Vita vya Mapenzi (35)

0

SEHEMU YA THELATHINI NA TANO
TULIPOISHIA...
“..Kwanza hongera kwa hatua nzuri uliyofikia na moyo wako wa kujituma katika kulilinda taifa lako ila ujue kuwa hiyo kesi ni ngumu sana, ngumu kuliko ugumu wenyewe! Ngumu kuliko mnavyoichukulia! ninyi mnadhani mnapeleleza kwa Siri kumbe kuna watu wako Pembeni wanawafuatilia kwa kila nukta bila ya ninyi kugundua..

KAMA UNASOMA SIMULIZI HII NJE YA APPLICATION YA CnZ Media INSTALL ILI USIPITWE NA MIENDELEZO

SASA TUENDELEE...
Msipokua makini mtajikuta mnavikwa taji la miba badala ya lile la maua..” IGP akatulia kidogo na kuendelea “Kuna vita ya kisiasa inaendelea Nchini kwetu, kambi kadhaa za wasaka uraisi zimeshajidhihirishwa waziwazi huku kila kambi ikiwa imejipanga vilivyo ima kwa kuuwa ama kuteketeza.. Kifo cha yule mwandishi wa habari ni matokeo ya minyukano hiyo baada ya Mwandishi huyo kukwaruzana na hao wenzie na kuamuwa kutoa siri zao.. Najua utajiuliza maswali mengi sana lakini nitakuelewesha yaliyo muhimu tu kwako kwa sasa” IGP Alituliza macho yake yaliyokua yamejificha ndani ya miwani yake kabla ya kuendelea tena

“..Kuna kesi kadhaa kuhusu mchezo wanaofanyiwa baadhi ya watu kupitia simu zao, wanaonekana kutuma meseji kwa jamaa zao huku ukweli wakiwa hawajatuma wao.. Ndoa zimevunjika kwa mchezo huo, watu wameuawa na wengine kufungwa kwa ushahidi wa Meseji ambazo hawakuziandika, sasa hiyo ni moja ya kazi za moja ya kambi kubwa ya wasaka uraisi iitwayo ‘Black Scopion’ Hawa huzitengeneza meseji hizi kwa hila za kimtandao kupitia katika mtambo wao maalum uitwao ‘DIVIER’ na kisha kuzituma kwa mtu wamtakaye lakini huko watakapozituma wanaamua wao zioneshe zimetoka kwa nani.. bila shaka umepata kusikia hiyo kesi!!”

“Naam,” alijibu Kenjah huku akitikisa kichwa chake chini juu kuashiria kuafikiana na hicho anachoelezwa

“..Sasa basi hicho ndicho kinachofanywa halafu huyo Mwandishi aliyeuawa akawa anatumika kuwachafua baadhi ya viongozi huku akijivunia meseji hizo za kisanii kama ushahidi endapo atakaemchafua atahitaji kwenda Mahakamani.. na watu wengi walikua wakiogopa kumshitaki kwakuwa walijuwa kuwa kuna meseji zao zimekua zikionekana katika simu za watu wao ijapokuwa hawakuzituma wao.. Kambi hiyo ya Black Scopion inayojihusisha na Mchezo huo mchafu inaongozwa na Joram Ndege ambae anajipambanua kua ni raia wa Kenya huku ukweli wa mambo yeye ni Raia wa Uganda..

Sasa kilichotokea ni kwamba kwakua huyo Msigwa alikuwa akiwatumikia vilivyo hao Black Scopion ikafika siku naye aliwataka wamsaidie kutuma meseji hizo kwenye simu ya mkewe huku zikionesha kua zimetoka kwa Yule kijana waliemsingizia kua ana mahusiano nae, Lengo likiwa ni kutafuta sababu ya kuachana na mkewe huyo kwakuwa inasemekana hazai.. na muda huo akawa ana mpango wa kumuoa mfanyakazi mwenzie aitwae Lilian ambae pia ni ‘Secretary’ wa Boss wake japo alikuwa akikumbana na upinzani mkali kwa mfanyakazi mwenzie aliyesemekana kua naye alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na huyo Lilian..”

Insp Kenjah alikuwa ametulia kwa umakini mkubwa akisikiliza kesi ile ngumu kuliko.. alijilaumu kujitwisha mzigo wa kesi ile lakini hakua na jinsi ya kujitua tena..

“..Alifanikwa zoezi lile marehemu Msigwa japo walikosea kidogo katika utekelezaji ambapo walituma meseji zile huku simu ya Yule mkewe ikiwa Morogoro, aliisahau kwa kaka yake alipokwenda kumjulia hali.. na hapo ndipo tuliposhangaa na kuanza upelelezi wa kina ambapo tukabaini mambo mengi sana. nakushirikisha haya ukiwa ni mtumishi muaminifu” IGP alikuwa akiongea kwa umakini sana kama ilivyo kawaida yake huku Kenjah naye akimsikiliza kwa umakini vilevile

“Mgogoro kati ya Msigwa na hao Black Scopion uliibuka baada ya Msigwa kutaka tena kutumia mtambo wa Divier kutuma meseji za uchonganishi kwenye namba za mke na wazazi wa huyo mfanyabiashara mnaemshikilia.. anaitwa nani vile?”

“Suhail Kusekwa”

“..Yeah, huyohuyo.. nasikia walikuwa ni marafiki wakubwa sana kabla ya kukwazana na kua maadui huku sababu za kimapenzi zikionekana dhahiri.. Sasa Joram Ndege akamkataza Msigwa kuutumia mtambo ule kwa migogoro yake binafsi.. Msigwa akachukia kukatazwa japokuwa anajua kabisa kuwa Mtambo ule ni kwa kazi maalum tu!

Hapo sasa nd’o akatishia sasa kutoa siri, ikabidi wamtulize kwa kumkubalia Ombi lake hilo huku nao wakimtaka atekeleze moja ya mpango wao wa kumchafua mmoja wa mahasimu wao kisiasa. Kilichotokea Msigwa akamchafua huyo Suhail kabla ya kumchafua mtu aliye elekezwa, matokeo yake akafukuzwa kazi hivyo kushindwa kutekeleza makubaliana yao akiwa pale Gazetini.. sasa hakuwa na sababu tena ya kuendelea kuishi kwa usalama wa kambi ya ‘Black Scopion’ ndipo ukapangwa mpango kabambe wa mummaliza na ilikusudiwa ifanyike katika mazingira ambayo atakuwepo yeye na Suhail ili kesi iwe ya Suhail huku wao wapate kujifichia katika hicho’kichaka’..”

IGP akavua miwani yake na kuiweka juu ya meza, akapikicha macho yake halafu akaifumbata mikono yake kifuani, akawa anajizungusha katika kiti chake huku akimuangalia usoni Inspekta Kenjah kwa utulivu

“Nakuelewa Afande,” Kenjah alijibu kabla hajaulizwa kitu, alijishitukia kuona amekaa kimya muda mrefu bila ya kuchangialolote

“Nataka unielewe kweli si maskhara.. Mtambo huo wa Divier mbali ya kubumba meseji hizo haram pia unaweza kunyaka mawasiliano ya simu hizi za kawaida.. na ndio maana hata upelelezi wako wote unaojidanganya kuwa ni wa siri wenzio wanaoupata kwa kila hatua.. hivyo kuanzia sasa nitakupa simu tatu zenye namba maalum ambazo utazitumia wewe na vijana wawili tu katika kuwasiliana muda wote wa kuipeleleza kesi hii! kila hatua utakuwa ukiwasiliana na mimi kwa namba yangu ya siri kama hiyo nitakayokupa.. haupaswi kumpa mtu yoyote namba hizo..

Mpelelezi wetu aliyezikusanya habari zote hizi amemaliza kazi yake mpaka hapo alipofikia, mazingira hayamruhusu tena kuipeleleza kesi hii hivyo sasa Joho hilo unalivaa wewe.. tunahitaji kujua ni wapi ulipo huo mtambo wao wa Divier, tunahitaji kujua ni Mwanasiasa yupi aliewaleta na kuwafadhili wauaji na wadanganyifu wote walio ndani ya Kambi hiyo inayojiita Black Scopion maana mpaka sasa hatujajua ni kambi ipi kati ya hawa Wasaka uraisi inayohusika moja kwa moja, tunahitaki kumkamata Joram Ndege akiwa hai au ikibidi akiwa maiti kabla hajaendelea kuteketeza Raia wetu, tunahitaji kujua Yule Binti aliyetekwa..Lillian amepelekwa wapi?

Pia hakikisha Yule kijana Mhariri aliepigwa Risasi anakuwa salama ili huenda akatusaidia upelelezi wetu kwa namna moja ama nyingine maana bila shaka sasa hivi wanamwinda wammalizie.. na kuhusu huyo Suhail hatuna umuhimu nae sana japo si vibaya kama utaendelea kumchunguza kujua alikuwa akigombea nini hasa na Msigwa mpaka akatuma zile meseji kwa watu wake..” Baada ya hapo IGP akavuta droo ya meza yake, akatoa Simu tatu na kuzikabidhi kwa Inspekta Kenjah

“Moja ya kwako, hizo mbili za utakaoshirikiana nao.. Je utahitaji nikupatie na utakaokuwa ukitumia nao hizo simu”

“Ninae mmoja Afande, anafaa sana, Ni Koplo Malando.. nitaomba mmoja unipatie wewe,” Aliongea kwa Kujiamini Insp Kenjah huku lengo lake likiwa lina maana kubwa kwamba ni lazima mpelelezi mmoja atoke kwa IGP kwakuwa ni lazima atakuwa na uwelewa mkubwa wa kesi hii hivyo kumrahisishia yeye kupata ‘Data’ zote lakini pia alichokuwa amekilengea ni endapo Mpango uta’fail’ basi n huyo mmoja ambaye ni chaguo la IGP naye atakuwemo hivyo kuzidhibiti hasira za Bosi wao huyo. IGP hakubisha, akakubali ombi lile na kumtoa mmoja wa Wapelelezi waliopo pale Ofisini kwake ili kushirikiana na akina Kenja katika sarakasi zile walizokua wakizianza, aliitwa Sajenti Malumbo.

*****

Suhail alipotoka pale Hospitalini akaamua sasa kurejea kituoni ambako kupitia Pete yake aliwaona wazazi wake wakiwa ‘Nyuma ya Nondo’

Akaondoka kwa kasi ileile ya ajabu mpaka Kituoni Kijitonyama, Alipofika akaingilia kwa nyuma ya Jengo lile la Polisi, akakata kona ya kulia na kutokezea mbele ya Kaunta ya kituo hicho.. hakutaka kushangaa akihofia kuonekana kabla yeye mwenyewe hajajikabidhi, akaenda mpaka ndani ambapo akapitiliza mpaka kule zilipo ofisi za wapelelezi, akagonga mlango kisha baada ya sekunde kadhaa akasikia sauti ikimtaka aingie ndani.. alipoingia tu akakutana uso kwa uso na Koplo Salum ambaye alishituka mithili ya aliyeona mzimu lakini akajikaza kiaskari

“Suhail..” aliita kwa wahka Koplo Malando

“Yes Afande”

“Ulikua wapi muda wote.. tangu ulipotoka?”

“Nilikua hapo nje Afande.. Si niliwaomba jamani mningojee kidogo? Au mlidhani nitakimbia? Siwezi kufanya hivyo”

Hali ile ilimshangaza sana Koplo Malando, ikabidi ampigie simu Insp Kenjah kumpasha habari ile, naye Inspekta hakuamini ila kwakuwa alikuwa njiani akielekea kituoni hapo akatuliza munkari na kukaza mwendo.

Dakika Ishirini baadae ndani ya Chumba cha upelelezi walikuwamo Inpekta Kenjah, Koplo Marando na Suhail mwenyewe! mjadala ulikua mkubwa sana kuhusu mahala alikokuwa Suhail, maelezo ya Suhail hayakuwaingia akilini kabisa kuwa alitoka nje kabisa ya jengo lile,

Alipoulizwa kama alionana na wale akina mama waliokua wameketi pale nje ya Ofisi ambao ni wazazi wake alikiri kuwaona lakini alidai aliwapita wakiwa wamejiinamia hivyo hawakumtambua,

Alipohojiwa juu ya kilichomtoa nje kwa haraka kiasi vile, hata yeye mwenyewe hakukitambua! labda ni majini au mashetani yalimpanda kichwani.. hilo ndilo liliku jibu lake!

Kwa Insp Kenjah hiyo haikuwa kesi sana, akamuamuru Koplo Marando awatoe wale wazee waliokuwa wakimshikia nafasi Suhail ili sasa mwenye nafasi arejeshwe ndani.. Japo kichwani mwa Insp Kenjah Suhail hakuwemo tena kwa maana ya kumuhusisha moja kwa moja na kadhia ile ya mauaji kutokana na maelezo aliyoyapata kwa IGP, na kutokana na hata Suhail mwenyewe anavyoonekana kujiamini na kujipambanua kutokuhusika kwake na Kesi ile.. alishaanza kufikiria hata kumpa dhamana lakini hakuona haja ya kumwacha harakaharaka

Wazee wakatolewa kisha Suhail akarejeshwa ndani!

Ilikuwa ni hali ya Sintofahamu inayoendelea kuwakumba wazee wale, walizidi tu kuchanganyikiwa maana kila muda matukio ya ajabu yalikuwa yanawadhihirikia. Kuanzia kuhusishwa na mauji kwa kijana wao Suhail, Kuugua kwa Sharifa, mara taarifa za kua Suhail ana mke mwingine tofauti na Sharifa, mara kutoroka na kurejea kwa Suhail pale kituoni.. hakika walilewa bila ya kunywa

Wakaondoka wazee watu, safari hii hawakutaka hata kukumbushia vile vitu ambavyo Suhail mwanzo aliwataka waende navyo nyumbani.. vitu vile pamoja na Pete(Khatam Budha) viliendelea kubaki palepale kituoni.

Bahati nzuri Kilingo nae alikuwa amewasili tena kituoni baada ya kuondoka na gari muda mrefu uliopita, aliyelekea Ofisini kwao alikohitajika kwa dharura punde baada ya kufukuzwa na Insp Kenjah, akawachukua wazee na kuianza tena safari ya kurejea Hospitalini kumwangalia Mgonjwa wao waliemuacha akiwa kitandani

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendeleza Simulizi

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)