FUPI TAMU (3) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumapili, 12 Februari 2023

FUPI TAMU (3)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

Jina: FUPI TAMU
Mwandishi: Edgar Mbogo

SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA...
Nakumbuka bahati ikuwa upande wetu, maana wakati nataka nimkumbushe mama mdogo kupitia kwa wakwetu, na Wakwetu alikuwa wakwanza kutuona, alipotuona tu! akatuita, “Irene vipi wangu mbona unanipita kama jiwe la kilomita?” aliuliza Wakwetu, akiwa mbali kidogo na sisi, hapo ma’mdogo akujibu, ila aka mtazama kaka Denis…

WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI

SASA ENDELEA...
Ambae nikama alijifanya kupotezea hivi, alafu mama mdogo akamtazama Eva, “Eva nisubirini hapo, niongee na mjomba” alisema mamdogo Irene na kumfwata Wakwetu, nikawaona wanaongea mambo flani flani, nikama mamdogo alikuwa anakataa kitu alicho kuwa anaambiwa na Wakwetu, lakini baada ya maongezi ya dakika kadhaa, tuka mwona kama wanakubariana, tuka mwona Yule jamaa akichagua samaki wawili wakubwa aina ya kambale, na kuwa weka kwenye mfuko, kisha akatutazama pale tulipo, “we dogo, unazubaa nini njoo uchukue mboga” alisema Wakwetu, nikamwona kama mamdogo, nikama alikuwa anamkataza, asimwite kaka, lakini alisha chelewa kaka Denis aliwafwata wakina mamdogo, na sisi tukimfwata nyuma yake, “beba mboga hii ya kula jioni, mbona unazuba sana dogo” alisema Wakwetu na kaka akatabasamu huku anapokea ule mfuko wa kambale, “shikamoo” alisalimia kaka Denis, “malahaba dogo” aliitikia wakwetu, kisha akamtazama madogo, ambae alikuwa ametazama chini kwa aibu, “sikunyingine utakiwi kuja sokoni we mtume tu huyu dogo, si atanikumbuka?” alisema Wakwetu kwa majisifu, mamdogo aliishia kutabasamu, kaka ndie alie jibu, “nitapakumbuka” niliona mamdogo akimkata jicho kaka Denis.

Baada ya hapo mamdogo akaaga na kisha tuka ondoka zetu, huku wakwetu akisisitiza, kuwa baadae atakuja nyumbani kwa kina Eva, “sawa utanikuta” kwa haraka haraka, nilisha wasikia watu wawili waki toa ahadi za kuja kwakina Eva ndani ya usiku mmoja.

Kagiza kalisha tanda, likiongezewa na wingu kubwa la mvua, ambayo inge shuka muda wowote, tulitembea kimya kimya, kila mmoja alisha choka, na mizunguko, sasa mimi na Eva tulikuwa tume shikwa mikono na mamdogo, kaka alikuwa amebeba mazaga yote aliyo nunua mamdogo sokoni, tulipofika pale dukani kwa kwa juma mpemba, nikamwona mamdogo akipita kwa kujificha ficha akisaidiwa na giza lililo kuwepo, lakini wakati tuna pita, tuka gundua kuwa mpemba akuwepo dukani kwake, na baada yake alikuwepo mke wake, yani mmoja kati ya wakezake, hapo safari ikaendelea kimya kimya, ikonyesha mamdogo na kaka Denis awajazoweana bado, kiasi cha kupiga story, wakati mwingine nilizania kuwa, ni kutokana na kuzidiana umri, au ni ile tabia ya mamdogo kuto kupenda mazungumzo mengi na wanaume, japo cha ajabu akuwa anawakataa waziwazi, na vitu vyao alikuwa anachukuwa.

“Pross, leo si utakula nyumbani kwetu” aliuliza mamdogo, hapo nika mtazama kaka kama atatoa jibu gani, lakini akawa kimya, “pross ujuwe mchumba wako leo yupo peke yake, anaogopa, si utakuja kuchaza nae kidogo?” safari hii mamdogo aliongea kwa sauti ya kubembeleza, “labda kaka akinileta” kwamala ya kwanza nilijibu mwenyewe, kweli nilikuwa na hamu ya wali na kambale, mana kipindi hichi wali ni moja ya vyakula nilivyo kuwa navipenda kupita kiasi, hapo hapo nika msikia Eva akinisaidia, “eti kaka Denny, si utamleta pross?” aliuliza Eva, “ngoja kwanza tuka age nyumbani, alafu nita mleta” hapo moyo wangu ulitabasamu kwa furaha, wali kambale siyo mchezo, maana katika kumbukumbku zangu tulimwacha dada anabandika maarage kwaajili ya jioni, siyo kwamba wazazi wetu walikuwa awana uwezo kifedha, ila ndio utaratibu walio jiwekea, kama mchana tuta kula ugari samaki au nyama, basi usiku wali maarage, na leo ndio ijumaa kuu, basin i maharage kwakwenda mbele.

Nikama ata mamdogo nae alifurai kwa jibu la kaka, maana nilimwona anatabasamu, wakati huo tulikuwa tuna ingia kwenye uwwanja wa nyumba ya kina Eva, “Irene, ndio warudi sasa” wote tuka geuka kutazama pembeni ya kibaraza cha nyumba ya kina Eva, nimwona mamdogo akistuka sana, maana wote tuka mwona bwana mpemba akiwa amesimama na baskeli yake, iliyo kuwa na kifurushi kwenye kitako na juu ya kurushi, kulikuwa na kitui kama kuku hivi, ambae tulithibitisha kuwa zinga la jogoo, baada ya kumsogelea mpemba, “he! mbona mapema?” aliuliza mamdogo, kwa mstuko mkubwa sana, “si zahivi bwanae, nimeleta nchele na kuku, mie nitakuja baadae” alijibu bwana juma Mpemba, huku akimkabidhi mamdogo lilejogoo, yeye akaanza kufungua mfuko uliokuwa nyuma ya baiskeli yake, huku nikimwona mamdogo anamtazama usoni kaka Denis, lakini niligundua alikuwa anaona aibu flani usoni kwake, bahati nzuri kakaakuwa anamtazama mamdogo, yeye alikuwa anamtazama mpemba alie kuwa anafungua ule mfuko, “dogo vipi mbona unazubaa, njoo unishikie baiskel” alisema mpemba, akimwambia kaka, ambae alisogea mala moja na kushikilia baskeli akiwa katika hali ya kawaida tu! aakuonyesha kuchukizwa wala kuona wivu, naazani alisha gundua kuwa mamdogo siyo size yake, na ukitazama ilikuwa kweli, maana kaka alionekana mdogo sana kwa mamdogo, ambaae licha ya umri na uzuri aliokuwanao, pia alionekana wazi, kuwa mwanamke mwenye hadhi ya juu, kwa mavazi na mwonekano.

Baada ya kumaliza kufungua mzigo wa mchele, na kumkabidhi kaka, Mpemba aliondoka zake, akituacha sisi na wakina Eve, hapo ikiwa kimya kimya, mlango ukafunguliwa na taa zikawashwa, tukaingia ndani kwa kina Eva, kaka na mamdogo wakaenda jikoni kuweka ile mizigo tuliyo tokanayo mbezi nah ii aliyoleta mpemba, atukuwasikia wanaongea lolote, ilikuwa kimya kimya, mpaka wakatoka, nakutukuta mimi na Eva sebuleni, “twende popa” alisema kaka huku anashika mkono na kuanza kutoka nje, hapo Eva akanikimbilia, “Popa, uje baadae, usipokuja uta kosa wali na kambale” alininong’oneza Eva, lakini nikama wote walisikia, maana siyo kuni nong’oneza ni kupayuka, maana ma mdogo na kaka walicheka, “mchumba wako atakuja bwana usiwe na wasi wasi” alisema mamdogogo, na mimi nika mtazama, mamdogo, nikamwona anamtazama kaka, ambae nae alikuwa anamtazama mamdogo, macho yao yalipo kutana nikawaona wakikwepesha macho, “aya situnaenda” aliaga kaka, na mama mdogo akasisitiza, “aya popa msichelewe, sie tupo peke yetu” alisisitiza mamdogo, na sisi tukaondoka.

Wakati tukiwa njiani tunaenda nyumbani, kaka akawa ana ongea na vitu ambavyo nilikuwa nashindwa kuchangia point yoyote, “yani ata simwelewi huyu dada, yeye kila mwanaume anasema anakuja usiku alafu yeye anakubari tu! wakikutana atafanyaje” moja ya maneno ambayo kaka Denis alikuwa anajiuliza, hapo mimi nilikuwa naombea kaka sije kubadiri maamuzi nikale wali na kambale, maana nyumbani nilikuwa na uhakika ya kuwa nyumbani ni wali na maharage, sababu dada wakazi nilimwacha akiyabandika jikoni, tilfika nyumbani na kulikuta mgongo wa chura likiwa limeshahegeshwa sehemu yake, kwahiyo ilionyesha wazi kuwa tayari baba na mama walisha wasili nyumbani muda mrefu uliopita, tukiaingia ndani na kuwakuta wakiwa wana tazama mkwanda wa video kwenye video yao ambayo ilikuwa ina onyesha kwa rangi mbili tu, nuyesi na nyeupe, na mimi nika jiunga kutazama video, muda ulikuwa saa moja nanusu, harage la nazi likinukia kwa fujo, kaka akawaamkia na kuelekea chumbani kwake, akiniacha mimi nina tazama filamu ya yesu, ulikuwa mkanda mpya nazani walikuja nao, jioni hile.

