Mwandishi: MoonBoy
SEHEMU YA HAMSINI NA SITA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Ila kwakuwa wanawake ni watu wenye akili mingi za kumbana mwanaume, basi kuna wale wajinga wajinga kama sisi bado tupo tunamalizia kuzifunga zile asilimia zao 90,.. Maskini ya mungu watabakiwa na asilimia chache sana, na hizo ndio asilimia za kuolewa,…
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI
SASA ENDELEA...
Sasa shemeji yake chidi sijui haoni maduka ya nguo, na sijui anabmaana gani kwenda kuomba nguo za kimaskini na wakati wao ni matajiri tena wa hali ya juu sana, sasa iweje leo akaombe kanga zilizochoka
"kwanza kabisa,… Nataka nizinunue zile kanga zako"
"heeeeeee mama king,.. Na utajiri wako woote unakuja kununua kanga kwangu,.. Tena zimeisha namna ile"
"mimi nitakununulia Kabati zima la nguo mpya tupu, lakini unipe hizo kanga zako zilizoisha isha, mi nimezipenda tu"
Yule mama mlala hoi alishangaa sana kuskia sauti ya mama king kutaka kuzinunua kanga ambazo zilikuwa zimechoka sana tena sana, tena kuna zingine zilikuwa zimechanika kwa pembeni lakini mama king au jasmini alikuwa akizitaka tu hivyo hivyo,..
Mlala hoi aliona kama ni ndoto kwa tajiri huyo kuja kumuomba nguo ambazo zimeisha…
"mmmhh sawa nitakupa, lakini ujue wewe ni tajiri sana, hivyo watu wakikuona nazo mtaani itakuaje"
"usijali wala sivai nje"
"ok nitakupa ila sitaki nguo zingine kama ulivyosema kuwa utanipa kabati la nguo"
"sasa wataka nini"
"kiasi chochote tu"
Mlala hoi aliona hio ndio chansi ya kupata chochote angalao asukume maisha,.. Ila huyo mlala hoi mwenyewe sio haba, si unajua mijimama ya tanga inavyojiachia,…
"ok nitakupa… Ila kuna kitu nataka unifundishe"
"kitu gani tena mama king"
"mama saimon… Unajua wewe ni mwanamke wa kitanga,… Ila mwenzio mi sijui hata kumtega mume wangu"
"heeeeeee mama king acha kunichekesha, ina maana na umbo lako hili zuri namna hii unashindwa kumtega mumeo"
"ndio,… Yaani nataka kila akija anikute nimevaa kanga moja, yaani sijui nifanyeje mana saa zingine anarudi akiwa kachokaaa sasa mimi sitaki achoke"
"mmmhhh ni hilo tu"
"ndio mama saimon"
Mama saimon kweli alikuwa ni jimama la kitanga, saa ngapi hawajaingizana chumbani, mama king kapambua nguo zake zote akabakiwa na chupi tu, kisha akaanza kufundishwa jinsi ya kumtamanisha mwanaume hata kama hapendi lakini akikuona tu, ni lazima apende… TAKA USTAKE UTAKULA TU yaani ni mtindo wa kufosiwa kimapenzi ila kwa hiari yako mwenyewe,…..
Baada ya Nusu saa kupita, mama king alikuwa kawiva mambo ya kitanga yaani Ibrahim atakoma,…
"hii laki tano si inakutosha"
Mama saimon hakuamini macho yake kama angeliweza kupewa pesa yote hio
"mama king, hii pesa ni kubwa sana nikisema ni ndogo nitapata dhambi sana"
"ok poa asante"
Mama king alifungiwa kanga zake kama pea tatu hivi…
Na kanga hizo kazichukiwa kwa ajili ya kumvalia mume wake kanga moja na chupi tu,.. Mana hua kanga mpya hazinogeshi na wala hazigandi kwenye mwili, ila kanga ilioisha inaganda mwili sasa kama una umbo, mungu wangu huyo atakaekuona sidhani kama atakuacha, yaani atatoka ute mpaka basi,
Tukija huku hotelini ambako kijana chidi yupo jikoni akikaanga chipsi za members wa hoteli hiyo, ili aonekane bora katika pishi lake,.. Wakati huo chidi akiwa yupo katika stoo ya mkaa, mara miriam kaingia pale jikoni na kumuulizia mpishi mgeni
"yule mkaka mgeni yupo wapi"
Aliuliza miriam huku akiangaza macho mana anatamani kumuona hata sura mana yeye ndio boss wa hapo kuacha mama yake,..
"yupo stoo"
"aah ok basi"
Miriam baada ya kuskia kuwa chidi yupo stoo aliondoka zake na kuachana na swala la kumuona sura,…
Chidi alipotoka stoo alikutana na wapishi wenzake wakimpa taarifa ya yeye kufatwa na boss,.. Miriam ni mschana mdogo sana ila kwa pesa walizonazo lazima umuone mkubwa mno…
"chidi, boss alikuwa akikuulizia"
"boss nani tena"
"boss mdogo"
"aahhh ok nitakwenda kumuona"
Basi chini akiwa kwenye interview ya mapishi tena alikuwa bize mno…
Masaa machache mbele chidi akawa keshamaliza kukaanga chipsi hizo, sasa wahudumu wakaanza kuzisambaza kwa memba wa hoteli hio,… Yaani kila mfanyakazi mkubwa wa hoteli hio ni lazima aonje pishi la kijana chidi maana kusifiwa sana na mama sarah kuwa huyu kijana ni Profesional wa kupika chipsi, hivyo maboss wake wakampa kazi ya kuwaonyesha kiwango chake,…
Baada ya lisaa limoja chidi aliitwa ofisini kwa boss mdogo,… Chidi alienda katika ofisi ya miriam huku akiwa kainamisha kichwa chake chini,
"ivi mimi ninatisha ee, si ndio"
Aliongea miriam huku akimwangalia kijana chidi,
"hapana boss"
"sasa kwanini kila unapofika kwangu macho yako yanakuwa chini kwanini"
"samahani boss"
"hebu niangalie haraka"
Chidi alifosiwa kumuangalia miriam uso kwa uso, mpaka miriam akajikuta uso wake unakunjuka, yaani alikuwa ana hasira lakini zilipungua baada ya kumuona kijana chidi,…
"ivi kuna mtu alikulazimisha kuifanya hii kazi"
"samahani boss, nina kazi kule jikoni naomba niende"
"afu unaonyesha we ni kiburi sana si ndio"
"hapana boss, nisamehe kwa hilo"
"haya shika fomu hii ya kujaza… Utajaza majina yako yote hapa ulipotoka namba zako za simu kila kitu ili tukuekee NSSF yako sawa"
"sawa boss"
Chidi alikaa pale na kuanza kuijaza ile fomu,… Lakini kabla hajajaza katika upande wa majina alikumbuka maneno ya kaka yake yaliomwambia kuwa
"unapofanya kazi mahari usipende kutumia jina sahihi, jina sahihi linaseidia lakini pia lina haribu, hivyo jaribu kudanganya ili kutakapotokea balaa, basi iwe ni vigumu kupatikana haraka, lakini ukiandika jina sahihi kukiwa na balaa, watafika hadi mlangoni kwenu… Mimi mwenyewe hapa naitwa Ibrahim, lakini kuna mahari mimi naitwa bakari, hivyo usiwe mkweli kwa kila kitu"
Alipomaliza kukumbuka hilo, hakutaka kuchelewa, chidi aliijaza ile fomu yote kisha akampa miriam ambae ndio boss wake,..
"tayari boss"
"okeee… Oohhh kumbe unaitwa Omary"
"ndio boss"
"Omary Rashidi?"
"nipo"
"ahahahahaha Sema jana na leo"
"sasa boss mi si nimeanza kazi leo, sasa hio jana alikuwepo nani"
"ooohh ok poa nenda kaendelee na kazi"
Chidi aliondoka lakini miriam alikuwa akimwangalia sana kijana chidi,…
"hiki kitoto ni kihensam mmhh"
Basi yalikuwa ni maneno ya miriam akimsifia kijana chidi kwa uzuri aliokuwa nao,…
Masaa yalisonga mbele na ilipofika mida ya saa 12 na nusu jioni muda wa kuondoka wale wa mchana na kuingia wa usiku,..
Kijana chidi alipitiwa na mama sarah ili akachukuwe chupi yake kule kwa kijana chidi….
"heeee mamy kumbe ulikuwepo hapa nje"
"ndio…. mana najua huu ndio muda wenu kutoka"
"ok… Sawa"
"sasa… Nataka twende nikachukue ile chupi yangu kule kwako"
"ati nini"
"kwani umesahau"
"aahhh ok sawa sawa"
Sasa chidi alikuwa na wasiwasi juu ya mama huyo kwenda kule, mana licha ya yeuw kutotaka kwenda kwake, lakini kule bafuni kuna chupi ya sarah, sasa huyu mama nae anataka waende wote kule nyumbani,… Sasa chidi kwakuwa ni mgeni kwenye hio hoteli alijikuta anatoka na Eploni ya kazi,..
"heeee sasa hii Eploni ni ya nini huku"
"ayaaa, nimesahau…"
"irudishe mi nakusubiria"
"hapana we tqende tu"
Mama sarah kawasha gari kisha haoo wakaelekea kwa chidi,.. Lakini chidi aliomba gari iharibike ili safari iishie hapo hapo, mana ile nguo kule hajaificha wala nini,… Tena mbaya zaidi zimeanikwa kwenye kamba moja, sasa itakuwaje…
Chidi alikuwa anawaza sana jinsi itakavyokuwa kule ndani…
Walifika nyumbani kwa chidi… Yaani chidi alitamani awe wakwanza kuingia ndani kwake,.. Sasa mbaya zaidi hata mama nae ana haraka ya kuondoka zake yaani kaja kuichukuwa tu hio nguo yake, kana kwamba hata chidi hana haja ya kuingia huko,.. Japo funguo anazo mwenyewe,..
Chidi alifungua mlango huku mama sarah akiwa nyuma yake, kana kwamba akifungua tu, mama yupo ndani mana hata yeye ana haraka… Chidi alifungua mlango na mama kaingia ndani tena kwa haraka haraka mno
Chidi alibaki kashika kichwa, atajibu nini kama ataiona ile chupi ya sarah, na licha ya kuiona tu bali anaweza hata kuijua mana ni chupi ya mtoto wake, ila chidi hajui kama sarah na mama huyo ni kitu na mtoto wake…
Mama sarah yeye alikuwa anawahi kuchukuwa nguo yake ya ndani ambayo aliiacha toka jana, hivyo leo aliamua kuipitia,… Lakini kule kulipowekwa nguo ya mama hio bado kuna nguo nyingine tena ya mschana wa haja, Kawaida ya mashoga mamy hua hawapendi vijogoo vyao (viserengeti boy) viwe na wasichana wengine, yaani wanataka wawe wenyewe tu katika swala la mapenzi,.. Mana unakuta mama anamgharamikia kijana wake, kumbe kijana huyo huyo anamaliza pesa sehemu nyingine, yaani wamama hawa wapo tayari kukupiga hata risasi mana kaona kama unacheza na akili yake, bado unacheza na pesa zake, yaani yeye anakupa pesa afu wewe unampa mwingine, heeee atauwa mtu siku hio… Na hicho ndicho anachokihofia kijana chidi, anaogopa mama huyo atajua kuwa chidi ana mschana mwingine,.. Na mbaya zaidi mschana mwenyewe ni mtoto wa huyu mama, ila hakuna anaejua hilo…
Sasa chidi kufungua tu mlango mama kapita mbio kuelekea bafuni kuchukuwa nguo yake, chidi alishindwa kumfatilia kwa nyuma mana angeshtuka zaidi, hivyo wacha aende aone afu atafute uongo, mana Mashalah wanaume tumejaaliwa kwa uongo, yaani piga ua ukiwa na demu asilimia 80 ya maneno ya mwanaume huwa ni uongo, hivyo wadada mna kazi ya ziada kwa kuupokea uongo wetu,… Mtanisamehe ila ukweli ndio huo..
Sasa ile mama anakaribia katika mlango wa bafu mara simu yake iliita,… Kucheki alikuwa ni mtoto wake sarah, ikabidi apokee simu hio, sasa hio nafasi chidi akaitumia kuingia bafuni na kuitoa ile chupi ya sarah, akaichomeka kwenye mfuko wa Eploni (nguo ya kazi) ambayo alitoka nayo kule hotelini,… Kisha akajifanya kaingia kunawa ili asishtukiwe alifata nini huko ndani,.. Mara mama kaingia na kuichukuwa nguo yake
"yes imekauka…. Twende wewe mi nachelewa"
Mama sarah alimwambia chidi kuwa waondoke mana wanachelewa…. Unajua pale wakati wanakuja, chidi alimwambia mama sarah kuwa, yeye anaenda kwa kaka yake atarudi baadae,.. Ila mama akamfosi aje huku afu atampeleka kule chidi anapopataka yeye,… Chidi hakupata hata nafasi ya kuweka ile nguo, ilibidi atoke nayo mana mama kamsimamia kwa haraka ili asimcheleweshe,… Basi chidi alipanda kwenye gari kisha, haoo wakaondoka zao..
Chidi alifikishwa sehemu fulani hivi ambapo ni karibu na nyumbani kwa kaka yake, chidi hakutaka mama huyo ajue nyumbani kwa kaka yake, hivyo alishushiwa mbali kidogo, chidi akachukuwa toyo kisha akamalizia safari yake,… Alipofika getini alibonyeza alamu, Mlinzi alitoka akafungua mlango kisha chidi akaingia, mana anajulikana na sio mara ya kwanza kuingia hapo…
Ikiwa ni mida ya saa moja kasoro hivi za jioni,..
INAENDELEA...
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi