FUPI TAMU (2) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumapili, 12 Februari 2023

FUPI TAMU (2)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

Jina: FUPI TAMU
Mwandishi: Edgar Mbogo

SEHEMU YA PILI
ILIPOISHIA...
Sikujuwa ni kiasi gani lakini baadae nika juwa kuwa zilikuwa ni shiringi elfu moja, zilikuwa na thamani kubwa, kipindi hicho, maana anakumbuka, nguo yangu ya sikuku mwaka ule, ilinunuliwa kwa shilingi mia mbili, nilimwona ma’mdogo anashangaa kwa kiasi kukibwa cha fedha alicho patiwa na na Juma Mpemba…

WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI

SASA ENDELEA...
Hapo Juma mpemba, ambae alikuwa anakaa mitaa ule ule, na wake zake wa wiwli ambao kilammoja alisha pata nae watoto, bi mkubwa akiwa na watoto wanne, bi mdogo alikuwa na watoto wawili wa kike, ambao katiyao wawili tulikuwa tuna soma nao, akatuacha tuondokezetu, sisi na mama mdogo tukaondoka zetu kuelekea Mbezi mwisho, ambako tulipita bara bara ya zamani, huku mala mala kwa mala, tukipishana na vidume vilivyo msemesha mama mdogo, maneno ambayo ayakuni flaisha,

“we! mwanake ebu simama tuzoze kidogo” kuzoza ni kuongea, au kujadiriana jambo flani, wengine walipiga miluzi, na mambo mengine ya kuhudhi, Kitu ambacho mimi na Eveline tuligundua, ni kwamba ma mdogo apendi kuongozana wala kuwa karibu na wanaume, japo akuwa na ujasiri wa kuwapa majibu ya mojakwamoja kuwa akuwa tayari kuwa nao kimapenzi, na kwa uzuri wake, ilikuwa vigumu kuepuka usumbufu wa wanaume hao.

Nakumbuka wakati tupo mbezi sokoni, kuna jamaa mmoja muuza samaki, ambae pia anakaa kule mtaani kwetu, namkumbuka kwa baiskeri yake, ambae kwenye main guide (medigadi) nyuma ya tairi, aliandika Wakwetu, alimweleza mamdogo maneno kama yale aliyo elezwa na na Mpemba, yani yule muuza duka, mwisho jamaa huyu muuza samaki wakavu, aka funga kambale wawili na kumpa ma’mdogo Irine, “nenda kale nyumbani, nazani nitakuja ijumaa, shemeji yako uwa anapenda sana kusafiri kipindi kama hiki” mpaka hapo tulikuwa tumesha sikia ahadi mbili, ambazo binafsi siku msikia mamdogo akitoa majibu, ya kukubari ahadi zile, au kuzi kataa, na licha ya hivyo tulisha ona kikataa kuongea na wanaume wengi sana.

*****

Leo mimi na Eveline tulitaka kuona kama ma’mdogo atakubri kuongozana na kaka Denis, na ukichukuia hii ndio njia ya kwa mpemba, na leo ndio siku ambayo mpemba aliahidi, kuja kwa kina Eva, na kweli wazazi wa Eva walishaondoka, kuelekea mrogoro, “Pross unaenda kanisani bila kumpitia mchumba wako?” alisema ma mdogo, huku akinichezea kichwani, sikujuwa ni jibu nini, nikajichekesha huku na mtazama kaka Denis, “na juwa Popa uwezi kumkimbia mchumba wako, na hivi alivyo pendeza, si watu watakuibia huko kanisani” alijibu kaka, japo mwanzo siku lielewa jibu lile, na kulichukulia kiwepesi, lakini nikaelewa, baada ya kumsikia mama mdogo ambae alianza kukutabasamu kidogo, akijibu,

“Eva mwambie Poross, ni wasi wasi wake tu!, aibiwi mtu” kwa maneno, nikama ilitoa kibari cha kuongozana, tukaanza kutembea kuelekea Mbezi kanisani, safari ilianza kimya kimya, na baada ya kutembea kama mita mia mbili hivi, kaka akaanza uchokizi, “Eve, leo umependeza utazani ndio siku ya siku kuu, mpaka Popa anaona wivu” hapo Eveline aka mtazama ma’mdogo, nikama alikuwa ana msubiri amjibie, mana tulisha ufahamu ule mtindo wao wakuongea, “Eva mwambie Pross, ndio kawaida yetu kupendeza” hapo kaka Denis akacheka kidogo, nikifwatia mimi kumsaidia kucheka, ata Eva nae kacheka, ma’mdogo yeye aliishia kutabasamu, huku safari ikiendelea, tukikaribia madukani.

Nika mwona ma’mdogo anaongeza mwendo, kila tulipo karibia maduka, huku akiwa amemshika mkono Eva na kumfanya apate shida kuruka vidimbwi vyamajini, “Pross mwambie Eva atembee taratibu, atacha uaviatu vyake vizuri” kiukweli kutokana na sura ya kaka Denis, na umri wake mdogo zaidi ya ma’mdogo, usinge weza kuwa fikilia vibaya, ilionyesha wazi kuwa ma’mdogo nimkubwa kwa ma’mdogo Irene, “Eva mwambie mchumbma wako, hapa kuna wa doezi, ndio maana tuna arakisha” alijibu mamdogo, hapo akuna ambae akujuwa kuwa anaambiwa kaka Denis, hivyo atukuwa na budiku ongeza mwendo, ili kuufwata mwendo wa ma’mdogo.

Lakini aikusaidia, maana ile tuna livuka duka la mpemba tu, Juma mpemba akachomoka toka dukani kwake akiwaacha wateja watatu waliokuwa wana subiri huduma, “Irene leo wapiti mbio mbio, kama wafukuzwa” alisema Mpemba huku akitukimbilia, “tumechelewa kanisani” alijibu mamdogo, huku anasimama, “Pross mshike mkono mchumba wako, mtangulie taratibu” alisema Ma’mdogo, huku anamwachia mkono Eva, ambae alienda kuudaka mkono wa kaka wa kushoto, “ujambo kijana?” alisalimia Juma Mpemba, na kaka akaitikia, kisha aka mwamkia, mpemba akaitikia, na sisi tukiwa tuna ndelea kutembea taratibu, huku wote watatu tuna tupa macho ya wizi kumtazama ma’mdogo, ambae akutumia muda mrefu, tukaona aona anaambiwa mamneno flani na kupewa kitu flani ambacho tulijuwa itakuwa ni fedha, kisha akatukimbilia, huku Juma Mpemba akisisitiza kuwa mamdogo asi sahau kupitia wakati wa kurudi.

“Pross, utani kumbusha kupitia wakati wa kurud” sikuelewa kwanini mamdogo alikuwa mwepesi wa kupokea fedha na vitu vya watu, wakati walikuwa wana mlalamikia kuwa akuwapa jibu walilo kuwa wanaliitaji, ambalo ata kwa udogo wangu nilijuwa, ni kuwa kubaria wamle kitumbua, “tuta kukumbusha” hapo nilijibu mimi, maana kaka Denis alikuwa kimya, nikama alikuwa anatafakari jambo, ukimya ambao ulimwambukiza ata ma’mdogo, na hapo safari ikawa kimya kimya, mpaka tulipofika kanisani, na tuka tawanyika, wakati sisi tukielekea sehemu walipo kaa wanaume, Eve na ma’mdogo, wakaelekea upande wa wanawake.

Saa kumi jioni tayari tulisha toka kanisani, nakumbuka nikama kulikuwa na dalili yamvua nyingine kushuka jioni ile, maana wingu lilitanda kwelikweli, juu ya anga, niliingiwa na unyonge, maana sikuona dalili ya kaka kuwatafuta wakina ma’mdogo, ukweli safari ya kuwa na kaka Denis, sikuipenda ata kidogo, kwanza akuwa na ela ya kununua pipi, maana zaidi ya shilingi sita ambazo tulizogawana yeye akichukuwa shiringi tano na mimi shilingi moja, ambazo tulizitoa sadaka, akuwa na ela nyingine, na alicho nikela zaidi, ni kitendo cha kunilazimisha nitoe sadaka, maana nilitaka kuibana, ili nikanunue pipi wakati wa kurudi.

Nilitoka kanisani nikiwa nimenuna kwa hasira, na mbaya zaidi ndio tulikuwa tunaondoka, bila kuwasubiri wa kina Eva na ma’mdogo, ambao najuwa kabisa wata faidi pipi wakati wakurudi, lakini nahati ikawa upande wangu, maana ile tuna ikamata barabara huku kaka amenisika mkono, katikati ya kundi la watu waliokuwa wanatoka kanisani, mala nika stuka, mtu ame nigusa begani kutoka nyuma yangu, kutazama nyuma alikuwa ni Eva, aliekuwa ameshikwa mkono na ma’mdogo Irene, nakumbuka nilijisikia amani kubwa moyoni mwangu, maana nilitabasam mpaka wana Eva walijuwa kuwa nilikuwa nawaitaji, kutokana na kugeuka kwangu, kaka Denis akageuka kutazama nyuma, macho yake yaka kutana na macho ya mamdogo, ambae alitabasamu kidogo, japo kaka nikama alilipotea zilie tabasamu la mama mdogo,

“Pross, una mwacha mchumba wako, umsindikizi sokoni” aliuliza Mamdogo, hapo sikuangaika kujibu. nilijuwa lile swali ni la kaka, wakati huo watu wengi waliokuwa wana elekea majumbani mwao, walikuwa wanamshangaa ma’mdogo , kwa uzuri wake, wengiwao wakiwa ni wanaume, ambao awakujali kuwa wapo na wakezao, au familia zao, maana licha ya kupendelewa uzuri wa sula na umbo. pia ma’mdogo, alikuwa anajipenda sana, kwa urembo na mavazi, “Porss, uogopi kufumaniwa na wenyewe” aliniuliza kaka, hakika nilishindwa kumwelewa kaka Denis, na ukichukulia nilikuwa na juwa kuwa safari za mamdogo ni zakufaidi, nika jibu mwenyewe,

“siogopi” huku nikijitoa mkono wangu, kwa kaka ambae nilisha ona kuwa hakuwa na mpango wa kuongozana na mama mdogo, pengine kwa wivu au roho ilimuuma, kwa kile kilicho ketoa pale kwa mpemba, “eti Pross utafumaniwa nanani wakati wewe ndie mwenye mchumba” alisema ma mdogo, ambae nilimtafthiri juu juu, sikujuwa alikuwa ana maanisha nini, “mh! Pross Eva ana kupa moyo, wakati wewe siyo hadhi yake” alisema kaka, wakatu huo walikuwa wanaongea kwa sauti ya chini, “wala asikutishe Pross we jiamini, kwa ni wenye ela ndio wananini, kama ela si tunazo zakwetu”, alisema mama mdogo huku anamtazama kaka kwa macho ya tabasamu, na kuzodoa, “poa twenzetu, lakini sisi yetu macho” alisema kaka na wakati huo alikuwa ananidaka mkono, kisha tukaelekea mbezi sokoni.

********

Safari ilianza kimya kimya, huku na watathimini kaka na mamdogo Irene, kaka licha ya kuwa mrefu kiidogo kuliko mamdogo, na mwili mkubwa, kiasi, lakini bado alionekana kuwa ni mdogo kwa umri, wakati ma’mdogo alionekana wazi kuwa ni mkubwa, lakini alikuwa anavutia sana, japo nilikuwa mdogo sana, lakini niliona jinsi mama mdogo alivyo kuwa anavutia, maana ukiachia umbo lake ambalo wakubwa walikuwa wanaliita namba nane pia alikuwa na sura nzuri, na alipenda kujilemba kila wakati, na kwenya mavazi ndio usiseme, ila alikuwa mpole sana, tofauti na zamani, alipokuwa anakuja kuwatembelea wakina Eve.

Wakati tuna endelea na safari, mimi na Eve tuligundua tabia mpya ya wakina kaka na mamdogo, maana mala kwa mala walikuwa wanatazamana usoni na kuishia kutabasamuliana, huku mala nyingi kaka aki tazama kwenye makalio ya mamdogo, ambae alikuwa mbele yatu, ame mshika mkono Eve,

Baada ya kutoka pale kanisani kituo cha kwanza kilikuwa kwenye maduka ya karibu na stend kakaribu kabisa na sokoni, hapo mamdogo akanunu biscut box moja, na kutu gawanyishia mimi na Eva, alafu safari ikaendelea kimya kimya, kuingia sokoni, “Eve mwulize mchumba wako kamaana penda kachumbali tununue nyanya” nilimsikia mamdogo, akimwambia Eva, na kwa kuwa tulisha zowea kuwa kila swali anajibu kaka, wote tuka mtazama kaka, “kwani we Pross unakulaga kwa kina Eva?” aliuliza kaka Denis, na hapo ma mdogo akaongea wazi wazi wazi, “kwani vibaya akila kwa mchumba wake?”

Hivyo ndivyo ilivyo kuwa kila kilicho takiwa kuulizwa kaka ilipitia mimi na alicho takiwa kuulizwa mamdogo aliulizwa Eva, ilimladi nikama walikuwa wanakwepa maongezi ya moja kwamoja, kwetu ilikuwa kama burudani, lakini tulipenda kuona ndugu zetu au watu wetu wakaribu, wakiwa wakiwa pamoja, maana usingeweza kumkuta mamdogo akiongozana na mwanaume kama hivi, kingine kilicho changia pengine ni umri mdogo wa kaka Denis,

Nakumbuka tukiwa sokoni, wakati tuna pita sehemu ya wauza samaki, tuka kutana na yule jamaa anae mpaga mamdogo hela na samaki, mama mdogo nikama akutaka kupitia, wala kuonekana mbele ya yule jamaa ambae baiskeri yake imeandikwa wakwetu, ukweli nazani siyo peke yangu ata Eva alitamani tupitie, ili tupewe ela ya pipi, lakini mama mdogo akuonyesha dalili ya kupitia, ndio kwanza alikuwa anaongeza mwendo.

Nakumbuka bahati ikuwa upande wetu, maana wakati nataka nimkumbushe mama mdogo kupitia kwa wakwetu, na Wakwetu alikuwa wakwanza kutuona, alipotuona tu! akatuita, “Irene vipi wangu mbona unanipita kama jiwe la kilomita?” aliuliza Wakwetu, akiwa mbali kidogo na sisi, hapo ma’mdogo akujibu, ila aka mtazama kaka Denis…

USIIKOSE SIMULIZI INAYOFUATA

Umeyaona Matangazo?
Usisahau Kunipa Sapoti kwa Kuyabonyeza ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Burudani

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni