MUUZA CHIPS (94)

0
Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA TISINI NA NNE
ILIPOISHIA...
"mmmhhhhh siingilii mambo yenu bwana"

Basi chidi alichukuwa taulo na kuingia bafuni, lakini ile kufika tu bafuni anakutana na chupi za miriam.. Kwa hasira alizitoa na kwenda kuzichoma yaani hakutaka hata kuziona katika macho yake,..

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
"yaani toka niende jela mtu hata kuja kuniona haji, ni mtu gani huyo"

Aliongea chidi huku akimalizia kuchoma chupi za miriam ambazo kaziacha…

"chidi chalii yangi.. Hizo ni hasira tuu.. Basi choma na hizi nguo zingine za kwenye mabegi huku"

"aahhh hayo madera na kanga bado mapaya hayo atavaa mke wangu"

"mkeo nani uyo"

"si Sarah"

"Duuuuuuuuuuuuuuuu"

"duuuuu nini sasa"

"roho inaniuma kumuacha boss miri"

"atajua mwenyewe uko, siwezi kuishi na katili mimi… Tena nimalize kuoga unipeleke kwao nikampe kadi yake"

Chidi alimchukia sana miriam yaani hata hamu nae hana, yaani kuskia tu mdogo wake yupo kwa sarah, baasi mapenzi mazito yote yakahamia kwa sarah… Chidi aliingia zake bafuni na kuendelea kuoga…

Tukija huku kwa sarah akiwa keshafika nyumbani, tena alikuwa akicheza na mdogo wake chidi vizuri mana tayari ombi la kumleta chidi kwao limeshakubalika, siku hio ni siku ya Jumamosi mama yake karudi mapema,..

"shikamoo mamii"

"marahaba vipi,.. Naona leo una raha kweli mwanangu"

Aliuliza mama yake, huku nae akionekana kufurahi baada ya kuona mtoto wake ana furaha mno.. Lakini mama alijua tu furaha hio ni kwasababu ya kumtoa chidi mikononi mwa polisi,..

"mama kuna kitu nataka nikuambie"

"kitu gani tena mwanangu"

"kesho staki utoke, nataka nimlete mchumba wangu umuone na itakuwa siku ya kuvalishana pete"

"waoooooo yaani kesho nitakuepo home, ila huyo mchumba wako,.. Ana heshima na kakupenda wewe au kapenda mali zenu tu"

"kiukweli tunapendana sana mama,.. Yaani naomba umpokee"

"usijali mwanangu, kikubwa tu awe na heshima nzuri"

"kwa hapo mi nadhani utafurahi mwenyewe"

Tukija huku Dar es Salaam kwa Ibrahim akiwa ndio kwanza bado yupo hospitalini, lakini keshapona sema bado hajapata chumba cha kuishi, hivyo hapo ndio alikuwa anataka kutoka ili kwenda kutafuta chumba,.. Mana kama ni pesa ya kupangishia chumba anayo,.. Ibrahim alitoka hospitalini hapo na kuianza safari ya kuingia uswahilini, na hapo alipo ni mgeni hajui atapata wapi chumba,…

Alipita njia nyingi ikiwa ni mida ya saa 10 jioni chakula cha mchana hajala lakini anajipa moyo tu atapata chumba na kuyaanza maisha upya..

Sasa kutokana na njaa alionayo Ibrahim aliona kihoteli cha mama ntilie, na kihoteli hicho hicho ndicho kinachuzwa na salma, ambae ni shemeji yake kwa chidi…

"hodi jamani"

Alibisha hodi huku akiwa kashika tumbo kumaanisha ana njaa kali mno, salma kumuona alimkimbilia kama mteja lakini kati yao hakuna anaemjua mwenzake,… PATAMU APO… Yaani Ibrahim anajua kuwa mdogo wake alioa kule kijijini lakini mke hamjui, mana Ibrahim alitoka kule kijijini kabla chidi hajaona,.. Mana Ibrahim ana miaka kama 7 hivi toka atoke kijijini, na chidi ana miaka mitatu toka aoe kule kijijini, hivyo Ibrahim hamjui shemeji yake ila walikuwa wakiwasiliana kwa simu tu, lakini kwa sura hakuna anaemjua mwenzake..

"karibu kaka"

Salma alimkaribisha Ibrahim bila kujua kuwa huyo ndio yule shemeji yake aliokuwa akiwasiliana nae wakiwa kijijini… Unajua hakuna kitu kibaya kama mtu kupotelea mjini.. Mana Ibrahim aliondoka kijijini kabla hata chidi hajamaliza shule, hivyo kuoana kwa chidi na salma, Ibrahim alikusikia tu akiwa mjini, na hakuja mpaka leo mwaka wa saba huu toka atoke kijijini…

"Ahsante dada angu"

Salma ni mdogo sana kiumri lakini kwa maisha ya Dar es Salaam yalimpenda na kumfanya awe na mwili mkubwa, ukimuangali utasema bonge la mama kumbe ni katoto kadogo sana..

"nikupatie chakula gani kaka"

Yaani Salma aliongea kwa heshma ya hali ya juu, mana kaambiwa na huyu mama mwenye hoteli kuwa awaheshimu wateja na awe mnyenyekevu sana kwa wateja wake.. Ibrahim alishangaa ivi wanawake kama hawa wapo kweli dunia hii…

"nipatie wali samaki"

Basi salma kwa heshma ya wateja alianza kuchakalika haswa, tena ndio ana siku kama ya tatu au mbili toka aanze kazi hapo..

Ibrahim alikula mpaka akashiba kisha akalipa pesa ya chakula

"Ahsante kaka"

Yaani hio Ahsante mpaka salma kainama kifogo ile kiheshma… Ibrahim anazidi kushangaa..

"Samahani dada,.. Ivi hapa naweza kupata sehemu ya kupika chispi hapa hapa"

"hhhmm mimi sio mwenyewe, kuna mama ndio anamiliki hapa ila katoka kidogo"

"aaahhh atachelewa sana"

"kaondoka muda ila sidhani kama atachelewa"

"wacha nimsubirie kidogo.. Mana natafuta chumba, huko mtaani kwenu hakuna chumba huko"

"hhhhhhmm hakuna"

Basi Ibrahim aliendelea kukaa hapo mpaka giza likaingia lakini mama huyo hatokei,… Ibrahim hapo alipo hajui atalala wapi.. Mida ilizidi kwenda lakini mama mwenye kihoteli hatokei.. Lakini ghafla simu ya salma inaita, kuangalia jina alikuwa ni huyo mama

"haloo mama shikamoo"

Yaani salma alijikuta anakuwa na heshima ya ajabu, yaani kusalimia tu kwenye simu mpaka ainame kidogo, kitu ambacho Ibrahim kinampa shida sana na kushindwa kumwelewa ni mschana wa dizaini gani na katoka wapi..

"marahaba ujambo"

"sijambo mama"

"vipi kazi zinaendaje"

"aahhh tunashukuru mungu hali sio mbaya mama"

"ok.. Sasa wewe funga hapo uende nyumbani, mana mimi nimebanwa huku hivyo siwezi kufika hapo"

"sawa mama"

"eeeehh funga sasa hivi mana inakwenda saa nne hii"

"sawa mama"

Simu ilikata kisha salma akaanza kazi ya kuingiza vitu ndani, majiko mikaa… Ibrahim aliona ngoja amseidie mtoto wa kike kuingiza vitu mana kama ni kuchelewa keshachelewa, na hapo alipo Ibrahim ana pesa kama laki nne hivi..

Sasa ilipofika saa ya kuondoka Salma alikuwa na pesa ya watu ya mauzo, sasa anaogopa kwenda mwenyewe nyumbani kwake,..

"kaka naomba nisindikize mpaka pale kwenye toyo"

Aliongea salma huku Ibrahim akikubali

"sawa twende tu usijali"

Ibrahim hakumsindikiza mpaka kwenye toyo badala yake alimpeleka mpaka kwake kabisa na salma kahakikisha kaingia ndani..

"sasa utalala wapi kaka.."

Aliongea salma huku akimuonea huruma kaka wa watu,…

"usijali, wacha nikajibane tu kwenye vibanda huko ili kesho niamkie kutafuta chumba"

"hhhmmmm sawa, mana mi siwezi kukulaza huku mana mi. Mtoto wa kike"

"lakini mimi hata kwenye kochi tu nitalala tu"

Salma akiangalia chumba chake kina godoro peke yake yaani hata vyombo vyenyewe hakuna, ana ndoo ya maji tu,..

"yaani kaka hata sofa sina.. Yaani mimi mwenyewe maisha nimeanza jana tu"

"haaaaaaaa kumbe hata wewe ni mgeni mji huu"

"aio mgeni sana ila ni stori ndefu kaka yangu"

Stori zilinoga hapo huku mida ikizidi kwenda… Salma aliona huruma kumuacha kaka wa watu na wala hakuwa na shida,..

Salma kwa huruma aliingia jirani na kuomba mkeka,.. Mambo yakawa mazuri kwa kijana Ibrahim… Na salma alikuwa na godoro lake peke yake, tena lilikuwa jipyaaa, Ibrahim kuona maisha ya salma yalivyo aliona afadhali hata ya yeye… Basi wawili hao wakawa wamelala chumba kimoja ila salma yeye alikuwa halali mana hawezi kumwamini Ibrahim moja kwa moja kama ni mwema au sio mwema… Masaa kadhaa mbele salma aliamka na kuwasha taa… Alimkuta Ibrahim kalala mpaka anakoroma, kana kwamba hana mpango wa kuwaza mambo mengine…. Sasa salma alianza kumwangalia Ibrahim kwa ukaribu mana alikuwa kalala fofofo kwa kuchoka,..

Salma alimkagua mwanaume wa watu mwanzo mwisho.. Lakini sasa salma alipomwangalia vizuri Ibrahim, kuna kitu alikiona…

"khaaaaaa mbona sielewi mimi"

Aliongea salma huku anakuna kichwa

Ibrahim anakuja kupata hifadhi kwa mke wa mdogo wake lakini mbaya zaidi ni kwamba, hawajuani hata tone la maji,.. Ibrahim alikuwa hospitali na hakuwa na sehemu ya kulala, lakini kwa bahati nzuri anakutana na mschana mzuri na kuamua kumseidia sehemu ya kulala, lakini mschana huyo ni mke wa chidi wa zamani na ana mtoto nae,.. Ibrahim hamjui mke wa mdogo wake, na hata mke wa chidi nae hamjui kaka yake chidi,.. Mana alipoolewa hakumkuta Ibrahim bali alisikia tu kuwa chidi ana kaka yake anaitwa Ibrahim,.. Sasa salma baada ya kumseidia mkaka huyo, lakini yeye hakuwa akilala, aliamka usiku wa saa nane na kuanza kumwangalia kaka wa watu,.. Lakini sasa salma alipomwangalia vizuri Ibrahim, kuna kitu alikiona…

"khaaaaaa mbona sielewi mimi"

Aliongea salma huku anakuna kichwa na kuendelea kusema kuwa

"sasa kama ana pesa mbona anateseka hivi, si aende gest"

Aliongea salma,.. Kwahio salma kumbe kaona pesa zikiwa mkononi mwa Ibrahim, mana kaogopa kuziweka mfukoni zisije zikadondoka bure, mana Ibrahim kwa sasa anaiheshimu pesa kuliko kiti chochote kile..

Lakini salma hakuwaza kitu alijua tu huyu ni mwanaume anaejua thamani ya pesa ni nini na ndio mana hajahangaika kutafuta gesti.. Salma alitabasamu kidogo kwa kujua tu kuwa Ibrahim alikuwa mtu anaebana matumizi ya pesa.. Huezi amini salma alichukuwa kanga na kumfunika Ibrahim kama mtoto..

"lala salama"

Aliongea salma huku akiamka kwa tabasamu zito.. Kumbe salma tayari keshamkubali Ibrahim, yaani kwa kuona tu, Ibrahim kalala kwenye mkeka alafu kashikilia pesa mkononi.. Basi huyu ndio anafaa kwa upande wake… Salma keshapenda mtoto wa watu… Alipojibwaga kwenye godoro lake jipyaa, alijifunika huku akimwangalia.. Na kujisemea kuwa

"lakini pia ni hensam kiasi chake"

Aliongea salma huku akijichekea mwenyewe hapo kwenye godoro.. Yaani wote wameridhika na maisha hayo wanayoishi….

KESHO YAKE MIDA YA SAA MBILI ASUBUHI

Tukiwa jijini Arusha kwa akina chidi na rafiki yake saidi wakiwa wanakunywa chai,

"sasa chidi sjui niende kazini"

Aliongea saidi huku wakiendelea kunywa chai,..

"ah ah saidi,.. Usiende kwanza mi nataka unipeleke kwa akina miriam mi sipajui kwao"

"chidi, ivi upo siriasi humtaki miri"

"Ohooooo yaani we utaona, we nipeleke kwao"

Kweli chidi hakuwa wa mchezo mchezo katika mapenzi

"duuuuuuuu"

"skia saidi, mwanaume usipokuwa na msimamo katika mapenzi, utakuwa sio mwanaume"

"ni kweli lakini kwa miri? Sikupatii picha aisee"

"kwani miri ana nini haswa"

"aaahhhh yule mtoto, kaacha mali zao zote kaja kuishi maisha haya hapa geto"

"hilo sio tatizo chalii yangu we subiri kitu nafanya"

Wakati huo huku nyumbani kwa sarah alikuwa ni mtu mwenye furaha toka jana,.. Akiwa yupo kitandani kaandaa pete ya kumpa chidi ili amvalishe mana chidi hana uwezo wa kukununua pete, mana sio pete tu kama pete, ni pete ya gharama kubwa, hivyo hapo kaishika huku akiibusu kana kwamba saa ikifika atavishwa na kijana chidi ambae ni mpenzi wake,…

"Enheeeee nataka miri aje ashuhudie kuwa chidi ni mpenzi wangu na sio wake"

Sarah alikusudia kabisa na miriam awepo katika swala hilo la kuvishana pete, Yaani sipati picha itakuwaje hapo,.. Sarah alichukuwa simu yake na kumpigia miriam. Simu ikiwa inaita ghafla mama yake sarah kaingia chumbani kwa sarah,

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)