Mtunzi: ___
SEHEMU YA SABA
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Kwa sasa niko katika mkasa mzito ambao unaweza kuhatarisha usalama wa jiji endapo mtu huyo mwenye roho ya kinyama hatapatikana”.
Habari hiyo ikamvutia Joram. “Mtu gani?”, Joram alihoji mara moja.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
“Hujasikia tu? Nadhani wewe hupitwi na neno”.
“Kusikia?”.
“Kuhusu msichana huyo aliyeuawa kikatili kuliko ilivyowahi kutokea. Polisi wamefanya kuokota viungo vyake kimoja baada ya kingine ndipo ukapatikana mwili mzima wa marehemu. Mtu aliyefanya mauaji hayo ni mnyama zaidi ya wanyama wengine wa kawaida. Mtu mwenye kumchinja msichana mrembo kama yule”.
“Sijakupata Inspekta, yaani…” kisha Joram akapunguza kasi kuhoji kuhusu tukio hilo kwa kituo. Inspekta Kombora akamweleza yote kuhusu tukio zima lilivyotokea usiku huo huko Mburahati.
Hakukuwa na sababun za kuupeleka mwili huo hospitali”, Inspekta Kombora aliongeza. “Viongo vyote vya marehemu vimeletwa hapa katika chumba cha maabara. Kama utapenda kutazama vitu vya kutisha unaweza kwenda maabara, inatisha sana”.
“Nitapenda kumwona tafadhali”.
Inspeta Kombora akaiacha ofisi yake na kumuongoza Joram kuelekea maabara ambako alifungua friji na kutoa kichwa cha msichana mrembo. Joram alikitambua kichwa hicho kuwa cha Waridi. Kwa mara ya kwanza katika maisha yake, alihisi machozi yakimdondoka. Aliyafukuza macho hayo kwa tabasamu huku akinong’ona kama mtu anayesali. “Ni Waridi! Mungu akurehemu. Naamini ni mapenzi yako kwangu ambayo yamekufanya ustahili adhabu hiyo ya kinyama. Naahidi nitakulipia kisasi”.
Sala hiyo ilimfikia Inspekta Kombora. Akamgeukia Joram kwa mshangao na kusema, “Kumbe unamfahamu msichana huyu? Tafadhali turejee ofisini ili unisimulie kuhusu mkasa mzima ulivyotokea”.
“Sijawa na cha kusimulia”, Joram alijitetea. Hata hivyo alilazimika kusimsimulia Inspekta Kombora yote aliyoyajua. Alieleza jinsi alipomwona Waridi kwa mara ya kwanza pale baa akiwa ametegwa kwa sumu iliyokusudiwa kumwua yeye. Akaeleza pia yaliyotokea katika chumba ambacho waridi aliandaliwa kwa sumu ile ile ili amnyweshe Joram kwa hila. Ambacho Joram hakueleza ni jinsi alipofika hapo kabla ya wakati na kubahatisha, ingawa kwa taabu, kumwona mwuaji yule akitoa maelezo kwa Waridi. Hilo aliliacha ili apambane nalo binafsi. Hakupenda kuwaachia polisi ambao aliamini wangeweza kuharibu mapngo wake wa kumtia mikononi mwuaji.
“Ina maana binti huyu marehemu ndiye yule msichana aliyetoroka hospitali baada ya kuokotwa kando ya baa”, Joram akatikisa kichwa kukubaliana na swali la Inspekta Kombora.
“Ndiye. Basi anastahili kifo cha aina hiyo. Kwa nini hakutoa taarifa polisi, tungeweza kumsaidia. Alishirikiana na wahalifu kuandaa njama za kufanya uhalifu”.
“Inawezekana au isiwezekane”, Joram alijibu kwa mkato. “Aweza kuwa alilazimika au kulazimishwa. La muhimu sasa ni kumpata huyo mwuaji”.
“Ndio… apatikane haraka. Wewe humjui?”.
Joram alikanusha. “Angalia bwana mdogo. Ninavyookufahamu mimi bila shaka wajua mwengi zaidi ya haya uliyonieleza. Nawe kama uonavyo hawa ni watu hatari kuliko unavyofikiri. Usiwachukulie mzaha, Ucheze nao kama ilivyo kawaida yako”.
“Kawaida yangu sina mzaha wa mwuaji Inspekta”, Joram alijibu. “Tena naamini kuwa nitawafikisha mikononi mwako mapema zaidi. Ninayo nafasi nzuri sana. Sasa hivi wao wanadhani kuwa nilikunywa ile dawa na sasa niko mahututi au marehemu tayari. Imani hiyo itawafanya wapate jeuri ya kuendelea na mipango yao kama walivyokusudia. Nataja kujua lengo lao, wanakusudia kufanya nini, na watu hawa ni akina nani, baada ya kufahamu hivyo nitawaleta mikononi mwako.
“Kazi hiyo ndiyo iliyonifanya nijibadili kuwa katika hali hii Inspekta. Nimeona nitoweke machoni mwao. Kusudi langu kwako ni kukuomba uitangazie dunia kuwa nimefariki ghafla. Nadhani watafurahi na kuendeleza mipango yao. Ndipo nitakapofufuka na kuwashangaza kwa kuwatia mikononi.
Walijadiliana kwa muda ofisini. Kombora akawa ameafikiana kwa taabu sana na Joram. Nia ya Joram ilikuwa awaachie polisi kufanya kazi yao kwa makini. Lakini maelezo ya Joram yalimtua Inspekta Kombora hata akakubali japo kwa shingo upande. “Kumbuka ninavunja sheria zote za kushiriki katika uongo mkubwa kama huu. Hivyo. usiniangushe kwa kushindwa kutimiza ahadi yako ya kuwatia watu hawa mikononi mwa sheria”, Inspekta Kombora alimwambia Joram.
“Wanifahamu vizuri Inspekta. nakuhakikishia kuwa Siwezi kushindwa kamwe”, Joram alimjibu akiweka vyema ndevu zake za bandia na kuvaa miwani yake. Akautwaa mkongojo wake na kuiacha ofisi ya Inspekta Kombora kwa mwendo ambao ulimfanya Inspekta huyo ambaye hucheka kwa nadra sana aangue kicheko kipana.
Usiku huo taarifa ya habari ya Radio Tanzania Dar es Salaam ilibeba habari ambazo ziliwashitua wasikilizaji wengi kote nchini.
“…Joram Kiango yule mpelelezi mashuhuri wa kujitegemea amefariki ghafla akiwa nyumbani kwake kwa maladhi ambayo bado hayajathibitishwa. Madaktari wanaendelea na uchunguzi watatoa taarifa za kifo hicho hivi karibuni baada ya uchunguzi,,,”
Haikuwa habari njema hata kidogo. Wala hakuna aliyetarajia kuisikia. Kila aliyemfahamu Joram alitegemea kuwa kijana huyo angeuawa au kufa kwa risasi au madhara mengine kutoka kwa adui zake. Kufa kwa maradhi! haiwezekani!.
Taarifa za habari za sauti ya Kenya na Ujerumani ziliidaka habari hiyo haraka na kuitagaza kwa mapana zaidi… “Yule kijana machachari”… Walisema wakenya, “The Iron boy…” walimwita hivyo wajerumani… “Amefariki leo ghafla. Yawezekana na njama za wahujumu ambao walimuogopa sana kijana huyu kama moto”.
Ndipo watu walipolazimika kuamini. Wengi walisikitishwa na kifo hiki. Wengine walitoa machozi. lakini Wachache walishangilia.
Nyumba hii iliyobomolewa kwa bomu ilikuwa katika mtaa wa Manda Magomeni Mikumi. Ilikuwa nyumba ambayo kwa muda mrefu haikutumiwa kutokana na kutokamilika kwake tu. Joram alikuwa ameichagua nyumba hii kwa ajili ya kujificha baada ya kuitazama mara kwa mara kila alipopita katika mtaa huu na kuona ilivyokaa vizuri kwa siri. Ilikuwa imezungukwa na kichaka cha miti ambayo awali ilikusudiwa kuwa bustani. Haikuwa rahisi kwa mtu wa nyumba jirani kufahamu yanayotokea katika nyumba hii kwa jinsi zilivyotengana.
Zaidi, ilikuwa na njia nyingine ya uwani ambayo ilipitia katika uchochoro hadi mitaa ya nje kabisa. Kuhamia hapa ilikuwa siri yake binafsi ingawa Inspekta Kombara alimsihi sana amfahamishe wapi amejificha, Alikuwa amehamia hapa usiku wa manane baada ya kujipitishapitisha ili kuhakikisha kuwa hafuatwi au kuonekana na mtu. Mzigo wake pekee ulikuwa ni Suitcase yake ambayo ilichukuwa vifaa vyake muhimu ikiwa pamoja na silaha ndogo,
Usiku huo wa kwanza alilala vyema. Alfajiri aliamka na kujiandaa kwa kuvua ujana na kuvaa uzee. Baada ya kukamilisha taratibu za uzee alilificha vizuri begi lake na kutoka hadi polisi ambako alikamilisha mipango yake na kurejea mafichoni akisubiri muda alioupanga ili aanze harakati zake.
Joram alikuwa na hakika kuwa kazi hii isingemchukua muda kuimaliza. Jambo lililomtia matumaini ni kule kujua kuwa adui zake walikuwa wakisubiri kifo chake ili waanze shughuli zao. Kadharika, mmoja kati ya adui hawa hakuwa mgeni kwake. Alichungulia alipokuwa akitoa amri kwa marehemu Waridi na kuipata picha yake. Insingemchukua muda mrefu kumfahamu kikailifu.
Kitu kimoja Joram hakujua. Hakujua kuwa makazi haya ya siri aiyohamia hayakuwa yake binafsi. Yalikuwa malazi ya Luta Magambe, mmoja kati ya mamia ya vijana wazurulao katika Jiji la Dar es Salaam. Luta alikuwa ameingia Jijini miaka zaidi ya kumi iliyopita, akitokea kwao kijijini katika moja wapo ya Wilaya za mkoa wa Kagera. Alikuja Dar es Salaam kwa nia njema ya kutafuta kazi baada ya elimu yake ya msingi. Jiji likamlaki kijeuri kama linavyowalaki wote. Kazi haikupatikana kwani hakuwa na mtu wa kumfanyia “mpango” wala pesa za “motisha”.
Akaambulia kuangukia katika vibarua vya kutwa. Pesa alizopata zikawa ndogo mno kulingana na mahitaji ya Jiji. Kila siku akawa mtu wa “Kuchacha”. Hilo likamtuma kutumia muda wake wa ziada kuwachomolea wasafiri wa Uda na Daladala. Tabia hiyo haikuchelewa kumfikisha Keko akiwa na majeraha mengi usoni. Alipotoka Keko hakuwa luta mwenye nia njema tena, bali mtu ambaye yuko tayari kufanya lolote mradi apate chochote.
Msimamo huo mpya ulimanya apoteze chumba na kukosa marafiki wa haja. Rafiki zake pekee walikuwa wahuni wenzake na walikutania “kazini”. Baada ya “kazi’ kila mmoja alijua lake.
Siku alizopata, alistarehe kwa kulewa, kujipatia wasichana wazuri na kulala vizuri katika majumba ya wageni ama kwenye nyumba za wasichana hao. Alipokosa alijutia na kujisahaurisha kwa kuvuta bhandi na kujilaza katika jumba hilo bovu.
Hivyo kwenye alfajiri hiyo aliona kama mwujiza kuona ‘mzee’ huyu mwenye dalili ya pesa na sura ya Kialhaji akitokea ndani ya moja ya vyumba vya jumba hili akiitumia njia yake ya siri! Mara moja wazo likamjia Luta?. Kwamba mzee huyu alikuja katika ghofu hili kwa sababu maalumu. Sababu ambayo Luta aliamini kuwa haikuwa nyingine zadi ya kuficha pesa au vitu vya thamani, Wazo hilo likamtuma kuanza upekuzi akitafuta chochote ambacho mzee huyo alikificha. Hakupata kitu. Hata hivyo alikuwa bado akiendelea na upekuzi wake ‘mzee’ aliporejea. Hima akajipenyeza katika chumba cha pili ambamo alijificha vizuri. Joram hakumuona. Darubini ya adui yake Joram kutoka nyumba ya pili pia haikuweza kumuona. Alitulia akimchungulia Joram ambaye aliketi akifanya mambo yake.
Kisha Bagambe alimuona mtu mwigine akinyatia nyumba hii mkononi kashika vitu ambavyo alivificha kwa hadhari chini ya mlango, Baada ya mtu huyo kushika hapa na pale aliondoka eneo hilo kwa hadhari na ukimya ule ule.
Kitu gani kitatokea?, Bagambe alijiuliza, Hakika moja alikuwa nayo. kuwa hii ilikuwa nafasi yake pekee ya ‘kuukata’. Kwamba leo lazima ungekuwa mwisho wake wa maisha ya kubahatisha na mwanzo wa maisha mapya. Ingekuwaje vngine na eti bahati zinamfuata hadi huku badala ya yeye kuzifuata kwenye vituo vya basi? Hakuona sababu ya kuendelea kusubiri.
Kwa hadhari mfano wa paka anayemnyemelea panya, aliiendea sehemu hiyo aliyoona kitu kikifichwa. alipofika alipekua taratibu. Kisha aligusa waya fulani ambao hakutarajia kuuona hapo. Aliutazama waya huo kwa mshangao. Mshangao ambao ulikatizwa na mlipuko mkali uliomfanya apae juu na kutua chini akiwa tayari ametawanyika vipande mfano wa nyama za kopo, zinazoandaliwa kwa ajili ya kusindikwa.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)