Mtunzi: Omary John Mndambi
SEHEMU YA AROBAINI NA NNE
TULIPOISHIA...
TULIPOISHIA...
Verity alikuwa amefurahishwa sana na penzi la mme wake akawa anajutia kwa kukosa uvumilivu siku zote kumbe kwa mme wake kuna mambo matamu kiasi kile.
IKIWA UNASOMA SIMULIZI NJE YA APP YA CnZ Media IPAKUE ILI USIPITWE NA SIMULIZI
TUENDELEE...
Alishindwa kuvumilia akainua kichwa chake akakilaza kwenye kifua cha Gwakisa na kumwambia …
“Asante sana mme wangu nakupenda sana”
Gwakisa hakujibu neon ila alipelaka mkono wake hadi kwenye kichwa cha mkewe akawa anamkuna nywele zake ishara ya huba na upendo.
Hazikuisha dakika nyingi joto lao likawa limepanda tena, hawakuwa na cha kuzuia kwani wao ni mke na mume ikabidi wapeane tena, walipeana haswa mpaka kila mmoja akajiona amechoka na kisha wakapumzika baada ya kuoga vizuri.
Baada ya muda kidogo walipitiwa na usingizi wakalala fofofo, walikuja kuamka baadae sana usiku ukiwa umeshaingia wakaamua kutoka waende kula mtaani.
Wakiwa mtaani wamekaa wanakula na kunywa ilipita taarifa kwenye Tv iliyoonyesha kuhusu mazishi ya Dr Kelvin baada ya uchunguzi wa kipolisi kukamilika.
Mke wa Dr Kelvin alionekana analia huku kakumbatia watoto wake ambao nao walikuwa wanalia sana,
Taarifa hii ilibadilisha hali ya Verity kabisa kwani alianza tena kukumbuka, furaha ilipotea moyoni na usoni na Gwakisa alilitambua hili japo hakujua kwavipi mke wake anahusiana na hizi taarifa hivyo akachukulia kawaida tu.
Walimaliza kula na kunywa kisha wakarudi nyumbani ambapo walilala mpaka kesho yake, Kulivyokucha Verity waliongozana na Gwakisa hadi hospitali ili kupima hali ya mkewe.
Walipokelewa vizuri na vipimo vikachukuliwa kisha baada ya muda kidogo wakaitwa ofisini kwa daktari ili wasomewe majibu ya vipimo.
…………………………………
Husna Ramadhani ni nesi ambaye aliponea chupuchupu kufa baada ya kubakwa na watu ambao walimbaka pia Dr Kelvin na kumfanya apoteze maisha. Alikuwa amesharuhusiwa kutoka hospitali na alikuwa nyumbani kwake anaendelea kumeza dawa ambazo alikuwa ameandikiwa.
Mawazo lukuki yalikuwa yameuganda moyo wake kwa kitendo ambacho alikuwa amefanyiwa, alijiona amezalilishwa sana, jamii yote ilikuwa imeshajua kuwa amefanywa vibaya.
Alijiona hana tena thamani kwenye uso wa dunia, kwakuwa alikuwa na likizo ya ugonjwa alibaki nyumbani akiwa anajiuguza.
Baada ya wiki mbili likizo yake iliisha hivyo akaenda kazini, hakuna kitu kilichomhuzunisha kama kufika kazini na kukuta watu wanamtenga na kumsema vibaya.
“Kumbe alikuwa anatembea na Kelvin, atakuwa nae ameathirika sio bure”
Neon hili lilimtisha sana Husna akaamua kupima afya yake, huku akiwa mwenye hofu nyingi alichukua vipimo vilivyokuwa vingi tu pale ofisini kwao na kukaa kando sehemu ambayo hakuna mtu angemuona.
Alijichoma kidoleni kisha akaminya kidole kuruhusu damu itoke ya kutosha kisha akaiweka kwenye kipimo chake akachanganya na maji maalumu ya kupimia kisha akatulia kwa muda akisubiri majibu.
Taratibu mstari mmoja ulianza kutokea, huu ni mstari ambao huashiria kuwa kipimo kinasoma, endapo ukibaki huu mmoja ina maana hujaathirika, ikiwa miwili basi umeathirika.
Zilipita dakika kama tatu hivi ule mstari ukawa umekolea vya kutosha ila kuna kitu kilianza kumtisha….kuna mstari mwingine ulianza kuonekana…
Mapigo ya moyo yalienda kasi kama treni ya umeme, kila alipoangalia vyema ndio ule mstari ulikuwa unajitokeza vizuri, baada ya kama robo saa hivi hakuna kilichokuwa kimejificha tena, mistari ilikuwa miwili kuashiria kuwa Husna Ramadhani nesi ambaye alibakwa akiwa na mpenzi wake marehemu Dr Kelvin alikuwa ameathirika na HIV.
“Nimekwisha!” alijisemea Husna kwa huzuni.
Akiwa kwenye dimbwi la mawazo simu yake ilitoa mlio wa sms akaufungua, alikutana na ujumbe kutoka kwa mpenzi wake ambaye waliahidiana kuoana.
“Nilikuwa nakwambia siku zote kuwa unani-cheat,
Umenkuwa ukinibishia kwa nguvu zote lakini malipo ni hapa hapa duniani”
“Nilikwambia utulie na mimi lakini uliniendesha na kunitesa bila kujali kuwa namimi nina moyo wa maumivu…ona sasa umeumbuka na dunia nzima imekuona…asante kwa mateso yako Husna, mimi na wewe kwasasa basi…”
Huu ujumbe toka kwa mpenzi wake ulitia chumvi kwenye kidonda cha Husna, nikweli alimnyanyasa sana mpenzi wake kwasababu ya Dr Kelvin, nikweli kwamba mpenzi wake alilia sana machozi akiomba ahurumiwe kwani mateso ya Penzi yanamuumiza lakini Husna hakujali.
Leo ameumbuka na dunia imemuona, alijutia sana na mbaya zaidi ameathirika na hapohapo kaachwa na mpenzi wake.
Husna alikuwa kama amechanganyikiwa, ghafla roho yake ilitamani kufa, alijiona hana sababu ya kuishi hapa duniani, alichoamua ni jambo moja tu…Kufa!
Alichukua boda boda akakimbilia kwake, alipofika aliingia ndani akachukua karatasi akaandika alichokusudia, alipomaliza alichukua chandarua akaitendenezea kamba.
Alipohakikisha kwamba imekuwa kamba nzuri akaitengenezea kitanzi kisha akaifunga kwenye mbao iliyopita juu ya banda la kuku.
Hakuchelewa akachukua stuli akapanda juu yake na kujivisha kile kitanzi, alipoona kimekaa vyema akasukumiza Kistuli na kubaki amening’inia.
Alisikia maumivu makali mno lakini hayakudumu, ndani ya dakika mbili alikuwa ametokwa na kinyesi kingi na mkojo huku uso ukianza kuvimba.
Dr aliyekuwa ameshikilia karatasi ya majibu ya Verity alikuwa na tabasamu usoni huku akiwaangalia Verity na Gwakisa kwa kupishana.
“Hongereni sana”
“Una maana gani Doctor?”
“mkeo ana mimba ya mwezi mmoja”
“Eeenh…” Hilo ndilo neon pekee alilotamka Verity kisha akawa mpole, hali ilikuwa tofauti kwa Gwakisa kwani alikuwa ni full kicheko, alifurahia sana kusikia kuwa mkewe ana mimba, alisubiria sana siku moja aitwe baba na leo ilikuwa imefika.
“Twendezetu mke wangu, twende tukasherekee”
Verity alinyanyuka kivivu kisha akapelekwa mpaka kwenye gari akafunguliwa mlango akakaa na Gwakisa nae akaingia sehemu ya dereva akafungulia mziki mkubwa kisha akawasha gari wakaelekea nyumbani.
Alipofika alishuka haraka akafunga mlango wa gari kisha akaelekea kwenye mlango wa Verity akaufungua na kumtoa mkewe kisha akambeba juu juu mpaka ndani na kumbwaga kwenye kochi.
“Unjisikia kula nini Love?” gwakisa ndie alikuwa anauliza akimaanisha kuwa yuko tayari kupika…
Verity kwenye akili yake kulikuwa kunazunguka vitu kibao tofauti na Gwakisa ambaye alikuwa ni shangwe tu.
“Bwana nakula chochote tu” alijibu VERITY.
“Sasa mbona kama huna raha jamani au hujafurahi mimi niitwe baba?” aliuliza Gwakisa japo hakujali sana.
Alichoamua kufanya ni kuandaa chakula alichojua kuwa mkewe anakipenda sana kisha akakiweka mezani na kumbeba tena juu juu
“Njoo ule mama K wangu”
Verity alikuwa anadekezwa kupita kiasi, wakati mwingine alikuwa anafurahi lakini kuna mda roho ilikuwa inamsuta…
“Hii mimba haiwezi kuwa ya Gwakisa, lazima ni ya Dr Kelvin” verity alikuwa anajisemea mwenyewe moyoni mwake.
Akili yake ilirudi ikakumbuka walivyokuwa wanafanya mapenzi na Dr Kelvin…alikumbuka kauli za Dr Kelvin kila walipokuwa wanamaliza mzunguko alipokuwa anamwambia…
“Kwa goli hili nililopiga lazima upate mimba tu”
“Unasemaje? Nipate Mimba? Nitamwambiaje mme wangu mimi”
“Hahahaaaa ni bora nikupe mimba mimi maana usipofanya hivyo hutazaa”
“Acha ujinga wewe”
“Niache ujinga kwani hujui kuwa mme wako hazai…mme wako ni tasa na mimi ndio nilimpima ila tu sikumwambia tatizo lake, na najua kuwa hata mtoto wako wa kwanza ulimchakachua…”
Verity alipokumbuka haya yote ndipo akaamini kuwa ile mimba haikuwa ya Gwakisa kwani kwa ngono aliyokuwa anafanya na Dr Kelvin na kwa yale maelezo yake inawezekana yana ukweli…
“Una mawazo gani mbona huli?” Ilibidi Gwakisa aulize maana hakumuelewa mkewe…
“Oh nipo sawa tu, ni mawazo tu yah ii hali mpya”
“Usijali mama nitakulea kama yai”
Walimaliza kula na kuelekea chumbani ambapo siku hiyo Gwakisa hakutaka kutoka kabisa, aliamua kubaki na mkewe ndani.
Masaa yalisogea na usiku ukaingia wakalala usingizi hadi kesho yake ambapo majukumu na shughuli zingine ziliendelea.
…………………………………..
Sam alishtuka kuona mkewe anatokwa zile damu, hofu ilimtanda na kuanza kurudi nyuma nyuma, alikumbuka kipindi kile ambapo alimpiga tena akajikuta anajutia ghafla.
Mkewe alikuwa anajinyonga tu huku kashikilia tumbo lake…
Sam alijitosa na kumbeba kwenye mikono yake mpaka nje akafungua mlango wa gari na kumuweka humo, alizunguka upande mwingine akafungua mlango wa dereva akakalia usukani na kutoka nduki mpaka hospitali.
Alipofika hakusubiri alimchukua na kumbeba juu juu mpaka kwa nesi aliyekuwa zamu huku kamshikilia mikononi vile vile…
“Dr muangalie mke wangu…”
Yule mama nesi alishtuka maana aliona michirizi ya damu miguuni ikabidi aulize haraka haraka…
“Ana nini?”
“Ana mimba” alijibu Sam
“Mimba? Haya mlete huku”
Sam alimbeba vile vile mpaka wodini akaelekezwa amlaze kitandani, haraka haraka alitundikiwa dripu zikaingizwa kwenye mishipa na kisha akapimwa na kusafishwa wakati huo Sam akiwa ametolewa nje.
Alipokuwa pale nje simu yake iliita, kwakuwa alikuwa na stress nyingi alishindwa kuipokea akaichunia lakini iliita tena zaidi ya mara mbili ikabidi aitoe mfukoni.
Alipoangalia aligundua mpigaji ni NISHA,
“Hallow”
“Haloo vipi Sam”
“Safi niambie”
“Nakuomba uje hapa nyumbani mara moja ni ishu muhimu sana”
“Niko hospitali mke wangu anaumwa…”
“Tafadhali njoo haraka huchelewi kurudi ni muhimu sana.”
Sam alifikiria haraka haraka na kuamua haraka haraka kuwa aende kwa Nisha, aliwasha gari na kulikimbiza akafika kwa Nisha na kumkuta akiwa ndani kajilaza na Kanga yake.
“Wao baba kijacho karibu” Sam alishtuka kusikia lile jina akajiuliza ina maana Nisha amejua kuwa mkewe ana mimba ndio maana anamuita Baba kijacho… amejuaje sasa?
“Unamaanisha nini?”
Nisha aliokota karatasi zilizokuwa kwenye kochi na kumkabidhi Sam…
“Soma baby, nina mimba yako…”
“Una nini?”
“Nina Mimba yako Sam, wewe ni baba kwasasa”
Sam hakutaka kusikia neno lingine, alimsukumiza Nisha akaanguka na yeye akatoka haraka akazama kwenye gari lake na kuacha vumbi.
“Hivi hawa wanawake wa siku hizi mbona hawana akili? Wanadhani uongo ni mali au?” sam alikuwa anajisemea mwenyewe ndani ya Gari.
Hasira alizokuwa nazo zilikuwa hazielezeki kwani alijiona akitoneshwa kidonda kwa mara nyingine, yaani ametoka kudanganywa na Mkewe alafu Nisha nae anamdanganya.
Ndani ya akili yake Sam aliamua jambo moja ambalo hakutaka kulipinga, badala ya kwenda hospitali aliendesha moja kwa moja mpaka chuoni kwa mdogo wake alipokuwa anasoma.
Alipofika alienda moja kwa moja hosteli kwao kwani giza lilikuwa limeshaingia, alimpigia Simu na kumuomba atoke waonane.
Naomba Bonyeza Matangazo Kila Unapoyaona ili Kunipa Nguvu ya Kuendelea Kuwaletea Simulizi
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
JIUNGE KWA UPDATE NA BURUDANI ZAIDI
WhatsApp Channel=> CnZ Media(Follow)
Telegram Channel=> CnZ Media(Join)