KUTI KAVU (3) Jina: KUTI KAVU Mwandishi: Changas Mwangalela SEHEMU YA TATU ILIPOISHIA... Njiani Dominic aliendesha gari kwa kasi, kwa nia na madhumuni ya kuwahi nyumbani na kumpasha mapenzi wake kuwa; matatizo yote yaliyokuwa yakisababishwa na ukosefu wa pesa sasa yametamatishwa, baada ya yeye, yaani Dominic kupata kazi katika kampuni ya mawakili ya KWITALE ADVOCATES & COMPANY. WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI 👉GUSA HAPA👈 SASA ENDELEA... Punde si punde Dominic alikuwa nyumbani, Domi alishuka kwenye gari kwa haraka akaanza kukimbia kuueleka mlango wa nyumba, huku moyoni akiwaza namna Doi atakavyofurahi baada ya kuwa amempasha juu ya habari hizi njema. Kinyume na matajio yake Domi alikutana na kufuli kubwa lililokuwa likining’inia mlangoni. Mapigo ya moyo wake yakabadirika ghafla na furaha yake ikatumbukiwa nyongo. Mambo yamekwenda kinyume kabisa na jinsi…