THE NIGHTMARE (5)

0

SEHEMU YA TANO
ILIPOISHIA...
Alijikuta outomatic akijisemea kwa mshangao baada ya kumuona dada mmoja mrembo mwenye asili ya kiarabu akiingia mule ndani. Hakuvaa ushungi kama alivyowazoea kuwaona waarabu wengi ambao alikutana nao. Huyu alivaa suruali ya jeanz nyeusi na juu akiwa na kikoti chake cheusi.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
Kati kati kulikua na nguo Fulani nyeupe iliyonakshiwa vizuri kwa mtindo wa V.

Nakishi hiyo ndio iliwachengua wanaume wote waliobahatika kugeuza shingo zao na kumuangalia mtoto huyo wa kiarabu mwenye uzuri wa ajabu.

Kwani aliacha sehemu kubwa ya kifua chake wazi na kuziruhusu baadhi ya sehemu ya maziwa yake kuonekana. Kifua cha binti huyo kilibeba maziwa makubwa kiasi lakini yaliyosimama bila kupigwa jeki. Pia chuchu zake zilichongoka utafikiri zilikua zinataka kutoboa nguo aliyovaa.

Mate ya uchu yaliwajaa wanaume karibu wote na kuwafanya wengine kusogeza viti vyao kama ishara ya kumwambia akae nae siti moja.

Catework za yule binti zilifanana na mabinti wanaoshandania urembo wa dunia. Alitembea huku anazihesabu hatua zake taratibu huku macho yake yakiwa hayaonekani kwa sababu ya miwani nyeusi aliyovaa.

Wakati sharji na yeye akiungana na wanaume wengine kumshangaa mrembo huyo. Alishangaa zaidi baada ya mrembo huyo kusimama mbele yake na kuvuta kiti na kukaa naye meza moja.

Alipomuangalia tu usoni yule binti, alipokelewa na tabasamu pana lililosimamisha mpaka vinyweleo vya mikono yake.

“mambo”

alisalimia yule dada na kuvua miwani aliyo vaa. Hapo Sharji alizidi kudata. Kwani uzuri wa yule binti ulipunguzwa kidogo na ile miwani. Maana alipovua alikua amefanana kabisa na migizaji wa filamu za kihindi Deepika Padukone.

Lakini alipotabasamu alifanana na Manduri Dixit na alipocheka ndio kabisaa. Dimpose zilisababisha Sharji ajione yupo meza moja na Prity Zinta.

“karibu” aliongea muhudumu baada ya kupeleka oda ya Sharji.

“na mimi nitengeneezee kama hivi.” Aliongea yule dada baada ya kuona chakula alichokiagiza Sharji.

“uko poa” alisalimia tena yule dada baada ya kuona salamu yake ya kwanza imemezwa baada ya muhudumu kuingilia kati.

“niko poa sana,” alijibu Sharji huku akizidi kumuangalia yule dada ambaye kiumri alionekana ni mkubwa kidogo kwake.

“huwa unapendelea sana kula chakula hicho?” aliuliza yule dada kama njia ya kufungua tena mjadala, maana baada ya salamu kimya kilipita kama dakika tatu nzima.

“ ndio, japokuwa kuna vyakula vingine vipo ninavyovihusudu.” Alijibu Sharji.

“mimi si mpenzi kabisa wa chipsi kuku, nimeagiza tu kwakua nimekuona unakula.” Aliongea yule binti na kumshangaza kidogo Sharji, maana alijua kuwa madada wengi wa mjini ndio chakula chao wakipendacho zaidi.

“ kwa hiyo unataka kuniambia unapendelea sana ugali eeh?” aliuliza Sharji kwa kudhihaki.

“umejuaje?..ukiwekea chipsi kuku hapa na ukaleta ugali samaki, mimi nachagua ugali samaki. Tena kukiwa na mlenda pembeni ndio hunitoi kabisaa. Yaani kama wewe ndio ungelikua unakula hicho chakula, nisingesubiri oda yangu. Tungekula pamoja halafu oda yangu ndio ungekula wewe.” Aliongea yule dada na kumfanya Sharji atabasamu.

“karibuni sana, mjisikie mpo nyumbani.” Hiyo ilikua kauli ya muhudumu baada ya kumletea yule binti oda yake.

Dakika moja baadae yule binti alinyanyuka na kumuaga Sharji na kwenda kulipa oda yake. Sharji alibaki kumshangaa sana yule binti kwakua hakula kabisa kile chakula. Zaidi alionja chipsi moja na kunyanyuka kama vile hakupendezwa na ladha ya kile chakula.

Wakati akiwa amepigwa na butwaa, alishuhudia yule binti akipanda pikipiki kubwa aina ya baja yenye bomba mbili na kuondoka zake.

Baada ya kumaliza kula chakula chake, Sharji alimchukua kuku aliyemuacha yule binti bila ya kumgusa na kuanza kumla. Alipomaliza alinyanyuka na kwenda kulipia oda yake.

“ushalipiwa kaka na yule dada uliye kaa nae, pia kuna mzigo katukabidhi tukupe.” Aliongea cashier na kumkabidhi bahasha ndogo ya khaki.

Alivuta taswira toka yule dada anaingia pale hakua amebeba mzigo wowote, hata hiyo Sharji alipuuzia na kuichukua ile bahasha na kuondoka nayo.

Safari ilimpeleka mpaka nyumbani ambapo alimkuta kaka yake amesharudi toka kazini. Alishangaa kidogo uwepo wa kaka yake pale nyumbani mapema kiasi kile.

Alijua si kawaida yake, maana hata kama akitoka mapema. Basi lazima ampigie mmoja kati ya mademu zake na kwenda kutanua nao. Hiyo ndio ilikuwa starehe kubwa ya kaka yake ambaye alikua hachagui week end wala jumatatu. Kwake ni bata kila siku.

“vipi brother, mbona mida hii home?” aliuliza Sharji huku akiliendea friji na kuchukua kinywaji alichokua anakipenda na kurudi sebuleni ambapo kaka yake alikua anacheza game.

“ nimeamua tu, si unajua kesho safari, xo part itakuwa humuhumu ndani mpaka mida mibovu. Muda si mrefu wataingia washikaji kwa ajili ya mkesha wa safari.” Aliongea Karimu huku akiwa bize na Game.

“achana na game bro, kuna bonge la ishu nataka kukupa.” Aliongea Sharji na kumfanya Karim aachie padi na kusikiliza.

“unajua brother kuna mademu halafu kuna wanawake ambao ukiweka ndani basi huhitaji pambo lingine maana anatosha kuwa pambo la nyumba?” aliongea Sharji na kumfanya kaka yake kuwa makini. Maana alikua mgonjwa wa wanawake wazuri. Akitajiwa tu warembo basi zipu humtaka kufunguka kwa umelu wa wasichana wazuri.

“bila shaka umekutana na kifaa cha ajabu sana. Nipe sifa zake nimpe maksi.” Aliongea Karimu na kumuangalia Sharji ili avute taswira ya picha halisi kwa kile atakachokiongea mdogo wake.

“punguza mchecheto bro, unajua mazali mengine yanatuangukiaga vijukuu vya mitume kama sisi. Maana wakati nimeenda best bite kupata makulaji. Ndipo alipoingia demu mmoja mwarabu mrefu. Ananukia hatari. Hizo nguo alizo vaa basi, katokelezea mbaya.

Hakuna mwanaume rijali aliyekua hajageuza shingo yake kumuangalia. Basi mtoto kama kafumba macho vile. Kawapita watu wote na kukaa na mimi. Hapo ndipo nilipohisi kuwa pritty zinta yupo mbele yangu. Demu akaagiza chakula nilichoagiza mimi kisha tukaanza kupiga story mbili tatu. Sema nilivyomcheki alikua mkubwa kwangu. Basi demu alipoletewa oda yake, kala kidogo tu kisha akanyanyuka na kwenda kulipia bili yake. Mwanao nilipomaliza kula, nikagonga na kuku wake aliyemuacha kisha nikaenda kulipa. Nilistaajabu kukuta yule demu kanilipia na kuacha zawadi kwa ajili yangu..”

Aliongea sharji huku akionyesha baadhi ya vitendo alivyoweza kuviigizia. Wakati wato huo Karim alikua makini kusikiliza huku akitabasamu.

“amekupa zawadi gani?” aliongea Karim kwa shauku kubwa ya kutaka kujua zawadi aliyopewa mdogo wake.

“lakini napata wasi wasi kidogo, maana yule dada hakuingia na kitu chochote. Hata hakuwa na mkoba useme aliutumia kuweka hiyo zawadi. Sasa amewapa wale wahudumu saa ngapi?” aliongea Sharji na kutaka ushauri kutoka kwa kaka yake.

“kwa hiyo haujaifungua?” aliuliza Karim na kumuangalia mdogo wake.

“ndio.” Alijibu Shari na kumuangalia kaka yake aliyekuwa bize kuyasoma na kuyatafsiri maelezo yake.

“kailete hiyo zawadi.”

Aliongea Karim na Sharji akatii amri na kwenda kwenye gari yake alipoiweka. Alirudi na ile bahasha na kumkabidhi kaka yake.

Uzito wa ile bahasha walishindwa kutabiri kitu kilichokuwa mule ndani. Kwa utaratibu mkubwa, Karimu alianza kuichana ile bahasha na kukuta karatasi lililoviringishwa mafungu mawili yenye ukubwa unaofanana. Walitazamana kwa sekunde kadhaa kisha wakashauriana waendelee kufungua ili wajue kilichopo ndani.

“Damn..woooooh!”

Huo ulikua ukulele wa Karimu baada ya kukuta maburungutu makubwa ya hela za kimarekani. Yalikua mabunda mawili yaliofungwa vizuri yakiwa na noti za dola mia mia.

Thamani ya maburungutu yale walipoyalinganisha na thamani ya hela za kitanzania. Walijikuta wamepata zaidi milioni 300 za kitanzania.

Huku Shariji na kaka yake wakiwa hawaamini kile walichokiona, kwa mbali walikiona kikaratasi kikipepea. Walijua moja kwa moja kilikua kimetoka mule ndani ya ile bahasha. Wakakifuata na kukisoma. Hicho kikaratasi kilikua na namba ya simu na jina la kike lililosomeka BARQIS.

“Barqis, kweli atakua mwarabu. Maana hili jina limekaa kiarabu arabu sana.” Aliongea Karim huku akiziandika zile namba kwenye simu yake.

“vipi, nimpigie?” aliuliza Karim baada ya kumaliza kuinakili ile namba.

“hamna shida, we twanga tumsikie.” Aliruhusu Sharji na kaka yake akabofya kitufe cha kupigia simu na kuanza kusikiliza sikioni kwake.

“inaita” aliongea Karimu kwa sauti ya chini baada ya kusikia muito wa qaswida ya kiarabu.

“haloo”

Ilisikika sauti nyororo masikioni mwa Karimu. Aliweka koo lake vizuri tayari kwa kujibu.

“haloo, mambo.” Aliongea Karim na kumfanya mdogo wake kumsogelea karibu ili asikie sauti ya upande wa pili.

“safi, samahani naomba niongee na mdogo wako” iliongea sauti ya upande wa pili na kumfanya Karimu ashangae.

“hayuipo hapa, ameenda kuoga.” Alidanganya Karim.

“basi akirudi mwambie anipigie kupitia simu yake.” Aliongea yule dada na kukata simu.

Karimu alijaribu mara kadhaa kupiga simu, lakini haikupatikana. Alimuangalia mdogo wake ambaye naye alikua haelewi chochote.

“kwani wewe umeshawahi kuonana nae kabla au ulimpa information kuhusu mimi?” hatimaye Karim alijikuta anamuuliza mdogo wake swali lile.

“yaani leo ndio siku ya kwanza kumtia machoni.” Aliongea Sharji.

Wakati wapo katika mjadala juu ya yule msichana kuwafahamu wao vizuri, Simu ya Sharji ilianza kuita na kwenye kioo cha simu hiyo ilitokea namba ngeni. Walipoiangalia ilikua inafanana kabisa na ile ya Balqis. Waliangaliana na kutafakari kwa kile kilichotokea. Hata Shariji mwenyewe hakujua kua yule binti ameitoa wapi nama yake kwakua hawajapeana namba za simu kule mgahawani.

Simu iliita mpaka ikakatika. Ilipoita tena kwa mara ya pili, Sharji alikata shauri na kuipokea bila kuongea chochote.

“mambo SHARJI”

Salamu hiyo ilimfanya sharji atoe macho kama mjusi aliyebanwa na mlango.

“Safi, tu.” Alijibu Sharji kiuoga.

“nimefurahi sana kuisikia sauti yako Sharji.” Aliongea Balqis.

“ha..hata mimi, sema umelijuaje jina langu?.” Aliuliza Sharji huku akijaribu kupeleleza maelezo ya Balqis.

“wewe hunifahamu mimi, ila mimi nawafahamu kuanzia nyinyi hadi wazazi wenu. Mama yangu na mama yenu wamesoma chuo kimoja” aliongea Balqis na kushusha preasure aliyokuwa nayo Sharji.

“weka loud speaker!”

Aliongea Karim kwa sauti ndogo ambayo ilisikika vizuri na Sharji.

“toa loud speaker bwana.”

Aliongea Balqis baada ya Sharji kubonyeza kitufe cha kupaza sauti.

“kwanini hutaki nisikie maongezi yenu?” aliongea Karimu kwa sauti ya ukali kidogo.

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)