis, usitoke, we kaa tu!” alisema baba Eva, na kaka akatulia kwenye kochi, “kwa mujibu wa kijana wetu Jems, ni kwamba, mke wake aliondoka miezi, mingi iliyo pita, sasa amekaa na anaona unakaribia mwaka, mke wake arudi, hivyo ameona bola aje amchukue mke wake, na kama kulikuwa natatizo, basi wayamalize, ili waanze maisha mapya” alisema Ponera, na kisha kutulia kidogo, hapo baba Eva na mama Eva wakatazamana, kidogo, kabla awaja mtazama kaka, ambae alikuwa ametulia kimya kamavile jambo lile kwake nigeni na alimuhusu,

“mh! hapo kidogo bwana ponera sijakuelewa, nikwamba bwana Jems anasema mke wake aliondoka bila yeye kujuwa sababu, au ipi?” aliuliza baba Eva akimtazama mshenga bwana Ponera, ambae alimtazama Jems mwenyewe, kwamba ajibu swali lile, nae akajuwa anatakiwa kujibu, “chanzo cha kuondoka kwake kiukweli ni kwamba tulikwalizana kidogo tu!, siku ya pili akaondoka zake” alisema bwana Jems ambae ni baba yake mdogo Eva, “lakini shemeji si mlisha pelekana mahakani na mkagawana vitu, bado unasema mkeo aliondoka na sasa unataka mje kurudiana?” aliuliza mama Eva kwa sauti ya kusuta, huku akimkazia macho baba yake mdogo Eva, yani huyo James yule alie taka kungopnga Eva na gari,

“lakini shemeji kukosana kwa wanandoa, nikawaida kuachana na kupata ni kawaida, mi naomba tukae tuyazungumze, maana nimegundua kuwa mke wangu Irene, ni mwanamke mwenye mapenzi yakweli kuliko wanawake wote niliowai kuwanao” alisema Jems kwa sauti ya kubembeleza, na kukili madhaifu, “lakini bwana Jems ulikuwa na sababu ya kuja kufanya vurugu nyumbani kwangu, ata baada ya kuachana na Irine, ukafikia ahatua ya kutaka kumgonga binti yangu na gari?” alisema baba Eva, na hapo tukamwona James akiinamisha kichwa chini, akishindwa kujibu swali lile, mpaka katekista alipo msaidia, “ndio maana tumekuja kuomba msamaha, ili awa walio unganishwa na mungu, waendelee kuwa kitu kimoja” ilikuwa ni sauti moja tulivu iliyojaa busara,

“ok! sisi atuwezi kuamua lolote, japo sidhani kama inawezekana” alisema baba Eva, kisha akamtazama Eva alie kuwa anacheza na mimi, “Eva nenda kamwite mamdogo, chumbani kwake” alisema baba, na hapo Eva akachomoka mbio kuelekea chumbani kwa mamdogo, ambako akukaa sana alirudi na kuleta ujumbe, “anakuja” kisha akajiunga na mimi kuendelea kuchezaz, japo atukuwa makini na mchezo, zaidi ya kufwatilia maongezi yale ya watu wakubwa, dakika mbili baadae nikamwona mamdogo anaibuka kwenye kolido la yumbani, akiwa ame mbeba mtoto mkononi,

hapo nika mtazama ba mdogo Jems, ambae alikuwa ametoa macho kwa mshangao, nazani akuamini kama mama mdogo ana mtoto, akama anavyo shuhudia, mamdogo akaja moja kwa moja na kumkabidhi kaka, kisha yeye akaanza kusalimia wageni, huku bado ba mdogo wake Eva ana kodoa macho, akiwatazama kwa zamu mamdogo na kaka alie shika mtoto, hakika akuna ambae akuona mshangao wa bamdogo Jems mle ndani.

Mamdogo Irene yani shemeji yangu, aliendelea kusalimia wageni, mpaka alipomfikia bamdogo, ambae aliitikia kama vile amshikwa na butwaa, pale nazani ali bamdogo alikuwa anashangaa vitu viwili, kwanza uziri na unawili wa mamdogo, ambae licha ya kutoka kwenye uzazi lakini alikuwa amependeza na kuzidi kuwa mzuri, huku umbo lake likiwa lime zidi kuvimba asa sehemu za makalio, na kifua, pili bamdogo alikuwa anashangaa kuhusu mtoto aliekuwa amekuja nae mamdogo, na kile kitendo cha kumkabidhi kaka.

Mdogo alipomaliza kusalimia akaenda kukaa karibu na kaka, hapo mshenga aka ambae nikama alikuwa ameshikwa na mshangao, aka mtazama baba Eva, ambae pia alikuwa anamtazama, mshenga, “mzee Ponera, nazani sasa unaweza kuendelea maana mhusika amesha kuja” alisema baba Eva, hapo mzee Ponera akajikooza kidogo, kishaaka mtazama Irene kwa macho ya kukata tamaha, “Irene tumekuja hapa kwaajili yako, mumeo amekuja kuomba msamaha, ili mrudiane mkaendeleze maisha yenu, kama mlivyo kuwa mwanzo” alisema mzee Ponera, na hapo mamdogo akamtazama kaka, kisha akamtazama Jems, alafu akamtazama mzee Ponera,

“kwanza kabisa samahanini sana, nitaomba niwatambulishe mume wangu mtarajiwa, maana aitakuwa vyema kama nitaanza kuongea kabla yeye sija mjulisha lolote, japo nilisha mdokeza mwanzo” alisema mamdogo, na hapo nikamwona bamdogo Jems ana inuka toka pale alipokaa, “Irene aiwezekani unifanyie hivyo, wewe ni mke wangu dini ailuhusu, wewe kuolewa tena” alisema bamdogo Jems, na haraka sana, mzee Ponera akamzuwia, “itashindikana vipi na wewe ulinikataa na kuni fukuza nyumbani?” aliuliza Irene, huku anamkazia macho bamdogo Jems, “lakini Irene kumbuka sikuile nilikuwa nimelewa, nimala ngapi yalitokea mambo kama yale na tuka ya zungumza?” aliuliza bamdogo, huku watu wengine wakiwa kimya wakiwasikiliza wawili awa,

“sawa ilikuwa pombe, na kitendo cha kuamua kuishi na manamke mwingine nacho kilikuwa pombe?” hapo bamdogo akakaa kimya akitazama chini, “nakuuliza Jems, ukaamua kuleta hapa nyumbani kwa dada yangu, kunionyeshea, kuwa umempata mwanamke mwenye kizazi, nayo ilikuwa pombe, inamaana pombe ilikaa kichwani miezi yote hii?” aliuliza mamdogo, lakini bamdogo akusema kitu, “aya sasa leo umekuja kufanya nini, inamana pombe imeisha?” aliuliza mamdogo, na safari hii bamdogo aliinua kichwa, huku machozi yakionekana machoni pake, “mke wangu, nishetani tu alinipitiaukweli yaliyonikuta nimejifunza mengi sana” alisema bamdogo, kwa sauti ya kuuzunika na kujutia,

“lakini aitasaidia kitu Jems mimi tayari, nina mchumba na tumesha pata mtoto mmoja” alisema mamdogo, na hapo nikamwona bamdogo, akizidi kutokwa na machozi, “Irene, kumbuka ndoa yetu ni yakanisani, nipo tayari kulea mtoto wako kama mwanangu, naomba turudiane” safari hii sauti ya bamdogo, ilitoka sambamba na kilio cha chinichini, “ingekuwa lahisi, kama maneno ayo ungeyaongea siku ile, ambayo ulikuja na yule mwana mke, lakini kwa sasa, aito wezekana” alisema mamdogo Irene, na hapo Katekista akaingilia kati, “Irene, ndoa uwa ni moja tu!, hivyo nivyema kama ukimsikiliza mwenzio kisha mkaelewana, ukweli kuna makubwa yame mkuta naimani imekuwa funzo kwake” hapo ikashauriwa kuwa Jems apewe nafasi ya kusikilizwa.

Nae akatulia na kufuta machozi, kisha akaanza kuelezea, “ukweli jamani kama ilivyo kuwa kwa mwanaume au mwanamke aliepo kwenye ndoa, anachotaraja ni watoto, kitendo cha mke wangu kuto kushika mimba kiliniumiza sana, na kuanza kumsimanga na kumpiga wakati mwingine, huku nikitoka nje ya ndoa kujaribu kutafuta mtoto, japo mke wangu alikuwa anaangaika mahospitalini na kwnye tiba hasiria, kuona anawezaje kutatua tatizo ili.

Ukweli nilikosa uvumilivu, nikajikuta na mfukuza mke wangu, ambae alinivumilia kwa mengi, maana alisha nifumania mala kadhaa, lakini tuliyaongea na yakaisha, ila mimi nika shindwa kumvumilia kwa tatizo la kutokushika mimba, ndipo nilipo nasa kwa yule mwanamke mwenye watoto wawili, nikiamini kuwa atanizalia mtoto, iliniepuke masimamngo ya marafiki na ndugu zangu, lakini baada ya kutatua tatizo ndio kwanza nikajikuta najiingiza kwenye matatizo makubwa sana, asa baada ya mke wangu Irene kunipeleka mahakamani na kuchukuwa baadhi ya vitu asavile alivyo pewa na kaka yake, akiniachia nyumba na vitu vya ndani.

Hapo ndipo nilipo pewa sharti la kama nataka kuzaa na mwanamke yule, kwamba nionyeshe kama nita wa jari watoto wake, kwa kuwaingiza katika familia na milathi yangu, na mimi nika kubari, hapo watoto wake wawili wakaandikishwa kama watoto wangu kwenye vyeti vyao vya kuzaliwa, pili ika waingiza kwenye jarada langu la milathi, pasipo kujuwa lengo la mwanamke yule, ambae sikuchache baadae aliomba tufunge kwanza ndoa ya serikari,

namimi nika kubari na kutekela jambo ilo, ambalo lilisaidia kuniweka maali pabaya zaidi, maana mezi michache mbele alianza vituko, vya kudai taraka, sababu nilisha ona akuwa na dalili ya kushika mimba, nikaona isiwe tabu, nikakubari mala moja kutoa taraka, ambayo ilinibana kwenye vipengele vya watoto, ambao kiukweli siyo wakwangu, jambo ambali mahakama, aikuweza kulisikiliza, na kunihamuru, nimwachie mama watoto ile nyumba na vitu vyote vilivyomo ndani, kwaajili ya kuishi na watoto,

huku niamuliwa nigawe mshara wangu wakila mwenzi kwa matunzo ya watoto, ambao kwenye vielelezo vyangu vinaonyesha ni wangu, na nimoja ya walithi wangu, ukweli nilizoofika sana juu ya ilo, nika fikia hatua yakuacha kazi, maana niliona aitokuwa vyema niwafanyie kazi watoto ambao sio wakwangu, hivi navyosema sina mbele wala nyuma, naanza upya kutafuta maisha, naamini hii ni lahana, ya mke wangu Irene, naomba unisamehe, kama ni huyo mwanao nita mchukulia kama mwanangu” alimaliza kueleza Jems.

USIIKOSE SIMULIZI INAYOFUATA

Umeyaona Matangazo?
Usisahau Kunipa Sapoti kwa Kuyabonyeza ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Burudani

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni