Mwandishi: MoonBoy
SEHEMU YA HAMSINI NA NNE
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
SASA HAPA WACHA TUUJUE UKWELI HALISI JUU YA WAWILI HAWA, MANA ULE UKWELI WA MWANZO NADHANI ULIKUWA NI UONGO… SASA HEBU TURUDI NYUMA KWENYE MAELEWANO YAO YALIKUWAJE
Sasa tukiwa tumerudisha siku nyuma, kama kumbukumbu jinsi ilivyotokea
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI
SASA ENDELEA...
Mama sarah na mama saida walikutana katika hoteli moja hivi ya hadhi ya kawaida tu, walikuwa wakiongea mambo mengi sana kwa ajili ya kuendeleza maisha ya kitajiri juu ya maisha yao,..
Sasa wakiwa wanaendelea na maongezi yao mara simu ya mama sarah iliita, kuangalia alikuwa ni kijana wake chidi,…
"haloo boy wangu mambo"
"safi mamy hali yako"
"aahhh nzuri tu.. Nilikuwa nakusalimia tu"
"ahsante sana boy wangu"
Simu ilikata huku mama sarah akiwa anarembua kwa jinsi anavyompenda chidi,…
"heeeee nani tena uyo, mpaka macho umebadirisha kabisa"
"hhhhmm we acha mama saida, si unajua wazee wetu wamechoka"
"nalijua hilo"
"sasa nina mtoto huyo, we acha ti, yaani nipo tayari kumhonga kitu chochote kile akitakacho, lakini asiwe mbali na mimi"
"kwanini mama sarah"
"yaani mtoto anapiga mashine, heeeee sijapata kuona"
Lakini sasa mama sarah akiendelea kumsifia chidi, huku mama saida alikuwa anakasirika, mama sarah hajui kama mwenzie kakasirika kwa kusikia kijana flani anasifiwa
"yaani huyo chidi, ni hensam kama yule mtoto wako ridhiwani"
Yaani mama saida kusikia hivyo ndio hasira zinazidi kumjaa….
Mama sarah alishangaa kuona rafiki yake anakasirika sana…. Lakini ghafla mama saida akacheka kicheko cha furaha, yaani kile cha kutabasam… Mama sarah nae akavuta tabasamu zuri huku mama saida akimwambia mama sarah kuwa
"ivi mama sarah, wewe unapenda pesa au mwanaume rijali"
Mama sarah kwa furaha akajibu
"mimi napenda vyote"
"no, nataka useme kimoja… Mfano nakupa Bilioni moja afu uachane na huyo mtu wako upo tauari"
"hhhhmmmm mama saida, una maana gani na huo mfano wako"
"huo sio mfano, bali namaanisha kweli"
"sasa unamaanisha nini"
"nahitaji hizo nguvu za kiume za huyo kijana,… Nina kazi nazo,.. Na ukifanikisha, Bilioni moja ipo mezani"
"Whatt???????"
"unashangaaa nini sasa??… Kama utaweza niambie twende mahari nikupe njia"
Katika sehemu kadhaa zilizopita mama sarah alionekana kwenda moshi kwa mganga ili waweze kummiliki kijana chidi yeye kama yeye,. Na alifanya taratibu zote sisi tukajua ni yeye kwa faida yake, kumbe wala hata sio yeye, bali kuna mtu ndio kamtuma ila katika sehemu zile mtu huyo hatukumuona au kuhadithiwa,.. Sasa leo ndio tunamjua mhusika kamili ambae anahitaji mbegu za kiume, tena za kijana rijali zaidi kuliko wote, hivyo huyu mama saida sio kwamba ni lazima awe kijana chidi tu, ila kwakuwa kazipata sifa zake hivyo akaona agande hapo hapo mana sifa zake keshaambiwa,.. Maskini kijana chidi anaandamwa na matatizo kama hayo kisa ni utundu au urijali wake ndio unaomtesa kutaka kuchukuliwa nguvu za kiume kwa njia ya ushirikina, na kama watapata mganga wa kweli basi zoezi hilo haliwezi kushindikana,… Mama saida alikuwa akizihitaji mbegu hizo ila hatukujua ni za kazi gani katika maisha yake,… YOTE HAYO TUTAYAJUA MBELE
"ivi mama sarah, wewe unapenda pesa au mwanaume rijali"
Mama sarah kwa furaha akajibu
"mimi napenda vyote"
"no, nataka useme kimoja… Mfano nakupa Bilioni moja afu uachane na huyo mtu wako upo tauari"
"hhhhmmmm mama saida, una maana gani na huo mfano wako"
"huo sio mfano, bali namaanisha kweli"
"sasa unamaanisha nini"
"nahitaji hizo nguvu za kiume za huyo kijana,… Nina kazi nazo,.. Na ukifanikisha, Bilioni moja ipo mezani"
"Whatt???????"
"unashangaaa nini sasa??… Kama utaweza niambie twende mahari nikupe njia"
Aliongea mama saida huku akitabasamu kwa kusikia kua kuna kijana rijali zaidi..
"mama saida, hivi unamaanisha milioni moja au bilioni moja, mana kama vile sijaskia vizuri hapo"
"i mean Bilioni moja tasilim, tena hata ukitaka before ya kazi nakupata"
Mama saida alikuwa ni tajiri kuliko hata akina miriam, mana akina miriam ni matajiri kuliko hata akina sarah, sasa leo tunakutana na kifaru anaetaka kutoa bilioni moja kisa ni mbegu za kiume tu,..
"siamini macho yangu mama saida…. Ila sawa kazi yako ni nyepesi sana kwangu, lakini huyo kijana wangu atakosa nguvu za kiume kabisa"
"yaani hata dede hatoweza,… Atakuwa zaidi ya shoga"
"mungu wangu mtoto wa watu"
"kama hutaki sema"
"wacha nikutafutie mwingine, lakini huyo mmmhhh niachie mama saida"
"hapana,… Namtaka huyo huyo,.. Yaani hata ukitaka nikuongeze pesa nipo tayari, lakini awe huyo kijana wako"
Sasa mama sarah aliposikia kuna kuongezwa pesa… Aliwaza mambo mengi sana
"mfano akinipa hio Bilioni moja… Afu nikichanganya na ile yakwangu ya kununulia hoteli moja.. Si ninaweza kuwa na hoteli mbili… Hapana, kama ni rijali nitapata tena, wacha nifanye maisha kwanza"
Mama sarah alijisemea kimoyomoyo huku akimwangalia mama saida..
"nipo tayari, na nitakuletea,… Ila nipe njia ya kufanya na nikizipata nifanye nini"
"hapo sasa sawa… Kinachofata sasa hivi twende Moshi"
"moshi??….moshi kufanya nini tena"
"kwa mganga"
"eeehhhh,… Haya twende basi"
Mama sarah alishangaa kumuona rafiki yake mama saida ana mambo ya kwenda kwa waganga, mama sarah hakupenda swala hilo, ila analifanya kwa shinikizo la pesa…
JAMANI HII NI KUMBUKUMBU ILI TUJUE KWANINI MAMA SARAH ANAHANGAIKA NA VIKOPO KISA NI MBUGU ZA KIUME, MWANZO TULIJUA NI KWA FAIDA YAKE, KUMBE HATA SIO YEYE ANAEZITAKA MBEGU HIZO… JE UNAJUA ZINA KAZI GANI???…. TWENDE SAMBAMBA
Wakiwa katika barabara ya kuelekea moshi, wakiwemo wamama wawili wenye pesa zao,….
Sasa siku ile mama sarah tulisimuliwa akiwa peke yake, kwenye gari lakini kumbe hakuwa peke yake,… Walikiwa wapo wawili lakini sisi tulimwona au tulihadithiwa mama sarah peke yake lakini walikuwepo wote humo ndani ya gari,…
Wakiwa ndani ya gari mama saida alikumbuka siku ya kwanza alipoambiwa na mganga kuwa
"unapokuja huku kwa mara nyingine, naomba usiongea na mtu yeyote wala simu yeyote ile.. kutoka ulipotoka, hata kama una mtu ndani ya gari usiongee nae"
Alikumbuka mama saida.. Sasa kama aliambiwa kuwa asiongeee Je? Mama sarah alipajuaje hapo kwa mganga na wakati hajawahi kwenda na wala hapajui tena hata kisikia hajawahi, lakini kaenda kama mwenyeji…
PATAMU APO
SASA TUACHANE NA KUMBUKUMBU YA HAWA WAMAMA, SASA TUJE KWENYE LAIVU, KISHA TUTARUDI KULE
Tukija huku kwa kijana chidi akiwa ndani ya jiko la kukaangia chipsi,.. Huku akishangaa kukutana na rafiki yake saidi,.
"chidi,.. Siamini kama upo hapa leo"
Aliongea kijana saidi huku akimkumbatia rafiki yake, mana toka chidi alipofukuzwa na kaka yake, basi aliweza kupoteana na kila mtu ambae alikuwa akimuona katika mazingira yale,..
"usijali jamaa yangu, leo nipo nawe hoteli moja"
Saidi alilia sana mana ni rafiki yake, na anakumbuka hata chumba cha chidi, huyu saidi ndio alikitafuta
"lakini saidi, wewe si unajua geto kwangu wewe"
"ni kweli,.. Napajua haswaa tena mimi si ndio nilikutafutia chumba"
"sasa kwanini hukuja, au we rafiki mnafiki"
"hapana chidi… Kaka yako aliniambia kuwa imekwenda kijijini mana usingeweza maisha ya mjini… Ila mimi sikuamini maneno yake kuwa wewe haupo mjini… Nilikuwa nakuja pale kwako kila siku, lakini kila nikija sikukuti asubuhi sikukuti, jioni sikukuti.. Ndio nikaamini kweli utakuwa umekwenda kijijini"
"aaahhh pole sana best yangu,.. Ila Usijali leo tupo pamoja"
Ni kweli chidi alikuwa haonekani nyumbani mana yeye alikuwa ni wakwanza kuamka na ni wamwisho kulala, hivyo kwa mtu aliokuwa akimfuatilia nyumbani ni ngumu kumpata mana anarudi saa 6 usiku anaamka saa 11 alfajiri,… Sasa kama unamfatilia utampata wapi…
"nyie watu?.. Habari zenu"
Iliskika sauti nzuuri ya kike, tena ilikuwa ya kipole sana na yenye msistizo wa kuwaita watu
"salama boss"
Wote waliitikia kwa pamoja kwa kumuita boss lakini alikuwa ni mschana mzuri sana, mtoto alikuwa ana rangi ya chocolate, umbo lake lilikuwa halina mfano, mtoto alikuwa ana kiuno kilichobonyea ndani,… Sasa ukimwangalia na hio suti aliovaa, mungu wangu kiukweli aliwavutia wengi sana, sema mbaya zaidi ni mtoto wa tajiri, na sii mwingine bali alikuwa ni MIRIAM mwenye jina la hoteli yao hio iitwayo MIRAS HOTELI
"ok, nimeskia kuna mtu mpya humu"
Aliongea kumaanisha kuna mgeni katika sekta hio ya chipsi,..
"ndio, nipo"
Alijitokeza kijana chidi huku akiangalia chini kumaanisha kuwa na heshma ya hali ya juu mbele ya boss wake huyo,.. Mana Miriam ni kama boss wa pili kutoka mama yake,.. Hivyo ana mamlaka ya kumgukuza mfanyakazi yeyote yule bila kuambiwa na mtu wala kukataliwa na mtu yeyote yule,.. Yeye ndio kifaru kama ilivyo kwa sarah kule kwenye hoteli yao…
"ok, kwa torati ya hapa, hua mgeni anatakiwa akaange chipsi kisha awapatie memba wote wa hoteli hio,.. Yaani viongozi wa juu ndio wanapaswa kupima upishi wako, mana hoteli hii ni hoteli ambayo itaweza kutumiwa hata na raisi, hivyo hatutaki mchezo katika vyakula, sawa"
"sawa boss"
Chidi alikuwa bado kaangalia chini kwa kuashiria heshma kwa boss wake, hivyo chidi aliambulia kuona miguu na umbo lakini sura hajaiona, na hata huyo bosa pia hakuiona sura ya chidi, kwasababu alikuwa kainamisha kichwa chini..
Miriam aliondoka na kwenda ofisini kwake huku akijiandaa kiandaa chipsi za viongozi wa hoteli hio ili wajue uwezo wake ulipo…
Chidi alianza kuchakalika kikazi zaidi na ni kweli chidi ni mtaalamu sana wa kukaanga chipsi,…
Lakini sasa huku kwa Miriam ambaye alikuja pale jikoni alikua akijiuliza kitu
"aahhh lakini mbona sijamuona sura yake, afu kana heshima ya hali ya juu, hebu nikamuone vizuri"
Miriam aliamka na kuelekea jikoni kwa mara ya pili ili akamuone huyo mfanyakazi mpya, mana mwanzo alikuwa kainama hivyo hajafanikiwa kumuona…
SASA TURUDI NYUMA KWENYE KUMBUKUMBU YETU KWA WALE WAMAMA WALIOPO KULE KWA MGANGA
Mama saida aliendelea kukumbuka siku hio ya leo jinsi alivyo ongea na mama sarah kuwa
"Grace,. Tukiwa safarini, hua siruhusiwi kuongea wala kupigiwa simu,.. Hivyo naomba tuwe kimya mpaka tufike kwa mganga"
Mama saida alimwambia mama sarah
"sasa kama hutoongea je mimi nitafikaje huko na wakati sipajui"
"mimi nitakuwa siti za nyuma kabisa, nitakuwa nakuelekeza kupitia kile kioo cha gari pale mbele"
Kwenye gari kuna kale kakioo kapo pale juu ya kichwa cha dereva, kile kioo ambacho unaweza kumuona abiria wa nyuma, hivyo kile ndicho kilichotumika kumwelekeza mama sarah mpaka kufika kwa mganga,….
Mama sarah na mama saida walifika kwa mganga na kuelezea shida yao,… Ila shida ya mama sarah kwa kijana chidi, ilikuwa ni kutaka kumuona huko alipo yupo wapi au yupo na nani,… Na hicho siku ile kilikuwa ni cha kweli, alimwona chidi akiwa anachota maji korongoni,.. Lakini hicho sicho kilichomleta,… Na hapo ndani walikuwa watatu, yeye mama sarah, mama saida na mganga, lakini siku ile tulihadisiwa watu wawili, sasa ukweli ni huu, walikuwepo watatu,..
INAENDELEA...
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi