Mwandishi: MoonBoy
SEHEMU YA HAMSINI NA TANO
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Ila shida ya mama sarah kwa kijana chidi, ilikuwa ni kutaka kumuona huko alipo yupo wapi au yupo na nani,… Na hicho siku ile kilikuwa ni cha kweli, alimwona chidi akiwa anachota maji korongoni,.. Lakini hicho sicho kilichomleta,… Na hapo ndani walikuwa watatu, yeye mama sarah, mama saida na mganga, lakini siku ile tulihadisiwa watu wawili, sasa ukweli ni huu, walikuwepo watatu,..
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI
SASA ENDELEA...
"ili mtoto wako awe kama wanaume wengine,… Nataka ulete mbegu za kiume kwa mwanaume rijali,.. Ukishazipata hizo uje na chupi yako ambayo umeitumia jana au hata leo, au uje nayo ila usiifue, uje nayo hivyo hivyo, na siku hio ukija uje na mtoto wako,.. Na vitu hivyo viwili tu"
Hayo yalikuwa ni masharti ya mganga,..
"ndio babu, tutaweza kufanya hivyo"
"kikopo hiki hapa, hakikisheni mbegu hizo mkizipata, zisipitishe masaa saba ndani ya kikopo hicho,.. Nazitaka zikiwa bado zamoto moto, na hiki kikopo kitazilinda ndani ya muda huo"
"ndio babu, tunakuahidi tutaweza"
Waliongea kwa pamoja wawili hao,.. Kisha wakaruhusiwa kwenda wakafanye kazi hio… Lakini mama sarah bado alikuwa na dukuduku la kitaka kujua, mama saida ana nia gani na mbegu hizo,.
"kweli napenda pesa, lakini mtoto wa watu maskini ya mungu Grace mie"
Mama sarah alijiongelea kimoyomoyo huku akiwa tayari kumuuliza mama saida,
Sasa wakiwa njiani, na wameruhusiwa kuongea ila ispokuwa wakati wa kuja ndio hawaruhusiwi, ila wakati wa kwenda wanaruhusiwa hata kupiga kelele,..
"mama saida… Samahani ndugu yangu, nina swali juu yako"
Aliongea mama sarah ili amuulize sabu ya kutaka mbegu hizo ni nini
"Usijali mama sarah, niulize tu na nipo tayari kukujibu, mana unaniseidia sana"
Aliongea mama saida huku wakipaki gari pembeni ili waongeee vizuri
"mimi nataka kujua kwanini unazitaka mbegu za kiume,… Na mbaya zaidi mganga anataka na chupi yako ambayo imetumika na isifuliwe, kwanini, hebu nijuze nami niifanye kazi yako kwa amani"
Mama sarah alimuuliza mwanamke mwenzie ili ampe ufafanuzi juu ya hitaji lake la mbegu za kiume
"mama sarah, kiukweli naumia kila siku katika maisha yangu,… Nina pesa nyingi sana nina watoto wawili, ni wazazi wangu wote wawili, na pia nina mume"
Aliongea mama saida huku akitokwa na machozi ya huzuni
"najua una familia kubwa sana mama saida, ila kwanini unataka mbegu za mpenzi wangu"
"afadhali wewe una mpenzi rijali kuliko mimi"
"kwani wewe una nini mama saida, mbona kila kitu unacho"
"mama sarah, wewe ni mwanamke mwenzangu, sitaki kukuongopea hata kidogo…. Nakumbuka siku ile nilipokuwa najifungua, kuna kitu nilikikosea pale hospitalini"
Aliongea mama saida huku akitokwa na machozi ya uchungu..
"una maanisha nini mama saida,.. Na ulikosea nini huko hospitalini? Naomba uniweke wazi ili nijue nakuseidia vipi"
Wanawake mnatakiwa kuwa makini sana pale mnapokuwa mnajifungua, coz kuna vitu visipoenda sawa unaweza kumharibu mtoto, haswaa mtoto wa kiume, hii hua wanasema kazaliwa na hali hio lakini haina ukweli wowote, bali ni pale anajifungua hakuwa makini au waseidizi hawakuwa makini,… Haya ni mambo ya zamani sana ila kwa sasa sijui kama ipo, mana mwanamke akijifungulia hospitali ni lazima awekewe umakini wa hali ya juu,… Hivyo kwa sasa tunaweza kusema ni ngumu kutokea ishu kama hio, ila ukumbuke hii ni stori ila vitu kama hivyo vilishawahi kutokea japo sijavishuhudia kwa macho yangu, lakini vipo na vinatokea, hivyo umakini unatakiwa haswa kwa hawa wasichana wasiojua mambo kama hayo.. Mana wamama wanayajua haya ya kua makini sehemu kama hio,…
Mama saida yeye sijui kakosea nini katika familia yake, lakini inaonekana ana shida sana na nguvu za kiume, sasa sijui zina faida gani kwake,..
"afadhali wewe una mpenzi rijali kuliko mimi"
"kwani wewe una nini mama saida, mbona kila kitu unacho"
"mama sarah, wewe ni mwanamke mwenzangu, sitaki kukuongopea hata kidogo…. Nakumbuka siku ile nilipokuwa najifungua, kuna kitu nilikikosea pale hospitalini"
Aliongea mama saida huku akitokwa na machozi ya uchungu..
"una maanisha nini mama saida,.. Na ulikosea nini huko hospitalini? Naomba uniweke wazi ili nijue nakuseidia vipi"
Mama sarah alikuwa akitamani sana kujua kipi kimemkuta rafiki yake, yaani licha ya kumpa kazi lakini bado ni mara wakubwa tu,..
"mama sarah, si unamjua mwanangu Ridhiwani"
"ndiooo, si kale kahensam kako"
"basi, ana shida ya nguvu za kiume"
"heeeeeee mama saida, unasema kweli… Na umejuaje kama yupo kwenye hali hio"
"niliambiwa na baba yake,.. Na baba yake alipomuuliza kuwa hali hio imeanza lini, akamwambia hajawahi hata kusimamisha"
"jamani, ridhiwani mwanangu poleeee….. Usilie basi mama saida"
"inatia uchungu mama sarah, naona watoto wa wenzangu wanabadirisha wanawake, lakini mwanangu ndio kwanzaa hata furaha hana"
Aliongea mama saida huku akilia kwa uchungu wa mtoto wake kushindwa kufanya chochote na mwanamke,…
Mama sarah nae alilia kwa kuskua hivyo mana wote ni wazazi ila sema mama sarah hakuwa na mtoto wa kiume, yeye alijaaliwa kupata wakike tena kama wa dawa vile…
"mama saida, kwa jinsi mtoto wako alivyo na heshima kiasi kile, lazima nimseidie mwanao, najua mtoto wako ni wangu… Nipo tayari kuifanya kazi hio"
Aliongea mama sarah huku akimpa moyo rafiki yake mama saida,.. Mama sarah yupo tayari kuzipata mbegu hizo ili wazipeleke kwa huyo mganga Ridhiwani apate kupona,..
"nitashukuru sana mama sarah"
"ila mama saida, kwanini yule mganga anataka chupi yako, anataka aifanyie nini"
"aliniambia kuwa hio siku nikizipata hizo mbegu niende nazo na hio chupi yangu iliotumika tena isifuliwe,.. Na nikienda niende na ridhiwani,..afu zile mbegu Mganga atazinenea maneno yake, kisha atazimimina kwenye hio chupi yangu, alafu anaitwa ridhiwani ajipakalie zile mbegu kwenye uume wake kwa kutumia chupi yangu,… Kwahio mganga kasema ni lazima iwe chupi yangu, yaani pale akiwa anapakalia hivyo, ni kwamba anazitafuta hisia kupitia chupi yangu,.. Hapo imetumika imani ya kishirikina zaidi, na bila hivyo mtoto wangu hatokuwa lolote grace"
Mama saida aliongea kwa kirefu mpaka mama sarah akashindwa kuongea kwa uchungu, hakuna kitu kinauma kama mama kugundua kuwa mtoto wake wa kiume hafanyi kazi (hasimamishi) inauma sana haswa kwa wamama,….
Basi mama sarah alikubali kwa moyo wote kuifanya kazi hio… Lakini moyoni mwake aliongea maneno kadhas kuwa
"maskini ya mungu chidi wangu utanisamehe tu, sikujui hunijui ila ridhiwani namjua, ni kama mtoto wangu.. Ila ukikosa nguvu za kiume nami nitakuwa na nani… Mbona napata mtihani mkubwa hivi… Au sijui nikuhamishe mji ili ishindikane kwa upande wako, MANA SIO LAZIMA UWE WEWE TU, HATA KWA WENGINE INAFAA"
NA HUO NDIO MWISHO WA KUMBUKUMBU ALIOTUPATIA MAMA SARAH,.. MWANZO ALITUDANGANYA LAKINI HII SASA NDIO YA KWELI, SABABU YA CHIDI KUTAMANIWA NGUVU ZAKE ZA KIUME…. SASA TUENDELEE NA SIMULIZI YETU, HAPA HAKUNA KUMBUKUMBU TENA…
Sasa tukija huku kwa jasmin ambaye ni mke wa Ibrahim akiwa bado hakati tanaa na shemeji yake, kila mara ni kumpigia simu tu,…
Safari hii simu hio ilipokelewa, na ni chidi mwenyewe ndio kapokea akiwa anaendelea kumenya viazi,..
"haloo shem shkamoo"
Alisalimia kijana chidi huku akiwa bize sana na kazi, mana kwa wakati huo ameambiwa akaange chipsi za member wote wa hoteli hiyo, ili waonje radha yake,.. Hivyo ni kama chidi yupo kwenye interview, kwahio hapo akikosea tu basi hana, hata kama kaletwa na boss mkubwa,..
"staki bwana chidi, mi nimeshakwambia kuwa mimi sio mkubwa kiviile, ni umbo langu tu"
"ok sawa, sema ulikuwa unasemaje"
"no, kwenye simu hatuwezi ongea, naomba uje nyumbani"
"nije kufanya nini huko"
"we njooo tuna maongezi na wewe"
"ya maana au umbea tu"
"yaani chidi mi nimekuwa mbea"
"samahani basi"
"ili nikusamehe, jioni njoo nyumbani"
"sawa basi nitakuja"
"kweli jamani shem?"
"ndio nitakuja"
Jasmini alifurahi mno kuskia chidi atakuja, jasmini alikata simu kisha akampandia hewani myne wake ambae ni Ibrahim,
"baba king, mdogo wako kakubali"
"kakubali kuishi nasi"
"No, kakubali kuja tuongee nae"
"ehehehehe safi sana mke wangu,.. Sasa andaa maneno ya kumshawishi ili tuishi nae mana nampenda sana mdogo wangu, ila kwa yale niliomfanyia, sijui kama atanielewa"
"Usijali mume wangu, hilo niachie mimi"
"nakuaminia mke wangu"
"sawa, but leo uwahi wahi basi"
"sawa mamy"
Simu ilikatwa, lakini jasmini alikuwa alifurahi huku akijiangalia umbo lake la kichokozi,.. Mana jasmini kaumbika ana shepu isio ya kifani,..
Jasmini alitoka nje ya shumba yake na kwenda kwa majirani ambao ni maskini sana, ila sijui kafata nini huko kwenye nyumba za walala hoi,…
Sema uzuri wake ni kwamba anaongea na watu vizuri na wala halingii utajiri wao, nyumba hio ambayo imeingiliwa na mwanadada tajiri, ilikuwa ikimfahamu vyema,..
"karibu mama king"
Alikaribishwa na mwanamke mmoja mlala hoi,
Lakini mama king au mke wa Ibrahim yete alikuwa akiangalia kanga ambazo zilikuwa zimeanikwa katika kamba,..
Mlala hoi alishangaa kuona mwanamke huyo tajiri kaja nyumbani kwake tena huku akiwa anaangalia kanga zake…
"mama king kulikoni na kanga zangu"
Aliongea mlala hoi huku akiwa muoga mana hua baadhi ya walala hoi wanawaogopa sana matajiri,..
"samahani mama nanii… Nataka tuongee zaidi"
Aliongea mama king huku akimshika mkono yule mwanamke na kuingia nae ndani,..
"heeeeee wewe mama king angalia usiniletee bakas kwa mume wako"
"heeeeee sasa wote ni wanawake, hilo balaa litoke wapi"
"aahhh anaweza hizi vibaya tu"
"usijali mama naniii… Sasa skia mimi nina shida"
Aliingea jasmini huku wakikaa kwenye makochi,..
"ivi na nyie kumbe mnakuaga na shida, haya shida gani tena"
"najua wewe ni mtoto wa kisambaa, mtanga halisi, nataka unifundishe kitu"
"mmmhhhh ni kweli mimi ni mtanga, ila wataka nikufundishe nini"
"kwanza kabisa,… Nataka nizinunue zile kanga zako"
"heeeeeee mama king,.. Na utajiri wako woote unakuja kununua kanga kwangu,.. Tena zimeisha namna ile"
"mimi nitakununulia Kabati zima la nguo mpya tupu, lakini unipe hizo kanga zako zilizoisha isha, mi nimezipenda tu"
Wanawake ni watu wenye akili nyingi sana, ila sema asilimia 90 ya akili hizo hua sio za maendeleo, asilimia 10 ndio zinakuaga na maendeleo lakini hizo 90 wao huwaza starehe, nikimaanisha wanawaza pesa kutoka kwa wanaume,… Wanawaza jinsi ya kumpata mwanaume yaani wao wanawawazia wanaume ili kujikwamua kimaisha,.. Hebu kama kuna mschana ambae hajawahi kula pesa ya mwanaume yeyote yule anyooshe kidole juu, hata kama ni ndogo lakini kuipata kwake hio ndogo ulitumia akili nyingi, mana wanaume wa sasa hivi tumeshaelimika kiasi flani, sio sawa nanzamani,… Ila kwakuwa wanawake ni watu wenye akili mingi za kumbana mwanaume, basi kuna wale wajinga wajinga kama sisi bado tupo tunamalizia kuzifunga zile asilimia zao 90,.. Maskini ya mungu watabakiwa na asilimia chache sana, na hizo ndio asilimia za kuolewa,…
INAENDELEA...
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi