MUUZA CHIPS (102) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Ijumaa, 26 Aprili 2024

MUUZA CHIPS (102)

UMEWAHI KUONA AU KUSIKIA KUHUSU PICHA ZA AI?
Sasa naomba nikufundishe bure kabisa nawewe uzitengeneze kirahisi kabisa

Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA MIA NA MBILI
ILIPOISHIA...
"saida mwanangu, sisi hatuna nia mbaya na wewe, tunataka tujue huyo kijana ni nani"

Aliongea mama yake saida huku akimwomba mtoto wake aseme kijana mwenye hio mimba…

"na usiposema uhame nyumbani kwangu, pumbavu wewe"

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Aliongea baba yake saida mana wote walikuwepo hapo..

"baba saida mbona unamfokea mtoto, we mbona… "

"shiiiiiiiiiiii kimyaaaaaaaa"

Mama saida alikatishwa maongezi aliotaka kuongea, baba wa saida alimsihi asiseme mana mama saida alitaka kusema mbona yeye alimpa mimba kabla hajamuoa, na mtoto mwenyewe ndio huyo saida.. Na katika familia hio watoto ni wawili tu, ambaye wakwanza ni saida na wapili ni Ridhiwani, ni hao tu na hakukuwa na mwingine, na ndio maana mama saida aliona uchungu wa kumseidia mtoto wake wa kiume…

"saida achana na baba yako, we sema huyo mwanaume ni nani"

Mama alikuwa anataka kujua mwanaume aliompa mimba mtoto wake ni mwanaume gani huyo… Baba saida alipoondoka, Saida alitoa simu yake na kumwonyesha mama picha ya huyo mwanaume,..

"hiii hapa mama… Huyu ndio alionipa mimba, nampenda sana mama"

Mama saida hamjui chidi kabisa bali anaijua namba yake mana alisharushiwa namba lakini hajawahi kumwona kwa sura yake,… Laiti angelijua huyo ndio kijana waliotakaga kumfanyia unyama kipindi cha nyuma, sasa sijui leo angelikuwa nani mkwe..

"saizi yako kabisa.. Lakini hali yao ipoje"

Mama aliuliza hali yao ipoje kumaanisha kuwa nao ni matajiri au choka mbaya,..

"una maana gani mama"

"namaanisha ni kama sisi au"

"kuhusu pesa si ndio"

"eeeennh"

"no ni wa kawaida tu"

"umeshaanza kutuunganisha na familia za kimaskini tena, kwanini usiolewe na jemsi"

"mama.. Mimi nipo tayari kuacha pesa zenu, ila siwezi kuachana nae.. Siwezi, nasema hivi, siwezi kuachana nae"

Mama alishangaa kuskia saida yupo tayari kuachana na mali zao lakini sio kumuacha chidi.. Yaani saida angelijua kuwa chidi mwenyewe ndio kwanza anakwenda kuoa huko kijijini kwao, saida yeye halijui hilo, sasa sijui itakuwaje pale atakapo jua kuwa chidi kaoa mwanamke mwingine badala ya yeye,.. Na wakati alimuahidi kumuoa na ndio maana kakubali kuibeba mimba hio..

Tukija huku kijijini kwa akina chidi wakiwa ndio wanaingia ndani ya jengo huku wakipokelewa na vigelegele,… Kumbe hata mama yake chidi na ndugu wengine walikuwa wanayo taarifa za ndoa, hivyo kitendo cha wageni kuingia hakikuwa cha kustukiza kwao, na hata maandalizi walisha yaandaa mapema mana siku ile chidi anaambiwa tu,.. Akampigia mama yake simu na kumwambia ajiandae na kupanga kila kitu… Kwahio hapo hakuna asiojua ishu hio,.. Kwasasa familia ya chidi inaishi kitajiri sana, mana baba yake katupia suti kali, mama mtu ndio usiseme, katupia zile za kinigeria,.. Yaani walipokutana na mama miriam na kutambulishwa kuwa huyo ndio mama mzaa chema.. Basi ilikuwa ni furaha kubwa sana,

Na wakati huo mababa nao wapo sebuleni wakiendelea kupiga stori,.. Yaani baba yake miriam na baba yake chidi walikuwa sebuleni wakiangalia TV huku wakipiga stori za zamani,.. Kwa sasa baba yake chidi anaongea kama tajiri wa zamani, mana na yeye ana pesa kwasababu ya mtoto wake chidi…

Lakini sasa mama miriam na mama chidi walipokuwa wanasalimiana,.. Ghafla mama anamuona mtoto wake wa kwanza ambae aliondoka miaka 7 iliopita, mama yake chidi mpaka anatetemeka kwa kumuona chidi,.. Ila hajakaa vizuri akashangaa kumuona salma akiwa sambamba na Ibrahim,.. Na wakati huo chidi na miriam wapo chumbani kwao na hawaruhusiwi kutoka kwa wakati huo mana kesho ndio ndoa yao,..

"sasa mama chidi, wacha nikawapokee wageni niliokuja nao ili waendelee kuzoea"

Aliongea mama miriam huku akiondoka kwenda kwenye yale mabasi ili kuwaingiza wageni ndani, mana hawakuweza kuingia ndani bila ya wenyeji,..

"sawa mama miri"

Wamama hao walijikuta nao wanapendana kwa dakika chache tu, yaani damu zikiendana basi hakuna kitu kitaharibika,.. Sasa mama miriam alipo ondoka

"haya wewe umekuja hapa ukiwa kama nani"

Mama hakutaka utani tena kwa Ibrahim

"mama, ni maisha tu"

"mbwa wewe unamwambia nani hivyo, eeh?…… Baba chidi…. Baba chidi"

Mama alimuita mume wake ili aonane na mtoto wake

"nini tena, na wakati nina mgeni huku"

"muone mtoto wako huyo"

"haaaaaaaaa.. Huyu mwehu katokea wapi huyu"

Aliongea baba yake mzazi huku akimsogelea kwa ukaribu…

Sasa huku ndani chidi aliskia kile kiito cha mama yake kumuita mumewe… Chidi alijua tu kuna tatizo huko nje,

"unaenda wapi mume wangu"

Aliongea miriam huku akimzuia chidi asiondoke mana chidi hajui mambo ya kuwekwa ndani,.. Mana hata ndoa ya mwanzo ya yeye na salma walifunga ndao ya mkeka tu,..

"nakuja mamuu"

Chidi alitoka afu nyumba ni kubwa na walikuwa mbali sana,.. Mana nyumba ni kubwa mno, yapata vyumba kama 70 hivi yaani ni bonge la jumba,.. Na nilikwambia ingejengewa mjini, basi ingegharimu hata bilioni moja,…. Kiukweli chidi wamejenga jumba kubwa sana, japo ana ndugu wengi wa pembeni lakini hata hivyo hawawezi kuimaliza kwa kuishi peke yao..

Sasa chidi ile anatoka nje, anakuta Ibrahim anatoka nje ya geti

"broo unaenda wapi tena"

"weweeee wacha ujinga mwache aende"

Aliongea mzee king huku akiwa anatetemeka kwa hasira,..

Lakini chidi aliona hapa kuna tatizo

"baba, hebu tuliongee hili swala, we ulifikiri wageni watatuelewa vp kama tunaanza kufukuzana"

"mjinga huyu kaka yako"

"sawaaaa mzee… Hebu tuyamalize, mana upande wa ukweni washamjua, sasa asipoonekana kwenye harusi itakuwaje"

Baba yake chidi kwa hasira aliondoka na kuona ni sawa, kama Ibrahim ataondoka, afu familia ya ukweni wanamjua itakuwa sio vizuri…

Basi chidi alikwenda kumuita kaka yake aliokuwa yupo nje…

"rashidiiii"

"naam mzee"

"njoo nao huku ndani"

Aliongea mama yake chidi kuwa aitwe Ibrahim na huyo salma waingie ndani

Wakiwa wapo katika chumba kimoja wakiwa wanayaongea… Walikuwa ni baba yake chidi na mama yake,.. Salma na chidi pamoja na Ibrahim

"mzee…. Samahani sana mzee wangu, najua nimefanya kosa, ni ujinga wangu, uzembe, ulimbukeni wa mjini… Kweli maisha yangu yalikuja kuwa mazuri, lakini maisha hayo yalinichanganya sana na kuisahau familia yangu…. Nilimnyasa nyasa sana mdogo wangu nikiwa naishi nae,… Mama na baba, naombeni mnisamehe, nimekosa sana tena sana.. Sikuwajali wazazi wangu, na huenda kutokana na hilo ndio mana hali yangu imekuwa mbaya… Nimejifunza wazazi wangu, nisameheni sana… Nipo chini ya miguu yenu"

Ibrahim aliongea sana tena wakati huo alikuwa analia kabisa, yaani machozi na magoti juu mbele ya wazazi wake,..

"ni kweli mzee, msameheni kaka angu, nanyi ni mwanaenu hata mkimkataa bado ni mtoto wenu tu.. Naombeni mumsamehe mtoto wenu"

Waliongea sana tena sana, mpaka wazee walielewa na kumsamehe mtoto wao, mana hakuna baya alilofanya zaidi ya kutowakumbuka kifedha… Sasa mama kahamia kwa salma,

"Enheeee na wewe, unataka kuwamaliza watoto wangu wote si ndio"

Aliingea mama huku akimkazia macho salma,..

"hapana mama… Ibrahim sikujua kama ana undugu na chidi, sikujua kabisa"

"muongo wewe, ina mana ulikuwa hujui kuwa chidi ana kaka yake yupo mjini"

"nilikuwa najua mama, ila simjui na sijawahi kumuona mama"

Salma alikuwa mpole sana tena sana

Baba yake chidi kuskia hivyo aliondoka zake mana yeye ni baba hivyo havimuhusu sana,..

"mama, kama unawasamehe wasamehe tu, mana hata mimi nilishangaa lakini haikuwa na jinsi mana wamekutana wenyewe huko Dar es Salaam, wala hawakuwa arusha hawa"

Chidi aliongea ili kuwatetea kaka yake na mpenzi wake japo zamani walikuwa ni mashemeji,..

"sasa kama kaweza kukukimbia wewe atashindwa kumkimbia kaka yako"

"hawezi tena mama, for now tuna maisha mazuri so hawezi ondoka coz aliondoka kwa tamaa tu"

Unajua hii familia haijui kama salma aliondoka na mwanaume, wao wanajua alijifanya chizi, na kuondoka zake lakini hawajui kama aliondoka na Jackson,

"lakini mbona mnaitia aibu hii familia"

Aliongea mama yake chidi,..

"nisamehe mama…. Ibrahim nampenda sana, na siwezi kumkimbia na kwa sasa sihitaji tena kuhangaika nataka nitulie kwenye ndoa"

Aliongea salma huku akifuta machozi kwa kulia,..

"mimi mnanichosha sasa nyie watoto aahh,… Haya nenda kamsalimie mama yako, afu uje mana nyie ndio mnajua maandalizi ya mjini mjini"

mama yake chidi alimwambia salma kuwa akamsalimie mama yake, afu aje waendelee kuandaa andaa,.. Mana salma nae si kaishi mjini hivyo mbwembwe mbwembwe za harusi anazijua vizuri na yeye ndio Best Woman,.. Hivyo anatakiwa akae karibu na bibi harusi

"sawa mama, ahsante"

Aliongea salma huku akiondoka,..

"na wewe chidi hebu ingia ndani, we haruhusiwi kuonekana hovyo hovyo bwana"

Aliambiwa chidi na kukimbilia ndani kwa mke wake mtarajiwa,.. Nyumba ilikuwa ni kubwa sana hivyo karibia nusu ya wageni waliweza kupata nafasi ya kulala, lakini nusu ni ya wale wasichana wanaopenda kukesha,.. Usiku huo baikoko ililia mambo ya ngoma za kisambaa zililindima eneo hilo, hata wageni walifurahia sana hali hio… Lakini ilifika muda wamama wote wa pande mbili walikutana na kuanza kuongea ile kiutu uzima,.

"aahh sisi kama familia ya kijana wetu, tulitaka tujua heshima ya mtoto wako kwetu, mana nasi tuna heshima zetu tunazozipenda.. Labda mtoto wako umemlea vipi"

Aliongea bibi yake chidi, na wakati huo hata bibi yake miriam alikuwepo hapo, yaani hapo ni wamama wawili na wabibi wawili tu basi

"Kiukweli mtoto wangu nimemlea kimaadili, yaani yale maadili ya kifamilia yote anayo"

"na je vipi mjukuu wangu atakuwa ni wakwanza kwake ama"

Aliuliza bibi yake chidi huku mama chidi akiwa kimya tu

"Kiukweli nina uhakika mtoto wenu atakuwa wa kwanza kwa mtoto wangu, ila sidhani kama watakuwa wamelisubiri hilo"

Aliongea mama miriam, lakini ghafla bibi yake miriam aliongeza kuwa

"ni kweli, mana vijana wa sasa hivi hawana kasumba ya kusubiriana, hawajui kama kuna mambo ya mahari"

"basi kama huna uhakika hebu tuwatenganishe usiku wa leo"

Maongezi yaliishia hapo na walimalizana…

BAADA YA SIKU HIO KUPITA

Na leo ni siku nyingine tena,.. Ikiwa ni mida ya saa 11 alfajiri, tukiwaona mabibi wakiwa na miriam chumbani kwake, huku chidi nae akiletwa katika chumba hicho, na wao hakuna walichokuwa wakikijua… Lakini muda huo huo mama miriam alikuwa ana hofu sana juu ya hilo, sasa sijui ni kwanini…

BAADA YA MASAA KADHAA KUPITA

Ikiwa ni mida ya mchana miriam na kijana chidi wakiwa katika jukwaa maalum la mabwana harusi, wakati huo shekhe akiwa pembeni tayari kwa kuwafungisha ndoa,…

"tuna furaha sana juu ya tukio hili kwa watoto wetu kufunga ndoa"

Aliongea shekhe huyo aliokuwa kashika vitabu vya mungu na kutaka kuwafungisha ndoa,..

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni