MUUZA CHIPS (45)

0
Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA AROBAINI NA TANO
ILIPOISHIA...
Sasa wakati huo Jasmini ambae ndio shemeji mtu ndio alikuwa nyuma ya chidi yupo tayari kumgusa, sasa akawa anaogopa kumgusa, anahofia kugusa mtu wa watu ambaye sie aliomtegemea,… Sasa sarah akahisi huyo mwanamke ana nia mbaya na chidi, bila kujua kuwa huyo ndio shemeji wa chidi…

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Saa ngapi sarah hajaja kumgusa yule mwanamke,…

"we dada vipi mbona unataka kumpiga huyu kaka"

Sasa hio sauti chidi aliisikia mpaka kwenye simu yake, mana huyo dada ndio huyo shemeji yake, na simu haikuwa imekatwa kama jinsi walivyopatana,.. Sasa chidi aligeuka fasta kuangalia hao wanaosemezana ni akina nani…

Sasa chidi kugeuka, macho yake yaliangukia kwa sarah mana anamjua na alishawahi kumseidia kwa kumpeleka hospitali, chidi akakata ile simu huku akimshangaa mtoto wa tajiri ambae ni sarah,

"heeeee sarah, ulienda wapi mamy"

Aliongea chidi huku akimshangaa sarah mtoto mzuri mwenye umbo zuri la haja,..

"chidii, toka kule nilikuwa nakufananisha sasa nimekuja kwa ajili ya huyu sjui alitaka kukuibia simu"

"weeeeee koma na ukomae, yani mimi niibe simu"

"we dada naomba unyamaze kimya mana hunijui mimi ni nani"

"hata kama wewe ni nani hainihusu… We chidi mimi ndio huyo uliokuwa unawasiliana nae"

Sasa shemeji mtu na sarah walitupiana maneno ya hapa na pale, mwisho Jasmini akamaliza utata

"kwanza umenijuaje kama ndio mimi"

Chidi alimuuliza shemeji yake na wakati bado hajamjua

"kaka yako aliniambia unaitwa rashidi (chidi) sasa na huyu dada alipokuita chidi nami hapo hapo mawazo yangu yakatua kwako mana pia nilikuwa nakuja kwako kabla ya huyu dada kuja hapa"

Aliongea mke wa Ibrahim huku akiwa na hasira na sarah,…

Sasa chidi akatumia akili,.. Alibonyeza kitufe cha kupigia kana kwamba namba ya mwisho ni lazima ipige hio hio ya mwisho,… Kweli simu ya Jasmini iliita

"heeeeeee mbona ndio huyu anapiga"

Alipoongea hivyo, sarah nae kadakia juu kwa juu

"umeona eee,.. Usione mahensam tu we ni kuwafwata"

Jasmini aliipokea ile simu lakini hakukuwa na mtu aliokuwa akiongea, mana chidi alibonyeza bila kuangalia,.. Chidi aliinyanyua simu yake na kuiweka sikioni, kisha akasema

"haloo"

Jasmini au mke wa Ibrahim alishusha pumzi kwa nguvu huku akishukuru kuwa ndio yeye shem lake,…

Pale pale chidi alimkumbatia shemeji yake tena ndio yule yule aliomuona mwanzo na kusema kaka yake hawezi kuoa mwanamke kama huyo…

Walipomaliza kukumbatiana, Jasmini alimkumbatia na halima ambaye ni wifi yake mdogo…

Sasa sarah akawa kabakia tu katulia anawaangalia,

"chidi, kwani huyu ni nani"

Sarah aliuliza kwa upole wa hali ya juu mno

"huyu ni mke wa kaka yangu"

Sarah kuskia hivyo tu, alianza kuomba msamaha kwa shemeji yake chidi

"naomba unisamehe dada angu, sikujua mi nilijua ni wadada wa mjini tu"

Hata Jasmini pia hakuwa amekasirika sana

"usijali mdogo wangu, najua ulikuwa hujui"

Basi Jasmini na sarah walipeana mikono ya kusameheana…

Sasa Jasmini papo hapo akasema anaenda kuchukuwa gari, mana aliiacha mbali kidogo,…

Jasmini aliichukuwa gari yake na kuileta pale ili kuchukuwa mizigo

Basi kijana chidi aliingiza mizigo katika gari ya shemeji yake kisha haooo wakaondoka huku sarah akifata kwa nyuma, ndani ya gari ya sarah alikuwepo kijana chidi huku wakiongea mengi, walipeana namba kila kitu, kisha chidi akashuka,…

Sasa huku kwa mama miriam nae kapigiwa simu ya dharura kwenda kuonana na watu fulani kikazi, hivyo ile subiri ya kumsubiri mama sarah ikaishia hapo,…

"haloo mama sarah, samahani ndugu yangu kuna dharura nimeipata sasa hivi naondoka"

"sawa basi tutafanya siku nyingine"

"sawa, lakini huku hakuna mtu, mana sarah nilimtuma aje huko stendi badala yako"

"aahhh ok, hata hivyo nakaribia hapo"

"sawa basi mi naondoka"

Basi mama miriam aliondoka huku mama sarah nae anakaribia kufika hotelini hapo,…

Masaa mawili mbele, sarah nae ndio anafika hapo hotelini akiwa na furaha ya hali ya juu mpaka mama yake akashangaa kwa kuiona furaha ya mtoto wake,

"una nini wewe"

Aliuliza mama sarah

"mama, yaani siamini mama angu"

"nini sasa"

"sasa hivi nipo tayari kukutambulisha mpenzi wangu mama"

"hhhmmm we mtoto una kichaa wewe"

"mama kweli vile,… Yaani kama nilivyojua tu kwenda kule stendi"

Sasa mama kusikia tu jambo la stendi, alianza kubadirika sura hapo hapo

"stendi kumetokea nini"

"mama…. Yaan hata sijui nisemeje mama angu"

"anaitwa nani,.. Na yupoje yupoje"

Heeeeee hata sarah alishangaa kuona mama yake anauliza sana maswali mengi juu ya huyo mpenzi wake,… Sarah alimwangalia sana mama yake huku akimuuliza

"mama, kulikoni na mpenzi wangu? mbona unamuulizia hivyo"

Mama alinuna na kuvuta mdomo wake huku akimwangalia mtoto wake kwa hasira, kana kwamba keshakua na keshajua wanaume anaotaka wampande

PATAMU APO

Sasa tuanzie pale stendi walipokuwa wanapakia mizigo, mana kuna vitu vilifanyika hapo katikati sikuvielezea,..

Basi chidi alipakia mizigo yote katika gari ya shemeji yake, huku sarah nae alikuwa akiseidia kuingiza baadhi ya vitu vidogo vidogo, baada ya kumaliza chidi alitaka kupanda katika gari ya shemeji yake na kumuacha sarah, lakini kabla hajapanda sarah alimshika chidi mkono na kumwambia,

"ina maana unaniacha mwenyewe"

Aliongea sarah huku akiwa kamshika mkono chidi wake aliokuwa akimuwazia kipindi chote hicho,.

"sarah dada angu,.. Sina maana hio, bali kule kwenye gari kuna mdogo wangu na yule ni shemeji yangu, sasa sijui nyumbani kwa kaka yangu ndio nataka niende ili nipajue"

"kwani humjui hata shemeji yako"

"licha ya shemeji yangu, hata kwa kaka yangu penyewe sipajui"

"khaaaa, sasa mlikuwa mnaishi vipi"

"wala tu, kila mtu alikuwa na maisha yake, ila broo kajenga huko chini mi sijui"

"mmmhhh sawa, nimekuelewa, ila naomba niwasindikize basi, lakini mi nataka niwe na wewe kwenye gari yangu"

"sawa, ngoja nimpe taarifa atangulie kisha sisi tuwe nyuma yake"

Basi safari ilianza shemeji mtu akiwa mbele na sarah na chidi wakiwa nyuma katika gari ya sarah,..

"chidi jamani, umekuwaje mweupe hadi nimekusahau"

Aliongea sarah huku akirembua macho yake mbele ya kijana huyo, na chidi nae kidoogo alikuwa na aibu ya kuangaliana na mwanamke haswa lika lake,…

"sasa umenijuaje kama umenisahau"

"si hio sura yako tu, na umbo lako"

"hahahaha kwahio rangi tu ndio tofauti"

"ndio"

Unajua chidi alipotoka kijijini alikuwa ni maji ya kunde, sasa alipofika mjini alibadirika na kiwa mweupe kitokana na kuwa karibu na moto, wakati ule akiwa anauza chipsi, hivyo ule moto ndio ulimkoboa kakoboka kobooo, kawa mweupe wa wastani tu ila sio ile kuzidi sana,..

"umpendae vp hajambo"

Aliongea sarah lakini moyo wake ulikuwa ukienda mnio kana kwamba chidi akisema hajambo, basi ajijue hana chake tena,…

"kwa bahati mbaya sina"

Sarah alipumua kwa nguvu huku akijisemea kimoyomoyo kuwa…

"afadhali tu hana,… Na hapa simlembi lembi tena, nampa makavu laivu kama ataniona malaya potelea mbali"

Sarah alijiongelea mwenyewe kimoyomoyo kuwa hapo hataki tena kumlemba, mana mwanzo alikosea hajawahi kumtaamkia kuwa anampenda.

Gari ya sarah ni automatically (.Gari inayojibadirisha Gia yenyewe.) Lakini alitamani ingelikuwa ni Manually (.Gari Unayoibadirisha Gia Mwenyewe.) ili apate nafasi ya kumshika chidi angalao hata paja lake, mana chidi alikaa pale mbele huku sarah akiwa kama dereva mwenyewe,…

"chidiii"

Sarah aliita huku moyo ukimwenda mbio, kuwa alikuwa tayari kuusema ukweli wake

Tukija huku kwa mama yake sarah aliokuwa yupo ofisini kwake, aliishika simu yake na kumpigia chidi

"haloo chidi,.. Nisamehe boy wangu, nilipata dharura ghafla, ila kwa sasa upo wapi nije"

"usijali mamy, nimeshapokewa na shemeji yangu"

"Eti eee?"

"ok basi tutakutana, namsubiria mtoto wangu akija tu nakuja huko kwako sawa"

"sawa mamy, ila kwa sasa kule sidhani kama nitakuwepo mana nitakuwa nipo kwa broo wangu"

"lakini si utarudi"

"ndio, lazima nirudi"

"ok poa boy wangu.. Nimekumisi boy"

"mimi je, hunishindi mimi"

"kweli??… Ebu nikiss basi"

Chidi aliona aibu kumkisi mama sarah mbele ya sarah, japo hajui kama watu hawa ni kitu na mama yake,

"no mamy,.. Nipo na broo hapa itakuwa mbaya"

"ooohhh sorry boy wangu, sikujua kama upo nae karibu"

"poa basi baadae"

Simu ilikatika huku mama sarah akipumua kwa furaha ya hali ya juu baada ya kujua kuwa chidi kapokelewa na shemeji yake…

Tukija huku kwa akina sarah,.. Ghafla simu ya sarah ikaita

"haloo mama"

Alikuwa ni mama yake ambaye muda sio mrefu aliongea na chidi,..

"sarah upo wapi mwanangu"

"mama nakuja nipo njiani,… Ila kwani we upo wapi? Mana nilikuja kule stendi nimekutafuta sijakuona"

"aahhh mimi nilishatoka muda tuu"

"ok, lakini huyo mgeni wako si umeshampokea"

"ndio tayari nimeshampokea"

Mama sarah alimdanganya mtoto wake, lakini sio kweli kama alimpokea huyo mgeni aliomfata….

"ok sawa mama nakuja sasa hivi"

"sawa mwanangu"

Simu ilikata… Sasa sarah akakosa ile confidence ya kuongea maneno matamu mana ile mudi ilipotea baada ya simu kupigwa… Sasa akawa anawaza sana aanze na nini,.. Akapata wazo moja la kuweka muziki katika gari

Aliweka nyimbo ya west life iitwayo Love me…

"unapendaga nyimbo za usiku"

Sarah alimuuliza chidi huku chidi akiisikiliza nyimbo hio,…

"ndio, napenda pia"

Sarah aliona kama vile haitoshi, yaani sarah alikuwa akihaha huku na kule ili tu amfanye ajue kuwa anampenda,.. Sarah ni mschana mwenye mitego ya kimapenzi na vile chidi ni rijali,.. Mmhhh

Sarah alijifanya anajikuna paja lake, na kusababisha upaja wake kuonekana, na vile alivyo mweupe duuu yaani chidi alijikuta anapepesa macho na kuangalia pembeni, kana kwamba chid hakupenda kuangalia… Sarah alikasirika sana baada ya kuona chidi hamuangalii paja lake,.. Sarah alipitisha gari njia tofauti na ile ambayo wanamfuata shemeji yake kwa nyuma,…

"sarah, unaenda wapi huko"

Sarah hakujibu kitu,… Aliiweka gari kwenye pakingi kisha vioo vya tintedi vikafanya kazi yake…

"chidi mpenzi mbona unashindwa kunielewa nahitaji nini kwako"

Sasa ile chidi anashangaa kuitwa mpenzi, sarah alijirusha mpaka kwenye mapaja ya chidi huku akimuwahi kwenye mdomo, mana denda ndio njia ya kwanza inayoamsha hisia za mapenzi Basi sarah na chidi wakakutanisha midomo yao, huku sketi ya sarah ikipanda juu, na saa hio sarah aliushika mkono wa chidi umshike paja lake……

"chidi jamani, toka siku ileeeee, nilikuwa naumia juu yako, nilikuwa naogopa tu kusema"

Sarah aliongea huku chidi akilitamani tena denda la sarah,… Kwa wakati huo sarah hakuwa na mamlaka yoyote yale ya kumkatalia chidi kwa kile akitakacho, chidi alitaka kurudia denda,.. Sarah kajilegeza legeee, chidi alifanya kile akiwezachi lakini hakumwingilia kimwili, ila alimshika shika sana mtoto wa watu, mpaka kuchoka bila kuingiliwa

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)