MUUZA CHIPS (95) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumatano, 24 Aprili 2024

MUUZA CHIPS (95)

UMEWAHI KUONA AU KUSIKIA KUHUSU PICHA ZA AI?
Sasa naomba nikufundishe bure kabisa nawewe uzitengeneze kirahisi kabisa

Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA TISINI NA TANO
ILIPOISHIA...
"Enheeeee nataka miri aje ashuhudie kuwa chidi ni mpenzi wangu na sio wake"

Sarah alikusudia kabisa na miriam awepo katika swala hilo la kuvishana pete, Yaani sipati picha itakuwaje hapo,.. Sarah alichukuwa simu yake na kumpigia miriam. Simu ikiwa inaita ghafla mama yake sarah kaingia chumbani kwa sarah,

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
"haloo miri mambo"

"safi sarah mzima wewe"

"mzima wa afya"

"Enheee niambie shost angu"

"sasa miri, leo navishwa pete na mchumba wangu, nataka uje bwana"

"wachaaaaaaa weeeeeeeee… Jamani raha ilioje iyoooo"

"kwahio si utakuja miri"

"weeeee mimi tena, yaani ndio wa kwanza bibie"

Miriam aliongea tena kwa mbwembwe zile za kishangingi haswaa,

"fanya hivyo basi mida ya saa 5 hivi"

"usiwaze baby Sarah yaani mimi ndio kimbelembele wako"

"nitafraije jamani miri"

"kweli Sarah, tena wacha nijiandae hapa"

Aliongea miriam huku kweli akijiandaa kweli kweli,.. Simu ilikatika kisha sarah akitabasamu kwa dharau huku akisema

"njoo uwe kimbelembele wa kulia,.. Na vile vichozi vyako vipo karibu tutaona sisi"

Sasa akiongea hivyo na mama yake alikuwepo karibu

"we unaongea na nani"

"ni miriam"

"sasa aje kulia kwasababu gani"

"atalia kwasababu yeye ndio alitaka kuanza kuvishwa pete na mpenzi wake lakini mimi nimemuwahi, hivyo talia mana nimempita mipango"

Sarah hakutaka kusema kuwa, miriam na yeye wanamgombania mwanaume mmoja,.. Mama sarah hakuta kuendelea na mengine aliondoka zake… Lakini huku sarah anawaza miriam akija itakuwaje mana itakuwa mziki wa kutosha yaani hapatokalika afu wote ni watoto wenye pesa, sema kwa akina miriam wana utajiri mkubwa wakifuatiwa na akina sarah,..

"atajiju mwenyewe anywe sumu asinywe potelea mbali na kupenda kwake.. Lakini chidi simuachi ng'ooo"

Sarah aliongea huku akiamka na kwenda kuoga, mana wakati huo ilikuwa ni kama saa tatu hivi,…

Tukija huku kwa akina chidi, wakiwa ndio wanatoka kwenda kwa miriam ili kumpelekea kadi yake,..

Lakini muda huo huo simu iliita, kuangalia jina alikuwa ni saida..

"haloo mamy mambo"

"yaani chidi mume wangu mbona hivyo lakini"

Aliingea saida ambae ana ujauzito wa kijana chidi, kama unamkumbuka saida ndio yule mwenye mdogo wake ambae hakuzaliwa na nguvu za kiume, na chidi ndio msaada lakini imegeuka kwa Ibrahim, hivyo Ibrahim kwa sasa ni doro kabisaa hata haisimami mana mbegu zilizomponyesha ridhiwani ni mbegu za Ibrahim..

"kwani nimefanya nini mamiii"

"yaani mwezi mzima hata simu hupigi jamani"

"no sio hivyo.. Mi nilipata matatizo, mimi niliwekwa ndani eti"

"ndani??…. Kwa kosa gani"

"we acha tu mamii ni matatizo tu"

Aliongea chidi huku wakiwa wanapanda gari kuelekea kwa miriam,

"ok basi naomba leo tukutane, ata uone mtoto wako anavyokuwa tumboni"

"sawa ila nitakapopata nafasi nitakupigia simu"

"wewe muongo, wala hutonipigia mi najua"

"lazima nikupigie hata kama ni jioni mladi tukutane tu"

"ok poa baby"

Simu ilikata huku chidi akiwa ndani ya tax kuelekea kwa akina miriam,..

Tukija huku Dar es Salaam kwenye kihoteli ambacho anafanya kazi salma,.. Ibrahim nae alikuwepo hapo kwenye kihoteli akiwa anataka kuongea na mama mwenye kihoteli ili aweke jiko lake la chipsi,.. Mama huyo hakuweza kukataa kwasababu hata salma alitia neno kuwa huyo ni kaka yake hivyo mama alikubali Ibrahim aweke jiko la kupikia chipsi,.

Baada ya Ibrahim kukubaliwa, walitoka pembeni yeye na salma, na kuongea

"sasa ibu, tunafanyeje hapo"

Aliongea salma huku wakiwa tayari wameshakuwa marafiki na wote wanafanya kazi sehemu moja, japo Ibrahim bado hajaleta majiko yake, na sio kuwa anayo, bali atatakiwa kununua majiko upya na vifaa vingine

"sasa hapa nina laki nne tu, sasa nikipangisha chumba itapungua tena afu mtaji wa chipsi nitapataje sasa"

Aliongea Ibrahim wakiwa wanajadiliana na salma,..

"sasa skia ibu, fanya hivi.. Hio pesa tufanye mpango wa mtaji, na kama ni kulala tutaishi wote, au kuna shida kwani"

"hhhhhhhmmmmm, lakini sasa"

Kabla Ibrahim hajamaliza kuongea alikatizwa na salma

"hakuna cha lakini ibu… Hata hivyo mimi sina mtu wa kuishi nae, sio mbaya tukaishi wote"

Salma aliongea huku akiangalia chini kwa aibu mana alimaanisha kitu kikubwa sana sema kama akili huna huezi jua kama kamaanisha nini… Ibrahim haamini kama ataishi na mtoto mzuri kama huyu, tena mwenye heshma zote za kuitwa mke..

Tukija huku jijini Arusha chidi akiwa ndio anafika katika nyumba ya akina miriam,.. Saidi ndio wa kwanza kugonga kengele ya kubishia hodi na wakati huo huko ndani miriam alikuwa akijiandaa ili kwenda kwenye kasherehe kadogo cha rafiki yake, bila kujua huyo huyo chidi ndio mvisha pete,..

Mlinzi alifungua geti na kukutana na sura ya saidi, mlinzi huyo anamtambua saidi mana wanakujaga huku kuchukuwa baadhi ya vitu vya hitelini,..

"vipi saidi"

"safi broo"

"ingia basi"

"hapana nilikuwa namuomba boss miriam"

"aahhh yupo ndani kwake huko"

"naomba uniitie tafadhali"

Wakati huo chidi kakaa pembeni tena mbali kidogo,..

Dakika tatu mbele miriam huyu kaja, lakini alikutana na saidi uso kwa uso

"waaaoooo saidi jamani mambo"

"safi boss hali yako"

"nzuri tu… Ivi saidi ulishakwenda kumuona rafiki yako? Anaendeleaje kule"

Kabla saidi hajajibu,.. Chidi katokea na kujibu

"kama wewe hujaja yeye atakuja kufanya nini"

Miriam kusikia sauti ya chidi tu mana hajui kama keshatoka sero,… Miriam alimkimbilia chidi kwa nguvu zote tena kwa furaha ilio ya juuu,.. Lakini chidi akarudi nyuma na kumwambia kuwa

"sitaki kuguswa.."

Miriam haamini kama chidi kaongea maneno hayo…

"omari, una nini lakini"

"nimesema usinisogelee… Kama ni kadi yako chukuwa afu hio pesa nilioitumia nitakurudishia pesa zako"

Chidi aliirusha ile kadi pale chini, kisha akawa anaondoka na kwenda kupanda tax, lakini kabla hajapanda tax hio, simu yake inaita

"haloo chidi jamani mbona huji"

Alikuwa ni sarah ndie aliopiga simu hio

"nakuja sasa hivi mamii wangu"

Chidi alikata Simu kisha akataka kuingia katika gari

"omi jamani mimi nimefanya nini lakini"

"mamuu staki mazoea na wewe… Wewe sio wa kumwacha mdogo wangu peke yake, mpaka mtu mwingine akaishi nae.. Je nikikuuliza mdogo wangu yupo wapi utanijibu nini wewe"

"yupo kwa sarah ambaye ni rafiki yangu"

"kwanini akakae huko kwa rafiki yako kwani hapa kwenu kuna nini"

Chidi alikuwa na hasira kali, lakini miriam alikuwa akilia tu na kuzidiwa kuongea

"omariii… Mimi nilikuwa nimefungiwa ndani jamani,.. Sasa ningewezaje kwenda kumchukuwa,.. Na huyo alie nae ni rafiki yangu na bila mimi hata yeye asingelijua alipo"

"hata kama… Alafu hata kuja kuniona kule sero hujaja, ivi si katili wewe.. Tena naona kama unanichelewesha hapa.. Dereva twende"

Miriam alilia bila kuongea lolote mana hawezi kuongea kabisa yaani yeye ni mtu wa kulia tu,… Chidi na Saidi waliondoka na kwenda kwa akina sarah…

"sasa chidi mi ngoja niende job nikawasili"

"ok we nenda wacha mi niende kwa sarah"

Kila mtu aliondoka njia yake, huku chidi akipelekwa na tax nyumbani kwa akina sarah,..

Dakika 20 mbele chidi alimpigia simu sarah kuwa kafika maeneo hayo ya kwao lakini chidi hajui nyumba ya akina sarah ila mtaa kaujua kasoro nyumba tu ndio haijui,..

Sarah alifika na kumchukuwa chidi mpaka nyumbani kwao,.. Chidi aliona viatu vingi sana hapo nje, kana kwamba huko ndani kulikuwa na watu wengi sana,

"subiri hapa kwanza nimuite mama akuone kwanza"

Sarah alimwambia chidi kuwa akae hapo kwenye korido ili aonekane kwa mama kwanza kabla ya watu wengine,..

"mama,… Sapraizi mama angu"

"Sapraizi ya nini tena"

"mkweo kaja… Yupo kulee"

Aliongea Sarah huku mama mtu akiwa na shauku ya kumwona huyo mkwe…

"kwahio sasa naendaje kumuona"

"we nenda tu mama kwani si mkweo.. We vaa vizuri hapo uende"

Mama alivaa fasta fasta mana ni mume wa mtoto wake hivyo heshima itawale juu yake…

Mama alitoka na mbwembwe zote, ili kwenda kumsaminisha mkwe kabla hajasaminishwa na watu wengine, Lakini mama sarah alishangaa kumuona chidi kakaa hapo koridoni,

"heeeeeeee we chidi umefata nini hapa, au nawewe umealikwa??"

Wakati huo chidi mwenyewe katoa macho tu, haelewi elewi

Baadhi ya Wamama watu wazima ambao ni mashuga mamy, hua wanapenda kutembea na vijana ambao ni lika la watoto wao, ila hua hawapendi watoto wao wajue uhusiano huo, yaani wanakuwa watu wa siri sana kuliko hata mahusiano ya kiuwanafunzi, yaani wato secret sana, ili tu kulinda watoto wao wasijue chochote kile kuhusu mahusiano ya mtoto mdogo na mtu mzima,… Ila mama atakasirika sana tena hata kuuwa anaweza pale anapogundua kuwa yeye mama mtu na mtoto wameshiriki kufanya mapenzi na mwanaume mmoja,.. Yaani kula kuku na mayai yake,..

Basi mama alipoambiwa kuwa atoke akamuone mkwe wake hapo koridoni

Mama alitoka na mbwembwe zote, ili kwenda kumsaminisha mkwe kabla hajasaminishwa na watu wengine, Lakini mama sarah alishangaa kumuona chidi kakaa hapo koridoni,

"heeeeeeee we chidi umefata nini hapa, au nawewe umealikwa??"

Wakati huo chidi mwenyewe katoa macho tu, haelewi elewi

"we chidi si nakuuliza lakini"

"mbona wewe umealikwa hata hujaniambia"

"nimealikwa… Yaani nyumbani kwangu nimealikwa"

Chidi kuskia nyumbani kwake alishangaa na kutoa jicho,…

"ina, ina, ina mana huyu ni mtoto wako"

"kwani we umeletwa na nani hapa"

"na sarah"

"kwaio.. Wewe ndio huyo mchumba"

Chidi alikosa cha kusema,… Hivyo alibaki kimya,.. Punde si punde halima kaja na kibox ambacho kina pete ndani yake

"kakaaa… Shikamoo kaka"

"marahaba ujambo mamy"

"sijambo"

Halima alimpa kaka yake kile kibox na chidi alielewa,…

"nenda kacheze sasa"

Chidi alimtoa halima ili mama sarah aendelee kuongea ila wakati huo sarah yupo ndani anajiandaa kwa sherehe,..

"we chidi,… Ivi kwanini umenifanyia hivi lakini"

"mamy Samahani, mimi pia sikujua kama ni mwanao"

Mama sarah alikuwa anataka kulia kwa hasira,.. Lakini ghafla mwanae katokea, hivyo mada ikabadirika papo hapo

"karibu sana baba"

Aliongea mama sarah huku akiinama ile kiheshima mana si mkwe,..

Sarah alisogea mpaka pale chidi alipo na kumshika shika mabega huku akisema

"chidi mpenzi…. Huyu ndio Mama yangu mzazi, mama mzaa chema"

"ooohhh mi nilijua ni mmoja kati ya waalikwa tu… Shkamoo mama"

Chidi nae kaamka ile kiheshima na kumsalimia mama sarah,.. Lakini mama sarah alikuwa anaumia moyoni tena anamchukia sana kijana chidi..

"marahaba baba karibuni nyumbani"

Yaani mama sarah alikuwa ana duku duku la moyoni tena duku duku la mana haswa, yaani kamchukia chidi mpaka basi,…

Sasa pale pale wakachukuana mpaka kwenye sebule ambayo ilikuwa ni kubwa sana, yaani ilikuwa ni kama sherehe ya kifamilia tu,.. Basi wale ndugu waalikwa walipiga vijiukelele vya hapa na pale baada ya kumwona mchumba wa mtoto wao,.. Yaani mama sarah alikuwa akitetemeka kwa hasira, yaani kaliwa yeye na mtoto wake tena mwanaume ni huyo huyo, bora ata wangelikuwa ndugu wawili, kuliko mtoto mdogo kama huyu kuwachanganya mtoto na mama yake,..

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni