Mtunzi: Maundu Mwingizi
SEHEMU YA PILI
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Alikuwa amepoteza maisha. Suhail akafuta machozi yaliyoanza kumtoka bila ya kutaka, akageuza uso wake upande mwingine kuikwepa taswira ile.
KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO
SASA TUENDELEE...
Hamaadi!
Akakutana macho kwa macho na yule mzee wa ki-asia aliyekuwa akimuangalia sana hapo awali, akiwa amelala juu ya dimbwi la damu, akionekana kuwa hai lakini hoi bin taabani. Alimsogelea haraka na kujaribu kumuinua ili amkokotee nje, lakini yule mzee akakataa, akawa anamtazama Suhail si kwa jicho lile la mwanzo kabla ya ajali bali sasa kwa jicho la kukata tamaa.
“Wacha…nikus…saidie mzee wangu! Ajali hii!” Suhail alimwambia kwa taabu.
“Amaa kweli aheri ya mrama kuliko kuzama!” Aliongea kwa taabu sana yule mzee , na Suhail akamshangaa.
“Unamaanisha nini mzee?”
“Bora chombo kiende mrama lakini kifike salama, kuliko kiende salama halafu kikaishia kuzama!” Mzee alimjibu kwa taabu. Maneno yale yalimuacha hoi Suhail.
“Bado sijakuelewa mzee…hebu tutoke nje ya hili basi kwanza…linaweza kushika moto hapa!”
“Tulimsifia sana dereva wetu kuwa ni bingwa, basi likaenda vema, tukajiona tumekabidhi roho zetu sehemu salama, kumbe haikuwa! Tukamsahau mpaka Mola wetu…na sasa tumeishia kuzama tu mwanangu…mi ndio basi tena!” Mzee alizidi kuongea kwa taabu kutokana na maumivu makali aliyokuwa akiyapata. Alionekana wazi kuwa amepoteza tamaa ya kupona.
“Mzee lakini hayo sio muda wake huu! Nadhani tungeangalia hali yako kwanza kwa sasa!” Suhail alimsisitiza.
“Wala usihangaike mwanangu, utapoteza muda bure. Afya yangu si muhimu tena, ninakufa tu mimi. Nimeumizwa sana, na nilijua tu kuwa leo ni lazima watanimalizia kwenye ajali hii. Hata wewe pia nimejitahidi kadri ya uwezo wangu kukukinga, bila ya hivyo nawe ungekuwa maiti saa nyingi tu.”
Nini??
Sura ikambadilika Suhail. Alimtazama yule mzee mwenye wingi wa kauli tata, kama anayemtazama jini.i
“Mzee kwa nini unasema hivyo? We’ ni nani kwani? Ulijuaje kama leo itatokea ajali hii? Na ni akina nani hao hasa wanaotaka kukumaliza?” Alimvurumishia maswali kwa wahka mkubwa.
Badala ya kumjibu yule mzee aliliachia tabasamu la dhaifu, la huzuni, la kukata tama. Tabasamu la kumuonesha Suhail kuwa alikuwa hajui chochote kinachoendelea. Walibaki wakitazamana kwa takriban dakika mbili hivi, kisha yule mzee akashtuka na kukaza macho kuelekea chini, upande wa pili wa viti alivyokuwa amelalia baada kutupwa tupwa huku na kule wakati wa ajali, kisha akawa anamuonesha Suhail kwa kidole chake usawa wa kule alipokuwa anatazama., Haraka Suhail akapeleka macho kule alipokuwa anaelekezwa. Hapakuwa na kitu chochote zaidi ya mifuko na mabegi yaliyosambaa hovyo kutokana na kuanguka kwa lile basi.
“Lete hilo begi kubwa jekundu…ni la kwangu usiogope.” Mzee alimtuma, na Suhail akashangaa kuona badala ya kujali afya na usalama wake kwanza, mzee alikuwa anataka begi, lakini hakubisha kijana wa watu. Akajikongoja mpaka lilipokuwa lile begi lile na kumsogezea kwa shida yule mzee., Mzee akainuka kwa tabu sana, kisha akafungua zipu kubwa ya katikati kwenye begi lile, na ndipo Suhail alipopigwa na butwaa, huku akishindwa kuamini iwapo alichokuwa akikiona ndani ya begi lile kilikuwa ni chenyewe, ama anaota. Akili yake ilijaribu kufanya kazi mara kumi kidogo, lakini bado hakupata jibu la kile alichokuwa akikiona..
Mzee aliliona hamaniko la Suhail lakini hakujali. Bila shaka alijua tu kuwa kijana angeshtuka, kwani lile begi jekundu lilikuwa limesheni pesa mpaka juu, tena zikiwa ni dola mia-mia tu za kimarekani.
Lah!
“Usichanganyikiwe kijana. Mimi nakufa, hilo halina pingamizi,ila nimekutunuku.Pesa zote hizi nakupa wewe na mali zingine ambazo utazijua muda ukifika.”
Ama!
Baada ya maneno hayo mafupi, ambayo kwa hakika Suhail alikuwa kama kwamba anayasikia kutokea mbali sana na pale walipokuwa, mzee akavua pete yake kubwa yenye kito cha rangi ya njano aliyokuwa ameivaa kwenye kidole chake cha kati na kumshika mkono Suhail, akamvisha ile pete.
Eh!
Suhail akajihisi akiingiwa ganzi mwili mzima. Haya mambo yalikuwa mazito sana kwake kuyabeba.
“Ah, sasa…hii pete nayo ni ya nini, mzee?”
“Hiyo pete inaitwa ‘khatam budha’.Itakufaa sana maishani… itakulinda na kukuongoza. Hiyo ni silaha na siri ya mali zote hizi unazoanza kuzimiliki sasa. Sina muda mrefu sana wa kuendelea kuishi hapa duniani kijana, hivyo nisikilize kwa makini sana...” Mzee aliongea kwa taabu, kisha akabaki akitweta. Halafu akashusha pumzi nzito, akameza funda kubwa la mate, na kabla hajaendelea akajaribu kuchungulia nje ya basi ambako tayari wasamaria wema walishaanza kuwasili eneo la tukio. Alipofuata uelekeo wa macho ya yule mzee, Suhail akaona kuwa baadhi ya waandishi wa habari pia walikuwa wamefika, wakionekana kuwahoji abiria walionusurika kule nje.Sasa mle ndani ya basi watu hai walibaki wao wawili tu, baada ya wenzao kutolewa nje.
“…Pesa zote hizo nakupa wewe, ni za kwako... lakini kwa sharti moja tu, ambalo si gumu sana. Unapaswa umuoe binti yangu na uishi naye kwa wema, amani na upendo. Ukawe mlinzi na kiongozi wake…Sitaki kamwe mwanagu aolewe na majini!”
Heeeh!
“Majini...?” Suhail alimaka kwa mshangao, na kabla hajajibiwa akaendelea,“ ...ki…kivipi mzee? Mbona sikuelewi? Kwani wewe ni nani hasa?”
“Mimi naitwa Mzee Shamhurish.Fanya hima umpate mwanangu!, Anaishi Bagamoyo…anaitwa Shekhia!”
“Whaat? Nani?” Swali la hamaki kutoka kwa Suhail ni kama lilihitimisha safari ya mwisho ya Mzee Shamhurish duniani, mikono ya yule mzee ilianguka, macho yakajifumba nusu, pumzi zikakata, roho yake ikatengana na mwili.
“Nooo! Hupaswi kufa kwa sasa mzee! Amka! Amka, please unijibu japo kidogo tu aaaah! Nnoo!” Suhail alikuwa anauongelesha mwili wa Mzee Shamhurish kama mwendawazimu huku akimwagikwa machozi bila kujijua., Kilichomshtua kuliko vyote ni jina la Shekhia, jina ambalo alilijua na alimjua vema huyo msichana aliyeitwa Shekhia S. Sufian. Ni msichana mrembo aliyekutana naye huko chuoni alipokuwa anasoma. Wakafahamiana na kuwa marafiki. Mengi yakapitikana baina yao, na wakaishia kuwa maadui wakubwa.
Suhail alizidi kupagawa. Hakuwa na hamu tena na zile pesa alizokabidhiwa, na alipoiangalia ile pete ndiyo hofu ilipozidi kumvaa.
“Ni kweli Shekhia alipata kuniambia kuwa kwao ni Bagamoyo. Je ndiye yeye aliyekusudiwa na mzee huyu? Kama ndiye basi NIMEKWISHA!”
*****
Wakati ajali hiyo iliyowaangamaza abiria wengi ikitokea, upande wa Pili huko Tabora Mchumba wake na Suhail aitwae Sharifa alikuwa akiendelea na usafi wa nyumba huku mama yake akiwa jikoni akiungurumisha chakula, Sharifa alikuwa ni msichana mchapakazi sana licha ya kua ameajiriwa lakini siku za jumamosi na jumapili badala ya kupumzika tu yeye hupendelea kujishughulisha na majukumu ya pale nyumbani ili kuwasaidia wazazi wake hasa mama yake, lakini pia siku hiyo alikuwa na hamu kubwa na hamasa ya kufanya shughuli zote za nyumbani kutokana na furaha kubwa ya kumpokea mchumba wake ambaye hajaonana nae yapata mwaka mmoja tangu alipokwenda Dar kumtembelea, kama ungempasua Sharifa katikati ya moyo wake basi si ajabu ungekuta jina la Suhail limeandikwa kwa wino wa dhahabu kwa jinsi alivyompenda, aliona kama masaa hayaendi vile, alitamani muda ufike haraka akampokee kipenzi cha moyo wake..
.kama ungempasua Sharifa katikati ya moyo wake basi si ajabu ungekuta jina la Suhail limeandikwa kwa wino wa dhahabu kwa jinsi alivyompenda, aliona kama masaa hayaendi vile, alitamani muda ufike haraka akampokee kipenzi cha moyo wake..
Wakati Sharifa akiwa anaendelea kufagiafagia ‘seating room’ pale nyumbani kwao ndipo ghafla ladha ya furaha iliyotanabahi ndani ya moyo wake ilipogeuka shubiri baada ya kutupa macho katika kioo cha televisheni iliyokua ikiripoti tukio la ajali mbaya inayohusisha Lori na Basi la Nbs alilokua amepanda mchumba wake. Aliisogelea kwa kasi Tv kama vile alievutwa na sumaku, kisha macho na masiko yake vikashirikiana kupata habari ile mbaya
“…AJALI HIYO MBAYA INAYOHUSISHA LORI LILILOKUA LIMEBEBA MAGOGO NA BASI LA NBS CLASSIC LILILOKUA NA ABIRIA YAMEGONGANA USO KWA USO KATIKA KONA YA MLIMA KISERA NJE KIDOGO YA MJI WA DODOMA NA KUSABABISHA VIFO VINGI NA MAJERUHI, UOKOZI UNAENDELEA ENEO HILO BAADA YA WASAMARIA WEMA KUWASILI…”
Wakati taarifa hiyo ikiendelea kusomwa Macho ya Sharifa yalikuwa yakiwaangalia baadhi ya majeruhi waliokuwa wakihojiwa lakini hakupata kumuona Suhail, alituliza macho yake katika kioo cha luninga yao lakini hakumuona kamwe ndipo uzalendo ukamshinda ukaangua kilio cha hali ya juu, ndipo sauti yake ikavuma mpaka jikoni alipokuwa ameketi mama yake, masikini ya Mungu Bi mkubwa Yule akautupa mwiko wa mboga na kutoka mbio kuelekea kule sebuleni ilipokua ikitokea sauti ya Sharifa
Hakika Mama huyu alimpenda sana binti yake, alimpenda kama binti yake wa kumzaa mwenyewe mpaka majirani wote walikuwa wakijua kua ni mwanae wa kuzaana pia humuita ‘Mama Sharifa’, lakini ukweli wa mambo ni kwamba Sharifa hakuwa mtoto wa kuzaliwa na Bi mkubwa Yule kwani Wakati mama huyu naolewa na Mzee Fungameza alimkuta Sharifa akiwa ameshazaliwa japo alikuwa ni mdogo sana, mtoto wa miaka kama minne tu hivi hivyo akamlea mwenyewe tangu hapo mpaka nae akajaaliwa kupata mtoto wake aitwae Florida
Malezi hayakua magumu kwa Bi mkubwa huyu dhidi ya Sharifa isipokua sehemu moja tu, Sharifa tangu akiwa na umri huo mdogo aling’ang’ania kufuata dini ya mama yake mzazi ambaye alikuwa ni muislamu, japokuwa mama yake huyo alitoweka katika mazingira anayoyajua Mzee Fungameza peke yake, hivyo japo Mzee Fungameza alikuwa ni Mkristo tena ni mzee wa kanisa alijikuta akilazimika kumuacha mtoto huyo afuate dini ya mama yake.
Baada ya mama Sharifa kuwasili sebuleni pale alikuta taarifa ile kwenye Tv ikimalizikia wakati huo Sharifa akigaagaa kwa kilio pale sakafuni
“We mtoto una nini lakini?”
“Mamaa! Mamaa! Uwiiii Suhail jamani mama,” Sharifa alikuwa akilia kwa kuomboleza kiasi cha kumtia hofu zaidi mama yake
“Suhail amefanyaje sasa?”
“Amepata ajali na itakua amekufa tu” Sharifa alikuwa akilia kwa uchungu sana. Wakati huo mama yake nae alikuwa kama amepigwa ‘shoti’ ya umeme kusikia habari hizo maana nae alikuwa akijua kua Suhail yuko safarani akielekea huko Tabora na hapakuwa na siri yoyote kua watoto wao walikuwa ni wachumba
“We nani amekuambia habari hizi?” Sharifa hakumjibu mama yake bali alimuashiria kwa kidole chake kua ameona kwenye Tv, haraka mama Yule akaiangalia Tv ambayo ilikuwa ikionesha kipindi cha maisha ya wanyama, Alikwishai chelewa habari ile, akajaribu kushika ‘remote’ na kubadili ‘channel’ kadhaa kama angeweza kuiona habari hiyo lakini haikuwa hivyo ikabidi tu sasa mama Yule ajikaze ili apate nguvu ya kumbembeleza binti yake
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi