Vita vya Mapenzi (34)

0

SEHEMU YA THELATHINI NA NNE
TULIPOISHIA...
“Nilikuwa nina shida na huyo Afande,” Alijibu kwa upole na nidhamu yule Msichana/Takadir

“Hakuna mtu uliyemuona akitoka humu ndani sasa hivi?” Koplo Salum alimtupia swali Dada Yule

KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO

SASA TUENDELEE...
“Hapana, sijamwona mtu yoyote.. kwani kuna nini Afande?” Takadir alijiulizisha huku akitupa macho yake katika mkono wa Insp Kenjah bila kuiona Pete aliyoikusudia.. japo ni kweli hakumwona mtu yoyote akitoka mle Ofisini ila akahisi kua kuna jambo zito maana ghafla ile miale ya Pete hakuiona tena.. akatumia uwezo wake wa kijini lakini hakuambulia chochote..

Wale maaskari wakaenda mpaka upande wa pili wa ile Korido inayokwenda mpaka katika ofisi ile waliyokuwemo wakawakuta akina Mama wawili wameketi pamoja katika Benchi

“..Eti huyu kijana aliyetoka kule ofisini amepita hapa?” Leonard Kenjah aliwauliza kwa wahka akina mama wale

“Kijana gani?.. hakuna kijana aliyepita hapa”

“Ninyi mnafanya nini hapa?”

“Hao ni wake zetu baba..” Sauti ilijitokeza nyuma ya Inspekta, ilikua ni sauti ya Mzee Fungameza

“Anhaa kumbe mnafahamiana, Hapa kuna mchezo mmetuchezea.. haiwezekani mtu ametoka sasa hivi na ninyi mpo hapahapa halafu mseme hamjamwona.. mnaficha ukweli eeh?” alibwata Kenjah huku akiwa amewatolea macho wazee wale

“Hakuna lolote tuliloliona hapa baba yangu..”

“Hakuna kitu kama hicho.. naomba nyote mtulie hapohapo, asiondoke mtu” Insp alitoa amri ile kisha akaanza kuelekea kule Kaunta, akakutana na Koplo Marando nae akitokea kulekule

“Vipi huko?”

“Nao wanadai hawajamwona mtu yoyote kule, itakua amejificha hukuhuku” wakarudi masikini ya Mungu vijana wale maofisa wa Jeshi la Polisi mpaka kule walipokua mwanzo, wakapekua kila kona bila mafanikio.

Wakarejea walipowaacha wale wazee wakawakuta wote wakiwa palepale isipokuwa mtu mmoja tu, yule dada wa kiarabu aliejitanda mtandio, Naye alitoweka katika mazingira ambayo hakuna jicho lililomdiriki

“Yule dada wa Kiarabu yuko wapi?” Inpekta Kenjah aliuliza huku akiwatazama kwa ghadhabu akina Mzee Fungameza na wake zao

“Dada wa kiarabu Yupi tena huyo?”

“Nyie ,mnataka kutuchezea akili sio? Kila mtu mnajifanya hamjamwona eeh?”

“Jamani hakuna mtu tuliyemwona sisi,, kwanza wakati ninyi mnatoka mle ofisini sisi tulikuwa wa mwisho kutoka.. na tulipotoka tukaja moja kwa moja mpaka pale mlipokua mkiwahoji hao mama zenu sasa huyo mwarabu sisi tumemwonea wapi jamani?”

Ilikua ni kizaazaa, Wakiwa bado katika hali ile ya Sintofahamu mara ghafla simu ya Inpektah Kenjah ikaita, alipoangalia simu yake ilikuwa ni namba ya Inpekta Jenerali wa Polisi, IGP Cathbet Charles Suca. akaonesha kwa kidole ishara ya kuwataka wawe watulivu wakati akipokea simu ile..

“Jambo Afande..” alianza Inp Kenjah

“Uko wapi Inpekta?” alisaili IGP

“Niko ofisini mkuu..”

“Wewe nd’o unayo kesi ya yule Mwandishi wa habari aliyeuliwa?”

“Ndiyo Mkuu”

“Nataka kukiona kichwa chako hapa ofisini kwangu sasa hivi” Kabla Kenjah hajajibu simu ilikuwa imeshakatwa.

Bila ya kupoteza muda Inpekta Kenjah akatoa maelekezo huku akiondoka “Koplo nimeitwa na mkuu.. IGP, Sasa hakuna cha ziada kwa sasa naomba uwaweke ‘lockup’ hao wazee wote mpaka nitakaporejea.. na wakiendelea kuleta ujanjaujanja wataozea jela mpka watakaposema Suhail ametorokea wapi pamoja na yule dada wa kiarabu..” Kusikia hivyo Mama Suhail akaanza kuangua kilio cha nguvu japo hakikusaidia kitu, masikini mama wa watu Polisi aliizowea kuisikia kwa jirani tu!

Inspekta Kenjah akaondoka akielekea kwa IGP huku Koplo Marando akiwasweka ndani akina Mzee Kusekwa na wake zao

*****

SHEKHIA Bint Sufian alisimama karibu kabisa na kitanda alicholazwa Sharifa, Dhamira yake ikiwa ni mbaya moyoni mwake. Macho ya Sharifa yalikuwa yakimtazama ila kwa ule muonekano tu alitambuwa kuwa dada Yule hakuja kwa wema kabisa, alitamani hata ainuke ili ajihami endapo litatokea la kutokea lakini hiyo ilikuwa ni ndoto ya mchana! viungo vyake vyote vya upande wa kulia vilishamsaliti kitambo,

Hakuweza kufanya lolote!

Shekhia alilitambua hilo hivyo hakujihangaisha kumfikiria mara mbili hasimu wake Yule aliye taaban kitandani, akanyanyua mkono wake akaupeleka mpaka kinywani kisha akaibusu Pete yake kwa sura iliyojaa hasira, kiburi na dharau. Usingeweza kulitoafautisha hilo busu lake na ‘Msonyo’ tu kutoka kwa shetani mwingine yeyote.

Kilichokua kikifuatia ni kumaliza N’gwe ya mwisho kwa kutoa Pigo takatifu, lakini akawa anasita, nafsi ikawa inamsuta, alijisikia vibaya sana kutekeleza jambo lile baya kabisa, Kumwua mtu asiye na hatia.. akajikuta anatiririsha machozi ya uchungu mashavuni mwake bila ya kujitambua.

Hali ile ikawa inazidi kumshangaza Sharifa, hakujua ni kipi kinachomliza Mwanadada yule aliesimama kisharishari mbele yake

“Pole sana Sharifa.. Sio kosa lako,” hatimae Alisema Shekhia huku akifuta machozi yake kabla ya kuugeukia mlango na kuanza kutoka mle Wodini akiwa hajatekeleza azma yake,

Alipofika Mlangoni kabla hajatoka nje ya Wodi ile akageuka tena na kumuangalia Sharifa akiwa kule kitandani amelala vilevile, akamuangalia tena kwa Uchungu, hasira na huruma kwa wakati mmoja mpaka yeye mwenyewe akawa anajishangaa.. akafikiri mara kadhaa kisha akaamua kumrudia tena mpaka pale kitandani..

Safari hii akiwa na dhamira ngumu!

Alipofika hakutaka kupoteza tena muda, alimuangalia kwa mara ya mwisho kabla hajazungusha Kito cha Pete yake iliyokua kidoleni.. alipokibenjua tu ‘kito’ kile cha Pete ikatoka miale hafifu ya rangi ya kijani, akaielekezea kwa Sharifa kwa sekunde kadhaa kasha alipoona amefanya alichotaka akaondoka harakaharaka na kutoka kabisa Wodini..

Alipofika nje ya Wodi ile akakata kona ya kushoto na kutokomea.. Wakati huohuo Kona ya kulia Suhail nd’o alikuwa akiingia hospitalini hapo baada ya kuletwa kwa kasi ya Upepo kutokea kule Polisi mpaka pale Hospitalini baada ya kuiamuru Pete(Khatam Budha) kufanya vile huku kukiwa hakuna hata mmoja aliemuona.. ilikua ni mchezo wa kawaida sana kutoka katika Pete ile

Alipofika tu akapitiliza mpaka Wodini bila hata ya kuanzia kwa Dokta kupata maelekezo, kwa kuwa alikwishaifahamu Wodi aliyomo mkewe hivyo hilo halikua tatizo kwake..

Hakuamini alichokiona baada ya kuingia mle Wodini, Hofu ilimvaa, woga ukamkumba akahisi kama anayeota vile. Mapigo ya moyo yakaongeza ‘Mdundo’

Akiwa amesimama mlangoni huku amepigwa bumbuwazi macho yake yalikuwa yakimtazama Sharifa aliyekuwa amesimama jirani ya kitanda chake! kilichomstaajabisha zaidi si kumuona mkewe bali kumkuta akiwa katika hali ile, akiwa amesimama huku akionesha kua haumwi chochote kile.. Laiti kama Isingekua uwezo wa Pete yake ile iliyokuwa ikimuonesha hali ya mkewe huyo kabla hajawasili pale Hospitalini basi asingeamini kama alikuwa mahututi muda mfupi uliopita.. alitaraji kukutana na mzoga tu hasa alipomuona Shekhia akiwa mle Wodini akionesha kila dalili ya Nia ovu

Sharifa nae kwa upande wake alikua akistaajabu juu ya tukio lililomtokea baada ya yule Mwanadada kummulika kwa Mwanga wa kijani kutokea katika Pete yake na hapohapo akashangaa amepona kabisa, viungo vyake vyote vikarejewa na uhai uliotoweka.. kila mara alijaribu kujikagua na kugundua kuwa alikuwa amepona kabisa, Bukheri wa A’fya!

Alichokifanya Shekhia ilikuwa ni kitu kidogo tu, Kubadili maamuzi ya kudhuru na kuamua kumponya mwenzie baada ya kuingiwa na huruma ambayo hata yeye mwenyewe hakujuwa imetokea wapi.

Suhail akamkimbilia mkewe na kumkumbatia kwa Nguvu akiwa haamini kabisa kama amemkuta mkewe huyo akiwa salama, wakati huo Sharifa alikua akitokwa na machozi ya furaha yaliyochanganyika na hofu..

“Mke wangu..”

“Mume wangu..”

“Mbona sielewi?”

“Hata mimi sielewi mume wangu.. najishangaa tu”

Wakakumbatiana tena kwa nguvu kisha wakasogea pale kitandani na kuketi, ndipo sasa Sharifa akaanza kumsimulia Suhail tukio zima lilivyokua kuanzia alipowasili yule dada mpaka alipotoa mwanga wa ajabu katika Pete yake na jinsi alivyojishangaa kupata nguvu na kuinuka pale kitandani.. ilikuwa ni stori ya aina yake kwa wote kati yao kila mmoja kwa namna yake. Suhail hakuamini kabisa na wala hakutaka kuamini kua Shekhia amemwacha Sharifa bila ya madhara yoyote.. Sharifa naye alijawa na kiu ya kumjua mtu Yule lakini hakupata nafasi hiyo tena

“Kwahiyo unasema haukumjua kabisa mwanamke huyo wala haukupata kumwona mahala popote?,” Suhail alimuuliza Sharifa huku akimshikashika nywele zake kwa kumliwaza na kumfariji

“Nakwambia sijawahi kumuona kamwe.. na sijui tu kuna nini kinachoendelea”

“Ukimuona tena unaweza kumtambua?”

“Bila shaka.. maana nimemuangalia kwa muda mrefu sana akiwa mbele yangu”

Wakaongea mengi sana mtu na mumewe mpaka wakaafikiana kua wamwite daktari aje ajionee hali ile ili ikiwezekana waondoke zao.. Madaktari nao hali ile ya mshangao ikawakumba, hawakuamini kuwa Msichana Yule amepona ghafla na kimiujiza, wakaanza kuitana wote na kumfanya Sharifa kuwa ni kivutio cha kitalii kwa macho na Bongo zao..

Japo madaktari walijiridhisha kuwa Sharifa amepona lakini walikataa kumpa ruhusa kwa haraka namna ile, wakamsihi Suhail amwache mkewe huyo aendelee kuwa katika uangalizi wao mpaka kesho yake ndipo wangemruhusu kwa kuwa hali ile hua inaweza kujirudia ghafla.. Suhail na mkewe wakakubali kwa Tabu! Baada ya hapo sasa Suhail akaondoka Wodini hapo akimwambia mkewe kua angerejea baadaye kidogo. Sharifa hakuwa akijua lolote kuhusu kesi ya mauaji inayomuhusisha mumewe kwa kuwa hakuambiwa chochote kutokana na hali yake ya kiafya kua mbaya sana hivyo alikubali na kumwacha mumewe akiondoka

*****

Ndani ya Ofisi ya IGP Suca utulivu ulitawala, Kelele pekee zilizokuwa zikisikika ni za Feni tu iliyokuwa ikizunguka taratibu! Tayari Inpekta Kenjah alikuwa ameshawasili na kumkuta IGP ambaye baada ya Salamu zao za kijeshi walianza mazungumzo ambapo IGP alimtaka kwanza Leonard Kenjah kumpa taarifa nzima ya mwenendo kesi ile anayoipeleleza;

Kenjah alieleza kwa kirefu na kwa ufasaha wa hali ya juu kwa kadri anavyoielewa kesi ile mpaka hisia zake juu ya baadhi ya maofisa wa jeshi la Polisi

“Sasa nisikilize kijana wangu,” Aliongea IGP kwa utulivu sana baada ya Kenjah kumaliza kuwasilisha.. Akaitengeneza vizuri miwani yake usoni kisha akaendelea “..Kwanza hongera kwa hatua nzuri uliyofikia na moyo wako wa kujituma katika kulilinda taifa lako ila ujue kuwa hiyo kesi ni ngumu sana, ngumu kuliko ugumu wenyewe! Ngumu kuliko mnavyoichukulia! ninyi mnadhani mnapeleleza kwa Siri kumbe kuna watu wako Pembeni wanawafuatilia kwa kila nukta bila ya ninyi kugundua..

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)