MTU WA UFUKWENI (8)

0
Mwandishi: Andrew Mhina

SEHEMU YA NANE
ILIPOISHIA...
Mahali hapo palifaa sana kupumzikia hata kama watu wengine hawakutaka kuogelea, watakaa mahali pale na kununua vinywaji.Ramson na Ringo walilazimika kuweka vinywaji ili kuwavutia wateja zaidi.

KUNA MATANGAZO YANATOKEA YAGUSE KILA UNAPOFUNGUA SIMULIZI ILI KUNIPA NGUVU YA KUENDELEA
INSTALL CnZ Media ILI USIPITWE NA MIENDELEZO KILA INAPOKUWA TAYARI

SASA ENDELEA...
Kwa ujumla palipendeza sana mahali hapa. Watu waliokuja waliongeza matangazo kwa kuwasifia rafiki zao juu ya ufukwe huo. Muda mwingine wa Mapumziko Ramson alikuwa akitengeneza cheni za Vikobe vya baharini na pia alibuni jinsi ya kutengeneza Frem za kuhifadhia Picha kwa vikobe hivyo ilipendeza sana.

Mapambo mbalimbali waliweza kuyabuni yeye na Rafiki yake yakiwepo hereni zinazotokana na vifuu vya nazi na vidude mbalimbali vya baharini. Bidhaa hizi zote ziliuzwa kwa bei nzuri ya faida kubwa, maana wengi walianza kuja na kuvutiwa na kununua. Taratibu walianza kuacha biashara ya samaki, badala yake walijikita kwenye biashara ya mapambo. Wakawa wanasimamia watu wanaokuja kuongelea na kuchukuwa picha za Arusi katika eneo hilo.

Waliingiza fedha za kukidhi mahitaji yao ya muhimu. Maisha ya Ramson na Ringo yalikuwa ni mazuri sana. Walishaanza kutoka katika hali ya kuishi kwa kubahatisha. Walikuwa wanaweka vinywaji baridi na walivitunza kwa kujaza mabarafu kwenye vyombo maalum. Zaidi ya hapo waliuza mavazi ya aina mbalimbali ya kuogelea, na mapambo mbalimbali ya asili ya pwani.

Hii iliwavutia wateja wengi sana na mara kwa mara Ringo alikwenda mjini kufungasha bidhaa za kuuza Ufukweni hapo. Miaka miwili ilipita tangu walipoanzisha ufukwe huo. Biashara ilishamiri sana na ufukwe huo ulijulikana na watu wengi. Kwa namna hiyo iliwalazimu Ramson na rafiki yake kufikiri namna ya kuweka sehemu ya kupaki magari. watu wengi walikuja na magari yao ila sehemu ya kuyaweka haikuwa inatosheleza.

Ilikuwa ni siku mpya, siku iliyopokelewa na mawingu machache angani, yaliyokuwa yakipita kwa haraka kuashiria kuwa anga lilikuwa na upepo mwingi. Asubuhi hii ilikuwa ya maandalizi na heka heka kwa Ramson. Leo hii alipanga kumtembelea Babu yake kijijini. vitu alivyonunua jana aliviweka vizuri kwenye mifuko na maboksi kusudi avipakie kwenye Taksi tayari kwa kwenda Kituo cha mabasi yaendayo kijijini kwao.

Ilikuwa ni kitambo kirefu kama cha wiki mbili zote babu yake hajamtafuta kwa simu, Hata yeye alipojaribu kumpigia simu yake ilikuwa haipatikani. Kutokana na sababu hiyo aliamua kwenda kuwaona. Asubuhi na mapema alipanda magari ya abiria maarufu kama dala dala yaliyomfikisha stendi ya magari yaendayo kijijini Taabu yanini.

Alipofika alibahatisha kupata Gari la kwanza kabisa liendalo kijijini kwao. Saa tano kamili gari lilikuwa limefika kijijini hapo. Marafiki zake wawili Walikuja kumpokea na kumbebea mizigo yake. Mmoja alibeba maboks mawili na mfuko mmoja wa Rambo kisha akatangulia na kumwacha Ramson akiongea na Jafa.“Una habari gani mtu wangu?” Alisema Jafa kwa sauti ya kimbea. “Kuhusu nini?” Aliuliza Ramson.“Wezi halisi si wamekamatwa juzi? Nakwambia watu wengi waliingia aibu na majuto sana kwa kukufukuza kijijini kwa kufuata majungu tu.” Alisema Jafa kwa kunong’ona kidogo.

“Enhee wezi ni akina nani?” Aliuliza Ramson kwa shauku ya kutaka kujua. “Huwezi kuamini mwanangu kuwa Watoto wa wakubwa wa kijiji hiki ndio wanaowasumbua watu. Alen Mtoto wa Mtendaji wa Kata, Abuu mtoto wa Katibu wa kijiji na Rama Mtoto wa Mwenyekiti wa kijiji. wote walikamatwa na kukusanywa kwenye ofisi ya kijiji mbele ya wanakijiji wote.” Alisema Jafa kwa kunong’ona kimbea.

“Kwakweli hizo taarifa zinatia uchungu sana.” Alisema Ramson…na kutulia kidogo kisha akauliza.. “Wamechukuliwa hatua gani sasa?” “Wachukuliwe hatua gani? Kwa kuzuga tu waliwekwa mahabusu kwa masaa machache, kisha baada ya Tukio hilo hawajaonekana tena ni zaidi ya wiki mbili sasa. Watakuwa wamewapeleka mafichoni ili hali ikitulia wardishwe kinyemela.” Alisema Jafa kwa masikitiko kidogo. “Okay Jafa! Poleni sana, mimi nimekuja kumwona babu na bibi yangu kisha nirudi zangu mjini.”Alisema Ramson kwa utulivu.

“Nilijua una habari juu ya bibi yako kuwa anaumwa.” Alisema Jafa. “Sina habari mtu wangu! Bibi Namkunda anaumwa? Basi ngoja niende haraka tutaonana baadaye.” Ramson aliachana na Rafiki yake na kuchapusha mwendo kuelekea nyumbani kwa Babu yake. Alikutana na Beka akiwa tayari amefikisha mzigo anarudi. “Asante Beka wote wapo nyumbani?” Alisema Aliuliza Ramson.“Ndiyo wapo tena naona kuna matibabu yanaendelea kwa ajili ya bibi.” Alisema Beka.

“Sawa ngoja niwahi.” Alitoa hela mfukoni na kuchambua kidogo kisha akampa noti moja. “Asante Bro.” Alishukuru Beka, lakini Ramson hakuwa na muda wa kuitikia kutokana na shauku ya kumwona Bibi yake ambaye inasemekana kuwa ni mgonjwa sana. Hali ya bibi kweli haikuwa nzuri baada ya kuingia ndani alimkuta bibi akiwa kalala chini hajitambui. Pembeni alikuwepo babu pamoja na mganga wa kienyeji akimwagua.

Hali ya hewa pale ndani ilikuwa imechafuliwa na madawa ya kienyeji. Madawa yaliyokuwa yanatolewa kwenye tunguli na baadhi ya vifaa vya kiganga. “Karibu sana Ramson Mjukuu wangu.” Alisema babu Kihedu kwa sauti ya unyonge. “Asante babu bibi anaumwa nini?” Aliuliza kwa hamaki. “Bibi yako katupiwa jini kali sana. Mtaalamu hapa ameona kila kitu na maadui zetu kanitajia mmoja baada ya mwingine. Tulia apate tiba halafu tutaongea mengi baadaye.” Babu alisema hivyo kwa masikitiko makubwa.

“Sawa babu pamoja na hayo uliwahi kumpeleka kwenye vipimo vya Hospitali?” Aliuliza kwa sauti ya msisitizo. “Kwa kweli Ramson Bado sijampeleka huko. Nilianza kwanza kutafuta tiba asili na ndipo nilipopata kila kitu kuhusu maadui zetu. kwa hiyo naona haina haja kuhangaika na Hospitali; huyu mtaalamu atamaliza matatizo yote haya.” Alisema babu Kihedu akimwangalia yule mganga aliyekuwa katika shughuli ya kutoa madawa kwenye mikoba yake.

“Hivi babu tangu bibi aumwe amechukuwa muda gani?” Aliuliza Ramson. “Wiki mbili alijibu babu kwa mkato.”“Sawa na huyu mganga ulimwita mara tu baada ya kumgundua bibi kuwa anaumwa?” Aliuliza Ramson. “Ndiyo Mjukuu wangu, mganga huyu nilimwita mapema sana na amehangaika sana pamoja na sisi na mpaka sasa anasema matatizo yote ameyagundua hivyo atampatia dawa mara moja za kumponya bibi yako.” Unajua Ramson Mawasiliano yamekuwa magumu sana.

Ile simu yangu imeharibika ndio maana hatukuwa tukiwasiliana. Hivi umeletwa tu na Mwenyezi Mungu.” Alisema Mzee Kihedu. “Hakuna shida babu lakini kuanzia sasa Naomba mganga aache kwanza tiba zake twende kwenye vipimo vya Hospitali sawa?” Alisema Ramson kwa mamlaka. “Wewe kijana una wazimu? huna adabu ee!” Aling’aka mganga wa kienyeji kwa sauti kubwa.

“Ramson acha tu huyu mganga amfanyie bibi yako dawa halafu tutajaribu kufuatilia mambo mengine kesho au kesho kutwa.” Babu alisema kwa udhaifu akiwa hana uhakika kama bora ni lipi kati ya dawa za Mganga na Hospitali.“Babu mimi nimesema huyu mganga akae kando kwanza bibi akaangaliwe kwenye vipimo vya kitaalamu.

Kama hakutaonekana ugonjwa tutajua kuwa karogwa kweli baadaye mganga ataendelea na kazi yake. Mimi naenda kuita Daktari babu sawa? Ramson alitoka na kutaka kuelekea Hospital, lakini kwa bahati Jafa alikuwa akipita nje ya nyumba yao akamwita na kumwagiza aende kumwita Daktari wa Dispensari ya hapo kijijini. Kisha yeye akarudi ndani.

“Nimeagizia mtu aende. Daktari atakuja hapa muda si mrefu.” Alisema Ramson. Alikuwa kama anasema peke yake, babu yake aliduwaa Wakati mganga wa Kienyeji akiwa anamwangalia kwa Jicho la shari! Baada ya muda Daktari alikuja na kuanza kumpima Bibi Namkunda vipimo mbalimbali. “Hee! mbona mmemwacha mgojwa kwa muda wote huu bila kumpeleka Hospitali, Mzee Kihedu vipi?” Aliuliza daktari kwa hamaki kidogo.

Bibi ana tatizo la Shinikizo la Damu kitaalamu wanaita:“Low Blood Pleasure!” Alisema Daktari kisha akatulia na kumwangalia Mzee Kihedu kwa makini. halafu akaendelea… “Hii ni Presha ya kushuka na Sukari iko juu sana. Pia anaonekana kuwa na upungufu wa damu mwilini. Tatizo lenu wazee wetu mnafikiri kuwa kila ugonjwa unaponywa na waganga wa kienyeji tu. Mnakosea.

Kwa sasa nitamtundikia Drip la Glucose kwa ajili ya kumwongezea nguvu kidogo kisha tutapiga Redio call Hospitali ya mkoa watuletee gari ya wagonjwa ili bibi awahishwe kwenye matibabu ya uhakika.”Alisema Daktari baada ya kukamilisha kazi yake. “Kijana inaelekea Adabu zako ni ndogo sana!” Alifoka Mganga wa kienyeji na kumwangalia kwa macho makali ya kutisha..Kisha akaendelea..“Wewe hujui dunia unavamia tu mambo, hasa baada ya kusomea mambo ya kizungu unataka kuleta dharau zako hapa. Tangu enzi za mababu watu walitegemea madawa ya miti shamba.

Wewe leo unataka kuleta dharau zako za kijinga hapa alaa!” Daktari baada ya kusikia maneno hayo makali ya mganga hakumjibu bali alimgeukia mzee Kihedu na Ramson na kuwaambia wamsubiri akaite gari ya wagonjwa. “Sawa Daktari tunakusubiri.” Alisema Ramson na babu yake alitikisa kichwa kwa kukubaliana.

“Mimi sasa naondoka!” Alisema Mganga baada ya muda kidogo kupita tangu Daktari aondoke. “Naona nimekuja kutukanwa tu na watoto wadogo hapa.” alifungasha zana zake na kuzitumbukiza kwenye mfuko. Kisha akanyanyuka kwa hasira. “Kwaheri bwana Kihedu. Ukinihitaji mimi sina kipingamizi.” Alisema huku akitoka mlangoni. “Sawa karibu sana.”

Ramson na babu yake waliitikia kwa pamoja na mganga yule aliondoka kwa hasira kubwa. Ramson alimwangalia babu yake na kutoa tabasamu hafifu huku akimtazama bibi yake aliyekuwa hajitambui pale kitandani. Huzuni ilimshika sana Ramson alikumbuka mambo mengi sana.Alijikaza sana kusudi asidondoshe machozi kwa sababu aliona hali ya bibi yake ilivyokuwa.

Hali ya Bi Namkunda ilishakuwa mbaya sana baada ya kuonekana kuwa alikuwa na kansa ya ini. Lawama nyingi alitupiwa Mzee kihedu kwa kumchelewesha kumpeleka Hospitali na badala yake kujihusisha na waganga wa kienyeji. “Kwakweli sikufikiri kuwa itakuwa ni ugonjwa wa aina hiyo. Vipi lakini mke wangu atapona lakini?” Aliuliza Mzee kihedu kwa masikitiko makubwa sana.“Tunajitahidi kwa kadri ya uwezo wetu na dua zenu tunazihitaji sana pia.” Alisema Daktari kisha akapotelea ofisini kwake kuendelea na majukumu.

Muda si mrefu akapita akiwa na baadhi ya vifaa akiwa ameongozana na madaktari watatu wakielekea kwenye chumba alicholazwa Bibi Namkunda. Wakiwa wamekaa kwenye viti nje ya Chumba hicho walikuwa wametekewa kabisa wasijue la kufanya. Hawakubanduka mahali hapo kwa muda mrefu sana kwani pia hawakupewa nafasi ya kuingia katika chumba hicho cha wagonjwa mahututi. Mchana wa siku hiyo iliwabidi waende kutafuta chakula kwenye Hoteli iliyopo karibu na Hospitali hiyo.

USIKOSE SEHEMU IYOFUATA

Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)