JINI HUSNAT (13) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatano, 22 Februari 2023

JINI HUSNAT (13)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Zuberi Maruma

SEHEMU YA KUMI NA TATU
ILIPOISHIA...
"nyinyi ni nani na mnataka nini kwangu?" mganga NDUMBWE aliuliza kwa ukali!.upande wa kwa wazazi wa VERGAN walikuwa wakitetemeka kwa moyo wa kibinadamu awakupaswa wakione walichokiona!,

WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
walilala palepale chini waliporushwa bila kujitingisha wakitetemeka! ilikuwa ni kama wameambiwa walale vile.jini husnat alibaki ameduwaa!!! akujua kilichokuwa kinaendelea na mwenzake VERGAN wenyewe walikuwa nje ya ufahamu!,watumishi wawili walibaki wakitetemeka wakimwangalia kwa huruma bosi wao mganga NDUMBWE

"upaswi kutujua tunaitaji viumbe vyetu!" viumbe wale walizidi kuongea kwa sauti ya kitetemeshi!,sauti yenye mkwaruzo kama wa radi!.mganga NDUMBWE akaachia cheko! cheko la dharau! cheko la majidahi,cheko la kiburi na akafatiwa na maneno ambayo yaliwatiya hasira wale viumbe!

"nyie viumbe mlolaanika,viumbe wachafu...."

*******

"Nyie viumbe wachafu! mlolaaniwa mkalaanika naomba mfutike katika mbon4 ya macho yangu kabla sijawaangamiza!"

Viumbe vile vikazidi kukasirika midomo yao kwenye mashavu kukajaa! yamkini kulikuwa na kitu WAKAKITEMA kwa pamoja! lilikuwa ni kombora la moto ambalo liliungana pamoja na kumwendea kwa kasi mganga yule mganga akaliangalia kombora lile kwa dharau na kulionyeshea usinga wake! kombora lile likatoweka!...naye akaunyoosha mkono wake ukaanza kutema cheche mfululizo kama risasi zichomokapo katika bomba la bastola lenye bomba tatu! ukienda kwa kasi upande waliopo viumbe wale! lilikuwa ni tukio la ghafla! kimuyemuye kikazuka! madubwasha yale walijitaidi kujikinga bila mafanikio hatimaye wakatoweka! wakimwacha mganga akiwa kachoka kwa ile vita kali

"mumeona mimi hawaniwezi! mumeona mimi ni kiboko yao! mizimu ya kusini mashariki,kaskazini,magharibi yote ipo upande wangu hawaniwezi...."

mganga akaendelea kujisifu

"muchanganyiko wa damu mulokunywa imewasaidia!....mizimu imetulinda sasa tunaweza kuendelea kuwarudishia ufahamu...." aliongea mganga huku akimwangalia jini HUSNAT

"mamaa twende mama hatari ulokuwa unaiogopa imepita mamaa...."

HUSNA akamtupia tabasamu!,mwanya wake mdogo ukaonekana katika meno yake meupe! tabasamu lile ilikuwa ni tafsiri nzuri kwa mganga NDUMBWE NDUMBWELE,sasa Vergan na wazazi wake walibaki nchi kavu,woga mkuu ukiwatawala,kimbelembele cha kumfata mganga nyuma nyuma kilifutika kwenye maji waliigia wa nne mganga,JINI HUSNAT,na wasaidizi wake wawili!

kitendo cha jini yule kukanyaga maji yale ya bahari macho yake aliya angaza angani shoti zikitoka! NGUVU ZAKE ZILIKUWA ZINARUDI,nguvu zake za kijini bado mganga na wafuasi wake waliendelea kuimba,ghafla JINI HUSNAT machozi mfululizo yakaanza kumtoka machozi ya damu!!!

ilikuwa ni ishara ya maumivu tele katika moyo wake mdomo ukaanza kumtetemeka kwa hasira! mabega yakaanza kupanda juu,kilio hafifu kikasikika jini husnat alikuwa akilia,akiwalilia ndugu zake....kisasii

*******

Ilikuwa ni furaha kwa mganga NDUMBWENDUMBWELE

kufanikisha kwa kazi yake!,sasa kazi ilobakia ilikuwa ni ndogo tu kumrudishia ufahamu VERGAN,na kumtuliza husnat hasira zake,asilolijua mganga yule ni kwamba hasira za vergan haziwezi kuzuiliwa pasina kulipiza kisasi,kisasi kwa himaya yake ilousika na mauaji ya wazazi wake.kisasi kilichokuwa katikati ya moyo wake,mganga akambembeleza sana jini husnat watoke baada ya kumbembeleza sana jini husnat akatii!,wazazi wa VERGAN walimshangaa husnat baada ya kupata nguvu zake....

"asalam aleykum warahmatulah taghala wa barakat"

jini husnat aliamkia kwa kirefu huku macho yake yakiwa kwa VERGAN

"walekumussalam" wakaitika! jini husnat alikuwa ni binti mwenye heshima wazazi wa vergan walivutiwa na binti huyu! baada ya salamu mganga aliitaji kumchukua Vergan na kwenda kumzamisha baharini! lakini husnat alimkataza akamwaidi kumponya yeye mwenyewe akamwekea mkono kichwani na kumsomea baadhi ya aya za QURUAN kitabu kitakatifu! vergan akarudiwa na fahamu zake! WAKAKUMBATIANA kwa furaha!!!

wote kwa pamoja wakiwa na furaha katikati ya usiku huo wakarudi nyumbani kwa mganga wakiwa wamepona!!!

...............

MASAA MAWILI MBELE KATIKA USIKU HUO HUWO
Nyumba ya kifahari ya mganga ilikuwa ni kubwa ivyo VERGAN na mpenzi wake walipewa chumba chao na chilo na mke wake naye walipewa chumba chao,ilikuwa ni wakati wa wapenzi hawa kukumbushana enzi zao kila mmoja alikuwa na hamu na mwenzake,wakazama katika mahaba mazito...,mahaba yalopelekea kutungwa kwa mimba bila wenyewe kwa muda huo kuelewa.mwisho wa mahaba yale kutokana na uchovu VERGAN alilala usingizi mzito,hali ilikuwa ni tofauti kwa JINI HUSNAT,usingizi aukutaka kumchukua mawazo ya hasira,chuki na kisasi vikimtawala akaamka kwa lengo kuu.....

lengo la kurudi kwao ujinini usiku huo huo kwa kazi moja tu ya KULIPIZA KISASI!

hasira zake kwa sasa azikuzuilika! wakati akijiandaa kutoweka ghafla likatokea asilotegemea,lililovunja mawazo yake yote na kumuweka katika

**********

Wakati jini HUSNAT akijiandaa kwa tendo lile la kutoweka! ghafla akatokea mvulana mzuri,mvulana wa kiarabu alovaa kanzu nzuri ambayo hata HUSNA mwenyewe alibaki akiikodolea macho kwa uzuri wake,kichwani alijifunga kilemba.alipendeza aswaaa!,mkononi,mkono wa kushoto alishka tasbih,na wakulia alishka ule msahafu mdogo(quran tukufu) wenye zipu,usoni alikuwa akiwakawaka katika paji la uso wake katika (singda) nuru.

"asalam aleykum warhamattulah taghala wa barakatu!"

"waleykumussalam warhamattulah taghala wa barakat"

alisalimia kijana yule alozuka ghafla maeneo yale.naye jini HUSNAT akaitikia huku akijistiri unywele wake ulofika mgongoni kwa kujifunga ushungi.yule mkaka akatabasamu kidogo meno yake ya dhahabu yalopangwa vyema katika mdogo wake na kumuongezea uzuri yakaonekana!

"mimi ni malaika!,mjumbe wa ALLAH!,nimetumwa kwako iwe kiumbe wake,mateso makali umepata!,umepoteza wazazi wako!,na unaitaji kulipiza,mwenye kutoa HUKUMU ni ALLAH pekee na si binadamu wala nyinyi majini!....samehe ndo NUSRAT kwako jini kuolewa/kumuoa binadamu MUNGU amekataza ila amenituma kwa kuwa mmependana muda mrefu...ruksa kuoana na sasa tumboni mna kiumbe....msilimishe kijana mfunge ndoa japo itabaki kuwa siri kwa baadhi ya watu kuwa wewe si binadamu ila wengi wao watawatambua kama nyote ni binadamu na utaishi kama binadamu japo utakuwa ng nguvu zako mengine ALLAH YAGHALAM,MUNGU mjuvi wa mengi muwe na maisha mema."

malaika yule akatoweka!

hasira ya jini HUSNAT kama barafu ikatoweka ghafla vergan akashtuka kumbe ndotoni alimwona malaika yule na ujumbe ule alipotoweka naye ndo akazinduka.wakaangaliana kwa tabasamu

"nimefrah umenibebea kiumbe!"

"mmh umejuaje?!" HUSNAT kwa sauti ya kimahaba akamuoji

"nisha anza kuwa na uwezo kama wako!" Vergan alitania

"maishaaa!!!" JINI HUSNAT alimdhihaki

"uamini sasa?"

"nnachotaka usilimu!"

"ungependa niitwe jina gani?"

"ningependa uitwe OMARI"

"mh kwa nini?"

"ni jina la baba yangu"

"sawa kipenz cha moyo mama NUSRAT....."

********

"Waooh umejuaje mama yangu anaitwa NUSRAT?!"

"ni malaika alokutokea kakwambia uwasamehe viumbe wenzako ndo NUSRAT kwako basi kama mwanangu akizaliwa wa kike aitwe NUSRAT!"

"waoooh! na pia nusrat ndo jina la mama yangu! ila je akizaliwa wa kiume aitwe nani?"

"ataitwa ZULUWALAD ili tuwapunguzishe hasira majini wenzako kwa kutambua bado tunawajali"

"mh! basi sawa mume wangu tulale sasa...." wakalala wakiwa wamekumbatiana.

............

Asubuhi walipewa ruksa na mganga ndumbwendumbwele ambapo kabla awajaelekea nyumbani walielekea msikitini! ambapo JOHN VERGAN alisilimu na kuitwa OMARY,siku chache badaye kharusi kubwa ilifungwa,OMARY na HUSNAT wakaishi kwa amani,kharusi iloacha gumzo nchini TANZANIA na hata chini ya bahari ujinini wakarudi kwenye nyumba yao ya kifahari wakimsubiria kijacho......

...........

Jini mkuu MUKRAHIYA baba yake ZULUWALAD hasira zilimpanda sana aliamua sasa kwenda duniani na walinzi wake kwa lengo moja tu! kumuangamiza OMARY na JINI HUSNAT cha ajabu walipoifikia nyumba ya JINI HUSNAT walikuta bahari nyumba awakuiona walipojaribu kuisogelea waligundua maji yake yalikuwa yakichemka! wakahamua vitavyao waviamishie kazini.nako mambo yalikuwa hivyo vivyo! walipowatafuta wabaya wao katika salelaiti zao awakuona kitu zaidi ya moto! ambayo kwao ni ishara mbaya,wakaleta waganga na waganguzi hali ikawa ile ile MUNGU ni mweza wa kila kitu aliwalinda Kina omary na husnat bila wao wenyewe kujijua.majini wabaya wakaachana nao.....wakakubali kushindwa.

MWISHO

Umeyaona Matangazo?
Yabonyeze Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni