MUUZA CHIPS (11) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumamosi, 20 Mei 2023

MUUZA CHIPS (11)

Je unajua kwamba Simulizi zote unazozipata hapa zipo kwenye app ya CnZ Media?

Humo Pia Utakuta:
๐Ÿ“– KUSOMA SIMULIZI
๐ŸŽฌ FILAMU na TAMTHILIA za KITANZANIA
๐Ÿ˜‚ VIDEO za KUCHEKESHA
๐Ÿ“‘ MAKALA za AFYA na MAPENZI

Install app hii GUSA HAPA utavipata vyote hivyo bure kabisa
Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA KUMI NA MOJA
ILIPOISHIA...
"chidi jamani, mi naondoka eti huna la kuniambia"

Chidi bado alikuwa mzito kujua ishu inayomfanya sarah aage age kila mara,

"sarah, we nenda tu, kama ni pesa tunayo wala usijali"

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Sarah alichoka na kuaga kamwisho mwisho

"sawa… Naenda,..but chidi niambie basi niondoke au?"

Kaka wa chidi aliondoka hapo chumbani, na kuwaacha chidi na sarah wakiwa wenyewe, Sarah alifurahi sana kwa kitendo cha ibra kutoka, baada ya kupigiwa simu na mtu tusiemjua, na aliondoka kwa haraka sana kana kwamba aliompigia ni mtu anaemheshim sana,

Sasa baada ya Ibrahim kuondoka, huku nyuma sarah alianza kuaga mara mbili mbili na yote hayo ni ili tu chidi ajue sababu ya kuagwa huko, lakini chidi hakuwa akifahamu chochote kile kilichokuwa kikimaanishwa na sarah, sarah alishampenda kijana chidi hata kama ni masikini lakini kapenda,… Sarah alionyesha dalili zote za kumtega kijana chidi lakini chidi waapi hajui kitu,…

"sawa…. Naenda… But chidi niambie basi niondoke au?"

Sasa chidi hapo ndio kidoogo skio na akili vikafunguka, kuwa sarah alikuwa akionyesha upendo wa dhati kwake..

"sarah, naomba uende tu, coz now mi ni mgonjwa, na hakuna chochote nitakachofanya"

Sarah aliposikia hivyo alitabasamu na kujisemea kuwa

"tayari keshajua dhamira yangu, safi sana"

Alijiongelea mwenyewe huku akitabasamu tu

"sawa basi, ugua pole"

"asante"

Sarah aliondoka zake na kumuacha chidi pale ndani,

Tukija huku kwa Ibrahim tunamwona anaingia katika nyumba moja na kukutana na mwanamke mmoja hatujui ni nani wake,

"kwanini leo umenifanyia hivi ibra"

Aliingea huyo mwanamke huku kama akilishika tumbo lake, kana kwamba mdada huyo ana mimba..

"nimekufanyia nini jamani"

"nimeshinda njaa, na bora ningelishinda peke yangu afadhali, sasa nimeshinda njaa na mtoto wangu"

"lakini Rehema mpenzi wangu… Kwanini unashindwa kuibajeti elfu 30 uitumie hata siku tatu"

"we mshenzi, nini yaan elfu 30 niitumie siku tatu, kwa umaskini gani au wataka mtoto wako atoke na kibiongo"

"hapana mke mpenzi wangu sio hivyo"

"hata niachie ya jioni uende zako"

"sawa"

Ibrahim alionekana kuoelekeshwa na mwanamke huyo, huku akiitoa waleti ya pesa..

"hapa nimebakiwa na elfu 40 tu, chukuwa elfu 20 hii"

"elfu 20…..yaani badala unipe yote tena hata yenyewe bado haijatimia afu unaniambia mambo ya elfu 20.."

"Rehema mpenzi wangu,.. Nina mgonjwa mimi, hata banda leo sijafungua kwasababu ya mdogo wangu, mdogo wangu anaumwa hivyo nikikupa yote, nitamuuguza na nini"

"nyooooooooo, kwaio mimi na mdogo wako nani wa maana"

"aaahhh wote ni wa maana kwangu"

"sema kimoja mimi na mdogo wako nani wa maana"

"ok.. Tufanye ni wewe tu"

"haya nipe hio elfu 40 yote na uondoke, au unataka niitoe hii mimba"

"hapana mpenzi wangu… Wewe ni mke wangu mtarajiwa na ni mama wa wayoto wangu"

Tukija huku kwa akina sarah, ndio anaingia nyumbani kwao na kukutana na mama mmoja hapo nyumbani kwao,..

"we sarah mwanangu unatoka wapi saa hizi"

"mama… Bila hata kusalimiana jamani"

"aalamu ya nini pumbavu wewe,.. Acha hizo tabia zako mama miriam atakuchukia, mbona mtoto wake yupo ndani lakini wewe kiguu na njia"

"mama, nisamee basi sirudii tena"

"alafu naskia kuna jambazi unae wewe"

"jambazi??…. Jambazi gani hilo"

"miriam kaniambia wewe una jambazi wewe"

"mama… Miri kakudanganya tu"

"sasa ole wako… Niskie tena….. Mi naenda nyumbani"

Sasa hapa ndio tunajua kuwa miriam na sarah hawakuwa ndugu, na inaonekana ukaribu wa mama zao ndio uliowafanya na watoto wao kiwa karibu,… Ila sarah ni rafiki na miriam wanaoishi kama ndugu wa damu mana kila mahala wapo wote, na ndio kama hivi sarah yupo na miriam na anarudi kama nyumbani kwao kwa jinsi wanavyopendana…

Mama alipanda gari yake na kuondoka, kisha sarah akapaki gari vizuri na kuingia ndani,… Kwa jinsi ilivyo. Ni kwamba nyumba hii ni ya akina miriam, Hivyo sarah anakuja kama kwa rafiki yake tu..

Miriam akiwa chumbani kwao akiangalia tv huku sarah ndio anaingia chumbani kwao,

"eeee mama jambazi huyooo karibu"

"yaani miri we mbea… Yan umemwambia mama mimi nina jambazi"

"sasa kwani.. Si ulisema mwenyewe ulimkuta kachubuka uso sjui nini,.. Sasa huyo si jambazi huyo kaiba huko kakoswa koswa kuuwawa ndio ukakutana nalo huko"

"nyooooo Eti jambazi"

"tuyaache ayo… Vp kazi uko"

"aahhhh fresh tu,… Heee we BBA kwani tayari"

"sasa we huoni ni saa ngapi now"

Sarah alishangaa kuona kipindi cha BBA kimeanza kurushwa kwani hua kautega muda wa kuanza kipindi hicho ila leo kachelewa na kukuta kimeshaanza..

"jambazi kakuchelewesha eeee?"

"lakini miri, kwani jambazi si langu, ni lako"

"mmmhhh sawa, ila siku akikuibia usilie na wala usilaumu"

"wala hana asili ya wizi kwa taarifa yako"

"sasa mbona ulimkuta kachubuka uso"

"je kama alidondoka je"

"mmmhhhh Haya bwana mama jambazi"

"yaani unanikera kuniita mama jambazi"

Basi ilikuwa ni utani wao na wala hawakuwa wakigombana kama mnavyohisi, Wanaongea kwa utani tu mana ni marafiki walioshibana toka utotoni mpaka wakasoma wote, na wakasoma chuo wote, na wakamaliza wote na sasa wapo wote…

Tukirudi huku kwa Ibrahim na mke wake mtarajiwa, Ibrahim aliweza kumpa ile pesa yote mke huyo na kumuona mke huyo ni kila kitu katika maisha yake,..

"hapa sasa tunaenda sawa, ila sipendi unishindishe njaa bwana"

Aliingea mkewe huyo huku akishika tumbo, na mimba yenyewe labda ndio ilikuwa inaanza lakini mtoto wa kike alikuwa kiburi sana, utafikiri mimba ina miezi nane, kumbe ndio kwanza hata kuonekana bado,..

"nakupenda sana mke wangu"

Ibrahim alimtukuza kuwa ni mke wake, lakini kwa muonekano wa hii hali, Kiukweli hafai kuwa mke maana kwa mwanamke anaeweza kutumia elfu 30 kwa siku ndani ya maisha haya ya sasa, Kiukweli hafai kuoa.. Lamini Ibrahim hakulijua hilo na kumuona kama halua,..

"vp nikupikie nini"

"aahhh wala usijali nitakwenda kupika nyumbani"

"afu mume wangu? Unajua juzi nilisahau tu"

"usisahau nini tena Rehema"

"sasa mbona kama una hasira"

"haya ok, sema"

"Juzi, baba mwenye nyumba kaja"

Ibrahim kuskia hivyo alishika kichwa huku kama akichanganyikiwa, mana nyumba anayoishi huyu mwanamke ni nyumba ya gharama sana, kwani kapangisha upande wa nyumba wenye vyumba vitatu, choo humo humo na bafu lake,…

"nini tena mbona kama umekunja sura hivyo"

"mke wangu,… Nafikiria hio laki nne na nusu nitainyea wapi saa hizi"

"ibra mume wangu, ina maana na biashara yako ya CHIPSI utakosa lakini nne na nusu kweli"

"ivi lakini unadhani ni elfu 40 ee, wacha mchezo na hio pesa Rehema"

"ok.. We fanya ufanyalo lakini sitaki kugongewa milango kila siku, we kaba iba pokonya, ulipe kodi ya watu"

Ibra aliondoka huku kichwa kinamuuma na kutamani hata akaibe kwenye miduka ya watu,..

Kiukweli Ibrahim anapelekeshwa sana na huyu mwanamke, na sijui ni kwanini au labda mwanamke keshafanya yake au ni uzumbukuku tu wa kijana ibra…

Ibrahim anafika nyumbani hakuwa na raha hata kidogo,

"chidi.."

"naam Kaka"

"nilitaka ukae nyumbani wiki nzima, ili upone vizuri, lakini naona mambo yamekuwa taiti sana hivyo, kesho Twende ukaanze kazi ili mimi niende kwenye lile banda jipya"

Ibrahim alimwambia ndugu yake kuwa kesho akamuache kwenye banda la CHIPSI la sasa hivi afu yeye akaendelee na banda jipya, ambalo ni la chipsi kama hilo hilo

Chidi hakuwa na pingamizi lolote lile alikubali na, kesho yake wakatoka saa 11 asubuhi kwa ajili ya maandalizi, chidi alikuwa bado anaumwa lakini atafanyeje kwasababu kaambiwa na kaka yake na hawezi kumpinga, Chidi anaelekezwa kazi na kaka yake ili kaka aangalie ustarabu mwingine,… Ibrahim alijitahidi sana mpaka kufikia hatua ya kufungua kibanda kingine cha chipsi,…

BAADA YA WIKI MOJA KUISHA

Wiki moja baadae chidi alikuwa tayari keshapona, na licha ya kupona pia keshakuwa mpishi mzuri wa chipsi, na hapo alikuwepo peke yake na kaka yake anaendelea na kibanda kingine,… Chidi akiwa bize na kazi yake,.. Alikuja mwanafunzi mmoja wa kidato cha tatu, ila alionekana kuwa mpole sana kwa kijana chidi,..

"mambo"

Alisalimia huyo mwanafunzi, huku akionyesha kutokuwa na pesa, lakini chidi na kaka yake walikuwa watu wa huruma sana, kwani kuomuona tu yule mschana alihisi atakuwa na tatizo..

"poa mzima wewe"

"safi tu"

Mtoto wa kike alikuwa ni mpole mno, ikiwa ni majira ya saa 6 hivi mchana,..

Ghafla wanakuja na wengine lakini wao walikuwa wamechangamka kiasi flani,

"we muuza chipsi mambo"

"poa nambieni sasa"

"safi tu… Iv yule mbaba mwingine yuko wapi"

"aaaahhh yule yupo mjini kati uko"

"ok, ebu tupimie chips za elfu mbili"

"sawa… "

Chidi aliingia katika mchakato mwingine huku akimsahau yule wa mwanzo,

"kakaa, nahisi njaa"

Chidi alimwangalia sana yule binti na asimpatie jibu, lakini kwakuwa walikuwa ni watu wa huruma, hakumbeza wala kumwangalia kwa dharau,…

"kwaio watakaje"

Sasa kabla hajajibu, wale wengine wakadakia juu kwa juu

"bwana tupimie achana na huyo, utafikiri hana wazazi, kila siku ni kuomba tu"

Kauli ile ilimkarahisha sana kijana chidi, na kuhisi kuwa mbona kama walikuwa wakimnyanyapaa mschana huyo ambae alionekana kuikosa pesa ya kununulia chipsi,…

"we kaka vp, au ushampenda nini, si ukamtolee mahari umuoe kabisa"

Sasa chidi ameshakuwa bingwa wa kupika chipsi, tena ni mwepesi haswa na hana wasiwasi tena, na kafundishwa ndani ya wiki mbili tu, Na sasa kaachiwa kibanda yeye peke yake kama alivyokuwa kaka yake, Kazi hio ina kero yake na pia ina raha yake kwa wale wanaoijua zaidi,.. Kibanda hicho kipo jirani sana na shule ya sekondari hivyo asilimia kubwa wanafunzi ndio wanaomaliza chipsi hizo, si unajua watoto wa mjini walivyo…

Chidi akiwa katika majukumu yake ya kikazi walitokea wanafunzi kadhaa akiwemo mmoja aliekuwa mtaratibu kiasi,

Wanafunzi hao waliagiza chipsi kwa kipato walichonacho wao,

Lakini wasichana wale walianza kumkebei yule mschana ambae hakuwa mpole kiasi kwa kuona kuwa anakosa fedha za kununulia chipsi, na ni mwanafunzi mwenzao lakini si unajua mambo ya shule yalivyo,… Kijana chidi alikuwa kimya na hakuwa na lakuingea ilibidi afate yake yaliomleta mjini,…. Wasichana wale walikuwa wana dharau kiasi kwa kumuona mwenzao hana kitu, wanafunzi kwa kutambiana ndio zao,..

"we kaka vipi, au ushampenda nini, si ukamtolee mahari umuoe kabisa"

"ok.. Samahani kwa kukuchelewesha"

Chidi alikuwa yupo tayari kwa kudharauliwa ilimradi tu aingize kipato katika biashara yake,

Chidi aliwatengea wateja wake kile wakitakacho na kumfuata yule mschana mwingine ambae alikuwa mpoole haswa,

"Enhe, Eti ulikuwa unasemaje mana wale wenzio walikuwa wanasumbua tu"

Chidi aliongea hivyo huku akimuangalia binti huyo,..

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni