KUTI KAVU (15) Jina: KUTI KAVU Mwandishi: Changas Mwangalela SEHEMU YA KUMI NA TANO ILIPOISHIA... Inaniuma sana kukuandikia haya ila sina budi mpenzi…” hakuendelea kusoma zaidi kwa sababu ya machozi yalyoanza kumtoka. Aliikunjakunja ile barua kisha akaicoma moto ili kuifuta kumbukumbu ya barua hiyo iliyokuwa ikimwumiza. WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI 👉GUSA HAPA👈 SASA ENDELEA... Miezi mitatu baadaye Domi alimtembelea Doi gerezani. Uwepo wake gerezani kwa siku hiyo uliibua faraja mpya kwa Doi. Faraja ambayo aliishuhudia ikififia kwenye siku ile ambayo kesi yake ilihitimishwa kwa hakimu kumsomea hukumu yake ya kifungo cha miaka mitano jela kwa mujibu wa sheria. Ni kipi alichohitaji tena zaidi ya faraja, hasa katika wakati mgumu kama huu, wakati ambao alikuwa anakitumikia kifungo chake! Ndiyo, alikuwa anahitaji faraja lakini si kutoka kwa Domi. Kwa Doi, Domi n…