KUTI KAVU (10) Jina: KUTI KAVU Mwandishi: Changas Mwangalela SEHEMU YA KUMI ILIPOISHIA... Balaa ambalo kwa jinsi anavyowajua wazazi wake lilikuwa limewazid uwezo mara sabini. Doi alimjua fika baba yake mzee Vioja, mzee aliyeogopa mahakama kuliko njaa! Mtu wa namna hii ni vipi angeweza kumpigania? Alipoyafikilia hayo matumaini yake kuiepa jela yakazidi kupungua nukta baada nukta WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI 👉GUSA HAPA👈 SASA ENDELEA... Baada ya Mudi kuondoka kutoka katika nyumba ambayo alimfumania mkewe mtarajiwa Zainabu Mpotoshi na kuwaacha Mapunda na Zai wakiwa katika hali ya sintofahamu. Mudi aliondoka akiwa na msongo wa mawazo huku akiwaraani kabisa wanawake wote kwa sababu ya kile alichofanya Zai. Aipofika tu nyumbani kwake, kwanza alihakikisha amemwona bi Udaku mtonyaji wake, ambaye kwa msaada wake ameweza kuyagundua madhambi ya Zai akamshukuru. Lich…