FUPI TAMU (15) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Alhamisi, 16 Februari 2023

FUPI TAMU (15)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

Jina: FUPI TAMU
Mwandishi: Edgar Mbogo

SEHEMU YA KUMI NA TANO
ILIPOISHIA...
huku niamuliwa nigawe mshara wangu wakila mwenzi kwa matunzo ya watoto, ambao kwenye vielelezo vyangu vinaonyesha ni wangu, na nimoja ya walithi wangu, ukweli nilizoofika sana juu ya ilo, nika fikia hatua yakuacha kazi, maana niliona aitokuwa vyema niwafanyie kazi watoto ambao sio wakwangu, hivi navyosema sina mbele wala nyuma, naanza upya kutafuta maisha, naamini hii ni lahana, ya mke wangu Irene, naomba unisamehe, kama ni huyo mwanao nita mchukulia kama mwanangu” alimaliza kueleza Jems.

WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI

SASA ENDELEA...
hapo kila mmoja akashusha pumzi ndefu, akionyesha kuingiwa na simulizi ile ya bwana Jems, “nazani Irene umemsikia mwenzio, sijuwi unasemaje mpaka hapo?” aliuliza mshenga huku anamtazama Irene, “mimi kama ni kusema, nazani nikwamba kwangu ajaacha kitu, sababu ata mala ya mwisho alisema nisiwaze kuwa atanikumbuka, na mimi nika muomba kuwa asije kunikumbuka kwa lolote, sababu niliitaji kuendelea na maisha yangu, kama nilivyo sasa,

nina mume na tuna mtoto, ebu fikilieni wazee wangu, nita mwachaje mwanaume ambae ameionyesha kila aina ya upendo, kisha nika jikabidhishe kwa mwanaume ambae amerudi kwangu sababu anamatatizo, itakuwaje pale ambapo atuto pata tena mtoto kama ilivyo kuwa mwanzo, kwa kweli ilo naomba mnisamehe, na ninaomba liishie hapa, sababu kuendelea kuliongea jambo ili, nisawa na kumkoa baba wa mtoto wangu” alisema ma mdogo na hapo baba Eva nae akasema, “mzee Ponera nazani jambo ili kiubinadamu aliwezekani, hivyo nivyema tuchukulie ndio limesha tokea, na bwana Jems, aendelee na maisha yake kama alivyo yachagua mwanzo”

Naam na hivyo ndivyo ilivyo kuwa kikao kikaishia hapo, wageni wakaondoka bila kula, sababu bamdogo Jems alikuwa analia kwa uchungu, akimlahani yule mwanamke alie kuja nae siku ile, akidai kuwa awezi kukubari yapite namna ile, lazima alipie alicho kifanya kwake, atukujuwa anamaanisha nini, lakini tukaja kujuwa siku tatu baadae.

Ilikuwa ni juma tano, kaka akiwa amebakiza siku mbili kusafiri kwenda songea kumalizia mwaka wake wamwisho wa masomo ya udoctor, siku hiyo baba alikuja na gazeti, na kumpatia kaka, ambae baada ya kulizoma akaambiwa alipeleke, nyumbani kwa kina Eva, ambako pia walipolisoma walishangaa sana, maana habari iliyoandikwa mle ndani ilikuwa ni mbaya na yakuhusunisha.

Kwamba babamdogo Jems, alienda kwenye ile nyumba ambayo alipolwa na yule mama wawili, ambae alimpokea na kumkaribisha ndani, akidai kuwa anamaongezi nae, na baada ya kuingia ndani wale watoto wawili wa yule mama waka aambiwa waende wakacheze ilimama yao aongee na mgeni, lakini muda mfupi baadae wakashangaa kuona nyumba inawaka moto, na watu walipojaribu kuuzima moto, awakufanikiwa, nyumba ilitetekea yote, huku watu wakiamini kuwa kuna watu wawili wamefia mle ndani, lakini baade wakagundua kuwa mle ndani kulikuwa na mwili wa mwnamke peke yake, ikabanika kuwa mwanamke huyo aliuwawa muda mfupi kabla ya nyumba aija anza kuungua kwa moto ulianzia kwenye magodoro, yaliyo wekwa milangoni na madirishani, maana mwanamke huyo alikuwa akiwa ameshomwa kisu mala kadhaa kwenye mwili wake, huku akiihisiwa mgeni wakiume alie kuwa ametembelea nyumba hiyo, ambae alitoweka, wakati watukio, kuwa ndie alie tekeleza tukio ilo.

Ukweli mpaka dakika za mwisho mtuhumiwa akuwa amepatikana, japo jeshi la polisi lilikuwa katika uchunguzi, wa kumsaka mtu huyo alie fahamika kwa jina la Jems.

Tukio ilo lilimnyima amani mamdogo, kwa kuofia kuwa Jems anaweza kumalizia kwake, kwa mdhuru yeye na mtoto, akuwa na shaka na kaka Denis, kwanza yupo mbali, pili aliamini kuwa Jems asingeweza kupambana na Denis, ambae anauwezo mkubwa wa kimapigano, hivyo kwamsaada wa mkurugeni wa idara ya mapato, mamdogo akaamishiwa songea, ambako baada ya mwaka mmoja kaka Denis, nae alipata kazi katika hospital ya pelamiho.

Naam mpaka sasa wanaishi pamoja kama mke na mume, wanawatoto saba, siwezi kuzitaja kazi zao, na wazfa walionao kutokana naheshima yao, sababu jukumu la kusimulia mkasa huu sija washilikisha, ila kwa kifupi mimi na Eva pia ni mke na mume, japo tumepitia mengi hapa katikati, na sasa tuna hisi kibaha mkoa wa pwani, endapo bwana Edgar ata pata nafasi, nita kuja kumsilia mkasa wa mimi na Eva, mpaka tuka fikia hatua ya kufunga ndoa,na sasa tuna watoto watatu.

Naam kama mlivyo msikia bwana Prosper (siyo jinalake) akisimulia mkasa huo, MFUPI LAKINI MTAMU, wa kaka na shemeji yake, ameahidi kuwa endapo tukipata nafasi ata kuja kueleza mkasa wake yeye na mke wake Eveline, ambao ata mimi nina hamu ya kuusikia, Japo ilikuwa FUPI LAKINI TAMU , napenda kusema, asanteni sana kwa kuwa pamoja naimimi mwanzo mpaka mwisho,

MWISHO

Umeyaona Matangazo?
Usisahau Kunipa Sapoti kwa Kuyabonyeza ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Burudani

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni