Notifications
  • MY DIARY (33)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA TATUTULIPOISHIA...Nilikuwa nachanganya staili za kijamaika na hizi za kwetu, sikuacha pia zile za Nigeria hapo nikapata vitu vyangu vya tofauti kabisa. Basi baada ya kujihakikishia kuwa nipofiti kwa mastahili yangu hayo nilisubiri siku ya shindano ifike nikafanye yangu. Siku ya shindano ilifika na mimi nilikuwa miongoni mwa washiriki walioingia tatu bora.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (32)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA MBILITULIPOISHIA...Lakini kuchepuka kwangu na kuingia mgombani haikumaanisha kuwa sheria ingeniacha hivi hivi.Ilifika mahali ikabidi nizime gari na kutulia tulii kusikilizia nini kitafuata.Tayari nilikuwa nimezungukwa na mapolisi ambao walikuwa wakinifuatilia kwa kutumia pikipiki.Kwa bahati nzuri dereva wa lile gari na yeye alishafika hapo na alishawaambia polisi kuwa mimi naugua ukichaa na nilifufuka kutoka mochwari.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA…
  • MY DIARY (31)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINI NA MOJATULIPOISHIA...“marehemu pia alinieleza kuwa ana miliki duka la vitu vya urembo wa kike ambalo pia Leah analisimamia ila hilo apewe mdogo wake Marry ambaye yupo hapa. Mama mdogo huyo mara baada ya kuyasema hayo alikaa zake chini. Baba mdogo ambaye hakurizika na maelezo hayo alisimama na kusema “kwa hiyo kama marehemu alijua kuwa atakufa hivi karibuni kwani nini hakufuata taratibu za kisheria za kuandika wosia na kurithisha mali.IKIWA UNASOMA…
  • MY DIARY (30)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA THELATHINITULIPOISHIA...Baada ya hapo Nnilimwomba mama mdogo ajikaze na kuwatarifu ndugu wengine habari hizo za msiba.Tulisaidiana hivyo hivyo maana sio siri kila mmoja alikuwa na uchungu sana kutokana na mazingira ya kifo hicho. Habari zilizidi kusambaa kwa kasi na majirani walianza kukusanyika hapo kwa mama mdogo.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Msiba ni msiba tu na ukitaka kujua binadamu…
  • MY DIARY (29)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA TISATULIPOISHIA...Hapo sasa nikazidi kuchanganyikiwa ikabidi nimuulize mama huyo alikuwa akifanyia shughuli zake za kujipatia kipato sehemu gani.? Yule dada akanambia kuwa anafanyia soko la ndizi huko Korongoni. Sikuwa na jinsi nilimuomba anipeleke lakini na yeye alisita sita kwa madai kuwa alikuwa na kazi nyingi za kufanya na bado anatakiwa ampeleke mtoto shule.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (28)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA NANETULIPOISHIA...Sisi tumesomea mambo haya bhana waliendela kuzungumza wale walinzi huku wakishuka ngazi kwa polepole. Hapo na mimi nikawa nimejifunza kitu kuwa kumbe unaweza kuingia na mtu guest akakuzuru kisha akaondoka zake.Sasa sijui kwenye zile guest zetu za uswahilini kama wanalijua hili.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Basi nilala japo usingizi ulikuwa hautaki kuja kwa…
  • MY DIARY (27)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA SABATULIPOISHIA...Alinamba eti hayo ya mimi kuolewa tuyaeke pembeni na kwa nini siku hiyo nisilale Moshi tukumbushie enzi zetu. Mwalimu John aliendelea kusema kuwa amenimiss sana na anomba nisahu yaliyopita na turudie yale maisha yetu ya zamani.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilijifanya simwelewi lakini ukweli ni kwamba nyota ya mwanaume huyu ilikuwa ni kali sana zaidi yangu na…
  • MY DIARY (26)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA SITATULIPOISHIA...Joyce alinambia yeye haendi kujipanga foleni kama makahaba wengine hivyo yeye hufanya biashara hiyo kitaalamu zaidi.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Alisistiza pia kuwa eti huwa anatumia kinga kuwakinga wengine. Wakati mwingine alinambia acha awaambukize kwa sababu wanaume wangekuwa na akili basi wasingeenda kununua mwanamke. Anasema kuwa laiti biashara hiyo…
  • MY DIARY (25)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA TANOTULIPOISHIA...Sikuisha hapo pia nilimpongeza kwa kunijali na kunipenda na kuhakisha kuwa siingii kwenye majanga kama yake mara baada ya kutoka jela. Siku hiyo nilimuelewa sana Joyce na nilikuwa tayari kumsapoti kwa lolote ili mradi tu atimize athma yake hiyo ya kuzaa. Tuliongea mengi sana na baadaye alinionesha picha ya mtu ambaye alitaka kuzaa naye.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA…
  • MY DIARY (24)
    Jina: MY DIARYMtunzi: __SEHEMU YA ISHIRINI NA NNETULIPOISHIA...Kwa kweli siku hiyo niliwaza sana na kutafakri vitu vingi. Wale wanachuo wenzangu wamenambia kuwa Msouth alikuwa kwa kimada mwingine na japo stori haikumalizikia ila ukweli ni kwamba alifumaniwa na kupigwa vibaya na huenda walimtupa mahali na ndio maana chanzo cha kifo chake hakieleweki.IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI👉INSTALL👈TUENDELEE...Nilijaribu kuijikontrol ili nisiwaze kitu…

MUUZA CHIPS (44)

Sehemu ya Arobaini na Nne, chidi akiwa ndio, na mdogo wake, shemeji yake kuwa, akapata wazo jipya, alikuwa akiongea na, aliwasha gari yake, simu yake
Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA AROBAINI NA NNE
ILIPOISHIA...
"nilikutania tu, wala hakuna lolote baya"

"mjinga wewe"

Basi chidi alikata simu kisha akakumbuka wazo hilo alilipataje na ni kwanini afanye hivyo….

ONA SASA ROBO SAA KABLA YA KUPIGA SIMU ILIKUWA HIVI KWA CHIDI

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
"hapa nampeleka huyu mtoto, lakini sijui imani ya huyo mwanamke ipo,… Kqma ana roho mbaya itakuwaje?

Alijisemea kijana chidi wakiwa ndani ya gari kabla hawajashuka kwenda kunywa chai,…

"mwanamke mwenyewe simjui, afu naenda mkabidhi mdogo wangu kweli,… Ila sio tabu, ebu ngoja nimpime imani yake kama kweli ana nia nzuri"

Chidi alipata wazo hilo la kumpima imani kama kweli ana imani ya kibinaadamu au anataka tu kuishi na mdo wake tu ilimradi ni mke wa Ibrahim,

Walipofika mambo hoteli, walishuka abiria wote ili kuoata chai, lakini waliposhuka mbele yao kama kilomita moja hivi kuna ajali ilitokea, hivyo shamra shamra za hapa na pale zilikuwepo huku magari ya zimamoto yakiwa yanapishana kwa ving'ora,… Sasa papo hapo chidi akapata wazo jipya,.. Wazo la mwanzo alitaka kumwambia shemeji yake kuwa, hatuji, wazazi wamekataa kuja na halima huko mjini,… Sasa alipoona ving'ora vinapita pita kwenda kwenye hio ajali, hapo happ nae akapata wazo jipya na kupiga simu kwa shemeji yake…. Na ndio pale kuna muda shemeji alipagawa baada ya kusikia ving'ora vya zimamoto vikilindima… Basi shemeji akajua hii ni ajali, kilio kilimuanza na hapo chidi akajua kiwa shemeji yake hana nia mbaya, na anafaa kuishi na mdogo wake,

TUENDELEE MBELE… HIO ILIKIWA NI ROBO SAA KABLA YA SIMU KUPIGWA

Chidi akiwa yupo MOMBO HOTEL akiwa yupo na mdogo wake,

"mamy yangu, kula wewe safari ndefuuu"

Chidi alimwambia mdogo wake hivyo huku wakifurahia maisha,… Kiukweli chidi na mdogo wake wa kike walikuwa wakipendana sana, mana ndio mdogo wake wa mwisho, yaani akitoka chidi ndio anakuja halima, japo baada ya chidi wazazi walitulia kidogo na ndio mana halima na chidi wamepishana miaka mingi sana mana wazazi walipumzika kama miaka kumi na zaidi, ndipo wakaamua kuendelea na kupata wa kike ambae ni halima,…

Masaa kadhaa mbele walimaliza kunywa chai huku chidi akimpitisha mdogo wake katika supermarket ili achukuwe chochote anachohitaji,..

"kaka… "

"sema dada angu"

"kwako kuzuri ee"

"ndio… Yaani ni kuzuri mno na utakuwa unaishi na kaka Ibrahim"

"mmmhhh kaka mi staki kukaa na kaka Ibrahim"

Halima pia alikuwa akijua kaka yake Ibrahim hakuwa na utani na watoto, yaani ukizingua tu hakuachi, yaani hapendi pendi ndugu sjui ni kwanini,…

"halima, kaka Ibrahim kaoa, na ana mke mzuri afu ana roho nzuri kuliko hata mimi"

"kuna TV"

"ndio, TV ipo ila nataka usome staki uangalie TV"

"kaka hata katuni tu"

"weeeeee, kwani kule kijijini kulikuwa na katuni"

"mmnhhh basi kaka, nitasoma"

Chidi alikuwa akiongea na mdogo wake na kumpa maneno mazuri tofauti na kile anachokitaka, chidi hakuwa akitaka mdogo wake afanye yale yasio na maana katika elimu ya sasa hivi

"halima mdogo wangu?… Nataka usome ili ukajenge ile nyumba kule kijijini sawa"

"haaaaaaaaaaaa kaka, kwaio mimi nikasomee ufundi au"

"ah ah sio hivyo,… Namaanisha usome kwa bidii ili uje upate kazi nzuri ili wazazi wetu wasiishi sehemu kama ile, sawa"

"sawa kaka… Nimekuelewa"

Safari yao ilikuwa ikizidi kusonga mbele

Tukija huku kwa akina Ibrahim, tunamkuta mke wa Ibrahim akiwa anapumua kwa nguvu kumaanisha afadhali, mana chidi alimdanganya shemeji yake kuwa wamepata ajali…

Masaa nayo yalisonga na sasa ni mida ya jioni kama saa 10, chidi akiwa ndio anakaribia kuingia katika jiji la arusha

Chidi alinyanyua simu yake na kumpigia mama sarah,

"haloo mamy"

"waaaooo chidi wangu, upo wapi sasa hivi"

"heeeeee nipo usa nakaribia kufika stendi"

"weeee, lazima nije nikupokeee yaani nimekumis we mtoto"

"eeti eee"

"sanaaaaa"

"sawa basi uwahi"

"yaani ndio natoka sasa hivi hapa"

"sawa"

Walikata simu huku mama sarah akijiandaa kutoka, mana usa mpaka stendi kwa basi ni karibu sana, haiishi hata nusu saa,..

"mama unaenda wapi"

Aliuliza sarah huku akimuangalia sana mama yake

"kuna mgeni wangu nampokea hapo stendi, we endelea kuwepo hapa sawa"

"sawa mama"

Basi mama sarah kawasha gari yake kisha huyoo anaelekea stendi ya basi ili kumpokea kijana chidi,..

Sasa wakati mama sarah anatoka, na mama Miriam nae ndio alikuwa anakuja kufanya biashara ya kuuziana hio hoteli ili iwe yakwake, mana alimkabidhi aisimamie kama rafiki yake, lakini huyo huyo rafiki yake ambae ni mama sarah, nae anataka ainunue iwe yakwake, sasa hapo wamepishana,…

Mama Miriam aliingia katika hoteli yake hio, ukumbuke hoteli zote mbili ni za myu mmoja ambaye ni mama Miriam au Agness,.. Sasa mama huyo kaja ili kufanya biashara ya kumuuzia rafiki yake hoteli moja,… Na rafiko yake huyo ambae ni mama sarah na ndio katoka sasa hivi tu,…

Wakati huo kijana chidi nae ananyanyua simu na kumpigia shemeji yake kuwa ndio anaingi stendi ya basi sasa hivi… Shemeji huyo alifurahi sana na haraka haraka aliwasha gari yake ya thamani kubwa, ili kwenda stendi…

Afu tukija huku hoteli, mambo yanakuwa hivi

"sarah mamy yako yuko wapi"

Mama Miriam alimuuliza sarah ambae ni rafiki wa miriam kama ilivyo kwa wamama hao,..

"mamy katoka sasa hivi tu, kuna mgeni kaenda kumpokea"

"hhhooo hatochelewa kurudi"

"sidhani mama"

Mama miriam alivuta kiti na kukaa ili kumsubiria,….

Sasa na huku kwa mama sarah, simu yake nayo ilikuwa ikizima chaji, kana kwamba hawezi kupatika kwa wakati huo akiwa hapo stendi

"hata simu yake haipatikani"

Aliongea mama miriam baada ya kumpigia simu mama sarah,… Sasa kwakuwa ishu hio ilikuwa na umuhimu sana hivyo mama miriam akaamua amtume sarah stendi ili sarah akampokee huyo mgeni, afu mama yake arudi huku ili mikataba na biashara iendeleee…

Sarah aliwasha gari yake na kutoka kuelekea stendi ili akashike zamu ya mama yake kwa huyo mgeni,…. Wakati huo mama sarah yupo stendi anazunguka huku akiwa kaichomeka simu yake katika chaji ya gari,

Wakati huo shemeji wa chidi ndio anakaribia kufika stendi,…. Sarah nae ndio anafika stendi,.. Na basi alilopanda chidi ndio linatua stendi….

PATAMU APO

Kama unakumbuka sarah na chidi walishawahi kukutana tena waliseidiana, nakumbuka chidi ndio alikuwa anaingia mjini, kwa bahati mbaya akapata majanga hapo hapo stendi, katika harakati za hapa na pale akapatikana hana hatia, lakini chidi alikuwa keshaumizwa kwa kupigwa na wananchi, lakini katika hali ya kumsubiri kaka yake Ibrahim aje amchukuwe hapo stendi, ndipo alipokutana na sarah,.. Sarah alipomwona chidi ana majeraha alimseidia kumpeleka hospitali na kujikuta nampenda kijana huyo, Sarah alivutiwa sana kimapenzi na kijana chidi lakini chidi hakujua kama sarah alikuwa akimpenda kimapenzi,.. Sarah alimtibu kijana chidi mpaka akapona, hata bili ya matibabu alilipia yeye sarah,… Sasa sarah hakumwambia chidi kuwa anampenda, ila nakumbuka kuna siku walipelekana mpaka nyumbani kutoka hospitali, Sarah alimwonyesha chidi kwa vitendo lakini chidi bado alikuwa haelewi, kana kwamba alikuwa bado ni mshamba mshamba hivi,..

Sasa toka siku hio, hawajawahi kukutana tena, yaani sarah aliizungukia ile nyumba ya akina chidi kila siku lakini hamkuti kijana chidi,… Ni kipinde kile anauza chipsi kwa kaka yake hivyo alikuwa bize sana, hata muda alikuwa hana, mana alikuwa akitoka saa 11 asubuhi na kurudi saa 3 usiku, hivyo kwa mtu aliokuwa akimfuata ni lazima amkose, na sarah hakuwa akijua mahali alipokuwa akifanya kazi kijana chidi, na ndio maana hakuweza kumpata kwa muda wote huo..

Sasa leo kijana chidi akiwa ndio kaingia stendi na mdogo wake halima,.. Chidi akiwa ndio anaangalia mizigo yake ikiwa inashuka katika basi hilo,…

Wakati huo mama sarah ndio anaiwasha simu yake, sekunde chache tu baada ya kuiwasha simu ikaita, kuangalia jina aliona ni AGNESS aliipokea na kuongea nae,

"haloo mama miri habari yako"

Aliipokea mama sarah na kuanza kuongea

"safi tu, sasa mimi si ndio nimekuja huku nakusubiria"

"ooohh umeshafika hapo"

"ndio, na nimekuja na makaratasi yote"

"ok, basi nisubiri nakuja sasa hivi"

"ok sawa"

Mama sarah alikata simu kisha akageuza gari yake na kurudi hotelini ambako ndipo anaposubiriwa na rafiki yake au ndugu yake,..

"ngoja niwahi kusaini mikataba ya kazi kisha nirudi kumpokea boy wangu"

Alijisemea hivyo huku akiendelea kwenda

Sasa huku stendi, shemeji mtu keshafika huku akizunguka na kubofya simu yake ili amuulize kashukia wapi, mana stendi ni kubwa sio ukiambiwa nipo stendi tu basi ukifika umuone, hapana bali utatafuta sana kama hamuna mawasiliano ya simu, Jasmini au mke wa Ibrahim aliiweka simu yake sikioni huku simu ikiita, chidi aliipokea simu hio ya shemeji yake

"haloo shem uko wapi mie nimeshafika stendi"

Aliongea Jasmini huku akiangaza macho yake huku na kule ili kuweza kumwona shemeji yake, wakati huo kijana chidi alikuwa akiendelea kuisimamia mizigo aliokuja nayo, matunda matunda na vitu vingi kama zawadi kutoka tanga,..

"njoo kuna gari moja mpya mpya hapa ila sijaisoma jina lake"

"ooohhh sjui ndio wewe hapo"

Unajua ubaya ni kwamba hawajuani, chidi hamjui shemeji yake na hata shemeji hamjui chidi, na ukumbuke hapo hapo stendi, sarah nae anamtafuta mama yake ili amwambie kuwa mama miriam anamsubiri kule hotelini, lakini kwa sisi tunajua mama sarah keshaondoka kitambo sana,….

"yupi uyo, ebu njoo hapa karibuni uniguse kabla hujakata simu"

Aliongea kijana chidi kuwa huyo shemeji yake aje amguse bega akiwa kabla hajakata hio simu

Sasa chidi kuangalia mbele ya macho yake aliina binge la dada, yaani mwanamke wa hali ya juu, akiwa kampa mgongo chidi alihisi labda huenda ndio yeye,

"hhhhmmm kaka hawezi kuoa mwanamke kama yule"

Sasa Aliongea hivyo kwa sauti kubwa bila kujua kuwa simu bado haijakatika,…

"unasemaje"

Chidi alishtuka mana alisahau kuwa alikuwa akiongea na simu,..

"aah ahh apana we njoo uniguse hapa ila usikate simu"

Sasa wakati huo sarah kwa mara ya kwanza ndio anamuona chidi,

"heeee yule sio chidi ninaemjua yule"

Alijiongelea sarah huku akiangalia kwa umakini mkubwa ili kuweza kumgundua kama ndio yeye au sie,.. Mana kwa sasa chidi kang'aa kuliko hata mwanzo walipokutana,

"heeeeee lakini chidi hakuwa mweupe kiasi kile"

Aliongea sarah huku akiendelea kuongea mwenyewe kimoyomoyo,…. Sasa wakati huo Jasmini ambae ndio shemeji mtu ndio alikuwa nyuma ya chidi yupo tayari kumgusa, sasa akawa anaogopa kumgusa, anahofia kugusa mtu wa watu ambaye sie aliomtegemea,… Sasa sarah akahisi huyo mwanamke ana nia mbaya na chidi, bila kujua kuwa huyo ndio shemeji wa chidi…

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
50 Muuza Chips Simulizi
Jiunge kwenye mazungumzo
Chapisha Maoni