JINI HUSNAT (12) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumanne, 21 Februari 2023

JINI HUSNAT (12)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: Zuberi Maruma

SEHEMU YA KUMI NA MBILI
ILIPOISHIA...
"afande huyu kijana anajua kila kitu anaitaji milioni 50 eti ndo atueleze"

"what?"

kikoti alistaajabu akaendelea

"afande marwa piga pingu ilo likaeleze kila kitu kituoni sijapata kuona jambaz jinga namna hii"

WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
machozi yakatiririka katika mashavu yake! akajiona mjinga kuwaza ujinga.akabebwa mzobe zobe mpaka kituoni aliposhushwa na kuanziwa mahojiano muda huo huo

"unaitwa nani"

"alex"

"majina yako matatu" kikoti alizidi kumuoji

"ALEX BANDAMA KINAINAI"

"kah" afande alistaajabu!

"unafanya kazi wapi?"

"vergan compuny!" kah kwa hiyo ndo umeshiriki kumteka bosi wenu? (hapana afande mi sijashiriki!) haya tueleze waloshiriki upate kuwa huru! (siwajui) alijibu MWANDISHI huku akilia...afande kikoti akusema kitu akaondoka aliporudi alikuwa na mkebe akaufungua kulikuwa na plaizi mikasi spoku na vifaa ambavyo akuweza kuvitambua kwa haraka! (ntaanza kwa kukuchomoa kucha moja moja mpaka utakapoeleza wanaousika kwa kupotea kwa vergan) MWANDISHI mdogo ulimtetemeka akutaka kuwa katika maumivu akaamua kuueleza ukweli! ukweli ambao katu aukuwaingia maafande akilini! (anayeusika katika upotevu wa vergan jini)

***********

Mwandishi hakuwa tayari kungofolewa kucha zake akaamua kusema ukweli! ukweli ambao aukuwaingia akilini kabisa polisi wale!

"vergan kachukuliwa na jini?"

"what?" kikoti na maafande wengine wakatazamana.kilichofatia ni kumvurumishia kipigo mangumi mateke,bila kujali damu ilokuwa ikimtoka! ila msimamo wake ukabaki palepale....serikali haikuamini mambo hayo ivyo kulionekana kuna kitu anaficha!

............

"nimeshakwambia mme wangu! yule si mtoto mdogo kusema maneno yale lazima twende kwa mganga tuka angalie huku polisi wakiendelea na msako"

MAMA VERGAN alikuwa ni miongoni mwa wazazi waliosikilizwa na wanaume zao,yani wao ndo walikuwa kichwa cha nyumba.mzee CHILO kila alichoambiwa na mke wake akuweza kuweka mkatao ilikuwa lazima akubali leo hii alimfikishia habari mke wake juu ya yanayoendelea kituoni kule,mke wake akamjia juu na kumlazimisha waende kwa mganga.chilo akukataa wakafunga safari na kuelekea kwa mganga maarufu sana kwa majini

................

KWA MGANGA

Ilikuwa ni nyumba nzuri ambayo usingeweza kuamini kama kuna mganga wa asili ndani ya nyumba hiyo ilikuwa ni nyumba ya kisasa yenye bati la vigae geti nje na hata mlinzi alikwepo.walipaki gari lao sehemu palipostaili wakatoka walipokelewa na watu wengi walokuwa wakisubiria huduma.walienda kizamu zamu mpaka zamu yao ikafika wakaingia: ilikuwa ni chumba kidogo ambacho mlangoni kwa ndani kilichomekwa fuvu la kichwa.aijulikani ni la kiumbe gani chini kulitundikwa jamvi na mganga yule aliketi akiwa kavaa nguo nyekundu pia chumba kile kilipigwa rangi nyekundu mpaka mapazia yalikuwa mekundu! "ibana iyanyeeee,ivyuna kyaleeee aaaah haaaaa haaaaa"

"ndiwaona mwaja(nawaona mnakuja)"

"ivua rwandu(vueni viatu)"

Mkalimani akawa anafanya kazi ya kuwatafsiria! mganga akachukua mbegu flani akazinuizia akazipiga chini mbegu zile zikatoweka akatoa kicheko na kuanza kuimba

rudi inyumenyume:(rudini kinyume nyume)" wakatii wakaketi chini mganga akapandisha maruani akaongea vitu visivyoeleweka mkalimani akatafsiri

********

Mganga akaachia cheko tena! na kuongea lugha isiyoeleweka!

"babu tumekuja na sh..."

mama VERGAN kabla ajamalizia tumekuja na shida akakatizwa."najua! najua! hahahaaaa najua kilichowaleta! ni vita kali binadamu mna roho mbaya sana!" wote wakashtuka!

"mimi ndo mganga NDUMBWENDUMBWELE najua mmekuja kwa shida ya kupotea kwa mwanenu VERGAN"

Mzee chilo na mke wake wakaangaliana kwa mustaajabu mkuu

"ndiy,..o....ba.bu"

"sema tawile!" mkalimani akamsahihisha

"tawile" wote wakajibu

"mumefanya vibaya sana! mwandishi kawaokoa kwa kuwaeleza ukweli mahali alipo mtoto wenu maisha yake yalikuwa hatarini kama jini yule angekuwa huru ivyo yapaswa mumuachie huru kwa kuwa kama si yeye msingepata akili ya kuja huku mumpe hela anayotaka kama mnayo...."

"tawile babu" wakaitika pamoja huku mzee chilo akiwaza yake kichwani.

"huyu mzee nuksi ndo maana mi siwaaminigi milioni 50..."

"usiniwazie vibaya mzee leo utatuamini tazama tv asilia tazama uone mahali alipo mwanenu tazamaaaaaaa"

Mzee CHILO alista ajabu kwa mawili kwanza uwezo wa yule mzee kusoma mawazo.akakaza macho yake katika kitambaa cheupe kutazama.

ghafla kama sinema katika kitambaa kile kukatokea picha.picha ilo onekana MKUTANO ULE wa hukumu ya jini HUSNAT na VERGAN

"mnaona? ila mmewai mimi ni mganga ndumbwendumbwele na uwezo wa kuwazuia na kuwaleta duniani hahahahaha ndumbwendumbwele! ashindw na kitu ni Uwezo MUNGU alonipa"

wakati kule jini maiti akinyanyua upanga wake huku NDUMBWENDUMBWELE alifanya mazingaumbwe sura ya jini maiti ikaivaa sura ya VERGAN.jini maiti akajiona na kusitisha zoezi lake

"ha ha ha ha ha mmewah mwanenu mngempoteza."

wazazi wale wawili walichoka.mganga akaanza kuimba akamchukua paka mweusi aloletewa na mfanyakaz wake akamchinja akamfyonza damu.ghafla akatoweka.alipo rudi wakarudi watatu JINI HUSNAT,VERGAN na NDUMBWE NDUMBWELE.PATASHIKA

"hawa wanapendana yapaswa waishi pamoja humu duniani kwa sababu huyu msichana atakiwi kwao tena.hahahaha" mganga yule aliongea huku akijitaidi kuwapatia ufa

********

Mganga alokuwa kiboko ya majini ukanda wote wa africa mashariki NDUMBWENDUMBWELE aliendelea na jitihada za kujaribu kurudisha fahamu za wateja wake ambao ni JINI HUSNAT na VERGAN kwa kuwamwagia maji ya bahari! ila hakukuwa na mabadiliko yeyote akagundua kitu ambacho akupenda akigundue lakini ndo ivyo alishakigundua KAZI ILIKUWA NI NGUMU ZAIDI YA ALIVYOTEGEMEA ilibidi/ilimlazimu hatumie "plan b" plani ambayo ilikuwa ni hatari kwa maisha yao kiujumla! njia ya kwenda kuwazamisha kabisa baharini! njia ambayo pia ingezirudisha nguvu za HUSNAT ambazo zingekuwa ni hatari! baada ya kuwaeleza hivyo wazazi wa VERGAN wakakubali waungane pamoja usiku huo kwenda baharini walimpenda sana mtoto wao WANGEJUA?!

.............

KATIKATI YA USIKU

UFUKWENI MWA BAHARI:

Hali ya hewa ilikuwa niya utulivu!,upepo mwanana ulipepea na kuleta ka upepo ka tamu kwa kubarizi!,mawimbi ya maji yalipiga taratibu na kuongeza ualisia wa ufukwe huo.eneo ilo la ufukwe katika usiku huo mnene lilitawaliwa na giza,giza ilo lilifanya kutisha kwa mandhari ya eneo hilo ila mtisho huo aukuwatisha viumbe saba walokuwa pembezoni mwa bahari wakifanya kilichowaleta.katika eneo hilo akukuwa na kiumbe kingine zaidi yao si wavuvi wala wanyama!,si ndege wala wadudu viumbe wale wote walijifunga kaniki nyeusi tiii! na walijichora usoni na mikaa walikuwa ni mganga

ndumbwendumbwele,alokuwa na hirizi kubwa ilokuwa ikipumua kifuani kwake akiivaa kama cheni shingoni,kichwani alijifunga kitambaa chekundu mkononi alishika usinga,pembeni yake walikwepo vijana wawili ambao mmoja alimshika njiwa mweusi tiii asiye na doa,mwingine alimshika paka mweusi mwenye macho ya njano alokuwa akilia muda wote.mama VERGAN alikuwa kashika kibuyu na kisu kikali na panga,mume wake alikuwa kashika nazi!,na mayai jini HUSNAT na VERGAN wenyewe awakushika kitu walibaki wamenata vilevile kama masanamu wakishangaa eneo moja palepale ufukweni vijana wale wakamchinja yule paka na damu yake wakaimimina katika kile kibuyu alichokishika mam

*********

Wakamchinja paka yule ambapo damu yake waliimimina katika kile kibuyu alichoshika mama vergan.walipomaliza wakamchinja na yule njiwa damu yake wakaichanganya na ya paka katika kile kibuyu wote wakachovya kidogo na kujipaka usoni,wakanywa na nyingine wakamwaga eneo la ardhi,baada ya kumaliza mganga NDUMBWENDUMBWELE akachukua maziwa na kufanya vilevile! wakanywa machache mengine akayamwaga palepale alipoimwaga damu.akachukua kisu na kujikata damu akaimiminia sehemu moja wote wakafatisha kwa zamu baada ya kumaliza kila mmoja kutoa damu yake kila mmoja akaonja ilobakia wakaimwaga palepale kama una moyo mwepesi usingeweza kunywa vile! ila wote walikuwa tayari! tayari kwa chochote MAAJABU!

cha ajabu zaidi pale walipojikata awakusikia maumivu yoyote wala jeraha! kaaah! huyo ndo alikuwa NDUMBWENDUMBWELE kiboko ya majini! baada ya kumwaga damu ile chini palepale alipomwaga damu,maziwa ghafla vikatoweka FADHAIKO

mganga akaachia cheko moja ishara ya ushindi

"ha! ha! ha! mizimu imekubali sadaka yetu sasa ni zamu ya kuwazamisha majini yani kama kuwabatiza jini HUSNAT akigusa maji ya kwao tu atarudiwa na fahamu! zake pamoja na nguvu zake alizonyanganywa na mfalme wake MUKRAHIYA ila VERGAN mpaka azamishwe kabisa katikati ya kina kirefu ivyo tutaanza na HUSNAT kama likitokea la kutokea awe msaada kwetu!"

"tawile babu" wote wakaitikia.

"mtanifata nyumanyuma"

aliongea mganga NDUMBWE akimvuta jini husnat!,jini yule akagoma! KIZAAZAA!

akamlazimisha lakini husnat hakuwa tayari! ni ishara mbaya,ni ishara ambayo kama angeijua asingemlazimisha ila usilolijua ni sawa na usiku wa giza.machoni mwa jini yule machozi yakaanza kumtiririka! machozi ya damu MAAJABU!

Tayari alishaiona hatari ilokuwa mbele yao.laiti kama wangegusa maji yale.mganga akujua yeye baada ya kuona husna anakataa! akachukua dawa flani na kumwagia husna KOSA!

husna akawa kama tahira akamtii mganga akamfata nyuma wakayasogelea maji katu mganga akujua hatari ilokuwa mbele yake na laiti kama angeijua!

********

Katu mganga akujua hatari ilokuwa mbele yao na laiti kama angelijua! wangelifata kile HUSNAT alichotaka lakini kila kiumbe MUNGU alikibarikia uwezo wake binafsi! wakasogea taratibu eneo lile la maji ile wanataka kuyakanyaga maji ukatokea mlipuko ulowarusha wote nyuma kwa ghafla muda huo huo hali ya hewa ikaanza kubadilika! ghafla! viumbe viwili virefu visivyo onekana mwisho wao miguuni wakiwa na kwato vikatoke KIMBEMBE!

Mganga ndumbwendumbwele akasimama akiwa tayari kwa lolote! viumbe vile taratibu vikaanza kufupika! vilikuwa ni viumbe vilivyotisha kichwani walikuwa na pembe mbili zilizochongoka!,kila kiumbe kilijaliwa jicho moja kubwa katikati ya paji la uso,jicho jekunduuu,lililowakawaka na lililotisha kwa aliangaliaye! walikuwa na meno mawili marefu yalochomoza nje ya kingo ya midomo yao,katika paji la uso juu ya jicho walikuwa na herufi 666,mikononi walikuwa na kucha ndefu zilizochongoka!,walicheka! kicheko icho kikawa ni maumivu kwa binadamu wale kasoro mganga na HUSNAT kwa sauti ya kukwaruza na yenye kitetemeshi wakasema:

"binadamu! mumeingia katika vita binadamu!!!" kila walipo ongea sauti ilijirudia mara mbili kama mwangwi.

"nyinyi ni nani na mnataka nini kwangu?" mganga NDUMBWE aliuliza kwa ukali!.upande wa kwa wazazi wa VERGAN walikuwa wakitetemeka kwa moyo wa kibinadamu awakupaswa wakione walichokiona!,

USIIKOSE SIMULIZI INAYOFUATA

Umeyaona Matangazo?
Yabonyeze Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni