Mwandishi: MoonBoy
SEHEMU YA AROBAINI NA SITA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Sarah aliongea huku chidi akilitamani tena denda la sarah,… Kwa wakati huo sarah hakuwa na mamlaka yoyote yale ya kumkatalia chidi kwa kile akitakacho, chidi alitaka kurudia denda,.. Sarah kajilegeza legeee, chidi alifanya kile akiwezachi lakini hakumwingilia kimwili, ila alimshika shika sana mtoto wa watu, mpaka kuchoka bila kuingiliwa
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI
SASA ENDELEA...
"chidiiiiiii"
"hhhhmmmmm,… "
"mbona unaniacha sasa"
"usiwe na haraka,… Kwenye gari hua sio vizuri"
"chidiiiii…. "
"sema mamy"
"ndoto yangu imetimia,… Nilikuwa nakuwaza sana na nashindwa kujua ningekupataje"
"kwanini usingeniambia mamy"
"kwani hata wewe ulikuwa unanipenda"
"ndio,.. Ila sema kwa pesa zako, hhmm nikahisi itakuwa kama ndoto kwangu"
"chidiiiii…. "
"nakupenda chidi wangu, na kukupenda sijaanza hapa, toka siku ile unaumwa mie nakupenda tu"
"hata mimi pia sema mie niliogopa kwa pesa zetu"
Sarah alilegea tena makusudi ili tu chidi asimuache hapo alipo,…
"sarah, please naomba tumuwahi shem basi"
Sarah aliwasha gari na kuanza kumkimbizia shemeji yake chidi au mke mwenzie,.. Au hata wifi yake pia ni sawa au hata dada yake pia ni sawa…
Alimkimbizia mpaka akamkuta, kisha chidi akapanda katika gari ya shemeji yake, na sarah nae akarudi hotelini kwao,
Dakika kumi na tano mbele, Sarah akiwa keshafika hotelini kwao alimkuta mama yake akiwa ofisini, ila sarah alikuwa ana furaha sana kuliko siku zote
SASA HAPA TUENDELEE NA PALE TULIPOISHIA
mama yake akashangaa kwa kuiona furaha ya mtoto wake,
"una nini wewe"
Aliuliza mama sarah
"mama, yaani siamini mama angu"
"nini sasa"
"sasa hivi nipo tayari kukutambulisha mpenzi wangu mama"
"hhhmmm we mtoto una kichaa wewe"
"mama kweli vile,… Yaani kama nilivyojua tu kuja kule stendi"
Sasa mama kusikia tu jambo la stendi, alianza kubadirika sura hapo hapo
"stendi kumetokea nini"
"mama…. Yaan hata sijui nisemeje mama angu"
"anaitwa nani,.. Na yupoje yupoje"
Heeeeee hata sarah alishangaa kuona mama yake anauliza sana maswali mengi juu ya huyo mpenzi wake,… Sarah alimwangalia sana mama yake huku akimuuliza
"mama, kulikoni na mpenzi wangu? mbona unamuulizia hivyo"
Mama alinuna na kuvuta mdomo wake huku akimwangalia mtoto wake kwa hasira, kana kwamba keshakua na keshajua wanaume anaotaka wampande
"hhahahahahahahaha, mwananguuu kwani mimi sipaswi kumjua mkwe wangu"
Mama aliona akimuulizia sana, sarah atajua kuwa mama yake ana tabia ya kutembea na vijana wadogo,.. Hivyo mama akajichekesha pale na kuliuwa hilo soo, mana mtoto angejua kuwa mama anatembea na vijana wadogo,..
"aahhhhh hapo sawa mama,… "
"ila huyo mkwe wangu ni mzuri au sura nyani, mana staki mtoto wangu mzuri mrembo uolewe na lijitu bayaa"
"mama we tulia tu utamuona mama angu"
"eti eeee"
"ndio"
Basi furaha kwa sarah iliendelea hivyo hivyo kwa siku yote hio…
Sasa tukija huku kwenye gari ya jasmini akiwa na Shemela wake chidi, tena ndio walikuwa wanafunguliwa geti na kuingia ndani
Chidi alikuwa akishangaa sana hilo lijumba la kaka yake, yaani ni bonge la jumba, yaani jumba jumba haswa, huko ndani ni gadeni mwanzo mwisho
"aaahhhh huyu kaka katoa wapi pesa zote hizi"
Chidi alijisemea kimoyomoyo huku akiogopa hata kuingia, japo bado hajashuka kwenye gari, sasa chidi kupiga jicho kwenye paking ya magari, kulikuwa na magari yasiopungua sita,.. Ukijumlisha na hilo ni saba, Ukijumlisha na la kaka yake huko kazini ni nane,… Khaaa chidi alikuwa haelewi elewi utajiri wa kaka yake umekujaje ghafla,.. Maana ni miezi 6 tu wameachana na ndugu yake, eti leo ndio anamiliki jengo kama hili,..
Chidi alishuka chini kisha wafanyakazi walikuja kuingiza mizigo ndani..
Chidi kila atakapokanyaga ni Vigae tu kila anapokanyaga ni Tailizi tu, khaaa, yaani ilikiwa imwogopesha sana chidi..
"shem ingia ndani, hao wataingiza mizigo yote"
Aliongea shemeji mtu kana kwamba hataki Shemela wake achafuke, mana chidi aling'aaa haswa,….
Kwa wakati huo ilikuwa ni mida ya jioni hivyo asingeweza kuondoka hapo,.. Hivyo kwa mara ya kwanza chidi atalala katika nyumba ya kaka yake,….
Ilipofika mida ya saa mbili usiku kaka yake ndio alikuwa anaingia…
"waaoooo chidi ndugu yangu, siamini kama leo tupo wote tena"
Chidi alitamani kumkasirikia kaka yake lakini aliona haina maana kama ni ujinga wake ni yeye na roho yake,…
"shkamoo broo"
"marahaba vp ndugu yangu…. Nimekumisi sana ila yote na yote naomba unisamehe, najijua nilifanya kosa juu yako ila nisamehe ndugu yangu"
"mimi nilishakusamehe kitambo tu"
"ahsante sana mdogo wangu… Laribu sana na jiskie upp kwako"
Ibrahim alimkaribisha mdogo wake kwa furaha kubwa sana….
Ilipofika saa nne chidi alionyeshwa chumba chake cha kulala, tena shemeji yake ndio kimbelembele kwa Shemela wake,…
Lakini chidi akiwa hapo kitandani alikuwa akiumizwa sana upataji mali wa kaka yake, umekuwa wa haraka mno, yaani hata muuza madini tu hatajiriki haraka namna hii,…
"huyu broo kaingilia wapi"
Alijiuliza kijana chidi hata usingizi hapo kitandani hauji kabisa, yaani anawaza jumba hilo la kaka yake…
Lakini kijana chidi akiwa kwenye mawazo alikumbuka kitu kwa shemeji yake…
"shem, chumba chako hiki hapa, na mimi ndio nimekichagua, ila kuna kile chumba pale usikifungue"
Chidi alishtuka baada kukumbuka maneno hayo ya shemeji yake wakati anakuja kuonyeshwa chumba chake cha kulala…
"kwenye kile chumba kuna nini pale,… Mbona anasema nisikifungue"
Alijisemea kijana chidi huku akitoka na kukifuata kile chumba…
"lazima nikifungue usiku huu huu,… Nisije kuingia pabaya na mdogo wangu halima"
Chidi alijisemea huku akiukaribia mlango wa chumba hicho,……
JAMANI NAOMBA MUSIRUKE HATA MSTALI MMOJA, MANA SIMULIZI ZANGU NATAKA ZIKUBURUDISHE NA PIA ZIKUELIMISHE… HIVYO NAOMBA SANA TUISOME BILA KURUKA MSTALI HATA MMOJA… TAFADHALINI SANA WADAU WANGU, MANA ASILIMIA KUBWA YA SHABIKI ZANGU NI VIJANA, NA NYIE NDIO NAWATAKA HASWAAA…
Katika maisha haya ya dunia ya sasa hivi, yametawaliwa na utajiri wa aina mbili,.. Kuna utajiri wa Mwenyezi Mungu, na utajiri wa shetani, kumbuka kuwa utajiri wa Mwenyezi Mungu haukauki na wala hauna masharti ya kuuendeleza zaidi ya kupambana na kazi zako mwenyewe.. Lakini utajiri wa kishetani ni utajiri ambao hupotea siku yeyote pale usipotekeleza matakwa yao,.. Na utajiri wa kishetani ni utajiri mkubwa na wenye kishindo kuliko hata utajiri wa Mwenyezi Mungu, hivyo usipokuwa makini unaweza kuingia huko kwenye vishindo na kuacha utajiri wenye makazi ya milele tena usio na bughudha na mtu yeyote yule,…
Kweli katika maisha tujue kuna mungu, na mungu huyo huyo katuleta yeye na ataturudisha yeye kwa mapenzi yake yeye mwenyewe,..
Lakini Kuna baadhi ya matajiri wengine wengi tu wana utajiri wa kutisha, lakini cha ajabu utamkuta hana mtoto, au hana wazazi wote wawili au mmoja, utakuta hana ndugu, ukiuliza utaambiwa kazaliwa mwenyewe,.. Kumbe kawamaliza kwenye pesa huko, watu wanajali pesa kuliko utu, dunia ya sasa imebinuka we kataa kubali, kijana wa sasa unakaa kijiweni na kumsema mtu ni freemason, yaani wewe umekaa tu kijiweni afu unaita wenzako freemason, hebu jiulize je wewe utakuja kuwa nani na wakati kazi hufanyi,..
Mimi hapa leo hii naandika simulizi kama hizi,.. Kesho nimekuwa maarufu zaidi ya Eric Shigongo, lazima muniite freemason, na wakati juhudi zangu mlikuwa mkiziona toka mwanzo na mnaziona jinsi silivyo, lakini leo nimepanda juu basi naitwa freemason kisa nipo juu na nina pesa,… Ukimwona tu mtu kapata vipesa vyake tayari ni freemason, unashindwa kufanya kazi kwa bidii, unawaza kuwa
"aaaaaahhhh yule si freemason bwana, kama sio ufreemason tungekuwa nae hapa kijiweni"
Akili nyingi za vijana wenzangu ndivyo zinavyowatuma kuwaona watu wakiwa katika hali hio, sasa unatakiwa ujue kuwa watu wenye pesa za kishetani ni wachache mno kuliko wenyewe pesa za uhalali, sema wanajumuishwa wote kwasababu kitu cha kishetani kinasambaa haraka kuliko kitu cha halali,
Mfano mzuri ni kama hivi,.. Kwa sasa mtu anaweza kukuamini kwa uongo kuliko ukweli,.. Yaani mtu umdanganye ndio arizike, lakini ukimwambia ukweli mtagombana, hivyo dunia ya sasa imetawaliwa na nusu ya usheni na ndio inazidi kusambaa kadri siku zinavyozidi kwenda,… Hebu sasa hivi kajifanye kama unamkopa rafiki yako pesa,.. Afu mwambie baada ya miezi mitatu nitakurudishia, hakiyamungu vile akikupa niite mbwa,… Lakini mwambie baada ya siku tatu nitakurudishia, hapo hata kama ana hakiba yake, lazima akupe mana ni rafiki yake.. Kwahio mpaka hapo dhihirisho ni kwamba, dunia inaelekea pabaya maana uongo umekithiri sana, mambo maovu yamekithiri sana, vitu visivyompendeza Mwenyezi Mungu vimekithiri sana,.. Eti mtu kafikisha miaka sitini na zaidi ndio anaanza kumkumbuka mungu,.. Wakati Mwenyezi Mungu anataka ile sehemu ya kuanzia miaka 18 mpaka 50, kuanzia miaka 18 kwenda mbele hapo ndipo mungu anapo pataka yeye, aone huo ujana wako unaufanyia nini,… Sio ufikishe miaka 60 ndio umkumbuke mungu… Yaani hujacheza mechi zote afu wataka fainali si ukichaa ni nini…..
JAMANI MTANISAMEHE SANA MANA SIMULIZI ZANGU, NATAKA ZIKUBURUDISHE NA PIA ZIKUELIMISHE, HIVYO MSINICHUKIE KWA KUTOA SPEECH FUPI KAMA HIO MANA NAKEREKA SANA NA TABIA ZA VIJANA WENZANGU…. SASA TUENDELEENI
Wakati huo kijana chidi akiwa ndio anatoka chumbani kwake kwenda katika chumba hicho ili kuweza kuona kile kilichofanya aambiwe kuwa asiufungue mlango huo, sasa chidi na vile ana mashaka na utajiri wa kaka yake hivyo akawaza kwenda kukitazama chumba hicho, chidi alikuwa akitembea taaratibu kabisa huku akiangaza macho huku na kule ili kusiwepo na mtu wa kumwona kwa wakati huo, chidi alifanikiwa kuufikia mlango huo,
Sasa ile anashika kitasa cha mlango, ghafla umeme ukakatika,.. Hivyo kukawa kiza kinene kuliko hata kiza unachokijua wewe ndugu msomaji, Chidi aliogopa na kuachana na lile zoezi, hivyo alirudi zake chumbani kulala, huku akili yake ikiwa haipati jibu sahihi kuhusiana na chumba hicho,
Asubuhi na mapema chidi aliamka na kuanza kufanya usafi wa mwili wake huku akiizungukia nyumba hiyo, chidi alikuwa akipiga mswaki huku akizunguka zunguka nyuma ya nyumba hiyo,..
"lakini hii nyumba sio mpya hii,.. Au atakuwa kanunua nini"
Chidi alikuwa akijiongelea mwenyewe huku akiendelea kutembea katika gaden ya nyumba hio,… Mana hio nyumba ilionyesha kutokuwa mpya, hivyo huenda kainunua tu…. Alizunguka sana katika nyumba hio huku imani yake ikimtuma kuwa huenda haukuwa utajiri wa halali katka upande wa kaka yake,
"kakini kama kaka ni freemason.. Mbona wazazi wetu wote wapo hai.. Au mbona mimi na mdogo wangu tupo hai"
Chidi aliwaza hayo kichwani kwake bila kupata jibu,..
INAENDELEA...
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi