KUTI KAVU (12) Jina: KUTI KAVU Mwandishi: Changas Mwangalela SEHEMU YA KUMI NA MBILI ILIPOISHIA... Sikutaka kuruhusu ukimya ule ushike hatamu kati yetu. Hivyo baada ya yeye kuwa kimya niliamua kumuuliza, “Samahani Doi, tunaweza kuonana kabla wiki hii haijaisha?” “Tunaweza. Lakini iwe weekend,” “Haina shida, nadhani Jumamosi itakuwa ni siku nzuri” Tulikubaliana kuwa tuonane siku ya Jumamosi, tukapanga mahali na muda. Hiyo ikawa ni siku ya pili. WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI 👉GUSA HAPA👈 SASA ENDELEA... Siku ya Jumamosi ilifika. Niliamua kuelekea maeneo ya fukwe za Coco saa moja kabla ya muda wa miadi ambao tulikuwa tumekubaliana na Doi haujafika. Lengo la kuwahi eneo lile lilikua ni kwa ajili ya kuandaa sehemu nzuri katika ufukwe ule, ili tuwe na faragha katika mazungumzo yetu. Sababu nyingine ilikuwa ni kuepuka uswahili wa kutokulinda muda, hasa zaidi ukizin…