MUUZA CHIPS (71)

0
Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA SABINI NA MOJA
ILIPOISHIA...
Chidi alikuwa anaongea na jamaa zake huku kweli hawaamini kama kweli chidi kamiliki kadi ya mtoto wa boss kama huyo,… Chidi hakuchelewa, alitoka mbio na kwenda benki, kisha akachomeka ile kadi kisha akacheki balance iliopo kwenye akaunti hio…

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
"khaaaaaahhh milioni miasita sabini (. 670.) Chidi haamini kama atakuta kiasi kama hicho kwenye hio akaunti…

Yaani hapo kuna milioni 600 (mia sita) na milioni 70 (sabini) hivyo bado milioni 30 (thelathini) itimie milioni 700 (mia saba). Chidi bila huruma wala uoga, akachukuwa ile ile shilingi milioni 70 yote, akabakiza milioni 600 (miasita) kamili

Milioni 70 ni kubwa hivyo iliwekwa kwenye kabegi kadogo hivi ka kushika hata mkononi,…

Chidi alichukuwa tax kisha huyoo mpaka nyumbani kwake… Alipofika alichukuwa ile pesa nyingine aliopewa na mama sarah, ambayo ni milioni 100 akachanganya ikawa milioni 170 keshi,.. Chidi alitoa milioni mbili na kuziweka mfukoni, wakati huo mfuko wake ulivimba mana milioni mbili mfukoni lazima mifuko ivimbe haswa kwa wingi wa pesa,… Ila hatujui anapeleka wapi hizo pesa, sasa sijui nae keshaanza kuhonga,..

Aliziweka pesa zake hizo kisha akatoka zake nje, na kupanda tax… Lakini alioofika njiani simu yake iliita… Kuangalia namba ilikuwa ni ngeni lakini aliipokea tu

"halooo"

"eeee mambo best"

"poa nani mwenzangu"

"naitwa saida… Samahani nina shida na wewe nataka tuongee biashara"

"biashara gani, mana mimi sio mfanya biashara"

"aahhh hata kufanya kazi pamoja ni biashara, hivyo biashara sio lazima kuuziana vitu"

"aaahhh ila kwa sasa nipo bize kidogo hivyo hebu niache kama lisaa limoja hivi"

"ok poa"

Alikata simu huyo dada anaeitwa saida, ila chidi hamjui huyo saida, lakini kwa nyinyi wasomaji, nadhani mnajua saida ni nani….

Chidi alifika kazini kwake, na kumkuta miriam ofisini kwake, Alimpa kadi yake na kumpa asante, ile chidi anaondoka tu akashikwa mkono huku miriam kama vile anataka kuangasha hilo jicho…

"nakupenda Omi… Please usinifikirie vibaya, ni moyo wangu umechagua pa kutua"

Aliongea miriam huku kama anataka hata kulia kwa msisitizo zaidi

Lakini chidi hakujibu kitu, alibaki kumuangalia tu…

"ok… Vipi tayari umeshatuma pesa nyumbani"

Aliuliza miriam huku huku akiweka kadi yake katika mkoba

"ndio… Na ahsante sana mamy"

"huna haja ya kunishukuru kiasi hiki"

"ok… Naomba nikaendelee na kazi"

"ok.. Naomba jioni nikusindikize kwako"

Chidi hakujibu kitu ila alionyesha ishara ya kukubali

Chidi alipofika jikoni kwao kwa wapika chipsi,…

"jumaaa…. Ngoja mshahara utoke tutakuchangia utume pesa nyumbani"

Waliongea baadhi ya wapishi ili wamchangie juma ili atume pesa nyumbani, mana juma kapata matatizo na huyo huyo juma ndio kasikiwa na miriam, afu miriam akajua ni chidi.. Kumbe sie…

"haina haja ya kumchangia…mimi nitampa peke yangu"

Aliongea chidi huku akiitoa ile shilingi milioni mbili na kumpa juma… Na yeue chidi ndio anajua bila huyo juma hio pesa asingelipata…

"aaahhhhh omi jamaa ngu, pesa zote hizi"

"katume nyumbani sasa hivi ili kama kuna mgonjwa apone haraka"

"ahsante sana ndugu yangu… Tulikuwa tunakuchukia sana lakini tulikuwa hatujui mtu tunamchukia yupoje"

"hakuna shida, we wahi katume hio pesa"

Ghafla simu ya chidi inaita tena, kucheki hiyo namba ndio ile alio ongea nayo muda sio mrefu, na dada mmoja anaeitwa saida

"haloo"

"eeehh chidi, nimefika hapa kazini kwenu"

"heeeee we umejuaje kama nafanya kazi hapa"

"najua na kuna mtu kaniambia.. Ila samahani naomba usiwe na hasira, njoo hapa kwenye meza tuongee biashara,.. Utanikuta meza ya mwisho ni mschana mweupe nimevaa gauni jekundu"

"mmhhhh ok nakuja"

Chidi kaja mjini kutafuta pesa, hivyo akiskia dili la pesa tu yeye hajivungi hata kidogo,…

"ndio yule nini"

Alijisemea chidi huku akimfuata huyo mschana, na ni kweli alikuwa ni saida mwenyewe,..

"we mkaka, ni mimi apa"

Aliongea saida baada ya chidi kutofanya haraka ya kumfuata,..

Chidi alifika pale kwenye meza kisha akakaa nae

"mambo chidi"

"poa nambie"

"safi tu"

Sasa kumbe wakati huo Miriam alikuwa anaona kila kitu sema alikuwa hasikii tu maongezi yaliokuwa yakiongelewa pale mezani

"we dija, hebu kawaulize wale wanatumia kinywaji gani… Wakishasema we njoo unipe Eploni yako nikawahudumie mimi"

"bosiiiii lakini we huruusiwi kutoa huduma"

"dija unabishana na mimi"

"ok sawa boss ngoja niende"

Kweli mtoto wa kike aitwae hadija alikwenda mpaka pale kwenye meza ya akina chidi na kuuliza

"samahani mnatumia nini"

"aaahhh tuletee juice tu"

Dija na chidi wanajuana mana ni wafanyakazi wa hapo hapo japo chidi yeye ni wa jikoni na dija ni muhudumu wa nje..

Dija alikwenda mpaka kwa miriam kisha akapewa Eploni na kuivaa kama muhudumu,.. Kisha akachukuwa juice mbili na kuzipeleka pale kwa akina chidi na saida,..

Wakati huo baadhi ya wahudumu walikuwa wanatetemeka mana wakikutwa na boss mkubwa, wataeleza kwanini miriam anahudumia wakati wao wapo…

Miriam alijifanya anaguta meza poole pole ili tu asikie kinachoongelewa na watu hao,.. Miriam ni wivu ndio unamsumbua na sii kingine

"chidi… Mi nataka nikupe kazi kwenye hoteli yangu,.. So naomba uache kazi hapa"

Miriam alishtuka karibia adondoshe juice

"we dada vipi, unaugua ukoma"

Aliongea saida kwa dharau huku akimuangalia juu mapaka chini mana hajui kama huyo sio muhudumu bali ndio tajiri mwenyewe,..

"samahani boss"

Aliongea miriam huku akijifanya kama muhudumu

"aahhhhh chidi samahani sana…. Ebu tuendelee…. Kwaio sasa. Mimi nitakulipa mara tatu ya hapa lakini acha kazi"

"we unajua nalipwa kiasi gani hapa"

"aahh kiukweli sijui ila nitakulipa mara tatu ya hapa, mana nimeambiwa unaweza kuandaa chipsi vizuri"

Sasa kama unavyojua saida wao hawana hoteli wala nini na kaja hapa ili ampate chidi hivyo hashindwi hata kusema anampenda, ni bora aonekane malaya lakini apate anachokitaka…

Saa ngapi saida hajaanza kusogeza mkono wake kwa chidi ili amshike mkono, heeeeee miriam si kaona… Tena katoa macho haswa huku akiuangalia ule mkono unaemsogelea chidi….

Ukumbuke kuwa mwanadada saida yupo katika mikakati ya kumpata chidi kimapenzi ili apate kile kinachohitajika kwa ajili ya matibabu ya mdogo wake ridhiwani,… Hivyo usishangae kumuona saida akijirahisisha kwa kijana chidi, hapo yupo kazini japo hajapenda lakini imembidi afanye hivyo ili kuokoa nguvu za mdogo wake,…

Saida kabla ya kumpigia chidi simu kwanza alipewa taarifa nzima kuhusu yeye, na aliotoa taarifa hizo ni mama sarah,.. Kuwa chidi ni Profesional wa kupika chipsi na anafanya kazi katika hoteli kubwa hapa jijini,… Hivyo kumtoa pale yataka akili ya ziada ili awe karibu nawe,.. Saida baada ya kupata taarifa za chidi ndio akaanza kumpigia simu huku akijifanya ana hoteli ya kumwajiri kijana huyo, chidi amekuja mjini kutafuta pesa na sii kuuza sura, hivyo kiwango alichokisema kwa kumlipa chidi, ni dhahiri kuwa chidi kuna uwezekano wa kuacha kazi hapo alipo… Saida alielekezwa mpaka mahari anapofanya kazi kijana huyo na kufika ili kuanza mazungumzo na yeye….

"aahhhhh chidi samahani sana…. Ebu tuendelee…. Kwaio sasa. Mimi nitakulipa mara tatu ya hapa lakini acha kazi"

"we unajua nalipwa kiasi gani hapa"

"aahh kiukweli sijui ila nitakulipa mara tatu ya hapa, mana nimeambiwa unaweza kuandaa chipsi bizuri"

Sasa kama unavyojua saida wao hawana hoteli wala nini na kaja hapa ili ampate chidi hivyo hashindwi hata kusema anampenda, ni bora aonekane malaya lakini apate anachokitaka…

Saa ngapi saida hajaanza kusogeza mkono wake kwa chidi ili amshike mkono, heeeeee miriam si kaona… Tena katoa macho haswa huku akiuangalia ule mkono unaemsogelea chidi….

Miriam leo ndio alimpasukia chidi kuwa anampenda, lakini chidi bado haamini kama kapendwa na mtoto wa tajiri kama huyo,… Japo sarah nae ni mtoto wa tajiri lakini chidi hana taarifa nzuri ya familia ya akina sarah, japokuwa anamuona na gari nzuri kila siku wanapokutana, hivyo chidi ana vijibahati vya kutembea na matajiri japo hana tabia ya kuomba pesa,.

Sasa wakati saida anasogeza mkono ili kumshika chidi,..

Lakini sasa chidi kabla hajashikwa alishangaa kuona vidole vya huyo muhudumu,.. Mana katika zele hoteli kubwa za heshima hua hakuna muhudumu anaepaka rangi kucha, mana sio kila unamhudumia ni mhuni.. Hivyo hoteli kubwa zenye hadhi huwa wahudumu kucha zao ni fupi alafu hazina hata rangi ya kupaka, sasa chidi akamshtukia huyo muhudumu lakini hakutaka kujionyesha kama kajua, na kamjua mpaka muhudumu mwenyewe, kwasababu wahudumu wa hapo kuna baadhi huwa wanavaa mask maalumu ili unapoongea na mteja usimkere, hivyo ukiwa kichwa rungu huezi jua…

Sasa ile saida anafikisha mkono kwa chidi, chidi akakwepesha mkono wake,.. Lakini chidi pia alionekana kumtamani saida mana saida ni mtoto mzuri na mwenye shepu lake la maana hivyo hakuna mwanaume atakaemkataa mdada huyo,.. Miriam baada ya kuona chii ana msimamo aliondoka zake na kujivunia kupata mwanaume bora na mwenye msimamo… Kwa sasa chidi anajua kuwa miriam anampenda,.. Hivyo hakuna tabu kwa sasa….

BAADA YA WIKI MBILI KUPITA

Ikiwa leo ni siku ya Jumatatu kama mida ya saa saba hivi, chidi akiwa yupo na kaka yake katika baa moja hivi wakipata moja moto moja baridi, lakini chidi yeye moja moto yake ni vinywaji vya kawaida tu, ila kaka yake alikuwa anabanjuka kweli kweli, tena anabanjuka vile vinywaji vya gharama kubwa

Chidi alikuwa anamuangalia sana kaka yake

"weitaaa zungushia wale pale kama walivyo"

Alikuwa ni kaka wa chidi akiwanunulia watu wengi vinywaji,..

"brooo…. Ivi hizi pesa hazina kazi… Ebu nipe mimi nikuonyeshee kazi"

Aliongea chidi tena huku akiwa na hasira ya hali ya juu,..

"weweeeeeeee unataka unifundishe matumizi ya pesa"

"sina maana hio… Ila ukumbuke kuwa mali sio zakwako kwanini usijivunie zako"

Chidi aliongea hivyo makusudi mana anakumbuka kuna siku sabra aliongea kuwa hata ile nyumba kule sio ya Ibrahim, bali ni nyumba ya mwanamke yaani ni nyumba ya akina sabra,..

"hata kama sio zangu… Natumia kwasababu sio zakwangu.. Nimpelekee mwanamke hela zote nina kichaa"

Aliongea Ibrahim huku akionekana kulewa sana, na hapo ni mchana kweupeee,.. Na wakati huo mpaka wafanyakazi wapo wanapata lanchi,…

Ghafla simu ya kijana chidi inaita.. Kucheki jina alikuwa ni Boss mdogo ambae ni mpenzi wake miriam..

"haloo boss"

Chidi wala hana majigambo kuwa mpenzi wake ni boss afu aanze maringo

"baby upo wapi lakini… Yaani wiki yote hii unasua sua kuja kazini sikuelewi Omari una shida gani"

"aahhh mi nimechoka na kazi bwana"

Chidi aliongea hivyo, mana ana kazi nyingine kutoka kwa saida

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)