MUUZA CHIPS (93) - CnZ Media

CnZ Media

Jisomee Simulizi Mpya Kila Siku

Jumanne, 23 Aprili 2024

MUUZA CHIPS (93)

UMEWAHI KUONA AU KUSIKIA KUHUSU PICHA ZA AI?
Sasa naomba nikufundishe bure kabisa nawewe uzitengeneze kirahisi kabisa

Mwandishi: MoonBoy

SEHEMU YA TISINI NA TATU
ILIPOISHIA...
Sasa tukija huku katika nyumba ya akina miriam wakiwa wamekaa kikao baada ya ile simu kupigwa na miriam, siku ile akiwa kafungiwa ndani,.. Sasa miriam keshafunguliwa siku ile ile lakini leo ndio kikao cha familia akiwemo dada yake wa mama, na dada wa baba, pamoja na dada yake miriam aitwaye neema, ambae ni mtoto wa mamkubwa wake,..

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
"huyo kijana yupo wapi"

Shangazi mtu aliuliza

"yupo jela toka majuzi"

Aliongea miriam huku machozi yakimtoka mana karuhusiwa kutoka chumbani lakini hakuruhusiwa kutoka nje ya nyumba yao,…

"mama miriam, kwanini una roho mbaya hivyo… Kama watoto wamependana yanini kuwazuia"

Aliongea shangazi yake miriam ambae ni dada wa baba yake, yaani baba yake miriam akimuona huyu mama ni dada yake…

"ni kweli mama suzi,.. Huyu mdogo wangu ana makosa, je yeye mume wako alipokuja nyumbani kwetu alikuwa tajiri.. Au wewe ulikuwa tajiri, mbona mnamfanyia hivyo kijana wa watu"

Aliongea mama mkubwa wake na miriam ambae ni dada yake na mama yake miriam, yaani hapo wamekuja wale madada zao, mana mabibi hawapo tena duniani..

Lakini mama miriam sijui ana maneno gani ya kuwaridhisha hawa watu, mana baada ya hawa madada kuongea, mama miriam aliwanong'oneza kila mmoja maneno yake, nao walionekana kutabasamu,.. Miriam alibaki kushangaa mbona watu wa kumtetea leo wanacheka cheka tu kuna nini kati yao.. Ukumbuke kuna siku baba yake miriam alitaka kuamsha fujo juu ya mtoto wake lakini mama akamtuliza na maneno ya kawaida tu ambayo mpaka sasa hatuyajui ni maneno gani…

Haikupita muda wale wadada wakaaga kana kwamba walikuja kusuruhisha tu, sasa kama imeshindikana basi,.. Miriam alijikuta kabakia yeye na dada yake ambae ni neema,..

"we dada ney mbona wameondoka sasa"

Aliongea miriam huku akiangua kilio kwa mara nyingine, mana shida yake ni chidi atoke kule sero,..

"mi sijui miri"

Aliongea neema huku akimchukuwa mdogo wake na kuingia nae ndani,..

Tukija huku kwa akina sarah na mama yake, sarah hata mwili ulianza kupungua toka alipojua tu kuwa chidi wake na miriam wana mahusiano ya kimapenzi, tena mapenzi mazito haswa..

"sarah,.. Ivi unajua kuwa jinsi ulivyo utaamsha ugonjwa"

"mama wala mi sina kitu nipo sawa tu"

"tatizo nini, inakwenda wiki sasa huna hata raha kwanini mwanangu?… Hebu niambie ukweli"

"ukweli gani tena mama"

"au kisa ni huyo shemeji yako kuwa sero"

"wala tu"

Yaani mama anaposema shemeji ndio anazidi kumuumiza mtoto wake, yaani mpenzi wake leo aje awe shemeji, ni kitu ambacho hakiwezekani kabisa,..

"basi nakuruhusu ukamtoe"

Aliongea mama Sarah na kumfanya sarah ashtuke na kupayuka kwa nguvu

"unasema kweli mama"

Hapo ndio mama akajua kuwa hapo kuna walakini kati ya sarah na chidi..

"ndio… Nilikuzuia usifanye hivyo lakini nakuruhusu"

Kumbe Sarah alizuiwa asiende kule sero kumuona chidi wala kumtoa,.. Na mama sarah yeye hakutaka kumtoa mana angepoteza uaminifu kwa rafiki yake agness na wakati walikua wote, yaani maisha waliyatafuta wote sasa kwanini waje wagombane kwa kitu kidogo kama hicho…

Sarah akiwa yupo sehemu ya paking anachukuwa gari yake, na kwenda polisi kumtoa kijana chidi, tena alikuwa ana haraka mno,…

Robo saa mbele sarah keshafika na kamaliza kila kitu juu ya chidi na saa hio walikuwa wanatoka nae,.. Tayari keshakatiwa mzamana lakini kesi bado inaendelea tarehe fulani,..

"yaani siku zote hiizo ndio unakuja leo"

Aliongea chidi huku akifungua soli ya kiatu chake,.. Kumbe ile kadi ya benki aliiweka kwenye soli ya kiatu hivyo hakuingia nayo sero bali ilibakia kwenye viatu,..

Sarah aliiona tena ile kadi lakini kwa leo hakutaka kuuliza tena mana keshajua ukweli kuwa hawa watu ni wapenzi lakini yeye anampenda mno hivyo wala hajali kama miriam yupo nae, na kitu kinachomfanya asijali ni kwamba chidi hawezi kumuoa miriam hata iweje haiwezekani,..

"chidi mpenzi wangu, mimi nilikuwa sijui,.. Ndio nimeambiwa na mama angu sasa hivi"

Sasa chidi ndio anashangaa, mama sarah ni nani mana hamjui mama yake sarah,

"mama yako… Mama yako ni nani kwani"

"huezi kumjua ila ndio kaniambia"

"na yeye huyo mama yako kajuaje kama mimi niko polisi"

"mama yangu na mama yake miriam ni mapatna na pia ni marafiki wakubwa tu"

"ooohh kwahio mama yako kaambiwa na mama yake miriam"

"ndio"

Lakini sasa chidi akakumbuka aliompeleka pale alikuwa ni mama sarah,

"au huyu grace ndio mama yake na huyu sarah nini… Mana ndio alionipeleka pale hotelini"

Alijisemea kimoyomoyo huku akimwangalia sarah,..

"una picha ya mama yako hapo kwenye simu"

"ndio tena nyingi tu si hizi hapa"

Sasa kabla chidi hajaangalia hizo picha ghafla simu yake inaita.. Kucheki aliopiga alikuwa ni saidi yule aliokwenda na kaka yake Ibrahim kumuuguza kule Dar es Salaam,..

"halo saidi vipi"

"poa chidi, sasa mi nakuja hapo hotelini si nitakukuta"

"hapana njoo nyumbani sasa hivi"

"poa ila kuna tatizo chidi"

"tatizo gani tena"

"ngoja nije nyumbani broo"

Chidi mawazo yalimjia upyaa yaani kajiwa na mawazo upya baada ya kuambiwa kuna tatizo..

"ona sasa picha za mama angu"

"aahhh hebu achana nazo kwanza kichwa changu hakipo bizuri.. Naomba nishukie hapa nichukue toyo"

"chidi jamani si useme nikimbize gari jamani, panda twende"

Aliingea Sarah huku akimbuta chidi ndani, wakati huo chidi keshashuka kwenye gari anataka kuita toyo,..

"chidi mpenzi wangu, wacha nikimbize gari nitakuwahisha"

Chidi alikubali kupanda gari mpaka nyumbani kwake na kumkuta saidi kakaa nje ya nyumba huku akiwa kajiinamia,

"saidi, we saidi kuna nini… Afu kaka yangu yupo wapi"

Aliongea chidi huku akiwa ananuka mijasho ya sero tu huko

"utanisamehe chidi… Kaka yako nimemuuguza vizuri mpaka akapona kabisa,.. Lakini kaka yako ka…..

Katika maisha ya kibinaadamu kupata matatizo ni jambo la kawaida sana kama utalisikia kwa mwenzako, lakini pale linapofika kwako, unaliona ni jambo zito sana,… Kijana chidi muda huu huu ndio anatolewa ndani ya sero, afu hajakaa vizuri saidi kuna taarifa anaileta juu ya kaka wa chidi,..

Yaani hapo alioo kijana chidi moyo wake ulikuwa ukimwenda mbio kuliko kawaida, hayo yote ni matatizo tu,

Saidi alikuwa ana taarifa aliyotoka nayo Dar es Salaam, wakati wakiwa hospitalini

"saidi, we saidi kuna nini… Afu kaka yangu yupo wapi"

Aliongea chidi huku akiwa ananuka mijasho ya sero tu huko

"utanisamehe chidi… Kaka yako nimemuuguza vizuri mpaka akapona kabisa,.. Lakini kaka yako kagoma kuja arusha"

Aliongea saidi huku chidi akipumua kwa nguvu baada ya kusikia kumbe kagoma kuja tu,..

"saidi sasa hilo sio jambo la kutiana presha jamaa angu.. Haya sasa kagoma kwasababu gani"

"we acha tu kaka yako mbishi kweli,.. Ila kasema eti hatamani kuja huku mana akikumbuka maisha ya utajiri aliokuwa akiishi afu leo aje aonekane bwege, ni bora abaki Dar es Salaam"

Aliongea saidi huku chidi akikaa chini kwa mapumziko zaidi mana matatizo yamemuandama sana,

Sarah aliona hapa hakutokuwa na maongezi zaidi mana chidi alikuwa kachoka sana, Sarah alitoa pesa na kumpatia chidi kama lakini 5 hivi kwa ajili ya kuendelea na mambo ya sasa hivi,.. Sarah hakutaka kujali kuwa chidi ana kadi ya benki ya Miriam, na anajua kabisa kadi ya Miriam haikosagi pesa kabisa, lakini sarah hakujali hilo kama chidi ana kadi ya miriam,…

"tutaonana baadae chidi wangu ee"

Aliongea Sarah huku akitaka kuondoka, chidi alimwangalia sana sarah kushindwa hata kumshukuru,..

"mbona unaniangalia hivyo chidi"

Aliongea Sarah wakati chidi anamwangalia,..

"nashindwa hata jinsi ya kukushukuru"

"wewe tena"

Aliongea Sarah huku akirembua,.. Chidi aliamka na kumkamata sarah kisha akaanza kumnyonya denda, sarah hakujali kama mtu huyo alikuwa sero, kampa mate kama ilivyotakiwa,… Saidi kuona hivyo aliingia zake ndani kuendelea na mambo mengine…

"basi chidi niache niende baby.."

Aliongea sarah huku wakiachiana

"poa uje basi mida flani"

"ok poa.. But mdogo wako nipo nae home kwetu"

Aliongea Sarah huku chidi akishangaa, kuskia mdogo wake yupo nyumbani kwao

"kafika fikaje kwenu"

"siku ile nilipigiwa simu na miriam nije kumchukuwa"

"khaaaa.. Afu yeye akiwa wapi"

"sijui"

Sarah alianza kumkandia miriam taaratibu,

"ina mana miriam hakumrudia tena mdogo wangu"

"kwani we na miriam mpoje"

Sarah aliuliza na kujifanya hajui kitu lakini kajua kila kitu

"aahhh ni boss wangu tu"

"mmhhh sawa.. Basi mi naenda ila mdogo wako yupo salama na anajisomea vizuri tu, tena nina mpango wa kumtafutia shule"

Chidi alijikuta anampenda zaidi sarah kutokana na kuwepo kwa mdogo wake, lakini sasa bado chidi hajajua kuwa sarah na mama sarah ni kitu na mtoto wake, tena hata chidi hajui kama grace anaitwa mama sarah, ila yeye anamuitaga mamy tu…

"sarah… Sitaki kuongea mengi sana, ila ngoja nipumzike nitakutafuta"

Aliongea chidi huku akimshika sarah kiuno, na vile sarah alivyoumbika sio siri kambamba haswa…

"chidiiiii… Ivi unajua Mama angu analia sana juu yangu eti"

Sarah alianza kuongea vitu vya poiti anavyovitaka

"analia na nini sarah"

"katika familia yetu mimi nipo mwenyewe tu, hakuna mtoto wa kiume"

"kwani vipi Sarah"

"nahitaji mume chidi… Na sioni mume mwingine zaidi yako,.. Nipo tayari hata unioe leo,.. Kwanza sherehe sio lazima, mi hata ndoa ya mkeka nitakubali na hata dini nitabadili"

Katika maisha yote ya uchakaramu wa chidi hakuwahi kukutana na maneno yenye busara kama hayo,..

"sarah, hayo maneno umetoa wapi, mbona hata sijawahi kuambiwa na mwanamke yeyote yule"

"chidiiiiiiiii… Nipo tayari kuwa mkeo,.. Yaani nataka niwe chini yako"

Sarah alikuwa analia kabisa, yaani mpaka hapo tayari anamruka miriam kabisaa, na hata chidi sasa anarudi upande wa sarah..

"Sarah.. Sema nimechoka sana lakini ningelikwenda mpaka kwa wazazi wako wakanione"

"chidiiiiiiiii, mbona muda bado unaruhusu bado… Mi naomba tuende kesho juma pili mama yangu yupo nyumbani"

"sawa… Nitakwenda ila uje unichukuwe basi kesho"

"sawa baby…"

Sarah haamini kama keshafika sehemu alipo… Sarah wala hakutaka kuboronga mambo mengine, alipanda gari yake kisha huyooo kaondoka zake… Chidi anaingia ndani anamkuta saidi anaandaa mambo ya kula,..

"aahhhhhh chidi mwenzangu kwa watoto wenye pesa hujambo aisee"

"we acha tu, afu mtoto anataka nimuoe eti"

Aliongea chidi huku akivua shati ili aende akaoge,

"heeeeeeee we chidi? Unataka umuoe huyo sarah afu na miriam inakuwaje"

"nani huyo katili… Wala asinizoeee, tena akae mbali na mimi kabisaa"

Aliongea chidi huku akiwa kakasirika mno

"kwanini tena chidi na wewe ulisema unampenda sana"

"yaani anakula raha huko kwao na pesa zao, mdogo wangu kamuacha huku peke yake.. Afu anafanya kupiga simu eti aje achukuliwe,.. Sasa huyo ni mwanamke kweli"

"mmmhhhhh siingilii mambo yenu bwana"

Basi chidi alichukuwa taulo na kuingia bafuni, lakini ile kufika tu bafuni anakutana na chupi za miriam.. Kwa hasira alizitoa na kwenda kuzichoma yaani hakutaka hata kuziona katika macho yake,..

INAENDELEA...

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni