FUPI TAMU (9) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumanne, 14 Februari 2023

FUPI TAMU (9)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
📖 KUSOMA SIMULIZI
🎬 FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
😂 VIDEO za KUCHEKESHA
📑 MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa

Jina: FUPI TAMU
Mwandishi: Edgar Mbogo

SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA...
“ulisahau chupi kwa mamdogo” nilisema kwa sauti ya juu huku ninaangua kicheko, hapo kaka aliivuta kwanguvu ile nguo yake, na kuiweka mfukoni, kisha akaanza kutembea haraka kuelekea njia ya nyumbani, na mimi nikimmfwata pasipo kujuwa kuwa ayari watu waliokuwepo eneo lile wamesha gundua jambo kutokana na tukio lile,

WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI

SASA ENDELEA...
“kumbe dogo, anatembea na yule mwanamke” zilisikika baadhi ya sauti za watu wakiulizana kwa mshangao, ila mimi sikuwaza lolote juu ya hatari ya kugundulika kwa jambo lile, sababu kati ya watu waliokuwepo kwenye eneo la maduka, ni mpemba, “Pross ni mjinga sana wewe” alisema kaka Denis, huku tunatembea haraka haraka haraka, Eva nae akitufwata.

Tulitembea kwa haraka kutoka eneo lile la madukani, huku Eva akiniomba pipi nilizopewa na Fatma, sikusita kumpatia mbili, “alafu huyu mamdogo nae, si bola angeitupa au kuichoma moto, kuliko kumpa mtoto kama huyu, aniletee?” alisema kaka kwa sauti iliyo jawa na hasira, akiendelea kumshushia lawama na kumshuku kwa mambo mengi mamdogo, “au ameamua kunikomoa” alisema kaka, “hapana mamdogo ajanipa nime ichukuwa mwenyewe nika kuletea” alijibu Eveline, na hapo nikamwona kaka anasimama, na kumtazama Eva kwa macho ya mshangao, “mamdogo mwenyewe anafanya nini?” aliuliza kaka kwasauti ya mshangao, huku ana mtazama Eva, ambae akuonyesha kujari chochote,

“yupo nyumbani kichwa kina muuma, mpaka analia” alisema Eva, hapo nikamwona kaka kama kuna kitu anawaza, nikamwona kama kunajambo, alifanya hivyo kwa sekunde kadhaa, kisha akaanza kutembea na sisi tuka mfwata, “ameanza kuumwa saa ngapi, mbona jana alikuwa mzima kabisa?” aliuliza kaka Denis, huku tuna endelea na safari, maana toka madukani mpaka, kwakina Eva kuna kamwendo kidogo, “mi nimeamka na mwona analia, nilipomwuliza akasema kuwa kichwa kinamuuma” alijibu Eveline, na wakati huo tuka sikia sauti ya kengere ya baiskeli nyuma yetu, wote tuka pisha huku tuna geuka kutazama baiskeri, “ebu tupitie tukamwone” alisema kaka huku tuna subiri baiskeri ipite.

Ukweli, sikuweza kumjibu kaka Denis, zaidi mimi na Eva tulibakia tuna tazama kwa mshangao, na hasira upande unaotokea baiskeri, nazani kaka alizania kuwa tunashangaa baiskeri, ile ya gia, (gear) ambayo ilikuwa inaendeshwa na kijana mmoja maridadi sana, maana akuonekana kutujari, ila kaka alishtuka mala baada ya kumwona mwendesha baiskeri akisimamisha baiskeri yake karibu yatu, “ujambo Eva” alisalimia yule kijana alie mkazia macho Eveline, “sijambo” alijibu Eva kwa makato, kisha akaanza kutembea kueleke kule tulikokuwa tuna enda, na yule kijana maridadi ambae tulikuwa tuna mfahamu vyema, akakanyaga peda kumfwata,

“Eva mama mdogo umemwacha nyumbani?” aliuliza yule kijana ambae umri wake nikama uaikuwa analingana na kaka Denis, “anaumwa” Eva alitoa jibu tofauti kabisa, na swali alilo ulizwa, akionyesha kuwa akuependa maswali ya yule kijana, “ambae ata yeye mwenyewe aligundua swala ilo, maana alikanyaga pederi kwanguvu, na baiskeri yake ika shika kasi, na kuondoka zake, “mtu mwenyewe aleti pipi” alisema Eva, akionyesha chuki za wazi kwa kijana maridadi, ambae mala nyingi nae umvizia mama mdogo, lakini tatizo lake alikuwa tofauti na wakina Wakwetu, yeye baada ya kuleta pipi au ela, yeye uja na mauwa au post card, ambazo kwa kipindi hicho zilikuwa zinauzwa shilingi mia mpaka mia hamsini, “bola ata mpemba, yule sangazi yao wakina Falhiya (Fatma mdogo wake mpemba) amenipa pipi” niliongeazea huku tuna mtazama, kijana yule, ambae kipindi hicho mtu kama huyu, kwa umaridadi wake, alikuwa anaitwa be show, akipotea na baiskeri yake.

Mpaka hapo kaka alisha hisi kitu, maana tulimwona akiwa amezama kwenye mawazo ya kuzoofisha hali yake, (furaha) na ata tulipo fika usawa wa kwakina Eva, atukupitia tena kwa kina Eva kama alivyosema, baada yake alitazama kwa kina Eva, kama mimi na Eva tulivyo fanya, maana ata aEva akupitia kwao.

Tulimwona yule kijana amesimama kwenye mlango wa nyumba ya kina Eva, huku baskeri yake ameisimamisha pembeni ya kibaraza, nikama alikuwa anaanaongea na mtu alie kuwa ndani, pasipo kufunguliwa mlango, ilionyesha kuwa mama mdogo akitaka kumkaribisha ndani kijana yule, maana ya kuto penda kuonana nae uso kwa uso, sijuwi kwanini, maana siku zote alikuwa anaongea na kila kila mwanaume anae kuja na kupokea zawadi alizo letewa, kisha kutoa ahadi za kukutana, ambazo zote akuwai kuzitekeleza.

Tuliekea na nyumbani pamoja na Eva, huku njiani kaka akionekana wazi, kukosa amani moyoni mwake, sikujuwa sababu harisi ni hipi, kama ni kusikia mama mdogo alikuwa anaumwa kichwa kiasi cha kulia, au ni ile ya kumwona yule kijana, pale kwa kina Eva, au ni ile ya kuonekana kwa nguo yake ya ndani kule madukani.

*********

Yap, nakumbuka siku ile tulicheza na Eva ppale nyumbani, mpaka mida ya mchana, ambapo tuliondoka na gari letu vox wagon, (mgongo wa chura, wengine wanaita taxi kobe} tukiwa mimi, Eva, kak, baba na mama, mpaka madukani na kuingia moja kwa moja kwenye duka la mpemba ambae akuwepo mida hii, ambapo tulimkuta yule yule shangazi yao wakina Falhiya, mdogo wa mpemba, alie shindwa kuficha hisia zake juu ya kaka, maana alijicheka chekesha, na kumwonea aibu kaka, kiasi cha mama kugundua jambo, maana nilimwona akiwatzama kaka na yule Fatma, kisha akacheka peke yake, upande wangu mimi nilikuwa na subiria kupewa pipi, lakini baba yeye akuona kitu, zaidi alilipia mchele kilo ishilini, na kaka akaubeba na kutoka nao nje, wakati huo mimi nilie kuwa anasubiria offer ya pipi, na Eva alie kuwa anavizia offer yangu, tulibakia ndani ya duka, wakati baba na kaka wanapakiza mchele kwenye gari, mama akiwa chikia mlango wa buti la gari ilo, toka ujerumani, ambalo buti lake lipo mbele, na engine yake ikiwa nyuma.

Nikweli kama mimi na Eva tulivyo zania, kuwa offer ya asubuhi itajirudia tena, Fatma alitugea pipi golori, kila mmoja za kwake, idadi zilikuwa tano tano, lakini ukiachilia pipi, Fatma alinipatia kipande cha karatasi kilicho kunjwa vizuri, “kiweke mfukoni, utampa kaka yake akiwa peke yake” alisema Fatma kwa sauti ya kunong’ona, na mimi nikaiweka mfukoni ile karatasi, kisha tukatoka mbio kusogelea gari, ambapo tulipofika pale nje, nikama nilichezwa na machale, juu ya Mpemba, maana ukiachia jana usiku kupigana juu ya mama mdogo, ambae alikuwa na kaka nyumbani, pia mdogo wake Fatma alionyesha dalilizote za kumpenda kaka, na pia alikuwa ananipa pipi za dukani kwa kaka yake, japo wakati wa kuingia dukani sikumwona Mpemba, alakini hakiri ikanituma ni tazame huku nahuko, kama ninge mwona Mpemba.

Nikweli baada ya kutazzama kushoto na kulia nikamwona Mpemba akiwa amesimama kama mita hamsini hivi, pamoja na vija wawili, wanaonyeshaupande tuliokuwepo, hapo nika hisi hatari kwa kaka, nikatamani nimweleze, lakini nikashindwa kutokana na wakina mama kuwepo pale, nikapanga kumweleza wakati tuna rudi nyumbani.

Naam baada ya kumaliza kupakiza mchele kwenye Taxi kobe, wakina mama waliondoka kuelekea kimara, kwenye maandalizi ya shrehe ya ubatizo, utakao fanyika usiku waleo jumamosi kwenye mkesha, ambapo sherehe yenyewe ingefanyika kesho yake jumapili ya pasaka, “chakula kipo jikoni, ni kukipasha moto tu!” alisema mama akimsisitiza kaka, wakati wanaondoka, huku wakipishana na na gari aina ya Toyota dubble cabin, (sijuwi jina jingine la gari lile) “ba! mdogo huyooooo!!!!” alipiga kelele Eva huku anatoka mbio, kulifwata lile gari na mimi nika liunga nyuma yake kuliftwa lile gari.

Sasa tukawa tuna kimbia, yeye mbele mimi nyuma, tukimwacha kaka ana tutazama kwa mshangao, ukweli nikiwa na kimbilia gari nyuma ya Eva, niliweza kuona watu waliokuwpo ndani yagari, nikweli alikuwepo baba mdogo wake wakina Eva, yani mume wa mama mdogo Irene, lakini akuwa peke yake, kulikuwa na watu wengine watatu, seat ya mbele upende wa abiria, alikaa mwanamke mmoja mzuri mzuri hivi (lakini akumfikia mamdogo), wenye uso wa tabasamu kwa wakati huo, akiwa amepakata mtoto wa kati ya miaka mitatu au minne, na seat inayo fuata nyuma yao, kulikuwa na mtoto mwingine, wa kati ya miaka kumi au kumi na moja, yani umri wake ni kama wetu mimi na Eva.

Naam wakati tuna likaribia gari lile ambalo lilikuwa lina tembea taratibu, kutokana na ubovu wa barabara, nikamwona yule mwanamke alie kaa upande wa kushoto wa bamdogo, akitutazama, kisha akamwonyesha ba mdogo wake Eva, ambae alitutazama, kidogo, kisha akatazama mbele, kama vile atujuwi, nikazania ajatuona vizuri, nazani wazo langu lilifanana na Eva, maana alikimbia mpaka kwenye ubavu wa gari, na kugonga ubavu wagari, “ba’mdogo bamdogo, mimi Eva” alipiga kelele Eva ambae akujari kuwa gari linatembea, nazani ni kutokana na utoto aliokuwa nao, lakini uwezi amini, kilicho tokea.

Ba’mdogo wake Eva ndio kwanza akannyaga mafuta kwanguvu, na kuongeza mwendo, pasipo kujari ubovu wa barabara, hapo ata mimi nilihisi jambo ambalo silo la kawaida, nikaacha kulikimbiza gari, lakini ilikuwa tofauti kwa Eva, ambae aliendelea kulikimbiza gari, huku anagonga ubavu wa gari, pasipo mafanikio, maana waliokuwa ndani ya gari awakumjari, zaidi dereva aliongeza mwendo zaidi, huku Eva akiingia korongo na kujibwaga chini, vibaya sana.

Hakika ni kumbukumbu ambayo aija wai kunitoka kichwani, maana licha ya kuona tukio lile, dereva wa gari lile Toyota Dubble Cabin, ambae ni baba yake mdogo Eva, akupunguza ata mwendo, ndio kwanza aliongeza mwendo, huku Eveline akiangua kilio na kugaa gaa pale chini, watu wote waliokuwepo pale madukani walishangaa, kwa unyama wa dereva wagari lile, baadhi ya watu waliinuka na kukimbilia tulipokuwepo.

Kaka ndie alie kuwa wakwanza kumfikia Eva pale alipokuwa anagaragara, “Popa, kwanini mnakimbilia gari kama wajinga, ona sasa kilichotokea, kwani mnamfahamu yule dereva?” aliuliza kaka Denis kwa sauti ya hasira iliyo hambatana na mcheche wakupagawa, nazani alihisi kuwa Eva ameumia sana, “baba yake mdogo” nilijibu huku naanza kuziokota pipi alizo zingusha baada ya kuanguka, “baba yake mdogo?” aliuliza kaka, kwa sauti ya mshangao, huku akimwinua Eva toka pale chini, “ata kama baba yake mdogo, ange mgonga inge kuwaje?” aliongea kaka kwa hasira,

“vipi ajaumia?” aliuliza mmoja wa watu waliofika pale tulipokuwa, na kuanza kusaidia kumkagua Eva, ambae zaidi ya michubuko ya kwenye goti na viwiko, akuwa ameumia, ilizuka minong’ono ya chini chini, ambayo kiukweli mimi sikuwa naijuwa maana yake, lakini nazani kaka alijuwa maana yake, maana nilimwona akianza kuona kiaibu flani, “ndiyo huyu yule dogo wa asubuhi” ni moja kati ya minong’ono iliosikika…

USIIKOSE SIMULIZI INAYOFUATA

Umeyaona Matangazo?
Usisahau Kunipa Sapoti kwa Kuyabonyeza ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Burudani

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni