Mtunzi: Hussein O Molito
SEHEMU YA NNE
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Aliongea Khalidi na kuufungua mkanda wa suruali yake na kuanza kumtandika Karim.
“unanipiga mimi?...utaona!”
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
ENDELEA...
Aliongea Karim na kuondoka huku analia.
*****************************
Zilipita wiki mbili bila ya Karim kuonekana nyumbani kwao. Sabra alisikitika kidogo kutokana na kuwapenda sana watoto wake japokuwa huyo mtoto mkubwa hakuwa na adabu hata kidogo kwao.
Siku moja Khalidi akiwa katika gari yake akielekea kazini, ghafla kichwa kilianza kumuuma na macho yakaanza kumuuma. Akiwa katikati ya barabara, alijikuta akiyumba na kupata ajali mbaya baada ya gari yake kuacha njia na kupinduka.
Ambulance inafika eneo la tukia na kumchukua Khalidi akiwa katika hali mbaya kutokana na damu nyingi kumvuja.
Mbio za ambulance ziliishia katika hospitali ya ocean road. Watu wa emergency walijitahidi kumchukua haraka kwenye machela na kumuwahisha katika chumba cha wagonjwa mahututi.
Vituo mbali mbali vya televisheni na redio vilitangaza juu ya ajali mbaya iliyomtokea mfanya biashara mkubwa jijini Dar. Taarifa zilimfikia Sabra juu ajali ya mumewe na kuhabarishwa juu ya hali aliyokuwa nayo mume wake kwa muda ule na hospital aliyopelekwa katika jitihada za kuokoa maisha yake..
Alitoka bila kujitambua na kuingia kwenye gari yake na kwenda mbio hospitali ambayo mumewe amelazwa.
“ndio hivyo mama, huwwezi kuonana nae kwa hivi sasa kutokana na hali aliyokuwa nayo. Pia amepoteza kumbukumbu hivyo hawezi kumtambua mtu anayeingia wala anayetoka.”
Hayo yalikua maelekezo aliyoyatoa daktari aliyekua anamuhudumia Khalidi.
Siku zilizidi kusogea lakini hali ya Khalidi iliendelea kukatisha tama. Hakuweza hata kufumbua macho. Hata kuhema hakuweza hivyo alikua anapumulia gesi.
Sabra alidhoofu mwili kwakua hakua anakula wala kulala siku zote ambazo mume wake alikua kule hospitali. Hata watoto wake pia walipatwa na huzuni juu ya tukio lililomtokea baba yao.
“vipi daktari, mbona mgonjwa wangu mmemuhamisha?” aliuliza Sabra baada ya kufika hospitali na kukuta mgonjwa wake hayupo kwenye ward aliyolazwa mwanzo.
“pole sana dada, mgonjwa wako katutoka leo asubuhi.”
Yale maneno ya daktari yalisababisha mshtuko mkubwa kwa Sabra na kumfanya adondoke chini. Wakati Karim na Sharji wakiwa katika mshtuko baada ya kupewa taarifa na daktari juu ya kifo cha baba yao. Iliwabidi wajikaze kiume kwa kumfuata na kumnyanyua mama yao aliyeanguka baada ya kupewa taarifa juu ya kifo cha mume wake.
Walimpandisha kwenye kitanda kilichokuwa karibu na daktari akaanza kumpa huduma ya kwanza.
Watoto walishauriwa wasubiri nje ili waendelee kuangalia uhai wa mama yao kutokana na mapigo ya moyo wake kusimama. Walijitahidi kumuwekea life support machine ilimradi imsaidie kupumua lakini haikusaidia. Waliamua kuushtua moyo wa Sabra kwa kifaa maalumu lakini bado hali ilizidi kuwa mbaya kwa Sabra.
Baada ya nusu saa, daktari alitoka na kuwafanya wale watoto waliokuwa nje wakilia kwa uchungu juu ya kifo cha baba yao kumkimbilia huyo daktari ili awadodose chochote kuhusu mama yao.
“nyie si watoto wa kiume, mnatakiwa muwe na moyo wa kiume na kukubali kupokea taarifa zozote zikiwa mbaya au nzuri.” Daktari aliongea na kuwaangalia Karim na Sharji kwa zamu. Aliwasoma kwa umakini kisha akaendelea.
“najua ina wauma sana kuondokewa na baba yenu, ila hamna budi kukabiliana na mitihani ambayo mungu kawapa, …..nasikitia kuwaambia kuwa hata mama yenu nae hatunaye duniani.” Aliongea Daktari na kuwafanya wale watoto kuishiwa nguvu na kila mmoja kukaa upande wake na kuanza kulia kwa uchungu zaidi huku kila wakati wakitaja baba yangu mie na wakati mwengine wakitaja mama yangu mie..
***********************
Maisha ya upweke bila ya kuwa na wazazi wala walezi wa kuwasimamia yalianza muda mfupi tu baada ya mazishi ya wazazi wao. Karim alipewa majukumu yote ya kusimamia mali za wazazi wao kwakua Sharji alikua bado mwanafunzi.
Kampuni moja iliuzwa kutokana na kuwa na mnadeni mengi waliyokuwa wanadaiwa baada ya Karim kushindwa kuiendesha.
Sharji alipohitimu kidato cha nne, alinunuliwa gari na kaka yake kama zawadi ya kuondokana na maisha ya kuwa mtoto wa serikali na kuwa raia rasmi. Alipenda mdogo wake awe kijana anayeenda na wakati kama yeye. Hivyo alimpeleka club na sehemu mbalimbali za starehe kwakua alimuhesabia kuwa ameshakua
Mapenzi ya ghafla kati Karim na mdogo wake yalishika kasi kiasi cha kwamba walikua kama marafiki walioshibana. Hawakuwahi kugombana na kila mmoja alimfanya mwenzake kuwa msiri wake. Hata baada ya matokeo kutoka na Sharji kufanya vizuri kwa kupata Division II, lakini kaka yake alimkatalia swala la kuendelea na shule kwakua walikua na hela za kutosha za kutumia mpaka uzeeni.
Ta masha kubwa la mwanamuziki wa marekani Chris brown na Rihanna, ndilo liliwakosesha usingizi. Hawakutaka kulikosa hata kidogo.
Tarehe ya tamasha ilipokaribia. Walipanda ndege wawili hao na kwenda kwenye tamasha hilo lililomeza mashabiki wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Starehe juu ya starehe ndio zilikua ndoto zao kila walalapo. Hakuna walichokiwaza kwakua walitumiwa hela mara kwa mara na babu yao aliyekuwa makazi yake ni nchini Uingereza.
Pia kampuni yao ilikua inakua kutokana na misingi mizuri iliyowekwa na wazazi wao ambao kwa sasa walikua wameshatangulia mbele za haki.
Mahudhurio ya kazini kama Managing Director yalikua hafifu sana. Hata alipokua akionekana ofisini basi haikuchukua hata masaa mawili. Tayari alishaondoka. Hali hiyo ilifanya kampuni yao kupoteza sifa kama mwanzoni. Lkini hayo yote Karim hakujali kwakua alikua na wateja wengi ambao kuna wengine wanategea mikopo kutoka kwake.
Msemo wa tunakula ujana uliwakaa mdomoni kila watokeapo watu na kuwapa ushauri juu ya matumizi mabaya ya fedha waliyonayo..
Kila siku walibadilisha wasichana kama wabadilishavyo nguo. Hawakutongoza, ila pesa iliongea.
Hakika walikua zaidi ya masharobaro kutokana na kutopitwa na Fashion yoyote iingiayo mjini na wao kuwa watu wa mwanzoni kuzivaa.
Ukilinganisha na asili ya kishombe waliyorithi kutoka kwa mama yao ndio kabisa, walikua kivutio mpaka kwa watoto wa kizungu waliokutana nao katika hotel mbalimbali walizokuwa wanaenda.
“mdogo wangu nina bonge la Surprise.” Aliongea Karim baada ya kurudi tu kutoka ofisi kwake.
“ipi hiyo kaka.” Aliongea kwa shauku kubwa Sharji baada kusikia hayo. Maana alimjua kaka yake akiongea hayo ni lazima kuwe na kitu cha kumshangaza.
“najua kuwa hujawahi kusafiri kupitia majini, sasa wiki ijayo tutaenda visiwa vya Comoro kama picnic fulani hivi na washikaji kibao kupitia boti ya kukodi. Unaiyonaje hii?”
Aliongea Karim na kumuangalia Sharji ambaye muda huo tayari alijawa na furaha.
“ndio maana huwa sikupingi brother, napenda unavyonipenda na kila siku unavyonidhihirishia upendo wako juu yangu.”aliongea Sharji na kumfata kaka yake na kumkumbatia kwa furaha.
“usijali, we ungependelea tuondoke jumamosi au jumapili?” aliongea Karim na kumtazama mdogo wake kusubiri maamuzi atakayoyachukua.
“jumamosi itakuwa poa zidi.” Aliongea Sharji na kaka yake akatingisha kichwa chake kama ishara ya kukubaliana nae.
Baada ya hapo kila mmoja aliingia chumbani kwake na kujipumzisha. Kwani tayari ilishagota saa nne usiku.
Asubuhi kulipokucha, Karim alimuachia hela mdogo wake za kutosha kula hotelini cha na chakula cha mchana. Swala la kupika kwao lilikua swala gumu sana.
Karimu alifika ofisini kwake na kupokea nyaraka mbali mbali kutoka kwa secretary wake ambaye alikua kama msimamizi wa ile ofisi. Maana mambo mengi aliambiwa ayamalize yeye na kusababisha kupendwa sana na Karimu kwakua bosi wake alikua mvivu sana.
Siku zilisogea taratibu sana kwa Sharji kwa kua alikua na hamu sana ya kusafiri na boti kwakua ndio chombo pekee ambacho hajawahi kukipanda toka azaliwe.
Maandalizi yalizidi kupamba moto juu ya safari hiyo ya kwenda kustarehe kama camp kwenye visiwa hivyo vya Comoro. Kila kilichohitajika kilipatikana mapema. Walitenga bajeti kubwa itakayowawezesha kununua vitu watakavyotamani kununua wakiwa huko.
Waliingia dukani na kununua nguo mpya kadhaa kama kawaida yao na kuzipaki kwenye mabegi yao.
Pia hawakusahau kununua camera kwa ajili ya kurecord matukio mbali mbali watakayo yaona huko.
Mpaka kufikia siku ya alhamisi, tayari walishatimiza kila kitu. Kilichobaki ni siku husika kufika tayari kwa safari hiyo adhimu kwao.
Asubuhi ya siku ya ijumaa, Karim aliamka kama kawaida yake na kumuamsha mdogo wake na kumuachia kiasi cha fedha na yeye kuelekea kazini.
Sharji aliamka kivivu na kuchukua taulo lake na kuelekea bafuni. Alipomaliza kuoga na kupiga mswaki, alilipigilia pamba zake kati ya pamba anazozikubali zaidi na kuliendea geti la kutokea nje baada ya kujitazama kwenye kioo na kuridhika na alivyotokelezea.
Alipanda kwenye gari lake na safari ya kuelekea kwenye restaurant kwa ajili ya kupata kifungua kinywa ikaanza.
Akiwa njiani alianza kusikia harufu nzuri ya perfume ikitokea nyuma ya gari yake. Alipogeuka hakuona mtu yeyote aliyekuwa ndani ya gari zaidi ya yeye mwenyewe.
Alijinusa ili aangalie kwamba ni yeye ndiye anayenukia vile, lakini aliona ni kitu kisichowezekana maana harufu ya perfume yake anaijua.
Alichukua perfume ya kwenye gari lake na kujipulizia mkononi, aliponusa bado harufu hiyo ilikuwwa tofauti na anayoisikia. Alichoamua ni kufungua vioo na kuendelea na safari bila kujali chochote.
Alipofika maeneo ya best bite, alipaki gari yake na kuingia ndani. Aliagiza chakula na kutengenezewa oda yake, kisha akawasha mchuma na kurudi nyumbani.
Alipofika aliliendea friji na kuchukua kinyaji baridi akipendacho na kurudi sebuleni na kuanza kucheza game kwenye PS 3.
Kutokana na kupenda kucheza game, muda ulisogea mpaka kufikia saa tisa mchana. Njaa ilimuuma tena na kuamua kurudi tena best bite kupata chakula cha mchana.
Wakati oda yake ikiwa inatengenezwa, kwa mbaali akaanza kuisikia tena ile harufu ya perfume ikipuliza kutokea nyuma yake. Harufu hiyo ikamshawishi Sharji kugeuza shingo yake kutazama nyuma.
“waoooooh!”
Alijikuta outomatic akijisemea kwa mshangao baada ya kumuona dada mmoja mrembo mwenye asili ya kiarabu akiingia mule ndani. Hakuvaa ushungi kama alivyowazoea kuwaona waarabu wengi ambao alikutana nao. Huyu alivaa suruali ya jeanz nyeusi na juu akiwa na kikoti chake cheusi.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO