Nyumba ya Wachawi (7)
Zephiline F Ezekiel
6 min read
Mtunzi: Denis Benard
SEHEMU YA SABA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Wakati mvutano ukiendelea Faluu alikua akiwashangaa tu huku akishindwa aongee nini,
‘’Mjomba usijali kwa kila kitu kinachoendelea humu,kikuwa naomba uzoee sawa na usiwe na wasiwasi kabisa,amini kua huko nyumbani kwa mjomba wako’’ Mjomba wake Faluu aliongea.
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
‘’Sawa mjomba,lakini mnanipa hofu saana juu ya haya mazingira ninayokutana nayo humu ndani’’ Faluu aliongea.
Muda mfupi baadae Mfupa alirudi na kumletea chakula Faluu,mjomba alipokiona tu alishtuka na kumwambia Faluu ampatie kile chakula na baada ya kukiona aligundua kama kimewekwa sumu,aligeuka na kumuona Mfupa kwa hasira..
‘’Mfupa umefanya nini sasa?kwanini umeweka sumu?’’aliongea mjomba wake Faluu na baadae aliweka mikono juu na kuondoa ile sumu na kisha alimpa Faluu.
‘’Kula mjomba sasa kiko salama wewe kula’’aliongea Mjomba na kumgeukia Mfupa.
‘’Mfupa na wewe umekua mkubwa humu ndani siyo,mpaka inafikia hatua unafanya yako’’aliongea mjomba na baadae aliondoka na kumuacha Mfupa na Faluu mule ndani.
‘’Wewe ndiye unafanya mimi natukanwa siyo ,sasa utaona’’ aliongea Mfupa na baadae aliondoka.
Faluu alijikuta akiwa amebaki katika Fumbo kubwa sana,maana mpaka pale hakujua nini hatima ya maisha yake…….
Siku zilizidi kusonga huku kukitokea na kutokuelewena katika ile nyumba kati ya mjomba na Mfupa na Mfupa na Faluu,waswahili wanasema ilikua ni kama Mechi kati ya Simba na Yanga,kwa maana kila mtu alikua mbabe kwa mwenziye.Lakini kwa upande wa Faluu siku moja alionekana kua na mawazo sana,akiwa amekaa chini ya mti mmoja mkubwa akiwa anapunga upepo na kujiliwaza,alitokewa na mama yake,hali ile ilimshtua sana..
‘’Samahani mwanangu,usinikimbie na wala usiogope mimi ni mama yako,nakuona namna unavyopata shida mwanangu,naomba tu uelewe kua mimi mama yako nipo na wewe kila hatua unayopiga,kikubwa naomba uwe mvumilivu na ujue kua wewe ni motto wa kiume baba sawa,hivyo unatakiwa uwe shujaa usichoke’’aliongea mama yake na baadae alipotea ghafla.
(Faluu aliogopa sana)
‘’Sasa mama kama upo mbona unakimbia sasa na kuniacha mimi peke yangu,ila atakama umepotea hapa kaa ukijua mwanao nateseka sana kama unavyoona,ila kwa vile wewe umesema maneno hayo uliyosema basi mimi sina shaka mama yangu,lakini pia pamoja na hayo yote unakumbuka kua wewe ndiye uliyesema mwanangu unakua na wasiwasi na mimi,kwani leo ndio mara yangu ya kwanza kubaki nyumbani peke yangu?lakini nilipoenda shambani na kurudi sikukukuta’’Faluu aliongea huku akilia,maana kitendo cha mama yake kutokea pale kilimrudishia kumbukumbu zake za nyuma.
Baada ya kipindi hicho,maneno ya mama yake yalimtia moyo na kumpa ujasiri na kadri siku zilivyozidi kwenda ndivyo alivyozidi kuzoea mazingira ya pale nyumbani na kijiji kwa ujumla,maisha yalienda huku mauza mauza yakiwa yanaendelea kutokea pale nyumbani.Ulikua ni usiku mmoja Faluu alikua amelala katika chumba chake baada ya chakula cha saa8 usiku kama ilivyo kawaida,aliota ndoto moja akiwa ametokewa na mtu wa ajabu..
‘’Faluu nenda katika msitu mmoja unaitwa SHAI,ukifika kule utauona mti mmoja mkubwa sana kushinda miti yote katika msitu ule,najua msitu ule unatisha sana,lakini hakikisha unashinda na kukata mizizi ya ule mti sawa,ila usimuambie mtu yeyote hapa kwenu fanya siri ’’ile ndoto ilipoisha alijikuta akishtuka sana huku akitokwa jasho sana,kutokana na hali ile aliamini kua ile ndoto ni kweli na kitu hicho anatakiwa kukifanya.
Asubuhi ilifika na alifanya shughuli za pale nyumbani kama kawaida na alipomaliza alianza kutafuta utaratibu wa namna gani atafika huko SHAI maana hata msitu wenyewe haujui,Alitoka nje na kuanza safari huku akiwa hajui ni wapi akielekea,alipofika mbele alikutana na dada mmoja mzuri..
‘’Mambo dada!’’Faluu aliongea
‘’Safi tu,habari yako’’Alijibu yule dada huku akiwa anatabasamu
‘’Nzuri tu ,samahani mimi naitwa Faluu,siyo mwenyeji sana wa hiki kijiji,ila ninaomba unielekeze katika msitu mmoja hivi unaitwa SHAI,ndiko naelekea’’aliongea Faluu.
(Yule dada alishtuka sana)
‘’Mmmh,mimi naitwa JOYC,Faluu wewe ni mgeni katika hiki kijiji,halafu unataka kufika katika msitu wa SHAI,unajua huo msitu unatisha sana’’aliongea JOYC.
‘’Joyc historia yake nimeshaipata,lengo langu kukuuliza wewe ilikua unielekeze tu,kama hujui basi’’aliongea Faluu huku akiwa anaanza kuondoka akielekea sehemu asiyoijua.
‘’Hamna siyo hivyo,nakuonea huruma,lakini pia unaweza kuniruhusu nikusindikize huko,yaani twende wote’’Aliongea Joyc
(Faluu alishtuka sana)
‘’Hee!!wewe umesema kunatisha ,halafu unisindikize,mimi nilitaka unielekeze tu sawa na siyo unisindikize’’aliongea Faluu.
‘’Hamna nakusindikiza tu,tunaenda wote ‘’Aliongea Joyc
Baada ya mvutano wa muda mrefu,walikubaliana na hivyo Faluu na Joyc walianza safari kuelekea katika huo msitu wa SHAI,walitembea takribani masaa 5 huku wakiwa wanabadirishana mawazo ya hapa na pale,walipokaribia katika huo msitu walianza kusikia kama tetemeko na walipotulia,ilisikika sauti na vicheko vya ajabu ajabu,wote waliogopa ..
‘’Mmmh, Joyc kutaendeka kweli humu’’ aliongea Faluu huku akionekana kuogopa sana
‘’Ndio sasa kwanini tusiende?,Safari tuliyotembea kutoka nyumbani mpaka hapa ni ndefu,hapa mpaka tuingie ndani’’ Joyc alijibu...
Kutokana na maneno ya ujasiri kutoka kwa Joyc,yalimuongezea nguvu sana Faluu na kujikuta akiendelea kusogea katika ule msitu,lakini ghafla akiwa anatembea alisikia kicheko nyuma yake kilichomshtua sana na alipogeuka alimuona yule mtu ambaye huwa anapinga sana nyumbani(Mfupa),aliogopa sana.
‘’Na wewe umefata nini huku? Na umejuaje kama mimi niko huku? Na joyc umempeleka wapi’’ Faluu aliuliza huku akiwa anatetemeka .
(Mfupa alicheka sana)
‘’Unataka kujua mimi nimefikaje? Na Joyc wako nimempeleka wapi? Sasa ngoja’’aliongea Mfupa
Baada ya hapo alijibadirisha na kua Joyc na mara akarudi na kua yeye,kitendo kile kilimuogopesha sana Faluu na kila alipokua akigeuka huku na huku hakuona mtu yeyote zaidi ya miti na iliyokua imezunguka tu katika eneo lile.
‘’Haya sasa umeona namna nilivyofika na aliko Joyc wako?wewe umefanya mimi nadharaulika sana nyumbani sasa leo ni leo’’aliongea Mfupa..
‘’Mbona mimi sikuelewi Mfupa?nimefanyaje sasa?’’aliongea Faluu huku mawazo yake ya kihesabu siku hyo kua siku ya mwisho ya maisha yake.
Mfupa alimsogelea na kumkaba koo kwa nguvu kwa lengo la kumuua,lakini ghafla bila taarifa Mfupa alipigwa kofi moja la mgongoni….
Alipogeuka nyuma alikutana uso kwa uso na mama mmoja aliyekua na nywele nyingi Na sura ya kutisha na kumpoteza palepale katika yale mazingira na Faluu alishtuka sana alipomuona mama yake akiwa katika muonekano ule..
‘’Heeee!! Mama kumbe ni wewe’’ Faluu aliongea huku akilia, Mama yake hakumjibu kitun chochote na badala yake alimnyoshea mkono na kujikuta akiwa ametokea nyumbani kwa mjomba wake.
Alipokua katokea nyumbani alisikia sauti ikimueleza,
‘’Mwanangu kua makini sana na sauti unazozisikia sikia,cha msingi kaa ukijua kua hapo ulipo umezungukwa na maadui wako tena wakubwa’’ mzimu wa mama yake uliongea na kabla Faluu hajajibu chochote ulipotea pale pale..Kitu hiki kilimfanya Faluu kua na wasiwasi sana.
Baada ya kufika saa sita usiku huku Faluu akiwa ametulia katika chumba chake hana hili wala lile,alianza kusikia sauti za ajabu katika ile nyumba ya mjomba wake kama ilivyokawaida,aliogopa sana na kujikuta akitetemeka ,kichwa chake kilijaa na mawazo yaliyokinzana..
‘’Mmh! Watu hawa,hivi niende nikaone?’’ alikua akijiuliza huku akisamama na kusogea katika eneo lililokua likitoka sauti ile..wakati akiwa anajongea taratibu,alisikia sauti nyingine katika akili yake ikimueleza.
‘’Faluu unaenda wapi sasa? Tafadhali usiende,kwanini unajitafutia matatizo,twende tukalale’’ yalikua ni mawazo katika kichwa chake,alipofikiria mawazo yale katika kichwa chake,alisita kidogo na kumfanya asimame kwanza na kuyatafakari mawazo yale kwa sekunde 30 hivi,lakini wakati akiwa pale aliisikia sauti nyingine ikimueleza tena .
‘’Mbona unakua kama siyo mwananume?unaogopa nini sasa,embu twende bhana’’mawazo mengine ya kishujaa yalimjia katika mawazo yake na kumtia nguvu na baada ya hapo alijikuta akishawishika kusogea katika eneo la tukio ili ajue kinachoendelea.
Alipozidi kusogea katika eneo lile,alipofika dirishani na kuchungulia,alishtuka baada ya kuona eneo lote lile likiwa nyeupe na hakubahatika kuona chochote katika eneo lile,baada kuwa hivyo alikimbia na kwenda kujificha katika chumba chake,kwa bahati mbaya wakati akikimbia alijigonga katika ndoo zilizokua zimepangwa na kufanya wale watu washtuke.Aliogopa sana na kukimbilia katika chumba chake na kujificha kama moja wapo ya njia ya yeye kujiweka mbali na wale watu wabaya..
‘’Mungu wangu nimefanya nini mimi?mbona yananikuta haya mambo?nisaidie Mungu wangu’’Faluu Alikua akijiongelea huku tumbo lake likitetemeka.
Huku wale watu baada ya kusikia ile sauti walishtuka na kuanza kujiuliza,kulikoni hiyo sauti..
‘’Mmh!nini tena hiyo?mbona kama kuna mtu alikua anatufatilia?’’Mtu mmoja aliuliza na kabla mjomba wake Faluu hajajibu alisimama mtu mmoja na kuongea.
‘’Mpwa wa Huyu mzee alikua akitufatilia hapa na mimi baada ya kumgundua nilifanya vitu na kumfanya achanganyikwe na hivyo kumpeleka akimbie’’Aliongea mtu mmoja,.
‘’A...m, a.m,sijui mimi niseme nini? Lakini mimi sijui ni kwanini’’aliongea mjomba wake Faluu,huku akionekana kufikiria..
‘’Jamani tuendelee na shughuli yetu karibu kuna kucha sasa hivi’’aliongea mzee mmoja pale na baadae waliona waendelee kula chakula chao pale.Mwishoni baada ya kumalizia mtu mmoja alisimama na kuongea neno moja tu kabla hawajatawanyika pale..
‘’Sikiliza mzee ,mwambie mpwa wako aache mambo anayofanya,vinginevyo utatuona sisi wabaya sawa’’aliongea na baadaye waliondoka kiasi kama cha saa 10 alfajiri hivi.Mjomba wake Faluu alibaki na mawazo maana hakujua nini afanye na mwishowake alienda kulala.Ilipofika asubuhi Faluu alionekana kuwa na wasiwasi sana,alipokua akitoka nje alikutana uso kwa uso na mjomba wake na kumfanya arudi ndani ghafla,mjomba alimuona na kumuita ..
‘’Faluu,Faluu’’Mjomba alimuita
‘’Naamu mjomba’’Faluu aliitika
‘’Mbona unaniona halafu unarudi ndani?kulikoni?’’aliongea Mjomba..
(Huku akicheka,Faluu aliongea)
‘’Hahahah..hamna mjomba niko sawa tu’’Alijibu Faluu
‘’Huko sawa wakati mimi nikikuona tu kuna vitu naviona katika uso wako kama unavicha ?sasa sikiliza mimi mjomba wako nakupenda sana na sipendi yatokee mambo mabaya kwako sawa kua makini’’aliongea mjomba na baadae aliondoka
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi
Chapisha Maoni
Chapisha Maoni