THE NIGHTMARE (7)

0

SEHEMU YA SABA
ILIPOISHIA...
“kha!!!!”

Ulikua mshangao mkubwa kwa watu karibu wote baada ya kumuona Sharji akiwa na taulo akitoka chumbani kwa Balqis.

IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI

ENDELEA...
Wengine walicheka na kaka yake alionekana kutoifurahia hali ile.

“sasa wewe unatutia wasi wasi bure, si ungesema tu kama unaenda kulala kwa huyu dada?” aliongea kaka yake na kukirudia kile chumba alichompangia mdogo wake kulala.

“sasa mwenzako mbona haamki?....tumegonga sana tu.” Aliuliza Karimu huku akiendelea kugonga mlango na kuendelea kumuita kwa jina lake.

Wasi wasi juu ya usalama wa mwenzao ulianza kuwatanda. Maana walikaa kwa masaa matatu lakini hakukua na dalili za mlango kufunguliwa.

“tufanye nini jaamani?” aliuliza Karim baada ya kukaa muda mrefu.

“tuvuunjeni tu mlango.” Aliongea mmoja wa watu waliokuwepo kwenye ile boti.

Walikubaliana hivyo na kuchukua shoka lililokuwa kwenye boti hiyo na kuanza kuvunja mlango.

“MUNGU WANGU!!!!”

Wote walishika vichwa vyao kwa mshangao mkuu baada ya kumuona mwenzao akiwa chini ya kitanda huku katapakaa damu mwili mzima. Wasichana walianza kulia kwa uoga baaba ya kushuhudia kifo cha kutisha kilichompata mwenzao.

Kifo cha utata kilichotokea kwa mwenzao ndani ya boti kilileta taswira nyingine kwa wasafiri wote. Walichunguza bila kupata majibu yanayoridhisha. Wote wakaamini kuwa yule mtu alikufa kwa ajili ya majini yaliokuwa baharini.

Furaha yote ilitoweka na huzuni ikachukua nafasi yake. Wanawake ndio kabisa walikuwa wakikaa karibu na wanaume kwa kuwa walijawa na uoga.

“sasa nahodha , tufanye nini. Maana akili yangu haipo sawa muda huu.” Aliongea karimu na kumuangalia nahodha ambaye naye hakuwa na msaada kwa wakati hou.

“kama hakuna mawasiliano unafikiri kuna maajabu gani zaidi ya kusubiri meli ije itupe msaada?” aliongea Nahodha na kuwakatisha tamaa kabisa.

Masaa yalizidi kusogea bila dalili zozote za kutokea kwa meli au boti kuonekana maeneo hayo.

Kiza kiliingia tena na wote kwakua walichoka, walienda kulala baada ya kula chakula ambacho kiliishia usiku huo. Kila mtu kwa imani yake aliomba ili kama kuna jini basi asije tena kuwaua.

Sasa haikuwa siri tena, Balqis na Sharji walienda kulala chumba kimoja kwakua Balqis alitangaza kuogopa kulala peke yake na kumchagua Sharji kama mlinzi wake. Hata wanawake wengine waligoma kulala peke yao na kulala na wanaume.

Asubuhi ya siku ya tatu toka wasafiri ilifika huku wakipatwa na msiba mwingine wa msichana mmoja ambaye alipotea kimaajabu na kukutwa mbele kabisa ya ile meli akiwa amekufa.

Vifo hivyo mfululizo viliwafanya wakate tamaa ya maisha.

“najuta kwa nini nimeikubali hii safari.” Aliongea Balqis akimwambia Sharji aliyekuwa pembeni yake lakini kwa sauti iliyosikika kwa kila mtu.

“yaani mimi ndio sina hamu.” Aliongea Sharji

Malalamiko yalichukua nafasi kwa kila mtu aliyekuwa pale, lakini ukweli ulibaki pale pale kuwa ndio washaingia kwenye boti na sasa wamekwama na mauaji yanatokea kila siku.

Masaa yalizidi kusogea huku njaa ikianza kuwatesa kutokana na kuishiwa na chakula toka jana yake usiku. Mpaka kufikia saa kumi na mbili jioni, wote walilegea kwa njaa ya toka usiku wa jana yake.

“jamani mimi na wazo, mnaonaje tukeshe ili kama jini linakuja basi tulione kwa macho yetu.” Balqis alishauri baada ya kugota saa tano usiku.

“ni wazo zuri.” Alidakia Karim aliyekuwa pembeni huku akiwa amechoka kutokana na njaa aliyokuwa nayo.

“mimi ndio nitakufa kwa njaa usiku huu hata kabla huyo jini kunitafuna.” Aliongea dada mmoja aliyekuwa anagala gala kutokana na kusumbuliwa na vidonda vya tumbo.

Wakakubaliana kukesha macho mpaka asubuhi. Zoezi hili lilifanikiwa kwa kukucha salama bila mtu yeyote kupoteza maisha.

“kwa hii njia labda tutafaulu. Vipi kuhusu kukabiliana na njaa?” aliongea Sharji na kuungwa mkono na watu wote waliokuwa pale.

“hapo hatuna jinsi, ndio tutakufa kama kuku wa mdondo.” Aliongea Dada mmoja ambaye naye alikuwa hoi kutokana na njaa aliyokuwa nayo.

Dakikia kumi baadae walishuhudia mwenzao aliyekuwa anasumbuliwa na vidonda vya tumbo akiaga dunia mbele yao.

Hali hiyo iliwakatisha tamaa kabisa na kuwafanya wachanganyikiwe kupita kiasi. Kwa shida ya njaa na mateso hatimaye kiza kikaingia tena.

“vipi na leo tunakesha?” aliuliza Juma ambaye alionekana kidogo ana uvumilivu wa njaa.

“kama kufa tutakufa tu, haina haja ya kukesha.” Aliongea Sharji.

“ kama kulala basi tulale wote hapa hapa.” Alishauri Balqis na wote wakakubaliana hiivyo.

Usingizi wa mang`amu ng`amu ulipatikana kwa uchovu waliokuwa nao japo kuwa walikuwa na njaa ya ajabu.

Maji kidogo waliyokuwa nayo ndio yalikuwa tegemeo lao. Hata hivyo nayo yaliisha usiku huo huo.

Hatimye palikucha na kujikuta waliofanikiwa kuiiona asubuhi hiyo walikuwa watu wanne tu. Wengine wote walikufa kwa kuraruriwa vibaya kila sehemu na kufanya eneo hila kutapakaa damu. Hata wao pia walijikuta wamamwagikiwa na damu kiasi ya wenzao.

Waliobakia ni Balqis, Sharji, Karimu na nahodha. Walipigwa na butwaa lakini hawakutishika sana kutokana na mioyo yao kujaa ganzi kwa matukio yale waliyokuwa wakiyashuhudia kila siku.

Walijua zamu yao ilikuwa siku ile hata kama wasingeuliwa na huyo jini basi njaa na kiu vilitosha kuwapotezea uhai.

“mi naenda kulala ndani,…. Kama kifo changu kinaniita basi itakuwa nimeandikiwa hivyo.” Aliongea Balqis na kuingia ndani ya ile boti.

Cha ajabu alitokea upande wa pili na kujibadilisha kwa kutibua nywele zake na meno makali yenye urefu usio wa kawaida yakajitokeza.

Alionyesha mkono kwenye bahari na boti dogo la uvuvi likajitokeza. Alijitoa photocopy na kuwa Balqis wawili wanaofanana, hapo Balqis mmoja akayeyuka na kutokea kwenye ile boti ndogo ya uvuvi.

Hapo alijigeuza mvuvi na kutokea na vifaa vyote. Hapo Balqis alicheka na kujirudisha kama alivyokuwa awali na kurudi tena kwa wenzake aliowaacha.

“usingizi hauji mamaa” aliongea Sharji baada ya kumuona Balqis pale.

“kuna lalika basi na hii njaa niliyokuwa nayo?” aliongea Balqis .

Baada ya dakika kumi kupita, kwa mbali waliona boti ndogo ikija upande wao. Waliipigia mluzi na yule mvuvi aliwafikia mpaka pale walipo.

Walimuelezea shida iliyowapata. Yule mvuvi alisikitika kisha akaawaambia kama wakitaka msaada wake basi wawili wenye nguvu wapande boti yake wakamsaidie kuvua samaki kisha watawapitia wenzao na kurudi nao.

Chakula alichokibeba na maji viliwafanya wagombanie kama mpira wa kona. Baada ya kumaliza kula. Walipata nguvu kidogo na Karim akiwa na nahodha walipanda ule mtumbwi na kuondoka zao na kuwaacha Sharji akiwa na Balqis.

Walipofika mbali na pale walipokuwepo, yule mvuvi alisimamisha boti yake na kuwageukia Karim na yule nahodha wao.

“mnanijua mimi ni nani?” aliuliza yule mvuvi na kuwaangalia huku akiwakazia macho.

“hatukujui!” walijibu kwa pamoja huku wakiwa na mshangao kwakuwa hawakutegemea swali kama lile.

Hapo hapo alibadilika na kuwa Balqis. Wote walitoa macho hali ya kutoamini walichokiona.

Baiqis alibadilika na kutoa makucha na kumrarua yule nahodha huku Karimu akishuhudia.

“aaaaaagh!!!!”

Mlio huo wa uchungu ulisikika mpaka kwenye ile boti alilikuwemo Sharji na Balqis.

Dakika mbili baadae, Sharji anaiona ile boti aliyopanda kaka yake na yule nahodha ikirudi ikiwa haina dalili zozote za kuwepo na watu mule ndani.

Ile boti ilipokaribia maeneo yale, Shariji alishangaa kuona maiti ya kaka yake ikiwa imelala kwenye ile boti.

“MUNGU WANGU????”

Alishika kichwa Sharji baada ya kuona vile. Mara akaanza kusikia hatua za miguu zikimfata pale alipo.

“MAMAAAAAAAAA!!!!!!”

Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU IJAYO

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)