Lakini yote kwa yote nilikuwa nawaza wali na kambale, kule kwa kina Eva, nikawa nawaza kuwa kaka amesha gairi kwenda kwakina Eva, labda kutokana na mamdogo kupokea mialiko mingi ya watu, kwa wakati mmoja, japo sisi ndio tumealikwa na yeye mwenyewe.

kule chumbani kaka alikaa kama dakika tano tu!, mala akaja sebuleni, akiwa na mwamvuri, “baba mi natoka mala moja, kuna kitu napeleka pale kwa jilani, alisema kaka huku akionyesha upande wa kwakina Eva, hapo namimi nikainuka, haraka nikjuwa safari ya wali na kambale, imewadia, “kwani unaenda na huyu chek bob?” aliuliza baba mama baba kwamshangao, hapo sikusubiri kaka ajibu, “ndio na mimi naenda kwa kina Eva” mama akacheka kidogo, “we! mtoto wewe, mwenzio anaenda kumwona wifi, na wewe unataka kwenda” alisema mama kwa utani, kisha wote wakacheka, “siyo wifi, ni mama mdogo” nilijikuta nimesha lopoka, japo huyu wifi sikuwa na mjuwa anafananaje, zaidi ya kusikia wakina mama wakiita wifi, hapo wakacheka tena, “aya sasa, amja enda Popa ameshaanza kuropoka, sasa mkirudi tuta sikia mengi” alisema baba, wakacheka tena, japo mimi sikuona chakushekesha, sababu nilikuwa nawaza wali na kambale, japo nilielewa baada ya masaa machache, na mwisho baba akasema tuchukuwe funguo moja, ya mlango mkubwa, ili tukichelewa kurudi tufungue mlango wenyewe, bila kuwasumbua, “tuta wakea chakula chenu hapa mezani” alisistiza mama, huku baba akichombeza, unazani, “wata kula vinono huko huko, labda siyo Pross” hapo wakacheka tena, na sisi atukuchelewa, tukatoka nje, ambako tulikuta mvua imesha anza kunyesha taratibu, nashukuru mvua ile aikumfanya kaka aghari, akafungua mwamvuri, kisha tukajitosa, “ukisha kula tu! tunaondoka mi sitaki ushaidi, maana kwa jinsi nilivyoona pale, damu lazima imwagike” alisema kaka, sikumwelewa anamaanisha nini, saabu mimi hakiri yangu ilikuwa kwenye ubwabwa tu! “kwanini kaka, kwani wata chinja kuku?” nilimwuliza kaka, huku tunatembea taratibu, kukwepa madimbwi ya maji yaliyokuwa yametapakaaa, njiani, na mvua zikiendelea kunyesha mdogo mdogo, “we unazani wale jamaa wakikutana hapa, kitatokea nini zaidi ya ngumi?” hapo ndipo nilipojuwa kaka anamaanisha nini, kwanza niliona kama anadalili ya wivu, toka kule mbezi, pia alionekana kumchukulia tofauti mama mdogo, japo sisi atukushangaa tabia ya mama mdogo kupokea vitu toka kwa waume mbali mbali.

*****

Tulitumia mumfupi kufika nyumbani kwa kina Eveline, ilibakia kidogo nisukume mlango, lakini kaka akanidaka mkono haraka, na kunirudisha nyuma, kisha yeye akasogea mlangoni, na kutega sikio kusikiliza huko ndani, niligundua alikuwa anasikilza kama mmoja kati ya wanaume waliosema watakiuja kwa mama mdogo watakuwa tayari wamesha fika, lakini akaona kimya, hivyo aka goga hodi, lakini akuna alie itikia, akarudia mala kadhaa, lakini akukuwa na jibu, hapo siyo mimi pekee nilie ona dalili ya kukosa wali na kambale, ata kaka alisha kata tamaa ya kukaribishwa na wenyeji wetu, “Pross watakiuwa wametoka, ebu twende zetu home” alisema kaka Denisi, na hapo mimi niliumia rohoni, maana nilikuwa na uhakika mle ndani lazima watakuwepo, ila wameuchuna makusudi, hakika nilijihapia sitocheza tena na Eveline, “nani?” lilisikika swali toka kwa ndani,ilikuwa ni sauti ya Evekine, “mimi kaka yake Pross nime mleta Pross” alisema kaka ambae nikama alionekana kuchukizwa na kuchelwa kwa kuitikiwa hodi yake,

USIIKOSE SIMULIZI INAYOFUATA

Umeyaona Matangazo?
Usisahau Kunipa Sapoti kwa Kuyabonyeza ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Burudani

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni