Nyumba ya Wachawi (3)
Zephiline F Ezekiel
5 min read
Mtunzi: Denis Benard
SEHEMU YA TATU
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Baada ya Elly kubaki pale nyumbani kwao,alijikuta akipokea maswali mengi sana kutoka kwa watu waliokuwepo eneo la nyumba yao,wakitaka kujua zaidi nini na nini kiliendelea pale na namna alivyoathirika.
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
‘’Kijana pole sana kwa hili’’ aliongea mzee mmoja pale.
‘’Asante sana Mzee Koo,nimesha poa’’ Elly alijibu.
‘’Mmmh, embu naomba unieleze hasa,juu ya mazingira husika ya tukio hili lililokusibu’’
‘’Mzee wangu sijui hata niseme nini,lakini zaidi ya yote ,ndivyo ilivyokua.Zaidi ya yote naomba tu tujiandae,tukajaribu kumuona huyu rafiki yangu Faluu,ili tupate na nafasi ya kumzika mama yake,lakini ni tatizo,maana sijui hata hari yangu itakuaje baada ya kusema kitu hiki..’’alisema Elly
Wakati akiwa pale watu walitawanyika na wakakubaliana waende kujiandaa kabla ya kuaanza safari ya kwenda porini kumtafuta Faluu.Wakati Elly akiwa ametulia nyumbani kwao katika chumba chake akisubiri watu wakusanyike ili wakaendelee na majukumu yao,Kabla muda waliokubaliana haujafika,Alianza kuhisi hali tofauti katika chumba kile na kuanza kusikia milio ya ajabu
‘’Huuuu…! Huuuuuu!’’ kama upepo na wakati mwingine alisikia kama kuna mtu anamwita,hali ile ilimfanya aogope sana na kupelekea kushindwa kujizuia kukaa ndani,ndipo alipoamua kutoka nje ili akatafute msaada kwa watu.Wakati akiwa anataka kufungua mlango ilia toke,alikuta mlango haufunguki…ile hali ilimshangaza sana.
(Huku akitetemeka,alianza kupiga kelele)
‘’Mama…..!mama..!mama…!,jamani nisaidieni,Nakufa” Elly alianza kupiga kelele.
Wakati huo Elly akiwa ndani,watu walianza kukusanyika pale katika nyumba yao na zaidi ya 75% ya watu waliokuwa wanatakiwa kwenda katika shughuli ile walikua wamefika ,hivyo walikua wanamsubiri Elly tu maana ndiye kiongozi wa sehemu waliokua wanataka kwenda.
‘’Jamani,mbona hatumuoni Elly,eti..mama Elly,Elly yuko wapi??’’ Mzee mmoja aliuliza.
Lile swali lilimshtua sana mama yake Elly nakuanza kumtazama huku na huku,huku akianza kua na wasiwasi.
‘’Mmmmh,sijui alikua hapa hapa,ila muda Fulani aliniambia anaingia ndani ili apumzike wakati anasubiri mkusanyike,toka hapo sijamuona ,embu jaribu kumuona humo chumbani kwake’’ mama yake Elly aliongea..
Kutokana na kauli ya mama yake Elly,ilipelekea wanakijiji waliokuwepo pale kuanza kua na wasiwasi na hivyo kupelekea kua na minong’ono ya hapa na pale kutokana na tukio lile.Mmoja alijitokeza na kwenda kumuona katika chumba chake.Wakati yule mtu anaenda Elly alikua akipiga kelele,lakini sauti ya ajabu ilimueleza Elly…
‘’Wewe si unajifanya mjanja,sasa nataka nikuoneshe,maana naona kuna mtu anakuja kukuona’’
Ghafla walipotea katika chumba kile na Elly kujikuta akiwa katika pori zito lililompelekea kuogopa sana…
(Kwa sauti ya upole huku akitetemeka,Elly aliongea)
‘’Samahani,umenileta wapi huku,mbona mimisipaelewi,halafu pia tumekujakuja tu,naomba nirudishe nyumbani’’
Lile jitu lilicheka sana tena kwa mguvu huku ardhi ikitetemeka na baadae liliongeaa
‘’Elly rafiki yangu wewe unajifanya mjanja sana,uliambiwa na mkubwa wangu kua ulichokiona kule usiseme sehemu yoyote,lakini kwa vile wewe unaakili kutushinda ukasema,sasa mimi nimekuja kukuua leo,hilo tu ndio jukumu langu,hahahahhahahahah’’liliongea na baadae lilicheka sana…
Maneno yale yalimfanya Elly aone kama hakuna maisha tena kwa upande wake,hivyo alijikuta nguvu zikimuishia..
‘’Naomba….,niko chini ya miguu yako,yaokoe maisha yangu,sitafanya tena hayo mambo,nisamehe tadhali’’aliongea Elly huku machozi yakimtoka kama maji na macho yake yakiwa mekundu sana.
Wakati akiongea lilelijitu lilikua limetulia likimsikiliza huku likiwa limeinamisha kichwa chake chini,baada ya Elly kumaliza kuongea liliinua macho yake huku yakiwa yatoa moto na vidole vyake vikiwa vimetoa kucha ndefu sana na kila alipokua akiongea mdomoni mwake mlikua mnatoa moto huku akiwa anamsogelea Elly..
Baada ya Elly kumtazama na kuona muonekano wake mpya,alishtuka sana na kujikuta macho yake yanapoteza uwezo wakuona mbele kutokana na ule moto.Wakati lile lijitu likitaka kumuua Elly ghaflaulitokea Mwanga mkali sana katika eneo lile………
Baada ya mwanga ule kutokea,lile jitu lilipotea ghafla katika eneo lile na katikati ya ule mwanga alimtokea mtu mweupe mwenye mavazi meupe ,Elly alibaki akimshangaa tu,
(Akiwa anashangaa,Elly alimuuliza)
‘’Mbona mnanitesa sana na wewe ni nani?? ‘’Elly aliuliza
‘’Pole saana kijana,nimefatilia sana namna unavyoteseka na naomba uamini kua mtu mnayetaka kumtafuta nimzima kabisa na muda si mrefu utamuona,lakini swala ambalo napenda sana umfikishie ni hili,naomba umwambie kua katika maisha yake atateseka sana,lakini lazima awe na matumaini ya kufika kule anakotakiwa kufika’’aliongea yule mtu pale na baadae alipotea.
Baada ya kumaliza kuongea na kupotea,ilikua kama saa 9 usiku na ghafla alimuona Faluu mbele ya macho yake,Alishangaa sana …
.
‘’Daah,rafiki yangu Faluu ni wewe??ulikua wapi ndugu yangu na unaendeleaje??’’ Yalikua ni maswali mfululizo ambayo Elly alikua akimuuliza Faluu.
Katika kipindi chote hicho,Faluu alikua hamjibu kitu chochote na zaidi ya yote alikua akimtazama tu.Wakati akimtazama ulipita upepo katika eneo lile na dakika chache walijikuta wakiwa nje ya nyumba ya akina Elly,Elly aliona kama miujiza ujiza ikimtokea,maana mara yuko hapa,mara hayupo…..
‘’Mbona kama maisha haya mimi siyaelewi?,nini maana yake??’’alikua akijiuliza pasipo kua na majibu. Wakati wakiwa nje alikua akitoka mtu mmoja akienda kwake huku wakiwa wamekata tama juu ya kila kitu kilichokua kikiendelea juu ya kumtafuta Faluu na Elly..
(Alishtuka sana kuwaona pale)
‘’Jamani! Jamani! Jamani! Faluu na Elly hawapa nje”aliongea huku akikimbilia ndani,watu wote walishtuka na kujikuta wakishindwa kujibu chochote…na mwisho wa siku watu wote walikimbilia nje ili wakawaone vijana hawa maana akili zao zilikua zimechoka na kushindwa kuamua chochote kwa namna mambo yalivyowakabili.
Baada ya kufika nje walipatwa na mshangao sana,watu wakulia walilia,wakufurahi walifurahi,kila mtu alikua na hisia zake kwa kipindi kile,ilikua ni shangwe iliyochanganyikana na huzuni kutoka na mambo yaliyowakabili,wengi wao walimfata Faluu ili walau awaambie kitu chochote..
‘’Faluu baba embu ongea,nini kimekukuta?’’aliuliza mama mmoja huku akitokwa machozi..
Faluu hakua na cha kujibu na zaidi machozi yalikua yakimtoka tu pale,kutokana na hali ile,Elly alijibu..
‘’Mimi naomba mumuache Faluu,maana ninaamini hawezi kujibu chochote,hata mimi nimemkuta katika mazingira hayohayo’’aliongea Elly..
‘’Kwani umemkuta wapi??na kwanini umeenda peke yako??’’
(Huku akitabasamu kwa hudhuni,Elly alijibu)
‘’Wewe acha tu,ni historia ndefu,kwamaana sijui hata niseme nini hapa’’
‘’Kwanini unasema hivyo kijana??’’aliuliza mzee mmoja.
‘’Mimi ninachoweza kukumbuka ni kwamba,mimi nilikua nimelala ndani kwangu nikiwa nasubiri muda ufike kama tulivyokubaliana,lakini kilichonikuta nashindwa hata kuelezea,lakini zaidi ya yote nashukuru sasa Faluu rafiki yangu huyu hapa tu’’Aliongea Elly huku machozi yakiwa yanamtoka.
Kutokana na hali ile,ilipelekea watu waliokuwepo pale wawe na uzuni saana na baadae walichukuliwa na kupelekwa ndani na kusubiri utaratibu mwingine wa nini kiendelee.Kipindi hicho Faluu alikua mtazamaji tu.Ilipofika asubuhi kama ya saa kumi na mbili alifajiri,Faluu alisikia sauti kwa mbali ya watu wakilia,Sauti ile ilimfanya ashtuke sana na kutoka nje,ndipo alipoona watu wakilia na ghafla kumbukumbu zake zilirudi..Akajikuta mawazo yakimjia..
‘’Baada ya mambo yote ya msiba kuisha hakikisha unaenda kwa mjomba wako,hayo ndiyo maneno ya mwiso nilioachiwa na mama yako”
‘’Inamaana ni kweli mama yangu amefariki?? Inawezekana vipi?? Na kwanini aseme mimi niende kijiji cha pili?? Nini tatizo??’’ yalikua ni mawazo yalioambatana na maswali mengi huku machozi yakimtoka.
Mwisho wa siku alianza kupiga kelele na kutoka mle ndani akikimbia huku akielekea kwao ilikujua nini kinaendelea juu ya taarifa alizosikia kuhusu mama yake,watu walishtuka kutokana na kelele zile na kuanza kumfatilia kujua wapi anaelekea,pia kwasababu Elly alikua amebaki mle ndani walianza kumuuliza kama kuna chochote kamueleza..
‘’Vipi mbona ndugu yako ameshtuka na kuondoka ghafla hivi??kuna nini kinaendelea?’’Elly aliulizwa.
‘’Kwa kweli nashindwa jibu kamili la kutoa hapa,ila nililoona ni kwamba alisimama dirishani nakuwaona watu waliokua wakilia na baada ya dakika chache ndio hilo lilotokea likatokea’’aliongea Elly
Baada ya hapo waliacha kumuuliza maswali na badala yake walianza kumfatilia ilikujua wapi ameelekea,Baada ya Faluu kufika kwao huzuni iliongezeka zaidi baada ya kukuta nyumba yao yote imeteketea kwa moto,alilia sana..
‘’Mama hivi ni kweli umeondoka mama yangu na hii ndio njia uliyoondokea??, inawezekana vipi mama yangu? Maana nakumbuka hata uliponiamsha na kunitaka niwahi shambani na ukaniambia natakiwa nikazane maana maisha ya kufanikiwa yanataka mapambano,kumbe ndio ulikua unaniaga,hapana mama yangu ‘’ alilia sana Faluu na kujikuta akiwa akigaa gaa chini..
Kilio kile cha Faluu ni kama kilikua kikiamsha tena hisia za watu waliokuwepo katika eneo lile na hasa kutokana na hali ya kuondokewa na mama na nyumba nzima na kila kitu ndani kuteketea.Jioni yake walishughulikia maswala ya mazishi kwa maana ule mwili ulikua umekaa muda mrefu na hivyo kupelekea kuanza kuharibika.
Baada ya mazishi Faluu alikua hana sehemu ya kwenda,hivyo mama yake alimchukua na kumtaka aende kukaa kwake na watu wengine walijitolea kumsaidia vitu vingine.Siku mbili baadae akiwa amekaa nje ya nyumba yao,alijikuta mawazo yakimjia..
‘’ ’Baada ya mambo yote ya msiba kuisha hakikisha unaenda kwa mjomba wako,hayo ndiyo maneno ya mwiso nilioachiwa na mama yako’’
Maneno yale yalimshtua tena sana…………………………
Mawazo yale yalimfanya kua na wakati mgumu sana,maana hakujua ni maamuzi gani ambayo angechukua kwa kipindi hicho.Wakati akiwa amekaa pekee akiyatafakari maisha yake kwa ujumla,Alijikuta akisimama na kuelekea ndani asijue nini anaenda kufanya ndani,Alipokaribia mlangoni alikutana na Elly..
‘’Rafiki yangu vipi mbona sikuelewi?nimekutafuta tuje kunywa chai sijakuona na pia nikiangalia sura yako naona kama huko mbali sana?sikiliza hiki si kipindi cha kuwa mbali hivyo kimawazo,kwa maaana utakuwa unakaribisha vitu vinginee ambavyo kimsingi vitakuletea matatizo sana katika afya yako,kua makini sana na maisha yako yanayokuja basi na vitu vingine’’ aliongea Elly kwa uchungu sana.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni