THE NIGHTMARE (3)

0

SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA...
Akiwa hewani akikata mawingu kurudi Tanzania, kichwa chake kilikua na mawazo mengi sana juu ya mume wake. Aliikumbuka siku waliyofunga ndoa.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
Pia alijua kwanini mume wake alipendelea kufanya kazi uingereza na yeye kumfungulia ofisi huku huku Tanzania. Hakujua kuwa kazi anayoifanya mumewe ni ile ya kutembea na tajiri mkubwa uingereza. Alijuta kumfahamu kwa kile alichokiona kule Uingereza.

Alitua katika uwanja wa mwalimu nyerere salama usalimini na kupokewa na wafanyakazi wake. Wakati anasalimiana nao, kwa mbali alimuona Khalidi akija na ua. Walisalimiana na wote kwa pamoja wakamsindikiza Sabra nyumbani kwake kupumzika.

Baada ya maongezi ya hapa na pale, waliaga na wote wakaondoka na kumuacha Sabra akiwa na Khalidi.

“niambie, maana ulivyokua unaniaga ulikua na preasure kweli, kwema huko ulipokwenda?” aliuliza khalidi na kumuangalia Sabra usoni ambaye alijawa na huzuni.

“sio kwema Khalidi, hivi unajua kuwa tunaishi lakini dunia imeisha?” aliongea Sabra na kumuangalia Khalidi aliyekuwa makini kumsikiliza.

“nafahamu, maana matendo tutendayo binaadamu tunawashinda hata wanyama walionyimwa akili thabiti kama zetu.” Aliongea Khalidi na kumpa Sabra ufunguo wa kuendelea kuelezea aliichokua akikimaanisha.

“ile siku niliyokusababishia matatizo baada ya kuzimia, ndio siku niliyopewa taarifa zilizoushtua moyo wangu. Niliambiwa na mtu niliyekuwa sijamfahamu kipindi kile kuwa mume wangu ni shoga na muda si mrefu anaolewa kabisa na tajiri mkubwa huku Uingereza. Hiyo ndio sababu iliyonifanya niende kuhakikisha kama lisemwalo lipo!” aliongea kwa huzuni Sabra na kuendelea kushangaa jambo hilo kutokea kwa mtu aliyemuamini na kumpa dhamana ya mwili wake.

“he??.. sasa imekuaje ulivyokwenda??” alishangaa Khalidi mshangao mkuu.

“ umini usiamini, kwa macho yangu nimeshuhudia mumewangu anaolewa… sina hamu naye na najuta kumfahamu.” Aliongea na kuonyesha jinsi gani anavyomchukia kwa sasa.

Baada ya maongezi ya muda mrefu na kufarijiana, Khalidi aliaga na kuondoka zake.

Kesho yake akaingia ofisini na kufanya kazi kama kawaida. Wazo la kumpigia simu mume wake kuangalia kama atapokea au laa likamjia. Lakini aliambulia patupu. Hakuna hata line moja inayopatikana. Aliaachana nae na kuangalia mambo mengine.

Sekunde, dakika, saa, siku hatimaye ikapita miezi sita bila Sabra kupata mawasiliano na mumewe. Alichukia na kufunga safari hadi Uingereza kwa Samir na kumwambia amsaidie kufungua kesi na kudai talaka yake.

Mume wa Sabra alipigwa na butwaa baada ya kugundua mkewe amefahamu kila kitu kuhusu yeye. Hakua na jinsi, alifika mahakamani huku akiwa hana haya hata kkidogo juu ya mke wake aliyekua anamuangalia huku akimtahmini bila ya kupata majibu.

Zoezi la talaka lilifanikiwa bila Sabra kupata nafasi ya kukaa faragha na aliyekuwa mume wake. Hata yeye hakujali kwakua hakuwa mwanaume tena. Tayari alikua mke wa mtu.

Safari ya kurudi Tanzania ilikua ya furaha baada ya mahakama kumpa haki zote za huku Tanzania na kumpa faini mume wake ya malipo ambayo alipewa papo hapo kutokana na utajiri wa mume wake huyo wa zamani.

**********************************

Maisha ya upweke yalimchosha Sabra kutokana na mazoea ya kuishi na mwenza. Jambo hila lilimuumiza kichwa juu ya mtu wa kuwa nae kutokana na kutongozwa na watu wengi wenye hela zao na wenye nyadhifa mbali mbali za juu hapa Tanzania.

Mawazo yake ya kuishi Single yalianza kuyeyuka kwa sababu alikua anajisikia ashki kama binaadamu wengine.

Mara akajikuta anajishangaa mwenyewe baada moyo wake kuvutika taratibu kwa kijana masikini anayeishi kwa kutolewa na yeye mwenyewe. Hakujua kwa nini ila ukaribu wake na Khalidi ulikuwa unampa faraja sana.

Mara nyingine alipenda anavyoongea na mara nyingine Khalidi anapocheka huwa hoi bin taabani. Alikipenda kinywa cha Khalidi kilichokuwa kinatoa maneno yatiayo faraja na alama za ushindi kabla hata ya mapambano. Alipenda muonekano wa kipekee aliokuwa nao Khalidi hasa avaapo nguo alizozinunua yeye.

Alijitesa sana kwa mawazo juu ya mtu ambaye hata hakuonyesha dalili zozote kuwa na yeye alikua anamuhitaji. Wakati mwengine aliwaza labda Khalidi atakua anaogopa kumwambia kuwa anampenda kutokana na yeye kuwa tegemeo la maisha yake.

Wazo la kumpeleka nyumbani kwake na kumpa kazi ya usafi likamjia. Khalidi hakukataa kutokana na mpunga alioahidiwa kupewa mwisho wa kila mwezi. Mshahara wake ulimzidi hata mwalimu wa sekondari. Aliambiwa atalipwa shilingi laki sita na nusu na kila kitu ni juu ya Sabra. Kuanzia mavazi, chakula na kama ataumwa basi alikatiwa bima ya afya na bosi wake huyo mpya.

Khalidi alifanya kazi kuanzia asubuhi na kuondoka kwenda kwake usiku kila siku. Hata hivyo Sabra hakuridhika. Aliamua kumpa chumba mule ndani na wakaanza kuishi wote bosi na mfanya kazi wake.

Shoping za kufa mtu zilimfanya Khalidi ang`are kila sekta. Alianza gym kutengeneza mwili wa kuvalia vibody alivyonunuliwa. Alikata kitambi cha uzembe na kutengeneza six button. Alinyoa nywele zake na kuzipamba na duke na kuwa kama za kiarabu. Hakika Khalidi alianza kuwa na muonekana wa kistaa. Hata Sabra mwenyewe alipenda kuongozana nae japokuwa yeye ndiye anayemtia jeuri hiyo.

Mazoea yaliyopitiliza kati ya Khalidi na Sabra yakashika ujauzito na baadae kuzaa mapenzi.

Maufundi yasiyo na mfano ndio yaliyomfanya Sabra kumpeleka Khalidi kwa wazazi wake waishio Uingereza.

Maajabu yanaendelea kumtokea mtoto wa kitaa Khalidi na kuwa kati ya watu wanaotakiwa kuingia kwenye ndege. Hakuwahi hata kuota kama kuna siku atapanda ndege na kwenda hata Zanzibar tu. Lakini leo anagongewa visa inayomuwezesha kuhama si nchi tu, bali bara zima la afrika na kwenda Uingereza.

Alijihisi kama si yeye anayezikanyaga ngazi za ndege kubwa kama ile. Akiongozana na mpenzi wake huyo mwenye utajiri mkubwa, walienda kukaa kwenye siti zao na kusikiliza maelekezo.

Alibasamu wakati wote, hakusita kuipungia mkono ardhi ya Tanzania baada ndege kupaa kwa kasi. Alimuangalia mpenzi wake na wote wakatabamu.

Safari iliiva na kwa mara ya kwanza Khalidi anaikanyaga ardhi ya uingereza akiwa na Sabra. Walipokewa na wazazi wa Sabra na safari ikaanza kuelekea kwenye nyumba ya

mzee Bahaj.

Mazungumzo yalikuwa marefu kuanzia kumpa pole mtoto wao kwa kisanga kilichomkuta na kumpokea kwa mikono miwili mkwe wao mpya aliyetambulishwa na Sabra.

Sherehe kubwa iliandaliwa kwa matajiri hao na kuhudhuriwa na watu mbali mbali wenye nyadhifa zao huko uingereza. Khalidi alijiona kaibeba dunia nzima yeye na hakuna anayesikia raha kama yeye kwa kwa wakati ule.

Wiki mbili baadae walirudi Tanzania na Sabra akalisimamia swala zima la kumsomesha Khalidi lugha na computer.

Baada ya miezi sita , khalidi alihitimu vizuri na kuwa na uelewa wa kiingereza na computer vizuri. Hapo alipewa kitengo kimoja cha u-manager katika kampuni ya Sabra.

Baada ya kila mmoja kuridhia tabia ya mwenzake, walisafiri tena na kwenda uingereza ambapo waliwaeleza wazazi juu ya kuhitaji kuoana. Wazazi walitoa ruhusa na Khalidi na Sabra walifunga ndoa Tanzania kwa imani ya kiislamu.

Upendo wao ulikua mfano wa kuigwa kutokana na kutoathiri utendaji wa kazi na kufanya kampuni yao kukua kwa kasi na kufungua kampuni nyingine ambayo Khalidi aliiteuliwa kuwa msimamizi mkuu wa kampuni hiyo mpya.

Kila siku mapenzi yao yalizidi kupaa na mafanikio yao yalizidi kuongezeka na kuwa watu wenye fedha nyingi.

********************

Baada ya miaka mitatu waliamua kupata mtoto. Na mungu hakuwanyima, Sabra alishika ujauzito na kujifungua mtoto wa kiume. Walimpenda sana mtoto wao huyo waliyempa jina la Karim. Jina hilo ni la baba yake Khalidi ambaye alishatangulia mbele za haki.

Miaka ilizidi kukatika na kufikia hatua ya Karim kuanza shule. Hapo wakapata mtoto wa pili ambaye pia alikua wa kiume aliyeitwa Sharji, hilo ni jina la babu yake Sabra ambaye naye pia hakuwepo duniani.

Walimpeleka Karim shule kubwa nchini Kenya na alipomaliza elimu ya msingi walimuhamishia Uingereza kwa babu na bibi yake. Huko alisoma mpaka alipohitimu chuo kikuu na kurudi tena Tanzania na kuajiriwa katika kampuni ya ukandarasi wa barabara.

Wakati huo mdogo wake alikuwa anasoma kidato cha nne St.Marry hapa hapa nchini Tanzania kwakua hawakutaka kuwa mbali naye. Walipeda mtoto wao huyo kusoma hapa nchini kutokana na upweke watakaokuwa nao baada ya watoto wao wote watakaposoma nje ya nchi.

Kutokana na kupenda umwinyi, pia hela walizonazo wazazi wake, Karim hakutaka kabisa kufanya kazi. Aliridhika na hela alizonazo kwenye account yake alizokuwa akitumiwa mara kwa mara na wazazi wake ambazo hakuzigusa kipindi chote alichokua anasoma.

Utanashati wa Karimu na uzuri wa matamshi ya kiingereza, ulimfanya apendwa na madada wengi aliokutana nao club na kasino mbali mbali alizopendelea kwenda.

Tabia mbaya aliyokuwa nayo Karimu iliwaumiza wazazi wake kwa kuwa alikua akitumia hela nyingi kuliko kufanya kazi ambayo hataki hata kusikia hilo swala..

Kama wazazi walijitahidi kuchukua nafasi yao kumuelekeza Karimu jinsi maisha yalivyo na ugumu wa fedha katika utafutaji, lakini ilikua ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa. Hakuwasikiliza, zaidi kila watakapo iona sura yake asubuhi. Basi ni wazi alikua anataka pesa.

Kampuni zoa zikaanza kuyumba kutokana na mutumizi fedha bila mpamgilio maalumu. Hali hiyo iliwachosha wazazi wa Karim mpaka kufikia kujuta kuwa na mtoto wao hapa nchini.

“bosi mwanao ananisumbua, anasema nimpe laki tatu.” Aliongea muhasibu wa kampuni anayoisimamia Khalidi.

“mwambie aingie huku ofisini aonane na mimi.” Aliongea Khalidi kwa hasira.

Dakika moja badae aliingia Karimu akiwa amekunja uso.

“hivi ni mara ngapi nimekukataza kumsumbua huyu dada?” aligomba Khalidi.

“huyu usumbufu anataka mwenyewe, kama angekuwa anatoa hela ningemsumbua saa ngapi?” alijibu kijeuri Karim.

“kuanzia leo, hakuna hata shilingi mia tano utakayopata kutoka kwetu. Ukitaka hela nenda kafanye kazi. Na ukiendelea kumgasi mama yako basi utahama nyumba. Naona umeshakua sasa.” Aliongea Khalidi kwa Jazba.

“ sina shida na vijisenti vyenu… na kama kuhama katika kijumba chenu mimi nahama hata muda huu, usinizingue.’ Karim aliendelea kuleta jeuri mbele ya baba yake.

“unasemaje Karim?”

Aliongea Khalidi na kuufungua mkanda wa suruali yake na kuanza kumtandika Karim.

“unanipiga mimi?...utaona!”

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)