Mwandishi: MoonBoy
SEHEMU YA SITINI NA NANE
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
"lakini mbona kama nazidi kumtia uoga"
Aliingea hivyo miriam huku akielekea zake kwenye ofisi yake….
"duuuuuuuuuuuu mi ndio mana spendi cheo chochote kile, yaani nachukia sana kufatiliwa"
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI
SASA ENDELEA...
Aliingea kijana chidi huku akikaa kwa kuchoka
"lakini ulikitaka mwenyewe, sasa ngoja ukione cha mtema kuni"
Aliingea mpishi mwenzie mmoja huku wakiendelea na kazi ya upishi wao
"kwani mi nilikitaka basi…. Wao wenyewe ndio walinipa mcheo wao…. Ohhh mpishi mkuu mpishi mkuu,…. Nauchukia sana huu upishi ukuu"
Aliongea chidi huku akiwasha simu yake, SMS nyingi sana ziliingia na zilikuwa ni za huyo huyo miriam aliomsevu WRONG NUMBER…
"aaahhhh demu anakera huyuuuuuu khaaaa"
"demu nani tena Omi"
"aahhhh si uyo miriam aliokosea namba"
"chonga nae,… Usiwe na hasira kiasi hicho hao ndio starehe zetu"
"aahhh sio kwangu"
Chidi alizifungua zile sms lakini zote zilikuwa ni salamu tu na kuambiwa mbona hajibu sms…
Masaa yalisogea na sasa ni mida ya jioni kama saa 11 hivi,… Tukiwa huku kwenye mjengo wa kitajiri wa akina saida, wakati huo ridhiwani ndio alikuwa anarudi kazini, mana anafanya kazi kwenye kampuni yao wenyewe,.. Ridhiwani aliingia chumbani kwake huku akiwa kachoka sana,.. Aliingia bafuni baada ya muda katoka kabadili nguo kisha akaenda zake kuketi sebuleni na kuangalia TV,… Haikupita muda dada yake alifika
"mambo ridhi?"
"safi tu dada angu, hali yako"
"nzuri tu… Pole na kazi"
"aahh tunamshukuru mungu kazi zinakwenda vizuri"
"pole sana kaka angu"
Saida alitoa pele kwa kusudio fulani mana keshajua mdogo wake sio mwanaume kamili,…
"ahsante"
Ridhiwani yeye hajui kama hio pele alipewa kwa maana gani,.. Saida alitamani kulia pale pale lakini aliwahi kuondoka ili ridhiwani asijue kuwa kwanini dada yake analia mbele yake,..
Saida aliingia chumbani kwake na kujifungia huku akilia sana kuhusiana na mdogo wake huyo…
Tukija huku kwa kijana chidi aliokuwa akitoka kazini kuelekea nyumbani kwa kaka yake, ikiwa ni mida ya saa moja kasoro jioni…
Chidi alichukuwa pikipiki iliomfikisha mpaka nyumbani kwa kaka yake,… Lakini kufika getini hakutaka kuingia ndani kabisa bali aliishia pale kwa mlinzi, basi chidi na mlinzi wakaanza kupiga stori za hapa na pele,.. Wakati huo kuna giza giza hivi taa zilikuwa zimeenea nyumba nzima, lakini pale walipokaa akina chidi palikuwa na giza hivyo kwa kule ndani ni ngumu kuwaona kwa kuoitia kamera walizofunga huku getini,…
"vp broo karudi"
"aahhhh bado,… Kaka yako hajagi mida hii"
Alikuwa ni mlinzi ndio kamjibu kijana chidi wakati huo bado stori zinanoga sana tu
"aahhh mzee wa tungi yule hawezi kuwahi kurudi"
Chidi alipoongea hivyo aliamka na kutembea taratibu kuelekea ndani,… Lakini wakati huo chidi hajui kama kuna mgeni ndani, afu mbaya zaidi mgeni huyo anadai eti anamjua chidi, kitu ambacho hata sisi wasimaji tunabaki mdomo wazi kuhusiana na hilo…
"waaoooooo shem mambo"
Alikuwa ni jasmini aliomkimbilia kijana chidi kwa kumkumbatia,.. Lakini walipokumbatiana jasmini kuna neno alimwambia chidi….
"nina hamu kweli ila sintoweza mana mdogo wangu yupo"
Aliongea tena kwa sauti ya chini mno,..
"sawa"
Chidi hakutaka kuuliza sana kuhusiana na mdogo wake huyo, ila alitii amri kuwa leo awe na heshma kiasi fulani…
Sasa chidi akawa anaelekea kule chumbani kwake ambako sabra kakung'ang'ania kuwe kwake…
"shem shem… Subiri kwanza.. Huyo mdogo wangu kachagua kulala chumba hicho, sasa sijui utachagua chumba kingine"
Aliongea jasmini huku akifikicha vidole vyake na wakati huo ujicho wa jasmini ulikuwa ni ule wa kuita..
"sawa.. Nitalala chumba kipi"
Aliuliza kijana chidi.. Na shem akamuonyesha chidi chumba alichotakiwa kulala,.. Kilikuwa ni chumba cha jirani sana na kile cha mwanzo ambacho sabra kakigandia huko….
Kwakuwa kila chumba kina kitanda chake, hivyo chidi aliingia na kuoga kisha akawa kapumzika….
Mara ghafla chidi anaitwa
"shemmmmm"
Alikuwa ni jasmini ndio aliokuwa akimuita chidi
"naam"
"chakula"
Chidi aliamka huku akiwa kugonga kabukata chake, afu kavaa vest pale kwenye kifua kuna viunywele kidogo vinaonekana kwa mbali…
Sasa chidi alikuja kama nguruwe kichwa chini na kukaa kwenye kiti,… Sasa ile kuinua macho tu kakutana uso kwa uso na sabra,… Chidi alishtuka, ila wakati huo jasmini alikuwa bado anaandaa chakula,.. Hata sabra pia alishtuka kana kwamba alichokisema kuwa anamjua, sio uongo ni kweli na hata chidi pia alionekana kumjua… Tena chidi alipovuta kumbukumbu yake,.. Ni demu ambae alishawahi kumpa namba za simu ila hakumbuki ni wapi.. Yaani huyu sabra alishawahi kumpa chidi namba za simu, ila chidi hakumbuki… Lakini walionekana kujuana haswaa…
Kijana chidi alishangaa sana kukutana na sabra ambae hakumbuki walikutana wapi siku hio,… Chidi alikuwa akila chakula huku akivuta kumbukumbu juu ya mwanadada huyo ambae hata kumbukumbu haimjii kabisa lakini anamjua haswa kuwa huyu tulishawahi kukutana mahari,…
"huyu mtoto wa kike tulishakutanaga wapi huyu"
Alijiongelea mwenyewe kimoyomoyo huku akiendelea kula….
Mara chidi aliipata kumbukumbu sahihi siku waliokutana… Ilikuwa ni siku hiii wakiwa kwenye basi, kama unakumbuka siku ile chidi anakuja arusha kuna dada alikutana nae kwenye basi, na walileteana shida sana… Wacha nikupe kwa ufupi ili ukumbuke.. Ilikuwa hivi
"lete nauli ukae hapo"
Kijana chidi kwa kutia huruma alitoa pesa yote mpaka mfuko unaning'inia kwa kukosa pesa zingine,…
"mbona bado elfu tano"
"jamaa angu, sina hata shilingi na laiti kama usingeandika hio tiketi ningeshuka nikatafute gari nyingine"
Mara watu wakaanza kumuombea, chidi asamehewe,
"msamehe tu kijana mwenzio"
"amana mzee hawa wanafichaga pesa hawaa"
"lakini keshakwambia hana, au mpe pesa yake akupe tiketi yako"
"aahhh ebu kakae pale.. Unazingua tu"
Sasa siti alioandikiwa kulikuwa na mrembo mkali anajishaua huyo, hapo alipo yenyewe alikuwa na Headphone maskioni huku kashika lisimu likubwa mno, anakula mziki,…
"nikakae pale"
"kaaa pale hueleweki Kiswahili ww bwege nini"
Aahhh kijana chidi alikuwa akikutana na vikwazo kama hivyo,
Sasa chidi ikabidi akae tu mana ndio siti alioandikiwa
Sasa ile kukaa tu, yule demu kaanza mdomo
"we kaka vipi, ina maana huoni pakukaa mpaka uje hapa,.. Lione vile sjui halijaoga"
Watu wote walitulia kimyaaaaaa wakisubiri chidi ajibu kitu..
BAADA YA DADA HUYO KUKAA CHINI NA KUGUNDUA HAKUFANYA KITU KIZURI KWA BINAADAMU MWENZIE.. AKAJIKUTA ANAJISOGEZA TARATIIBU KWA CHIDI… NA MWISHO AKAMUANDIKIA KAUJUMBE WAKATI NDIO KESHAFIKA KWAO USA RIVER.. UJUMBE ULIKUWA HIVI….
"naitwa saumu, nashukuru kwa ukarimu wako, na nilikuwa na vingi vya kuongea sema muda hautoshi,.. But yote 9.. Kumi ni kwamba naomba unisamehe kwa yale nilioyafanya mwanzo… Nimekiri kosa langu kwako,… Natamani niwasiliane nawe, lakini nimeona aibu kukuomba namba ya simu lakini naomba tuwasiliane kwa namba hii ni yakwangu, Please usinisahau"
HUO NDIO UJUMBE ALIOANDIKIWA KIJANA CHIDI… LAKINI ALIPOTAKA KUMPA NA YEYE NAMBA YAKE,.. SAUMU AKAWA KESHASHUKA KWAO AMBAKO NI USA RIVER….
Chidi anamaliza kumbukumbu haamini kama ndio huyu… Na mbona kule alisema anaitwa Saumu lakini huku anaitwa sabra.. Chidi hakutaka kumuuliza kitu lakini alimjua vizuri sana, tena alimtia aibu kwenye gari siku chidi anakuja arusha… Ili kukumbuka vizuri nenda kasome Sehemu Ya 7 na 8 utamjua huyo sabra vizuri siku hio alimtiaje chidi aibu kwenye gari na kumwambia unanuka kama mbuzi,na hastahili kukaa na mimi siti moja… Chidi hakuleta vurugu yeyote siku ile, alikua mpole sana sasa upole wake ndio ulimfanya sabra au Saumu kujirudi na kumuomba chidi msamaha baada ya kumwambia hajaoga ananuka kama mbuzi….. Chidi roho ilimuuma sana hata chakula kilikuwa hakishuki kwa hasira, kila akikumbuka siku ile anaambiwa hajaoga ananuka kama mbuzi vile, kisa wao wanapesa… Chidi alikasirika kwa kukuta kumbe mtu huyo ndio anakuja kuishi nae nyumba moja….
Kijana chidi aliondoka mezani na kuelekea chumbani kwake mpaka kitandani tena akajifunika shuka kabisaa, sasa huku mezani sabra nae pia alikuwa hamkumbuki vizuri.. Sasa ndio anakumbuka kuwa huyo ndio yule kijana aliomnyasa nyasa kwenye gari kisa alikuwa anatoka kijijini bado mshamba mshamba,…
"mungu wangu, sasa nimemkumbuka maskini ya mungu kumbe katakuja kuwa kashemeji ketu"
Aliongea "kata" lakini sio "Ni" shemeji yetu, kwahio kuna hali ambayo ni ya tofauti katika hii nyumba, ila tutajua mbele
Jasmini alipokuja mezani alishangaa kukuta chidi hayupo mezani,
"kaenda wapi"
"kaenda kulala"
"mbona hajala sasa"
"mmhh mi sijui"
Jasmini alienda chumbani kwa kijana chidi, na kumkuta kajifunika shuka kabisaa wala hakuwa akitaka hata maneno na mtu
"we chidi, mbona hujala chakula na ulitoka kwa ajili ya kula"
"aahhh nimejiskia kushiba tu ghafla"
"jamani.. Au unaumwa"
"hapata siumwi wala nini"
Aliongea chidi huku akifunua shuka ili amuone shemeji yake,…
"chidiiiiii"
"naam"
"naomba nikunyonye japo denda tu"
"No mdogo wako ataona bwana"
"deeeeenda tu chidi please"
Kabla chidi hajakubali shemeji mtu keshamuwahi mdomo na kuanza kumnyonya chidi mate,.. Lakini kumbuka hakuna kitu kinachopandisha hisia kama denda,.. Demu akishakubalo kunyonywa denda geto, basi ajue kuna Asilimia 90 za kufanya mapenzi taka asitake lazima hisia zitamlazimisha afanye….
Tukija huku kwa akina Miriam, ambako leo sarah kaja kulala kwa rafiki yake miriam, mana kama unakumbuka sarah leo alioga katika bafu la mama yake hivyo kuna kitu aliona lakini alishindwa kumuuliza mama yake mana isingelikuwa tabia nzuri kumuuliza mama yako kitu kama kile,.. Hivyo alitulia tu na wala hakumuuliza…
"ivi miri umeishia wapi na yule mtu wako"
Sarah alimuuliza Miriam kuwa kaishia wapi na swaga za kumtumia sms chidi,..
"mmmhhh we acha tu shost, yaani anavyonikatia, sina hata hamu na yeye kwakweli"
"au kama vipi mpasukie ukweli tu"
"mmmhhh natamani kufanya hivyo ila nitaanzaje"
"ok ngoja nikupe njia… Yeye si mpishi wa chipsi"
"ndio"
"nenda kwenye chumba hapo hapo hotelini, afu mwagizie alete chipsi afu muda huo vaa nguo za kulalia"
"mmmhhh saraaaaaa mi sijazoe kukaa hivyo"
"booooo utajua mwenyewe kama humpendi sasa si umuache"
"nampenda, lakini naogopa"
"sasa nakupa njia lakini hutaki"
Sarah alikuwa akimshauri Miriam jinsi ya kumpata chidi, ila laiti angelijua kuwa chidi huyo huyo ndio hhuyo chidi wake, sijui ingelikuaje, na siku wakijuana kuwa wapo na mwanaume mmoja, sielewi kama urafiki utaendelea au vipi apo..
"kwaio unanishauri vipi sasa"
INAENDELEA...
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi