Mwandishi: MoonBoy
SEHEMU YA AROBAINI
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Hivyo mwanamke akatoa kauli ya kutaka mawifi na mashemeji waje waishi katika nyumba hio, mana ni jumba haswa, jumba lina rosheni mbili kwenda juu hivyo kwa watu wachache kuishi humo ni tabu,… Baada ya kuafikiana swala la kuwaleta ndugu wa mumewe basi wakwanza kumjulisha ni kijana chidi, ambae yupo huki huku mjini lakini wao wanajua yupo kijijini,..
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI
SASA ENDELEA...
Ibrahim aliongea na ndugu yake huyo lakini hawakuelewana vizuri kutokana na matatizo yaliotokea kipindi cha nyuma,..
Baada ya Ibrahim kushindwa kuelewana na ndugu yake huyo ilibidi namba ampatie mkewe ili ajaribu kuongea nae, lakini chidi alikuwa kichwa ngumu pale aliposikia kuwa aliokuwa akipiga ni mke wa Ibrahim na kujuwa kuwa huyo ndio yule yule rehema wa mwanzo aliomtesaga kaka yake,… Chidi bila aibu aliporomosha mitusi ya hali ya juu mno
"nani? Rehema?… Ivi mpaka leo bado unaendelea na kaka yangu wewe,.. Na ile mimba ulizaa sasa? We bwege si nakuuliza mbwa wewe, mwanaharamu wewe umemganda kaka yangu mpaka leo huna hata haya, nyooooo… Ebu kata simu huko, bwege wewe"
Aliongea kijana chidi huku mpaka anatetemeka,.. Lakini mwanamke huyo kwakuwa alikuwa ana shida sana ya kuishi na familia ya mume wake, hivyo bado alikuwa mpole juu ya chidi…
"Nisamehe, mimi sio rehema"
Aliongea dada huyo baada ya kuelewa kuwa kumbe matusi yote hayo hayakuwa yakimhusu hata kidogo, mana yeye sie rehema kama alivyosema kijana chidi,
Sasa chidi kuskia kuwa yeye sio rehema, ikabidi na chidi nae awe mpole kama maji ya mtu huku akiwa anatetemeka kwa hasira, yaani akiskia neno rehema, hua akili yake inavurugika mno,…
"samahani shrm kwa kukusumbua,.. Kwanza mimi naitwa zai, na wewe nakujua unaitwa rashidi, na namba yako nimepewa na kaka yako Ibrahim ambae ni mume wangu"
Aliongea mdada huyo huku akiwa anaogopa kusema pointi iliyomfanya apige simu…
"ok, nami naomba unisamehe dada angu sikujua kama ni wewe, mana najua mke wake wa mwanzo sikumpenda kwakweli na ndio maana nina hasira mno"
"pole sana, na hata kaka yako aliniambia"
"ok poa"
Chidi alitaka kukata simu lakini akasikia
"samahani shem, nina kitu nataka kukuomba"
Chidi ikabidi aiweke tena skioni huku akimuuliza
"unataka nini"
"nataka mdogo wenu aje asomee huku mjini, nipo tayari kwa kila kitu, mana si unajua bado hatujabarikiwa mtoto hivyo kwa mimi ninaebaki nyumbani, nakua mpweke… Please shem naomba uje mjini na huyo mdogo wako"
Aliongea mwanamke huyo huku akiskika kama vile anataka kulia lia hivi,..
"hapana dada angu, siwezi kumleta mtoto huku mana atakuja kuteseka sana"
"mimi nipo… Afu kaka yako sio fukara tena, sasa ni mtu na pesa zake hivyo please, naomba iwe hivyo, na licha ya huyo mtoto hata wewe pia nataka uishi karibu na ndugu yako, sio vizuri kutengana… Nyinyi bado ni ndugu hata mfanyeje"
"ok sawa nimekuelewa ila kwa mimi kuja kwako itakuwa ngumu"
"hatutoshindwana shem, ila please naomba uje mjini na mdogo wako huyo sawa,.. Hii si ndio namba yako? Nataka nikutumie nauli sasa hivi"
"ok, ndio hii"
Basi walielewana huku kijana chidi akijiuliza kuwa
"huyu jamaa kamuachaje rehema? Mana alivyokuwa anampenda sidhani kama kweli huyu sio rehema"
Chidi alikuwa akijiuliza sana kuhusiana na swala hilo,…
"lakini hapana sauti ya rehema naijua vizuri tu"
Chidi alipata jibu kuwa huyo hakuwa rehema bali ni kweli atakiwa ni mwanamke mwingine, na ni kweli huyu mke wa Ibrahim sio rehema,…
Sasa chidi akiendelea kukusanya pesa zake pale kitandani ghafla meseji inaingia ya TigoPesa
"heeeeee yaani pesa yote hii ni kama nauli tu, basi kweli kaka Ibrahim atakuwa tajiri kweli aisee"
Aliongea kijana chidi huku akiiyangalia ile meseji ya TigoPesa ilioingia hivi punde
Mara simu iliita kucheki ndio ile namba ya shemu wake
"haloo shem,.. Nimetuma laki mbili hapo ila ikiisha uniambie nikutumie nyingine sawa shem"
"sawa asante"
Chidi hakuwa akitaka mambo mengi kwa shemeji yake huyo,.. Tena alianza kumheshimu zaidi kwasababu mwanzo alimtukana bila sababu yeyote… Basi chidi alivaa nguo zake kisha akatoka kwenda mjini kufanya shoping ya nguo,.. Hivyo kwasababu alikuwa na safari ya kwenda nyumbani, aliingia duka la nguo za kike na kubeba vitenge na kanga nyingi sana bila kusahau nguo za ndani za mkewe ambaye yupo kule kijijini, tena alikuwa ana furaha sana kwa hilo,.. Kijana chidi alifungasha mizigo mingi sana bila kusahau zawadi za wazazi wake kama vile vitenge, kanga, magauni, madera, na kila kitu, na baba yake pia alimkusanyia baadhi ya nguo kali za kijanja janja mana wazazi wake sio kuwa ni wazee ila sema maisha ya kijijini si unayajua mwenyewe,…
Tukija huku hotelini anakomiliki mama sarah na mtoto wake sarah,…
"shkamoo mama"
Sarah alimsalimia mama yake baada ya kumkuta ofisini kwake,
"marahaba ujambo mama"
"sjambo, za toka jana"
"aahhh nzuri tu… Ahh jana nililala moshi baada ya kufuatilia vitu fulani hivyo nilichelewa nikaona wacha nilale tu"
Mama alianza kujibalaguza kwa mtoto wake, mana ni lazima angelimuuliza mama yake jana alikuwa wapi mbona hajamwambia, mana watoto wa kike na mama zao, utafikiri ni mashostito, kumbe ni mtu na mwanae,….
"sawa ila baba alikuulizia"
"weeee baba yako alirudi jana"
"ndio, ila nilimwambia kuna mahari umekwenda"
"safi sana, ndio mana nakupenda mwanangu, mana dady yako mkorofi yule alafu hebu shika hii pesa, kaniletee simu kama ile ulioileta kipindi kileee, nataka nibadirishe simu mwanangu"
"mmmhhh mama nawewe unapenda simu za kishamba, SAMSUNG GALAXY NOTE S7 zimeshapitiwa na wakati mama"
"sasa nitanunua simu gani mwanangu"
"mama, mimi juzi nilinunua IPhone 7+, ila sitaki tununue simu zifanane, wewe kanunue IPhone 8 imetoka juzi tu"
"iPhone 8 bado haijatoka"
"mama imetoka mi nimeiona juzi, tena bei chee kabisa"
"shilingi ngapi"
"Nakumbuka niliambiwa milioni mbili na laki tatu"
"hhhmm haya kama ni nzuri kailete"
Basi mama sarah ni watu wenye pesa zao licha ya kwamba wanamiliki hoteli ya akina Miriam, hivyo kwa utajiri wa akina sarah ni nusu kwa akina Miriam, hivyo akina Miriam wana utajiri mkubwa kiasi kuliko akina sarah, na hata hoteli wanayofanyia kazi ni ya akina miriam,.. Hivyo akina sarah hawasumbuliwi na vichenji chenji vya milioni mbili au tano, kwao ni kama laki mbili au tano,..
Masaa machache baadae sarah alirudi akiwa kashika box la simu aina ya IPhone 8 simu ambayo ndio inaanza kutoka kwa wakati huo,..
Sarah alimpa mama yake simu hio kisha mama bila kuikagua aliingiza katika mkoba wake, kisha akamuaga mwanae kiwa anatoka….
Wakati huo kijana chidi yeye yupo mjini akiwa ananunua zawadi kwa ajili ya familia yake kule nyumbani, mana toka aje mjini hajawahi kwenda japo hata mwaka hajamaliza…
Ghafla simu yake inaita kucheki jina alikuwa ni grace au mama sarah,
"haloo mamy"
"eee naomba uje hapa mjini kati nikupe simu yako"
"mbona mi nipo mjini mamy"
"upo sehemu gani"
"nipo hapa Female Doka"
"heeeeee female doka unafanya nini huko"
"njoo hapa mamy utajua tu"
Kweli hawakuwa mbali hivyo walikutana na chidi aliingia ndani ya gari huku akiwa kubeba nguo nyingi sana, zikiwemo za mke wake huyo salma wa Jackson,..
"unaenda wapi tena chidi jamani, au umekuja kufanya shoping yako"
Aliongea mama huyo huku kama anataka kulia mana alimuona chidi kakaa kisafari safari hivyo akili ilimtuma kuwa huenda chidi anahama mji,..
"mamy, wala usijali… Unajua ni muda mrefu toka nije mjini sijapata kwenda hata kuiona familia yangu, hivyo nataka niende kesho ili keshokutwa nirudi"
"ooohhh sasa kwanini hujasema nikupe pesa nyingi, yaani unaniuzi wewe na ukimya wako huo,.. Sasa mama mkwe wangu ungempelekea nini kama nisingelijua jamani chidi"
"aahhh hata hivyo imejitokeza ghafla tu"
"we chidi, hujui kuwa nampenda sana mama yako, hata baba yako pia, mana ni waleta chema juu yangu, sijui nilikujuaje chidi"
"usijali"
"kama ungelikuwa unaweza kuendesha gari ningekupa uende nalo chidi wangu"
"wala usijali, nitapanda basi tu"
"eti eee…. Ok simu yako hii hapa mpyaa, utaikagua mwenyewe afu chukuwa hii laki tano, mpelekee mamy yako zawadi yeyote anayoipenda sawa"
"asante sana mamy, mana nilikuwa nakaribia kumaliza pesa"
"usijali,… Yaani kuwepo kwangu hai, ni kufanikiwa kwako sawa"
"sawa mamy"
"ok, ukirudi nitakupeleka kwenye hoteli yangu, ukaanze kazi rasmi"
"haaaa kwahio tutakuwa karibu na wewe"
"ndio… Tena sio mimi tu nina mtoto wangu wa kike"
"haaaaa nae anapika chipsi"
"hapana… Yeye yupo kaunta yupo kama keshia tu, au meneja"
"sawa mama nitashukuru sana mamy wangu"
"usijali, mimi nakutakia safari njema kwako"
"asante mama angu"
Basi chidi alitoka na kuita tax huku mama akigeuza gari yake kisha huyooo,.. Chidi alikuwa kawafungashia zawadi wazazi wake pamoja na mke wake…
Tukija huku kijijini tunawakuta wawili hao salma na Jackson wakiwa katika maandalizi ya kufungasha vitu vyao, tena walikuwa wapo uchi hapo ndani, kana kwamba waliduuuuuuu mpaka wakachoka sasa wanataka kurudia kwa kitamanishana kwa kukaa uchi kila mtu, na wakati huo walikuwa wakifungasha vitu vyao,…
"baby, inabidi tuondoke na gari ya jioni"
Aliongea salma huku Jackson akiuliza kwa mshangao
"kwanini tuondoke jioni mke wangu"
Jackson alichanganyikiwa na Salma mpaka kumuita mke wake,
"nataka nikamuone mtoto wangu kamwisho mwisho"
"lakini si unajua umetoroka wewe"
"sawa, lakini mi nataka nimuone tu kwa mbali"
"aahhhh hapo sawa, nikajua unataka kumfuata mpaka kwa bibi yake"
"hapana"
Basi mizigo ilikamilika na wakaendelea na swagrati yao,.. Maskini salma alikuwa akimkumbuka chidi mana yeye ndio kamzoea kwenye mapenzi, sasa haamini kama leo atamuacha…..
KESHO YAKE MIDA YA SAA 9 ALASIRI
Tukiwa huku njiani tunamkuta kijana chidi akiwa juu ya basi moja la lakshari, basi la maana, wakati huo ndio kama vile safari inaendea mwisho ila palikuwa na kilometa chache sana hadi kufika tanga kwao, maeneo ya PONGWE, kama kawaida stendi ya kange pale gari ilisimama na kushusha watu ambao wanashukia happ mjini kati, ila uzuri wa gari hilo, linapitiliza kabisa na huko linakopitiliza ndipo huko huko anapoishi kijana chidi,…
Sasa wakati huo huku kwa akina salma na Jackson nao ndio wanaingia katika gari ya jioni jioni hio,.. Na njia ni hio hio moja, ambayo chidi anajia na salma anaondokea, kumebaki kilometa kumi chidi kufika nyumbani, yaani kama angeliwahi tu kidogo lazima angeliwakuta watu hao, mana ndio kwanza walikuwa wakiondoka hapo kwenye stendi yao ya hapo kijijini… Gari inaondoka na kuianza safari na wakati huo gari ya akina chidi ndio ilikiwa inarindima na safari kuja kijijini, na akina salma nao ndio wanarindima kwenda mjini,… Humo ndani walikuwa wakikumbatiana na kunyonyana madenda bila kujali kuwa wapo safarini,.. Kiukweli salma na Jackson walipendana sana, kwasababu mpaka mwanamke umuache mumeo uende mjini na mwanaume mwingine kweli?? Hii noma,…
INAENDELEA...
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi