MUUZA CHIPS (75)
Sehemu ya Sabini na Tano, na mama yake, kwa mama yake, ofisini kwa mama, akiwa kaangalia chidi, alimkuta ndio ananyanyuka, alipofika ofisini kwa
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mwandishi: MoonBoy
SEHEMU YA SABINI NA TANO
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Aliongea hivyo kumaanisha mama yake anamuita ofisini kwake,.. Chidi alishtuka na kujua enhee sasa kitakuwa kimenuka, mana kakaa nyumbani siku mbili mfululizo bila kuja kazini,..
Chidi alijikokota huku miriam akiwa nyuma yake,
KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI
SASA ENDELEA...
"we omari.. Akikuuliza we mwambie ulikuwa unaumwa sawa"
"sawa"
Miriam anajuwa ukali wa mama yake,.. Anajua mama yake ni mbogo hua hatakagi mambo ya kijinga
"ingiaaa"
Ni sauti ya boss ikimuamuru chidi aingie baada ya kubisha hodi,..
"shkamoo boss"
Alisalimia baada ya kufika katika ofisi hio, ghafla miriam nae katokea na kukaa katika kiti,..
"miriam… "
"abee mama"
"naomba uende ukaendelee na kazi"
"lakini mama.. "
"nimesema nenda"
Miriam aliogopa sana kuhusiana na chidi, ila hakuwa na budi yeye kwenda kuendelea na kazi kuliko kukaa hapo pasina lolote na wakati kule keshia hakukuwa na mtu yeyote yule,.. Baada ya miriam kutoka mama alimuuliza chidi
"wewe kijana… Ivi nataka kukuliza mimi nina undugu na wewe"
Aliuliza mama huyo huku akiwa kakunja sura haswa, mpaka chidi akawa anaanza kutetemeka kwa uoga
"hapana boss"
"sasa kwanini unachezea kazi yangu"
"nilikuwa naumwa boss"
"taarifa ulimpa nani"
"hakuna niliompa taarifa, ila naomba unisamehe boss"
"hilo ni moja…. Pili, ukaribu na mtoto wangu uliabza lini"
Mama aliuliza mana kaona live bila chenga watu wakikumbatiana na kubusiana,..
"hapana boss, sina ukaribu wowote na boss miri"
"unajua unanichefua we mtoto… Nitakupasua kichwa hicho… "
Mama miriam huezi amini pale alipo alitoa bastola na kumnyooshea chidi..
"wewe umekuja kufanya kazi au umekuja kutamani watu"
"nimekuja kufanya kazi boss"
Mama miriam alikuwa anatetemeka mkono huo huo ulioshikia bastola,.. Mana anajua fika huyu kijana ana mahusiano na mtoto wake,…
"sasa sikia, kaa mbali na mtoto wangu, laa sivyo nitakupoteza kwenye hii dunia… Ni bora uniibie mali kuliko uniharibie mtoto wangu"
Aliongea hivyo kisha akashusha ule mkono wenye bastola chini, na kuhema kwa nguvu zote….
"sawa boss nimekuelewa"
"tokaaaaaaa, mbwa wewe"
Chidi alitoka hapo akiwa na hasira nyingi, sana sasa miriam kumbe hakuwa mbali sana hivyo alimuona chidi akiwa anatoka ofisini kwa mama yake,.. Miriam alimkimbilia na kutaka kumkumbatia ili amuulize kaambiwa nini huko ndani
"omari… Omariii… We omari nisubiri basi jamani"
Huezi amini mambo yamekuwa si mambo, penzi limeingia doa… Ila sasa sijui chidi atakaza kuwa nae au ndio kwishnei tena…
Wakati huo miriam anaita pasina mafanikio yeyote ya kuitikiwa…
"jamani omari mpenzi wangu mbona ivyo"
Aliongea miriam baada ya kufika karibu na chidi,…
"kwani vipi"
Chidi aliuliza hivyo baada ya kuona miriam anamgasi sana
"mama kakuambia nini"
"kuniuliza kwanini sijaaga kama nilikuwa naumwa"
"lakini si unaendelea na kazi baby"
"ndio… "
"Ooohhhhh Thenx God for the last chance….ok twende zetu jikoni basi"
Miriam alimshika chidi kiuno huku akimwambia waende jikoni, kule wanakopika chipsi.. Chidi aligoma kwenda, tena alimgeukia miriam na kumwambia kuwa
"naenda mwenyewe"
Miriam alishtuka kuskia hivyo mana sio kawaida ya chidi kujibu hivyo…
Lakini kabla hajauliza kwanini chidi kamjibu hivyo, ghafla anakuja mhudumu na kumuita miriam
"Boss unaitwa na Boss mkubwa"
Maana yake ni kwamba miriam anaitwa na mama yake kule ofisini,…
"omari,… Nakuja huko jikoni, ngoja nikamsikilize mama kwanza"
Miriam aliondoka lakini kila akipiga hatua akili haimtumi kuhusiana na lile jibu la chidi kuwa hataki kuongozana na miriam kwenda jikoni, badala yake akasema naenda mwenyewe….
Miriam alipofika ofisini kwa mama yake alimkuta ndio ananyanyuka kwenye kiti ili aondoke zake… Miriam alimuwahi kumuuliza
"mama…. nimeambiwa unaniita"
Aliuliza miriam huku akiwa kaangalia chidi kwa heshima kubwa kwa mama yake
"ndio… Jiandae uende Uingereza kimasomo"
Uhusiano wa heshma ulikuwa unakwenda kuvunjika baada ya mzazi kugundua kuwa kuna uharibifu wa mtoto wake,… Nikisema uhusiano wa heshma namaanisha kwamba toka waanze uhusiano huo hakuna hata mmoja aliowahi kumuomba mwenzi wake tunda la msimu,.. Chidi kwa Miriam alionekana kupenda haswa, lakini hakuwa na jinsi mana bila hivyo atakufa kwa ajili ya mwanamke… Hivyo hana budi kuachana naye… Miriam aliitwa na mama yake wakati akiwa kasimama na chidi… Miriam alikatisha maongezi na chidi kisha huyoo akaitika wito wa mama yake
Miriam alipofika ofisini kwa mama yake alimkuta ndio ananyanyuka kwenye kiti ili aondoke zake… Miriam alimuwahi kumuuliza
"mama…. nimeambiwa unaniita"
Aliuliza miriam huku akiwa kaangalia chidi kwa heshima kubwa kwa mama yake
"ndio… Jiandae uende Uingereza kimasomo"
Miriam alitoa macho, japo ni madogo lakini yalitoka kwa kusikia anakwenda Uingereza kimasomo… Afu mama hakutaka maswali nengi juu ya neno lake, na licha ya kutotaka maswali, pia aliondoka kabisa hapo ofisini kwake na kuanza kuzunguka hoteli nzima ili kuweka mazingira vizuri, mana ana muda hajazunguka katika hoteli hio,… Miriam hakuwa na wa kubishana nae alirudi ofisini kwake na kujilaza na wala hakuwa na hamu hata ya kufanya kazi,..
Sasa huku kwa chidi nae kichwa kimejaa mawazo
"oya omari, vipi mbona toka ulivyokuja hapa huna hata raha"
"aaahhh.. Nimekaa nyumbani bila kuaga sasa boss naona kachafukwa"
Wakati huo hajui kama Miriam kaambiwa aondoke Tanzania, yaani hatakiwi kuonekana kabisa,…
"lakini si bado tupo kazini"
"ndio.. Kwa kazi bado nipo"
"daaahh afadhali jamas etu upo kazini"
Waliongea wale wafanyakazi wenzie,.. Kwa sasa hakukuwa na mtu aliokuwa anamchukia chidi, mana kuja kwa chidi mpaka sasa hivi wameongezewa mshahara umekuwa mzuri na inapendeza, na nzuri zaidi ni kwamba chidi anawafundisha jinsi ya kutengeneza chipsi nzuri na za kupendeza… Mana kiazi ni kimoja lakini mapishi ni tofauti, na kila mtu ana uprofessional wake juu ya kazi yake.. Hivyo chidi anajua kazi ya kuoika CHIPSI vizuri sana.. Mana hakuna chipsi tamu kama za mtaani, mana zile ni asili kabisa, lakini kwenye mahoteli huko,.. Zinatunzwa sana mpaka inapitiliza kwenye utunzaji…
Sasa Miriam akaona wacha akamshirikishe chidi kuwa yeye anakwenda Uingereza ili aone atalichukuliaje swala hilo…
Tukija huku kwa akina saina, tunamkuta saida anagombezwa na mama yake, baada ya mama kuona kimya kinazidi kutawala na mtoto hafanyi kazi kama inavyotakiwa
"mama, lakini tunaenda taratibu mama angu"
Aliongea saida huku akiwa kakasirika
"taratibu kitu gani mdogo wako anazidi kukua tu, sasa kwa taarifa yako zimebaki siku mbili tu, mdogo wako atimize miaka 21 kamili, na inatakiwa kabla ya kutimiza umri huo awe tayari kesharudisha nguvu zake… Yaani kesho kutwa ni siku ya kuzaliwa kwa mdogo wako… Na ikipita hio siku,.. Inabidi umpe sketi zako na chupi zako kila kitu avae uende nae huko kwa wanaume zako na yeye awe kama wewe.. Mshenzi wewe"
"mamaaaaaaa… Kwanini unaongea hivyo lakini"
"hiii kazi ilikuwa inafanywa na mtu, lakini nikaona niutumie uzuri wako mwanangu mana niliompa hii kazi alikuwa anatumia pesa nyingi sana afu hafanikishi… Sasa hata wewe mdogo wako mno unamfanyia hivyo"
"mama basi jamani… Nipe siku ya leo usiku"
"kama hutaki uniambie hata mimi nina kum*…. Naweza kwenda kumpa huyo kijana"
Saida kuskia hivyo alikimbia hata hakutaka kuendelea kumsikiliza mama yake… Saida alipanda gari, tusijue anapoelekea…. Wakati huo mama anachungulia dirishani ili kuona kama anaondoka au vipi,….
"hawa watoto bila mkwara hawafanyi vizuri, shenzi yake… Na nimempa mkwara wa kutosha, lazima afanye kazi"
Aliongea mama saida huku akijifuta jasho, mana aliongea maneno yenye uchungu wa hali ya juu, mpaka saida mwenyewe akaona akiendelea kukaa hapo abaweza kuachiwa hata laana, maba hayo maneno yaliomtoka mama huyo, ni maneno makali mno…
Sasa Tukija huku kwa akina sarah na mama yake.. Sarah akiwa yupo ofisini kwake akitaka kumpigia chidi
"jamani nimemmisi chidi wangu"
Aliongea hivyo huku akiitafuta namba ya chidi, kisha akampigia
"haloo chidi mambo"
"poa niambie"
"safi tu… Afu mbona kama huna raha baby"
"aaahh ni kidogo tu sio sana"
"eti eee, jamaaniiiiiiiiiiiiii leo nije kwako"
"mmmhh no, leo nimechoka sana mamy"
"nimekumisi jamani"
Alizidi kuongea sarah huku akijiona ni mwanamke mwenye bahati sana kwa kumpata chidi….
Wakati huo huo simu ya chidi ilikuwa inatoa muito wa kuwa kuna mtu mwingine aliokuwa akipiga,..
"sarah ebu subiri kidogo nakupigia"
Alikata simu ya sarah kisha akapokea simu ya saida,..
"haloo chidi mambo"
"poa niambie"
"safi tu… Vp leo tunaweza kukutana"
"hapana… Leo nitakuwa bize kidogo"
"basi leo nalalia kwako… Nataka unipe nyama yako tena"
"heeeeee we si jana umetoka geto kwangu wewe"
Sasa wakati chidi anaongea hayo, kumbe Miriam alikuwa anasikia kila kitu, mana ukumbuke alitoka kwenye ofisi yake ili akampe chidi taarifa kuwa ana safari ya kwenda Uingereza, sasa aliootaka kuingia ndio akasikia hayo maneno, ikambidi asimame kwanza ili asikilize vizuri.. Lakini mmoja wa wapishi wa chipsi alimuona shem lao limejaa kwa mbali, hivyo akamfuata chidi taratibu bila Shemela wao kujua
"oya omari, ongea taratibu shemela yupo nyuma yako"
Chidi aliposkia hivyo akabadirisha topiki
"sasa kwani jana kile kitabu hujakichukuwa"
Sasa topiki aliobadilisha yule saida haijui
"kitabu gani tena we chidi, au umenisahau jamani"
"aaahhh kama hujakichukuwa we njoo, utakichukuwa.. Nimekubali uje ukichukue (nimekubali uje ulale)" aliongea kimafumbo lakini saida hakuwa akielewa chochote kile,…
"chidi sikuelewi, mi nataka nije nilale kwako nina hamu"
"sasa si nimekwambia njoo…. Njoo uchukuwe kitabu ila utarudisha kitabu changu"
"chidi, mi staki kitabu"
"nimekwambia njooo mbona huelewi Kiswahili"
"unamaanisha umekubali nije kulala kwako"
"ndio"
"sasa mbona ulikuwa unanitajia mambo ya vitabu"
"nina sababu"
"ooooohhh basi nimeelewa,.. Apo utakuwa upo karibu na bi mkubwa si ndio ee"
"ndio… Kata simu basi"
Simu ilikatwa kisha chidi akajifanya hajui lolote kama miriam yupo nyuma yake,..
"nani uyo anataka kitabu"
Ni jamaa yake ndio alimuuliza makusudi tu ili miriam ajue kuwa hakukuwa na shida… Na miriam yeye hajui kama mwenzie alishikiwa bastola kule ndani kwa ajili yake
"aaahhh si yule mdogo wangu, jana kaja geto kuna kitabu nimemnunulia sasa kumbe alivyoondoka kakisahau, afu sasa hivi anataka kuja tena na wakati sipo"
"aaahhh we mpe tu"
Pale pale miriam alijitokeza lakini hakuwa na raha
"aaahhh shemmmmmm"
Walimuita wote waliokuwa hapo jikoni,
Lakini miriam hakuwa na raha kabisa na sio yeye tu, hata chidi hakuwa na raha hata kidogo,
INAENDELEA...
Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni