KUTI KAVU (11) Jina: KUTI KAVU Mwandishi: Changas Mwangalela SEHEMU YA KUMI NA MOJA ILIPOISHIA... Alijiinua kutoka katika mkao wake ule, na safari hii alijiegemeza kwenye mgongo wa kiti halafu akaendelea, “…. Ilikuwa ni wakati ambao nilikuwa mahakama ya mwanzo ya Temeke kwenye mafunzo kwa vitendo. Mara tu baada ya shughuli za mahakama kuisha, nilielekea kwenye kituo cha daladala tayari kuelekea nyumbani kwa mapumziko. WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI 👉GUSA HAPA👈 SASA ENDELEA... Watu walikuwa ni wengi sana kituoni na kusababisha kila gari lilokuja pale kuonekana lulu machoni pa wasafiri kwa sababu ya mahitaji yao ya huduma ya usafiri. Yalikuja magari kadhaa kituoni, lakini yote yalikuwa yamejaa kiasi cha kutokuwa hata na nafasi ya kusimamisha abiria ndani yake. Nilikaa pale kituoni nikiendelea kusubiri gari lenye nafasi angalau ya kusimama ili niwahi nyumban…