KUTI KAVU (5) Jina: KUTI KAVU Mwandishi: Changas Mwangalela SEHEMU YA TANO ILIPOISHIA... Siku hiyo alikuwa na pesa kiasi mfukoni mwake, akaamua kuja kupata chakula katika mgahawa wa SAVANA LOUNGE . Ni katika jengo hilohilo ndiyo Damian na Doi walichukua chumba tangu siku iliyopita. WAKATI UNAFUNGUA KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE WALAU KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA KAMA UPO NJE YA APP INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KWA WAKATI 👉GUSA HAPA👈 SASA ENDELEA... Domi aliingia katika mgahwa huo wa SAVANAH ambao uko ghorofa ya tatu, na Damian na Doi walichukua chumba ghorofa 18 katika jengo hilohilo. Baada ya kuegesha gari lake Domi aliingia mgahawani na kukaa kwenye meza ya pembeni, meza ambayo ilimpa uhuru wa kuona karibu kila pembe ya ukumbi wa mgahawa ule wa SAVANAH, meza ambayo Domi aliiona kuwa inamfaa zaidi. Domi aliagiza chakula na kutulia kwenye meza hiyo huku akila polepole. *** “Damian..” Sauti ya Doi ilisikika ikiita. Damian aliyekuwa anatazamana uso kwa uso na Doi aliitik…